Treni Yagonga Gari Makusudi

Treni Yagonga Gari Makusudi

Leo ni ajali ya pili hiyo maana asubuhi sana rav 4 imegonga garimoshi hilo kwenye makutano ya barabara ya kuelekea shekilango na ubungo maziwa.

Naanza kulinganisha Akili za madereva magari binafsi na Bodaboda, haiwezekani kila siku wenye magari wawe wanabutuliwa tu.
 
Uzembe wa madereva ni upande mmoja.....
Kisheria treni haigongi....ila kuna taratibu wanapaswa kuzifuata ili kulinda watu na magari yanayovuka treni. Kama eneo lina magari mengi wanapaswa kuweka geti na taa za kizuia magari pindi treni inapokaribia.

We dereva unaona kabisa kuna foleni alafu reli imekatisha na wewe unaenda kusimama kati kati ya reli utakuwa dereva makini kweli? Huu ndo uzembe huwezi simama kati kati ya reli na unaiona kabisa lazima uache gap
 
hebu ficha up......vu wako! sitaki kuamini kuwa wewe ni kilaza kiasi hicho!Hekima ya namna gani ulitaka itumike?Angeepukaje kuigonga gari hiyo?kwa kutoka kwenye rail na kupita pembeni?au kwa kufunga breki za ghafla?unayajua madhara ya breki za ghafla kwa treni?Unajua ni muda gani na kwa umbali gani treni inaweza kusimamishwa na ikakubali kusimama?kabla hujaandika jaribu kukifahamu unachotaka kukiandika.

Ungeisoma thread vizuri, ungejua alichokomenti RR ni busara zaidi ya wewe kumuita kilaza. Mara nyingi ni heri kuficha upumbavu, ili busara zako zionekana. Nimeshawahi kuwa dereva wa treni, hakuna nisichokijua kwenye principles za safe driving. Speed ya treni ya mwakyembe ambayo ina simama kila baada ya less than 5km, ikiwa na mabehewa chini ya 15, na mzigo mdogo sana wa abiria, treni inasimama on the spot, dreva akiamua.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: RR
We dereva unaona kabisa kuna foleni alafu reli imekatisha na wewe unaenda kusimama kati kati ya reli utakuwa dereva makini kweli? Huu ndo uzembe huwezi simama kati kati ya reli na unaiona kabisa lazima uache gap

Uzembe wa mtu mmoja hauhalalishi mtu mwingine afanye ajali ya makusudi. Ajali ya makusudi ni uzembe mkubwa zaidi. Dreva mzuri hujiepusha na ajali.
 
hebu ficha up......vu wako! sitaki kuamini kuwa wewe ni kilaza kiasi hicho!Hekima ya namna gani ulitaka itumike?Angeepukaje kuigonga gari hiyo?kwa kutoka kwenye rail na kupita pembeni?au kwa kufunga breki za ghafla?unayajua madhara ya breki za ghafla kwa treni?Unajua ni muda gani na kwa umbali gani treni inaweza kusimamishwa na ikakubali kusimama?kabla hujaandika jaribu kukifahamu unachotaka kukiandika.

Nandani hapa pu.......vu ni ww labda kama unafuta mkumbo tu bila kuelewa kilichozungumzwa mwanzo umeelezwa treni imepita kituo na kwenda kuligonga gari halafu imerudi nyuma mpaka kwenye kituo na kuchukua abiria sasa kwa nn huyu dereva wa garimoshi tusimuiye kichaa
Mm ni mpandaji mzuri sana wa hili mwakyembe sijaona likipita kituoni na kwenda kusimama mbele na kurudi tena kwa mwendo wa kutoka pale mwananchi mpaka tabata ? Huyo dereva wa gari moshi hana lolote zaidi ya wivu tu na utadhani amelazimishwa kulitumikia taifa nyang'anyi la tanzagiza
 
  • Thanks
Reactions: RR
Ni kituo cha mwananchi tabata.
Treni ameligonga kwa makusudi gari lilikuwa limekwama kutokana na traffic jam inayosababishwa na marori maeneo hayo ya relini.
Mara baada ya kuligonga gari ikiwa mwendo
mdogo kabisa lilirudi nyuma kuchukua abiria na kuendelea na safari.
Gari hiyo aina ya defender iliachwa nyanganyanga

NB
Tunasema treni imegonga gari kwa kuwa kila aliyekuwepo aliamini kwamba treni ingesimama au ilipaswa kusimama kwanza kuchukua abiria badala ya kuwapita abiria kwenda kugonga gari.

Aidha kila aliyeshuhudia aliona wazi kuwa kitendo hicho ni cha makusudi hasa ukizingatia treni ilikuwa mwendo mdogo na barabara inaonekana tokea mbali.

Ndugu unajua sheria angalau kidogo ya barabarani! Unavyosema treni imegonga gari makusudi unamaana ikiacha barabara yake na kuingia kwenye lami kulifuata gari ama! La hasha naamini lilikuwa ktk njia yake, basi ki ufupi hakuna gari inayoruhusiwa kusimama ktk njia ya treni,sheria inasema hivyo,kuwe na maloli or chochote kile haijustify kuvunja sheria. Nawasilisha
 
tuwe tunafwata taratibu na sheria zilizowekwa, na akili na busara pia.
watanzania tumekuwa na tatizo sugu la kutofwata sheria na taratibu za nchi. huo ulikuwa uzembe uliotokana na kutotaka kufwata sheria ya kutokaa katika reli.
sasa hv waenda kwa miguu wengi wamekuwa wakigongwa na magari kwa kutovuka katika sehemu maalumu za kuvukia waenda kwa miguu unakuta kila mtu kwa wakati wake sehemu yoyote ya barabara anachomoka na kuvuka barabara. hii inawaletea shida sana waendesha vyombo vya moto.
bodaboda wamekuwa wapita ovyoovyo tu akiona upenyo kakatiza na kusababisha ajali nyingi ambazo zingeepukika.

tujenge utamaduni wa kufwata sheria na taratibu za nchi. ndio maana tukienda nchi za wenzetu tunapata shida kwa sababu wenzetu wako vizuri katika kufwata sheria.

Mimi nimefanya kazi TRC taratibu ni kama ulivyozieleza wengi hatujui sheria zinazoongoza makutano ya Reli na Barabara yaani Railways Crossroads utakuta mtu kaweka kijigari chake kati kati ya Reli anasubiria foleni huo ni uvunjaji wa sheria wa makusudi, na endapo Treni itakupitia bado wewe mmiliki wa gari utakuwa na hatia maana umeizuia Treni isipite kwenye Barabara yake pia kuna tahadhali nyingi huwa zinaweka kwenye makutano hayo ila wale wote walioletewa leseni na Shangazi zao nyumbani huwa hawazijui na ndo maana hawazifuati na matokeo yake ndo hayo wanataka Treni isimame wakati wenyewe ndo wameizuia isipite mtakanyagwa sana na mtashitakiwa pia!
 
Ni kituo cha mwananchi tabata.
Treni ameligonga kwa makusudi gari lilikuwa limekwama kutokana na traffic jam inayosababishwa na marori maeneo hayo ya relini.
Mara baada ya kuligonga gari ikiwa mwendo
mdogo kabisa lilirudi nyuma kuchukua abiria na kuendelea na safari.
Gari hiyo aina ya defender iliachwa nyanganyanga

NB
Tunasema treni imegonga gari kwa kuwa kila aliyekuwepo aliamini kwamba treni ingesimama au ilipaswa kusimama kwanza kuchukua abiria badala ya kuwapita abiria kwenda kugonga gari.

Aidha kila aliyeshuhudia aliona wazi kuwa kitendo hicho ni cha makusudi hasa ukizingatia treni ilikuwa mwendo mdogo na barabara inaonekana tokea mbali.

Tii sheria bila shuruti
 
Mwenye Defender ana kesi ya kujibu
 
Eleweni hoja ya jamaa. Treni haina na urefu wa kufika barabarani inaposimama kuchukua abiria kituoni. Mwendesha treni amefanya makusudi, akakipita kituo ili akaligonge gari, baada ya kuligonga ina maana ameshapitiliza kituo chake, akalazimika kurudi nyuma ili awe usawa wa kituo chake achukue abiria, na hii inaonyesha alipitiliza makusudi. Kwa ufupi tusiishie kujadili sheria tu, tuangalie na nia ya muendesha treni
 
Mkuu mwendesha treni si tu alikua anamkomoa mwenye defender...alikua analitoa kwenye njia yake kisha ndo apakie abiria aendelee na safari...kwani mkuu mara ngapi tunasimama na magari yetu kutoa kizuizi(mwiba au jiwe) ili tupite vizuri?
 
Mkuu picha tafadhali..

train & car.jpg
 
Kama treni imegonga gai basi hiyo itakuwa ni kwa mara ya kwanza. Daima treni hugongwa na si viinginevyo. Safari nyingine reli itabaki wazi hata kama kuna foleni. Pole sana mwenye defender, labda insurance watamsaidia.
 
Ninavyofahamu mimi treni haiwezi kufunga breki ya ghafla na kwa kufanya hivyo mabehewa yote nyuma yanaweza kuacha reli na ajalai ikawa mbaya zaidi,kwahiyo kwa mafunzo ya udereva wa treni ni kuwa ni bora ugonge gari yenye mtu mmoja au watu wawili kuliko kufanya sudden braking ambayo inaweza kusababisha kitu kinaitwa jerking kwa hayo mabehewa na hatimaye derailment kitu kinachoweza kuleta vifo au majeruhi ya watu zaidi ya mia moja.Na vilevile kwa sheria za usalama barabarani huruhusiwi kusimamisha gari kwenye reli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom