Ushauri: Jinsi ya kudai kurudishiwa fedha ya kishika uchumba

Azoge Ze Blind Baga

JF-Expert Member
Mar 8, 2019
366
1,377
Wakuu salama hapa?

Kuna rafiki yangu alinitafuta akihitaji ushauri na kujua taratibu za kufuata ili aweze kudai na kurejeshewa fedha zake na mali zingine alizotoa kama kishika uchumba kwa mpenzi wake ambaye walipanga wawe mke na mume.

Baada ya jamaa kutoa kiasi fulani cha fedha na mali zingine kwa mama wa mwanamke kama kishika uchumba, jamaa aliondoka eneo ambalo alikuwa anaishi kwenda kutafuta hela sehemu nyingine ili mwisho wa siku aje amchukue yule mpenzi wake wakaishi pamoja huku taratibu za mahari na ndoa zikifanyika.

Ila baada ya muda kapata taarifa yule mama mkwe wake kachukua fedha za mwanaume mwingine na kumwozesha yule binti wakati anajua kabisa kapokea fedha za rafiki angu.

Je, utararibu upoje ili jamaa arudishiwe tu fedha yake, maana haiwezekani aache iliwe hivi hivi kwa tamaa za mama na mwanae.

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Wakuu salama hapa

Kuna rafiki angu alinitafuta kuhitaji ushauri na kujua taratibu za kufuata ili aweze kudai na kurejeshewa fedha zake na mali zingine alizotoa kama kishika uchumba kwa mpenzi wake ambaye walipanga wawe mke na mume

Baada ya jamaa kutoa kiasi fulani cha fedha na mali zingine kwa mama wa mwanamke kama kishika uchumba, jamaa aliondoka eneo ambalo alikua anaishi kwenda kutafuta hela sehemu nyingine ili mwisho wa siku aje amchukue yule mpenzi wake wakaishi pamoja huku taratibu za mahari na ndoa zikifanyika.

Ila baada ya muda kapata taarifa yule mama mkwe wake kachukua fedha za mwanaume mwingine na kumwozesha yule binti wakati anajua kabisa kapokea fedha za rafiki angu

Je utararibu upoje ili jamaa arudishiwe tu fedha yake maana haiwezekani aache iliwe hivi hivi kwa tamaa za mama na mwanae.

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
MLIANDIKISHANA MAHALI AU.....
 
Huo uchumi una UHAKIKA gani utatengemaa kwa muda unaotaka ili uoe!!!?

Hivi huu ujinga wa tafuta hela KWANZA ndio yee kwenye MAHUSIANO itaisha lini kwenye jamii zetu!!!?

Usipopata kingi je ndio usioe!!?utumwa mwingine huu!!
Haya yote yamesababishwa na Aina ya mabinti/wanawake waliopo kwa Sasa. Ni zaidi ya omba omba na wana tamaa Sana. Kwahiyo wanaume tunaogopa kuingia kwenye ndoa
 
Haya yote yamesababishwa na Aina ya mabinti/wanawake waliopo kwa Sasa. Ni zaidi ya omba omba na wana tamaa Sana. Kwahiyo wanaume tunaogopa kuingia kwenye ndoa
Uyo jamaa ana bisha kitu kiko wazi.utaingiaje kwa ndoa ujajiandaa kiuchumi?
Mwanamke gan atakukubali una kitu?
Kwanini vijana hawaoi?
NB:Mamb yamebadilika mkuu saiv ni pesa.
 
Back
Top Bottom