Trilioni 424? Tuacheni utani jamani

Ukichukua sample ya madini yaliyokuwemo katika mchanga unaoshikiliwa..ukafanya sampling kama base..ukaangalia idadi ya makontena yaliyosafirishwa kwa miaka 17 huwezi kupata hii hesabu kweli?ukiona hizi fedha ni nyingi then unakubali kuwa nchi yetu ni maskini wa resources?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali la kujiuliza ni hao tra walikua wapi miaka yote hiyo kutokukusanya kodi? Waliokua viongoz wa tra au mawazir miaka hiyo hatujaskia wakishtakiwa kwa uzembe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hili ni jambo la kushangaza sana, hao barrick gold kwa migodi yao yote duniani wanapata revenue kati ya 8.8 to 13 billion dollar kwa mwaka,sas mgodi mmoja tu wadaiwe dola 190bil

Hakika jambo hili limeichekesha sanaa dunia.
 
hili ni jambo la kushangaza sana, hao barrick gold kwa migodi yao yote duniani wanapata revenue kati ya 8.8 to 13 billion dollar kwa mwaka,sas mgodi mmoja tu wadaiwe dola 190bil

Hakika jambo hili limeichekesha sanaa dunia.
 
Mkuu ata ayo madini yaliokusanywa na kuchukuliwa na hio kampuni toka 2000 mpaka 2017 sidhani kama yanaifikia hio trilion 424.
HAHAHAHA WACHA MUVI IENDELEE tutaonekana vilazer zaid ya hapa
Acacia Mining has been slapped with a Tanzanian tax bill almost 200 times the firm's market cap

Oliver Gill

Oliver Gill is a City A.M. reporter, you can contact him on oliver.gill@cityam.c [..]

icoast-mine-gold-agbaou-456846888-597624c22906b.jpg

Acacia Mining refutes both the findings and the tax assessment of the Tanzanian authorities (Source: Getty)

Acacia's bust-up with the Tanzanian government today took yet another unexpected turn after authorities slapped the London-listed firm with a $190bn (£146bn) bill for unpaid taxes and penalties.

Shares in the firm collapsed over a quarter today. Acacia's market capitalisation currently stands at £750m.

Tanzania reckons Acacia has syphoned off large quantities of minerals without paying the associated export tax. Two presidential committees have alleged Acacia under-declared export revenues between 2000 and 2007 for the Bulyanhulu gold mine and 2007 and 2017 for the Pangea minerals mine.

Read more: Acacia loses millions in revenue due to new Tanzania mining rules

Acacia is yet to receive copies of either of the presidential reports but it "refutes each set of findings and reiterates that it has fully declared all revenues".
 
Tumeshindwa Vi vonder sasa Tunataka pesa za mtelemko wazeee wa Kitonga hahahahahahahah
 
Wameshagundua udhaifu wa mtu fulani mahali ulipo na ukitaka kumfurahisha mpitishe kwenye anga anazopenda hata Kama utakuwa unamdanganya hatakuwa na akili za kugundua kuwa kadanganywa kwa kuwa ni mtu mpenda sifa.
 
Hapa ndiyo utaona jinsi TRA wanavyokurupuka na assessments zao ambazo ni za juu mnooo kutubambikia Watanzania kodi kubwa kuliko maelezo na matokeo yake kuathiri biashara nchini kwa namna mbali mbali. Hii assessment ya ACACIA imewaacha uchi kabisa. Sijui watakuja na utetezi upi wa hii assessment kubwa kiasi hiki.
Mkuu ungesoma hiyo press release ya acacia ungejua source ya Tra kufukia hiyo figure.
 
Hivi ni kweli hawa waliopeleka hii assessment ya kodi kwa ilo shirika walipata kiasi icho? Jamni mbona hii ni hatari sasaa? Kiasi icho sasa ni trilion kama za zimbabwe au kama za hizi nchi zingine? hio kampuni inaweza kutoa wapi? Au wale wamejiandikia tu basi flani aone?

Figure hio ni sawa na kumpelekea muuza mkaa makadirio ya kodi ya gunia zake za toka 2013 hadi 2017 ziligharimu msitu mzima wa mbuga ya serengeti.

Tutumie elimu na weledi wetu vizuri waungwana, tueleweshane tu, africa moja hii, maana kuna mambo mengine unayaskia redion unajua labda mtangazaji kakosea kusema kiasi husika.

Endapo nchi yoyote ya kiafrica ikipata trilioni 424 papo kwa hapo basi itakua ni nchi ya nne kwa kua na uchumi mkubwa zaidi ndani ya bara hili na top 60 ya nchi tajiri duniani itakuemo vizuri tu.

Kwaio trilion 424 si ni sawa tu na matajiri watano wakubwa duniani wote wanyang'anywe mali zao ipewe ile nchi? Tobaa mbona tunaskia Bill Gates peke ake ana uwezo wa kuwapa buku buku watu wote duniani na chenchi ikabaki, jumlisha na wenzake tena?

Mambo nisiyopenda kuyaona africa ni eti kuchukua begi moja kubwa sanaa kwenda kununua tu nyanya sokoni, kua na noti hadi za milion 10.

Nliskia et Africa kuna shule za mabweni wanafunzi wake wanawekewaga mafuta ya taa kwenye vyakula vyao, au labda athari zake ndizo hizi sasa.

Tuache utani tuwe serius, haya ni mazingaombwe na yana aibisha watu wa ile nchi na kuonekana wao na shule ni mbali mbali.

NB. Hakuna nchi yoyote iliyotajwa jina hapa, tafadhali bhana tuheshimiane oooh.
Nimecheka sana hapo mwishoni mwishoni uliposema huku Afrika kuna shule za mabweni wanawekaga mafuta ya taa kwenye vyakula labda ndio mazara yake, anyway hata kama tulikula vyakula vya mafuta ya taa labda ndio tumeamka sasa kudai haki yetu maana mafuta ya taa yalitulaza muda mrefu
 
Hakuna utani hapo,either walipe au wachape lapa!Lini mzungu kakuonea ww mtanzania huruma?why mnyonywaji unamtetea mnyonyaji asiekufaidisha na chochote kwa kufanya biashara kwenye nchi yako?au ndio yale ya kutaka kupinga kila kitu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani ss ni watanzania tumeibiwa sana tuache utani.Kiukweli mahesabu hayo in sawa kabisa kwasababu kwa miaka kumi bila kulipa kodi staiki na faini zake ni sawa.Nionavyo mm inawezekana hata TRA.kuna vingine wameacha ,,,Tuache kujidharau namna hii.Wazungu wanatajirika na nchi zao kwa rasimali zetu Tz na Africa.Tuache uoga tumsapoti rais ahakikishe TRA eanapambana haya makampuni yalipe hizo PESA .Ili ss eanyonge tupumue na majasho yetu.na siyo wazungu wale raslimali zetu namna hii.Watanzania Tuamke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata pato la Marekani kwa mwaka halijafikia hapo.

Tril. 450 ni pesa nyingi sana.
Na ikumbukwe kuwa kuna nyingine tena zilizokuwa zinapotea au kulipwa japo kidogo mwanzoni kama mrahaba.
Na pia kuna za rushwa zilikua zinatolewa kwa ajili ya kuwalainisha baadhi ya wahusika ili waweke mikataba mibaovu.
Sasa najiuliza hayo makadirio ya mauzo ya hao jamaa kana ni makubwa hivyo inamaana wao waliuza na kupata faida kubwa kiasi gani ili wao watoe kodi kubwa kiasa hicho?

Hata tungekua tunagawana nao nusu kwa nusu ina maana wangekua wamepata faida ya zaidi ya Tril. 900. Ni pesa ambazo kwa mwananchi wa kawaida ambaye hakusoma hesabu vizuri hawezi kuandika tarakimu za hicho kiwango.

Kama tukikisia tu kuwa faida yao ni zaidi ya Tril. 900 je, mauzo yao yatakua ni sh. Ngapi tangu wameanza kama sio zaidi ya Tril. 70,000. Trillion elfu sabini?
Hayo madini mengi hivyo kama yameuzwa nje ya nchi toka nchi moja basi kuna uzembe mkubwa kwa TRA kwa miaka yote zaidi ya 20 na inabidi wahusika wote wawajibishwe idara yote ya TRA kwa kutusababishia hasara kubwa kiasi hicho.

Vinginevyo tutaaminu kuwa siasa imeingia TRA na kuweka utaalam pembeni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TRA daaahhh 424,000,000,000,000÷17 = 24,000,000,000,000. mimi nahisi hawa TRA ni wehu kwanini wanafanya mambo ya kitoto. Au wanataka wamfurahishe MALAIKA
 
Back
Top Bottom