Treni kusafirisha wananchi Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Treni kusafirisha wananchi Dar es Salaam

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, May 12, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,583
  Likes Received: 5,763
  Trophy Points: 280
  Treni kusafirisha wananchi Dar es Salaam


  KUNA habari njema kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuwa iwapo Serikali itakubali kutenga Sh bilioni 4.8 katika bajeti yake ijayo, mwanzoni mwa mwaka kesho, wataanza kutumia usafiri wa treni wakati wa kwenda na kurudi kazini.

  Mamlaka husika zimelithibitishia HABARILEO kuwa, iwapo Serikali itakubali kutoa kiasi hicho cha fedha, adha ya usafiri kwa baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam itapungua kwa kuwa watu zaidi ya 600 watakuwa wanasafirishwa kwa safari moja.

  Kampuni inayomiliki Rasilimali za Reli (Rahco) tayari imeshakamilisha bajeti inayotakiwa na imewasilisha serikalini bajeti yake maalumu kwa ajili ya kufanya matengenezo ya miundombinu ya reli ili itumike kusafirisha abiria katika Jiji la Dar es Salaam.

  Mtendaji Mkuu wa Rahco, Mhandisi Benhadard Tito aliliambia gazeti hili jana kuwa, fedha walizoomba ni za kukarabati mabehewa 14, injini tatu za treni, ujenzi wa vyoo vya umma, ukarabati wa reli ikiwemo kuboresha tuta katika reli itokayo Ubungo Maziwa hadi Stesheni.

  Tito alisema, katika ujenzi huo wa miundombinu, pia watajenga vituo sita ambavyo wasafiri watavitumia kusubiria treni ambayo itakuwa inafanya safari zake kati ya Ubungo hadi Stesheni iliyoko katikati ya jiji.

  Vituo hivyo vitajengwa maeneo ya Kamata, Buguruni Mnyamani, Tabata Relini, Ami, Makuburi na Mabibo. Ujenzi huo wa vituo utajumuisha maeneo ya abiria kuketi na kuweka vikinga jua na mvua.

  Tito alifafanua kuwa, kutakuwa na treni mbili zitakazofanya safari kwa siku, moja ikitoka Stesheni kwenda Ubungo na nyingine itatoka Ubungo kwenda Stesheni.

  Alisema, kila treni itakuwa na mabehewa sita, kila moja likiwa na uwezo wa kubeba abiria 100.

  Alisema hivyo katika safari moja treni hiyo itakuwa inabeba abiria 600. Pia alisema kunahitajika mabehewa mawili ya dharura pamoja na injini moja ambayo pia itakuwepo kwa ajili ya dharura.

  “Spea zote za kufanya matengenezo haya zinatoka nje ndiyo maana tumejiwekea muda wa miezi sita kufanya ukarabati wa kila kitu na ujenzi wa miundombinu mingine,” alisema mhandisi huyo na kusisitiza kuwa uwezo wa wataalamu kufanya kazi hadi kupatikana kwa mabehewa hayo upo ili mradi fedha zipatikane.

  Alisema, mradi huo wa kusafirisha abiria kwa kutumia treni upo siku nyingi, lakini umekuwa unakwamishwa na upatikanaji wa fedha.

  “Lakini kwa kuwa safari hii Rais Kikwete amelizungumzia kwa kina suala hilo na sisi tumeona tulifanye kwa kasi ili fedha hizo zikipatikana basi usafiri huo uanze kufanya kazi,” alisema.

  Alisema, iwapo fedha hizo zitapatikana itachukua miezi sita kuyafanyia ukarabati mabehewa, injini na ujenzi wa vituo na baada ya hapo hakutakuwa na pingamizi ya kuanza kwa safari hizo. Alisema kwa kuwa wataalamu wapo, suala hilo halitakuwa na tatizo.

  Alipoulizwa iweje waangalie tu kwenye njia ya kutoka Ubungo kwenda Stesheni wakati kuna reli nyingine ya kutoka Pugu kuja Stesheni, Tito alisema, wameamua kwanza kushughulikia njia moja kutokana na uchache wa mabehewa yanayomilikiwa na Kampuni ya Reli (TRL).

  Alisema kati ya mabehewa 97 ya TRL ni mabehewa 37 tu ambayo yanafanya kazi na mengine yapo katika hali mbaya.

  “Hivyo nakuhakikishia kuwa iwapo tutaamua kuanzisha safari hizo kwa njia zote mbili, basi treni ya kwenda Bara haitakuwepo kwani mabehewa yote yatakuwa yanatumiwa na treni ya Dar es Salaam,” alisema.

  Alisisitiza kuwa, licha ya kampuni yake kusimamia miundombinu, huduma za usafiri wa treni zitasimamiwa na TRL.

  Kabla ya Shirika la Reli kubinafsishwa liliwahi kutangaza zabuni kwa wawekezaji binafsi wenye nia ya kusafirisha abiria kwa njia ya reli wajitokeze.

  Lakini iliyokuwa Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC), ilizuia mpango huo kwa maelezo kuwa mwekezaji ambaye atakodishiwa TRC, ndiye ambaye ataruhusiwa kufanya biashara hiyo.

  Hivi karibuni, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba, ilitembelea reli hiyo kuona miundombinu yake kwa nia ya kujiridhisha kwamba inaweza kuanza safari za kubeba abiria.
   
 2. i411

  i411 JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 810
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Yangu mie macho nitaamini nikiona hizo treni za abiria zuikikatiza mabibo
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,583
  Likes Received: 5,763
  Trophy Points: 280
  Nasubiri nauli zao kama atujatembea kama uganda
   
 4. s

  samvande2002 JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2011
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  mara mabasi yaendayo kasi sana, mara treni, mara bajaji za wajawazito, ilimradi tu kuwadanganya raia...dah, ccm bwana
   
 5. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #5
  May 12, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Mabasi yaendayo kasi vipi mbona hatusikii tena,au ndo kamchezo? Kama mtu angezaliwa pengine alafu akaletwa hapa na akaambiwa mipango ya serikali za Tz anaweza akaomba apewe uraia saa hyohyo bila kujua anaingia choo cha kike,Tz bwana!
   
 6. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mimi nasubiri meli yetu kule ziwa Nyasa
   
 7. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #7
  May 12, 2011
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,356
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  ccm hiyo! haya hebu tusubiri tuone!
   
 8. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #8
  May 12, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kwa hakika mashaka ni mengi
   
 9. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #9
  May 12, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,922
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 160
  hata si somi hiyo habari...hamna kitu. Wameshindwa kumanage dala dala tu ndo uniambie walete treni. Labda si serikali hii
   
 10. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #10
  May 12, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  The Dar metro transit train project would have been completed as we are talking had it not been for the stupidity, jealousy and ignorance of the TRC workers whose intention was to block any good moves that were put in place by the RITES management.
   
 11. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #11
  May 12, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mungu uwahurumie na uwasamehe, lipi wamefanya likawa? TRC, ATC, TTCL, TANESCO, UDA?
   
 12. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #12
  May 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wamasai wanasubiri ile ahadi ya kuchimbiwa mabwawa ya kufugia samaki.
  Shule za msingi nazo zinasubiri Computer....
  Duuh!
   
 13. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #13
  May 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Where is the groan button??
  Jamani Mods naomba hicho ki button nimgongee huyu mtu, yeye na jamaa zake wamelifirisi shirika la reli halafu anakuja humu anaanza kutukana staffs wa TRL.
   
 14. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #14
  May 12, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  HONGERA SERIKALI YA CCM.....ili tuwapongeze mfanikishe na ili tuwazomee mlete sababu lukuki za kukwama mpango huu
   
 15. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #15
  May 12, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  So you wanna me banned just for voicing my opinion? JF thrives when there are battles of ideas, opinions, views etc
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  May 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,510
  Likes Received: 19,928
  Trophy Points: 280
  wameitoa aisee
   
 17. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #17
  May 12, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  hahaha mkuu VUVUZELA unanikumbusha wimbo wenu ule mnaocheza kwenye kioda(Ngoma ya wanyasa/wamanda) mnaimba; Wananchi wa ludewa tunalilia meli hahahahahahaah
   
 18. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #18
  May 12, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Vigogo wanaomiliki daladala watacha mpango huu ufanikiwe? Si itakula kwao,....
   
 19. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #19
  May 12, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kwani ule mradi wa mabasi ya kasi umekamilika?
   
 20. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #20
  May 12, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  The are the ones who were behind the fall of RITES
   
Loading...