Trend Reading: Salum Mwalimu, Mb. Mtarajiwa, Kinondoni!. Hata Wana CCM Wasioendekeza Ujinga, Watamchagua!.

Sina uhakika kama kweli CDM kitashiriki katika uchaguzi huu! Na kama watashiriki, je, mgombea ni mkazi wa Kinondoni? Je, ni kweli kwamba Mtuli hakueleweka juu ya sababu zilizomfanya ajiengue CDM? Je, ni kweli kwamba hakuna mwana CDM ambaye ni mkazi wa Kinondoni ambaye anaweza kuwawakilisha wana Kinondoni bungeni?
Najaribu kuwaza tu kwa sauti na sio kutokana na kuwa mbaguzi au mkabila! Samahanini!
Mkuu,ukumbali sana na jambo husika.mtulia alikua mwana cuf
 
Paskali naona umeanza kumkampenia Salum Mwalimu huku ukijivika uzalendo butu wakati wewe ni mfuasi wa Chadema. Usiwaite watu wajinga kwa kutokuiunga mkono Chadema maana kila mtu ana itikadi yake na chaguo lake. Imekuwa ni falsafa ya Wanachadema pamoja na viongozi wao kujiona wao ndo wana akili sana kuliko watu wengine kitu ambacho kwa wenye busara wanawaona sio watu sahihi ktk uongozi maana kiongozi bora ni yule mwenye lugha za staha na humuheshimu kila mtu. Tusubiri kampeni zianze uchaguzi ufanyike tutazijua chuya na mchele maana kama unavyodai mnanunuliwa basi CHADEMA ni MACHANGUDOA maana hao ndo hununulika
KWAN MGOMBEA WA CCM NI NANI?
 
N kwa sabab akili zenu sio za kichambuz
Upinzani hauwez imarika kama tupo na wenyeviti sampul ya lipumba

Jana tulisema chama hakitashiriki chaguz ndogo kwa kuwa sio huru na kwamba chama kitashirik pale tu TUME YA UCHAGUZ itarekebisha kasoro zote tulizoziainisha
Tukasusa chaguz watu wa kijan wakachukua majimbo kiulain

Leo tumekubali kuingia tena ulingon ilhal TUME imepuuzilia mbal madai yetu

Alaf unakuja na akil za mihemko
Pamba.vu!!!

Tunataka CCM itoke yap
Ila sio kwa chama chenye wanachama mambulula tusioweza kuhoj na kupatiwa majib kinaifu
Uko sahihi mkuu,ila je walisema hawata shiriki kila uchaguzi utao itishwa au ulikua ule tu uliopita?.
 
Nakubaliana na wewe ccm kushinda uchaguzi hawahitaji wapiga kura kama wengi wetu tunavyojidanga Bali wanahitaji mtangaza matokeo tu.hivi watu wamesahau why ni rahisi mtu kupenda katika tundu la sindano kuliko kubadirisha katiba ya Tanzania
Huu ndo ukweli mchungu
 
Paskali naona umeanza kumkampenia Salum Mwalimu huku ukijivika uzalendo butu wakati wewe ni mfuasi wa Chadema. Usiwaite watu wajinga kwa kutokuiunga mkono Chadema maana kila mtu ana itikadi yake na chaguo lake. Imekuwa ni falsafa ya Wanachadema pamoja na viongozi wao kujiona wao ndo wana akili sana kuliko watu wengine kitu ambacho kwa wenye busara wanawaona sio watu sahihi ktk uongozi maana kiongozi bora ni yule mwenye lugha za staha na humuheshimu kila mtu. Tusubiri kampeni zianze uchaguzi ufanyike tutazijua chuya na mchele maana kama unavyodai mnanunuliwa basi CHADEMA ni MACHANGUDOA maana hao ndo hununulika
Wewe mbona wazazi wako machangudoa hatusemi?
 
CHADEMA hamuwezi shinda hapo kinondoni hebu Cheki hii 1st eleven ya CCM , Foward kwenye Kampeni atakuwepo Polepole, Nape na Kinana, Katikati atacheza Makonda, Musa Zungu, Bulembo ,Mangula. Defence atacheza Msukuma, Mwigulu na Kigwangalla, Kipa atacheza Ole Sendeka. Kwa hii List sijui mtatokea wapi? Reserve List Mawaziri wote kwa ajili ya Kueleza Mafanikio ya CCM pamoja na Wakuu we Wilaya Wote was Dar es Salaam, Pia watakuwepo Wazalendo Wote waliojiunga na CCM kama Kafulila, Machali, Albert Msandu, Katambi, Masha n.k hamtatoka hapo CHADEMA kwa huu mziki
Ccm hawahita kura ili washinde,bali mtangaza matokeo tuu
 
Nadhani nivema kukaa nakuchagua mfumompya wakufanya Demokrasi yenyemfumo wa siasa na maendeleo! Lakini hii majungu mengi,na inadumaza akili za vijana.
 
CHADEMA hata wakeshe wanafanya kampeni hawawezi kushinda kwenye Jiji la Makonda , hivi mnamjua RC Makonda au mnamsikia hawezi kukubali Jimbo likaenda kwa hao Wahuni
Anayeamua nani awe mbunge ni Makonda au wananchi?
Halafu watu wanagonga Like kwenye mawazo ya kijinga namna hiyo!
Mawazo yanayotweza uwezo wetu wa kufikiri, kuamua na kutenda kama wananchi isipokuwa Makonda anaamua kwa niaba yetu!
Hii inathibitisha bila shaka kuwa, CCM huwa haishindi uchaguzi na raia tunashadadia upuuzi huo kwa kiwango cha kujivuni?
 
Wanabodi,

Declaration of Interest
Naomba nianze kwanza kwa kudeclare interest, kuwa mimi Pascal Mayalla ni kaazi wa Wilaya wa Kinondoni, ambako ni Mwananchi wa kawaida, sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa chama chochote cha siasa, na hili bandiko, sio la kumpigia debe mgombea yeyote, bali as good citizen of this nation, ukiona mtu yoyote au chama chochote, kinatuleta ujinga Watanzania, sisi ambao sio wajinga, we have a duty of care, kuwaelimisha wengine, na kuwahamasisha, wasikubali kuletewa ujinga na chama chochote, na kukubali kuuchagua huo ujinga, hivyo kuwa waliochagua ujinga, ndia wajinga Zaidi, kuliko hata aliyewaletea ujinga!, ila ukiletewa ujinga, ukaelimishwa kuwa huu ni ujinga, na bado ukachagua ujinga, then, utakuwa umefanya informed decision ya kuukubali ujinga huo, swali linabaki Jee Wana Kinondoni ni Wajinga?.

Jee Watanzania ni Mazuzu?. Tunaweza Kuletewa Ujinga na Kuuchagua Ujinga Huo?.
Bandiko hili ni muendelezo wa ile hoja yangu kuwa Watanzania kwa muda mrefu tumekuwa tukifanywa mazuzu na baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kwa kutuletea ujinga, na wanasiasa wajinga, just to take us for granted kuwa kwa vile ni chama kikubwa, kinapesa sana, kinapendwa sana, na kinakubalika sana, hata wakisimamisa jiwe, jiwe litachaguliwa!.

Ujinga huu ndio CCM imewafanyia wana Kinondoni kwa kuwaletea mgombea aliyewafanyia ujinga fulani kinondoni.

Ujinga wa CCM Kinondoni ni Upi?, Jee ni Ujinga Kweli?, Jee Wana Kinondoni ni Wajinga Kuchagua Ujinga?.
Ili kuielewa hoja yangu hii kwa kina, inakubidi ujipe muda kupitia bandiko hili
Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law!, Kuendelea Kuitumia ni Ujinga?, Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!.


CCM na Ujinga Uliopitiliza, Jee wana Kinondini ni Wajinga?. Ni Mazuzu?. Wanafanyiwa Ujinga, Jee Wataukubali Ujinga Huu?.

Kiukweli kitendo kilichofanywa na CCM kuwasimamisha wabunge wale wale waliotufanyia ujinga wa kujiuzulu, na kutuingiza ghara za uchaguzi wa mazudio kwa sababu za kijinga, ni ujinga uliopitiliza!.

Hii inaamisha CCM inawaona wana Kinondoni na wana Siha kuwa ni wajinga!, yaani mtu aliyeaminiwa na wananchi, na kuchaguliwa kuwa mwakilishi wao, halafu anajiuzulu kwa sababu za kijinga, kisha kugombea tena kupitia cha kingine, akitaraji atachaguliwa tena!, ikitokea ni kweli akachaguliwa, wananchi wa maeneo hayo, watakuwa ni wajinga wa kutupwa, kwa kufanywa wajinga na kuukubali ujinga huu!. Kwa sasa siwezi kuwasemea wananchi wa Siha, ila kwa vile mimi ni mkazi wa Kinondoni, na ni mpiga kura wa Kinondoni, kamwe siwezi kuukubali ujinga huu, hivyo nitawahamasisha wana Kinondoni, wanaojielewa ma kujitambua, wasiukubali ujinga huu wa CCM, kutaka kutufanya mazuzu!, hivyo kutoa wito kwa wana Kinondoni wote, wakiwemo wana CCM, kuutumia uchaguzi huu wa marudio, kutuma ujumbe Mzito kwa Chama cha Mapinduzi, kuwa Wana Kinondoni sio wajinga, sio mazuzu, na hawakubali kuletewa ujinga!, hivyo watamchagua mhombea yoyote, kutoka chama kingine chochote but not CCM!.

Namfahamu Mgombea wa Chadema Kinondoni, Salum Mwalimu!, Ni Jembe la Ukweli!.
Hivyo baada ya Chadema kumtangaza Salum Mwalimu, kugombea jimbo la Kinondoni katika uchaguzi wa marudio, naomba kwanza kukiri, mimi Pascal Mayalla, namfahamu Kijana huyu kwa karibu, alikuwa ni Mwandishi wa Habari na Mwenzangu wa Channel Ten, alipoajiriwa Channel Ten, alinikuta na nilimpokea, ni mchapa kazi hodari, hivyo kwa ujinga ambao CCM imewafanyia wana Kinondoni, naamini kabisa, hata wana CCM wanaojitambua, na wasiokubali ujinga, watamchagua Salum Mwalimu!.

Kinondoni, Msikubali, Kuwachagua Mala.. wa Kisiasa, Wanaohongwa Kuhama Vyama Vyao, ni Mala.. tuu kama Wale Wanawake Mala.. Wengine Wote!.
Kitendo cha mwanasiasa kukubali kuhama chama kwa kuahidiwa chochote, maana yake ni kukubali kuhongwa, na kuhongwa, kuko kwa aina nyingi, sio lazima kuhongwa pesa!, kuna waliohongwa ajira, kuna waliohongwa kugombea tena, juhongwa ni kuhongwa tuu, na kiyendo cha mtu yoyote kuhongwa chochote na kukubali hongo hiyo, huu ni umala.. wa kisiasa, hivyo kuna wanasiasa, wanaohama vyama vyao na kuhamia vingine, kwa ridhaa zao wenyewe, hawa hawana kosa lolote kwa sababu hii ndio demokrasia yenyewe.

Lakini wanaohama vyama kwa kuhongwa au kushawishiwa kwa namna yoyote, na kuukubali ushawishi huo, hawa ni wanasiasa mala.. wa kisiasa!. Na kuhongwa sio lazima pesa tuu, hata kuitwa Ikulu na kuombwa kuhama chama chako. huku ni kutongozwa, ukibali ni hongo!. Thank God, Mwamba wa Kaskazini, uliitwa Ikulu na kutongozwa uhame, kwa vile sio mala.., mwamba huu uligoma, ila ndio ulitifungua macho kuwa kumbe kuna hongo, watu wanatongozwa, na kuhongwa, uthibitisho wa kuhongwa huku ni kupokea hongo hizo wazi wazi na kila mwenye macho, anaziona!.

Kwa kufuata kanuni ya aliyekutwa na ngozi, ndiye aliyekula nyama, huu ni uthibitisho jinsi viongozi wetu wenye dhamana, wanavyofanya mambo ya kujinga ya kutongoza wanasiasa na kuwahonga!.
Kama Hiki Ndicho Lowassa Alichoitiwa Ikulu!, Then Tuna Rais wa Ajabu!, Kama ni Uongo, Lowassa Ashitakiwe Kwa Uchochezi!.
Kwa vile tuhuma hii haijakanushwa!, then huu ndio uthibitisho wa baadhi ya wanaohama kuhongwa!.

Jee Mtulia wa CUF Kinondoni, na Moleli wa Chadema Siha, Wamehongwa?. Hivyo ni Mala.. wa Kisiasa!.

Jibu ni yes!, hawa wote wawili, wametongozwa!, wakahongwa na kuhongeka!, hivyo wote wawili ni mala.. wa kisiasa!. Uthibitisho kuwa wamehongwa na kuhongeka, ni kiyendo cha kujitoa vyao vyao, na kujiunga CCM, na hapo hapo kuteuliwa kuwa wagombea wa CCM. Ugombea wa CCM, unapitia mchakato Fulani, kitendo cha wajiuzulu hawa kujinga CCM leo, na kuteuliwa bila mchakato wa kura za maoni, ni uthibitisho tosha, walikubali kujiengua vyama vyao kwa ahadi za kuteuliwa tena!. Hii I hongo na huu ni umala.. wa kisiasa!. Wana Kinondoni na Wana Siha, wasiukubali ujinga huu!.

Paskali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom