Trend Reading: Salum Mwalimu, Mb. Mtarajiwa, Kinondoni!. Hata Wana CCM Wasioendekeza Ujinga, Watamchagua!.


Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,574
Likes
31,823
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,574 31,823 280
Wanabodi,

Declaration of Interest
Naomba nianze kwanza kwa kudeclare interest, kuwa mimi Pascal Mayalla ni mkaazi wa Wilaya wa Kinondoni, kama mwananchi wa kawaida, sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa chama chochote cha siasa, na hili bandiko, sio la kumpigia debe mgombea yeyote, bali as good citizen of this nation, ukiona mtu yoyote au chama chochote, kinatuleta ujinga Watanzania, sisi Watanzania wenzenu ambao sio wajinga, na tumejaaliwa kauwezo hata kadogo tuu cha kuubaini ujinga tunaotaka kuletewa, then we have a duty of care, (tuna wajibu) wa kuwasaidia wenzetu wengine ambao ni less fortunate, kuwaelimisha kuhusu ujinga huo, na tuna jukumu la kuwahamasisha wenzetu, wasikubali kufanywa wajinga kwa kuletewa ujinga na bado wakachagua ujinga huo.

Tanzania Tuna Mapungufu Makubwa Katika Uelimishaji Elimu ya Uraia, Hivyo Kila Tunafanywa Wajinga kwa Kuletewa Ujinga na Kuchagua Ujinga!.
Watanzania wazalendo wa kweli, ni wale wenye moyo wa dhati wa kuwasaidia wenzao kwa kuwaelimisha na kuwahamasisha, wasikubali kufanywa wajinga, kwa kuukataa ujinga!. Wewe ukiwa ni mzalendo, ukaona chama fulani kinataka kuwaletea wananchi ujinga, hupaswi kunyamazia kimya ujinga huu, bali una wajibu wa kuwaelimisha wengine kuwa hiki mnacholetewa na chama fulani, ni ujinga, hivyo kuwaelimisha na kuwahamasisha, wasikubali kufanywa wajinga kwa kuletewa ujinga na chama chochote cha siasa, na wao kuukubali ujinga huo, kuukumbatia na kuchagua chaguo la ujinga huo.

Wanaoletwa Ujinga na Kuchagua Ujinga Huo Bila Kujua Wanachagua Ujinga, ni Watu wa Kuhurumiwa na Kuelimishwa.
Watu wenye kauli ya mwisho, wamchague nani katika uchaguzi wowote, ni wananchi wa eneo husika, ikitokea wananchi wa eneo fulani, wameletewa ujinga bila wao kujua walicholetewa ni ujinga, hivyo kujikuta wamechagua ujinga!. Watu wa aina hii, wanaoletewa ujinga na kuuchagua ujinga huo bila kujua kuwa wanachagua ujinga, ni watu wa kuhurumiwa na wanachohitaji ni kusaidiwa kwa kuelimishwa ili wasiendelee kufanywa wajinga, kwa kuletewa ujinga na kuuchagua ujinga huo!.

Wanaoletewa Ujinga, Na Kuelimishwa Wameletewa Ujinga, Lakini Bado Wakachagua Ujinga, Ni Wajinga Kuliko Waliowaletea Ujinga!. Jee Wanakinondoni ni Wajinga Kuliko?.
Ukiletewa ujinga, na ukapatiwa fursa ya kuelimishwa kuwa hiki ulicholetewa ni ujinga, lakini bado ukawa radhi kuuchagua huo ujinga kwa ridhaa yako mwenyewe, utakuwa umefanya informed decision kwa kuukubali ujinga huo, hivyo watu wa aina hii, watakuwa ni watu wajinga kuliko hata aliyewaletea ujinga|!. Swali linabaki kwa Wana Kinondoni, Jee Wana Kinondoni ni Wajinga?, Wanaweza kuletewa ujinga na wakauchagua huo ujinga?.
Hivyo hili ni bandiko elimishi, kuwaelimisha wana Kinondoni, ujinga wanaoletewa na CCM, ili mwisho wa siku, hata kama wataamua kuchagua ujinga, tutakuwa tunawajua ni watu wa aina gani kwa sababu angalau, walipata fursa ya kuelimishwa kabla!.

Jee Watanzania ni Mazuzu?. Tunaweza Kuletewa Ujinga na Kuuchagua Tuu Ujinga Huo Kama Mazuzu?.
Bandiko hili ni bandiko elimishi la muendelezo wa ile hoja yangu kuwa Watanzania kwa muda mrefu tumekuwa tukifanywa mazuzu na baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kwa kutuletea ujinga, na wanasiasa wajinga, just to take us for granted kuwa kwa vile ni chama kikubwa, kinapesa sana, kinapendwa sana, na kinakubalika sana, hata kikileta ujinga wa aina gani, ujinga huo utapita hivyo, hivyo kujiaminisha, hata wakisimamisa jiwe, jiwe litachaguliwa!.

Ujinga huu ndio Chama cha Mapinduzi, CCM kimewafanyia wana Kinondoni kwa kuwaletea mgombea aliyewafanyia ujinga fulani Kinondoni, licha ya ujinga huo, CCM kimewaletea tena mjinga huyo huyo na kuwataraji wana Kinondoni, watamchagua!.

Jee Ujinga wa CCM Kinondoni ni Upi?, Jee ni Ujinga Kweli?, Jee Wana Kinondoni ni Wajinga Kuchagua Ujinga?.
Ili kuielewa hoja yangu hii kwa kina, inakubidi ujipe muda kupitia kwanza bandiko hili
Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law!, Kuendelea Kuitumia ni Ujinga?, Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!.
Wanabodi,

Watanzania Tufanye Siasa za Ukweli, Tuachane na Siasa za Ujinga Ujinga.
Tufike mahali sisi Watanzania, wazalendo, wenye nia njema na maendeleo ya taifa hili letu masikini, tubebe jukumu la kuisaidia nchi yetu, na taifa letu, hatuwezi kukaa kimya kwa kuendelea kuwawabesha masikini wa Tanzania, mzigo wa gharama za uchaguzi wa marudio, kwa sababu za kijinga jinga kabisa, zinazotokana na siasa za ujinga ujinga!. Kitendo hiki cha masikini wa kutupwa wa Tanzania, wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea wa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, halafu kuja kubebeshwa mzigo wa kugharimia chaguzi za marudio kutokana na sababu za kisiasa za ujinga ujinga, na sababu zenyewe kuwa ni sababu za kijinga kabisa, its not only ni nonsense, but also ni dhambi kwa Mungu, kuwabebesha masikini hawa gharama hizi za ziada kutokana na ujinga tuu wa watu fulani in the name of politics!..

Kiongozi Akiishachaguliwa, Anakuwa ni Kiongozi wa Watu, na Sio Kiongozi wa Chama, Kwa Sababu Anachaguliwa na Watu na Sio Chama!.
Ujinga mwingine mkubwa kabisa ni huu, hata kama mgombea amedhaminiwa na chama cha siasa kugombea, akiishapitishwa na Tume ya Uchaguzi kuwa Mgombea, japo anatambulika kama ni mgombea wa chama fulani, lakini akiishachaguliwa, mwenyekiti wa mtaa, diwani, mbunge au rais, anakuwa sio kiongozi wa chama kilichomdhamini, bali anakuwa ni kiongozi wa watu, wananchi wote, kwa sababu waliomchagua sio wanachama wa chake bali ni wananchi wote wa eneo husika, wakiwemo wanachama wa chama chake. Mfano baada ya rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais kwa tiketi ya CCM, lakini hakuchaguliwa na wana CCM, amechaguliwa na Watanzania wote, wakiwemo wana CCM na wasio wana CCM, hivyo japo rais Magufuli alipendekezwa na CCM, lakini baada ya kuchaguliwa, hawi rais wa CCM, bali ni rais wa Watanzania wote, vivyo hivyo kwa wabunge, madiwani na viongozi wa serikali ya mtaa, kitendo cha kiongozi kujitoa chama na kupoteza ubunge, udiwani au uongozi wa umma, ni ujinga ambao haupaswi kuendelea kukumbatiwa!, it doesn't make sense kiuongozi wa umma kupoteza Uongozi wake at an expense ya chama cha siasa!, huyu ni kiongozi wa watu na sio kiongozi wa chama!. Tuuache jinga huu kwa kubadili sharia zetu!. Nini muhimu kati ya umma na chama?. Kuukosesha umma kiongozi waliemchagua kwa sababu za chama, sio tuu sio haki kwa wananchi waliomchagua, bali ni ujinga uliopitiliza, halafu kuja kulipisha wananchi hawa gharama za uchaguzi wa marudio ni ujinga mwingine na dhambi juu yake ukizingatia kiwango cha umasikini wa nchi yetu.

Nini Kifanyike, A Way Forward.
Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini mwetu kwa sasa.
  1. Iwekwe faini maalum kwa kila kiongozi wa umma, atakayejiuzulu nafasi yake kwa sababu za kijinga jinga, ikiwemo kukatwa mafao yake na ikibidi kufilisiwa ili kugharimia gharama za uchaguzi wa marudio kwa kulitia hasara taifa.
  2. Viongozi wote wanaojiuzulu kwa sababu za kijinga, wasiruhusiwe tena kugombea nafasi zile zile walizojiuzulu, kama sababu za kujiuzulu kwao, mimi nimeziita ni za kijinga, tusiwakubalie wajinga hawa kugombea tena, ili wasije kutuletea tena ujinga ule ule na kutugharimisha masikini sisi kugharimia uchaguzi wa marudio.
  3. Chama kitakacho wapitisha viongozi wajinga hawa, kugombea tena, huku kutakuwa ni kuwafanya wananchi wa eneo husi kuwa ni wajinga, kwa kuiongozi wao kuwaletea ujinga kwa kujiuzulu, halafu anakuja kuomba tena achaguliwe tena!.
Hitimisho.
Tanzania is too poor to spend billions on by elections caused by foolish and nonsense reasons, nikimaanisha nchi yetu Tanzania ni masikini wa kutupwa, kuhalalisha matumizi ya mabilioni ya fedha kuendesha chaguzi ndogo za marudio kwa sababu za kijinga. Ili Taifa letu lipate maendeleo ya kweli, ni lazima sisi Watanzania tukubali kuwa wakweli toka ndani ya nafsi zetu, tusikubali ujinga huu wa kuhama vyama, uendelee kutugharimisha sisi masikini wa kutupwa, tunaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu kuendelea kugharimishwa na wajinga fulani kwa sababu za ujinga wao!, ni kutufanya wajinga!.

Paskali
CCM na Ujinga Uliopitiliza, Jee wana Kinondini ni Wajinga?. Ni Mazuzu?. Wanafanyiwa Ujinga, Jee Wataukubali Ujinga Huu?.
Kiukweli kitendo kilichofanywa na CCM kuwasimamisha wabunge wale wale waliotufanyia ujinga wa kujiuzulu, na kutuingiza gharama za uchaguzi wa marudio kwa sababu za kijinga, ni ujinga uliopitiliza!.

Hii inaamisha CCM inawaona wana Kinondoni na wana Siha kuwa ni wajinga!, yaani mtu aliyeaminiwa na wananchi, na kuchaguliwa kuwa mwakilishi wao, halafu anajiuzulu kwa sababu za kijinga, kisha kugombea tena kupitia chama kingine, akitaraji atachaguliwa tena!, ikitokea ni kweli akachaguliwa, wananchi wa maeneo hayo, watakuwa ni wajinga wa kutupwa, kwa kufanywa wajinga na kuukubali ujinga huo!. Kwa sasa siwezi kuwasemea wananchi wa Siha, ila kwa vile mimi ni mkazi wa Kinondoni, na ni mpiga kura wa Kinondoni, kamwe siwezi kuukubali ujinga huu, hivyo nitawahamasisha wana Kinondoni, wanaojielewa ma kujitambua, wasiukubali ujinga huu wa CCM inaotuletea, kutaka kutufanya mazuzu!, hivyo kutoa wito kwa wana Kinondoni wote, wakiwemo wana CCM, kuutumia uchaguzi huu wa marudio, kutuma ujumbe mzito kwa Chama cha Mapinduzi, kuwa Wana Kinondoni, we might be ignorants kwa kutokujua, but we are not stupid!, nikimaanisha tunaweza kuwa tulikuwa wajinga kwa kumchagua kiongizi mjinga kwa mara ya kwanza, bila kuujua ujinga wake, lakini sisi sio mazuzu, Chama cha Mapinduzi, kututeulia mjinga huyu, halafu tuje tumchague kwa mara ya pili, tutakuwa ni ma stupid!. Ili Kinondoni kuonyesha kuwa we not stupid na hatukubali kuletewa ujinga, nahamasisha wana Kinondoni, kumchagua mgombea yoyote, kutoka chama kingine chochote but not CCM!.

Namfahamu Mgombea wa Chadema Kinondoni, Salum Mwalimu!, Ni Jembe la Ukweli!.
Licha ya kukiri kuwa sina chama, lakini kunapotokea fursa ya kumbaini mtu fulani anaweza kuwa kiongozi mzuri, nami ninajukumu la kuwaelimisha wengine, uzuri wa mtu huyo, na huwa nafanya hivi hata kwa wagombea wowote wazuri wa vyama vyovyote.
Mfano katika mchakato wa CCM, hata kabla wengi hawajajua kuwa mgombea wa CCM atakuwa ni John Pombe Magufuli, mwaka mmoja kabla Magufuli hajateuliwa na CCM, niliweka angalizo hili
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Na miongoni mwa wagombea urais wa CCM waliogombea na Magufuli, mimi pendekezo langu lilikuwa
Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa!
na hata sasa rais wetu ni Dr. John Pombe Magufuli, hata tawala milele, muda wake utafika, naye ataondoka na watakuja wengine, hivyo baada ya kuuona utendaji wa rais Magufuli, nimetoa ushauri huu, Watanzania tusiendelee kusubiria tuu kumpata rais kwa bahati, bali tuanze mtindo wa grooming, tukimuona mtu fulani ana uwezo, tusisubiri hadi Magufuli aondoke, ndipo watu waanze kupigana vikumbo kuusaka urais, bali tumgroom
Prof. Mbarawa ni Presidential material! Tuwaspot na kuwagroom Presidential materials au tumwache tu yeyote awe?
Huu ni uthibitisho kuwa mimi sina chama hivyo mtu akiwa ni mzuri, haijalishi ni wa chama gani, tutamuunga mkono, ndani ya CCM kuna watu wazuri, tuwaunge mkono, na pia kuna watu wa hovyo, tusiwaunge mkono, na kwenye upinzani pia kuna watu wazuri, tuwaunge mkono, na watu wa hovyo, tuwakatae!. Hivyo hata kama ningekuwa mwana CCM, hala chama change cha CCM kikatuletea mtu wa hovyo, kama huu ujinga wa Kinondoni na Siha, halafu Wapinzani wakatuletea mtu safi!, tutamchagua mgombea wa upinzani, na hiki ndicho hata Mwalimu Nyerere alichofanya Butiama ile 1995 kumsuport mgombea wa upinzani!.

Hivyo baada ya Chadema kumtangaza Salum Mwalimu, kugombea jimbo la Kinondoni katika uchaguzi wa marudio, naomba kwanza kukiri, mimi Pascal Mayalla, namfahamu Kijana huyu kwa karibu, alikuwa ni Mwandishi wa Habari na Mwenzangu wa Channel Ten, alipoajiriwa Channel Ten, alinikuta na nilimpokea, ni mchapa kazi hodari, hivyo kwa ujinga ambao CCM imewafanyia wana Kinondoni, naamini kabisa, hata wana CCM wanaojitambua, na wasiokubali ujinga, wakiujua wasifu wa Salum Mwalimu, watamchagua Salum Mwalimu!.

Kinondoni, Msikubali, Kuwachagua Mala.. wa Kisiasa, Wanaohongwa Kuhama Vyama Vyao, ni Mala.. tuu kama Wale Wanawake Mala.. Wengine Wote!.
Kitendo cha mwanasiasa kukubali kuhama chama kwa kurubuniwa, au kuahidiwa chochote, maana yake ni kukubali kuhongwa, na kuhongwa, kuko kwa aina nyingi, sio lazima kuhongwa pesa!, kuna waliohongwa ajira, kuna waliohongwa kugombea tena, kuhongwa ni kuhongwa tuu, na kitendo cha mtu yoyote kuhongwa chochote na kukubali hongo hiyo, huu ni umala.. wa kisiasa, hivyo kuna wanasiasa, wanaohama vyama vyao na kuhamia vingine, kwa ridhaa zao wenyewe, hawa hawana kosa lolote kwa sababu hii ndio demokrasia yenyewe.

Lakini wanaohama vyama kwa kuhongwa ahadi au kushawishiwa kwa namna yoyote, na kuukubali ushawishi huo, hawa ni wanasiasa mala.. wa kisiasa!. Na kuhongwa sio lazima pesa tuu, hata kuitwa Ikulu na kuombwa kuhama chama chako. huku ni kutongozwa, ukibali ni hongo!. Thank God, Mwamba wa Kaskazini, uliitwa Ikulu na kutongozwa ahame, kwa vile yeye sio mala. wa kisiasa, mwamba huu uligoma, ila ndio uliotufungua macho kuwa kumbe kuna hongo, watu wanatongozwa, na kuhongwa, uthibitisho wa kuhongwa huku ni kupokea hongo hizo wazi wazi na kila mwenye macho, anaziona!.

Kwa kufuata kanuni ya aliyekutwa na ngozi, ndiye aliyekula nyama, huu ni uthibitisho jinsi viongozi wetu wenye dhamana, wanavyofanya mambo ya kujinga ya kutongoza wanasiasa na kuwahonga!.
Kama Hiki Ndicho Lowassa Alichoitiwa Ikulu!, Then Tuna Rais wa Ajabu!, Kama ni Uongo, Lowassa Ashitakiwe Kwa Uchochezi!.
Kwa vile tuhuma hii haijakanushwa!, then huu ndio uthibitisho wa baadhi ya wanaohama vyama, wamehongwa!.

Jee Mtulia wa CUF Kinondoni, na Moleli wa Chadema Siha, Wamehongwa?. Hivyo ni Mala.. wa Kisiasa!.
Jibu ni yes!, hawa wote wawili, wametongozwa!, wakahongwa na kuhongeka!, hivyo wote wawili ni mala.. wa kisiasa!. Uthibitisho kuwa wamehongwa na kuhongeka, ni kitendo cha kujitoa vyama vyao, kuwasaliti wananchi waliowachagua na kujiunga CCM, na hapo hapo kuteuliwa kuwa wagombea wa CCM. Ugombea wa CCM, unapitia mchakato fulani, kitendo cha wajiuzulu hawa kujiunga CCM leo, na kuteuliwa bila mchakato rasmi wa ki CCM kufanyika, zikiwemo kura za maoni, ni uthibitisho tosha, walikubali kujiengua vyama vyao kwa ahadi za kuteuliwa tena!. Hii ni hongo na huu ni umala.. wa kisiasa!. Wana Kinondoni na Wana Siha, wasiukubali ujinga huu!.

Paskali
 
K

Kimla

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2008
Messages
1,665
Likes
1,746
Points
280
K

Kimla

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2008
1,665 1,746 280
NAAMINI MAGUFURI HANA SHIDA ANAWEZA KUTUACHIA HUYU HARAFU YEYE ACHUKUE KULE KWINGINE.UZURI SALIMU MWALIMU HAJAWI KUMSHAMBULIA MH RAIS.

Baada ya Chadema kumtangaza Salum Mwalimu, kugombea jimbo la Kinondoni katika uchaguzi wa marudio, naamini hata wana CCM wasiokubali ujinga huu, watamchagua Salum Mwalimu!.

Inaendelea

Paskali
 
ndunajr

ndunajr

Senior Member
Joined
Apr 28, 2015
Messages
170
Likes
176
Points
60
ndunajr

ndunajr

Senior Member
Joined Apr 28, 2015
170 176 60
Baada ya Chadema kumtangaza Salum Mwalimu, kugombea jimbo la Kinondoni katika uchaguzi wa marudio, naamini hata wana CCM wasiokubali ujinga huu, watamchagua Salum Mwalimu!.

Inaendelea

Paskali
Ujinga gani? wa kuhama hama vyama? jimbo lile liko ki mkakati usitegemee Mwalimu akachukua pale. CCM ya sasa ni ya hesabu kali. Si wajinga kabisa wale watu.
 
R

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
15,690
Likes
21,278
Points
280
Age
21
R

Retired

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2016
15,690 21,278 280
Baada ya Chadema kumtangaza Salum Mwalimu, kugombea jimbo la Kinondoni katika uchaguzi wa marudio, naamini hata wana CCM wasiokubali ujinga huu, watamchagua Salum Mwalimu!.

Inaendelea

Paskali
Paskali CDM wameamua wapi please niwekee hapa maana wengine tuko mashenzini....
 
R

Rodney01

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2013
Messages
734
Likes
585
Points
180
R

Rodney01

JF-Expert Member
Joined May 14, 2013
734 585 180
Salum Mwalim anaweza kuja kushinda endapo tu Cuf wangekubali kumtoa mgombea wao na kumsupport Mwalim but otherwise chadema kushinda kinondoni hiyo ni ndoto..Cuf ndio chama pekee cha upinzani kikubwa sana maeneo ya kinondoni...nimekulia huko so ninauwakika na hichi ninachokisema.
 
kavulata

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Messages
4,306
Likes
2,417
Points
280
Age
53
kavulata

kavulata

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2012
4,306 2,417 280
Baada ya Chadema kumtangaza Salum Mwalimu, kugombea jimbo la Kinondoni katika uchaguzi wa marudio, naamini hata wana CCM wasiokubali ujinga huu, watamchagua Salum Mwalimu!.

Inaendelea

Paskali
Mtolea hawezi kujiuzulu mwenyewe na kulisababishia taifa hasara ya kufanya uchaguzi tena kisha achaguliwe tena. Utakuwa uzuzu wa wananchi wa kinondoni wa hali ya juu aiseii!!.
 
U

urumrawi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Messages
1,496
Likes
1,482
Points
280
U

urumrawi

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2017
1,496 1,482 280
Baada ya Chadema kumtangaza Salum Mwalimu, kugombea jimbo la Kinondoni katika uchaguzi wa marudio, naamini hata wana CCM wasiokubali ujinga huu, watamchagua Salum Mwalimu!.

Inaendelea

Paskali
Never underrate CCM Mkuu
 
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
27,700
Likes
31,731
Points
280
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
27,700 31,731 280
Baada ya Chadema kumtangaza Salum Mwalimu, kugombea jimbo la Kinondoni katika uchaguzi wa marudio, naamini hata wana CCM wasiokubali ujinga huu, watamchagua Salum Mwalimu!.

Inaendelea

Paskali
HataPolepolekama ni mkazi wa Kinondoni atampigia kura Mwalimu
 
Imvubhu

Imvubhu

Senior Member
Joined
Aug 27, 2017
Messages
182
Likes
162
Points
60
Imvubhu

Imvubhu

Senior Member
Joined Aug 27, 2017
182 162 60
Naunga Mkono. Hoja Fikirishi kwa waelewa. Salum mwalimu yuko vizuri, hakurupuki na hana siasa za kishabiki. All the best nadhani Wanaccm watampa pia Kura. Mtua ameharibu sana CV yake. Unagombea kuingia upande wa pili kwa mbeleko ya Mkiti, sio njema sana kwa demokrasia ya chama tuliyoizoea.
 

Forum statistics

Threads 1,249,418
Members 480,661
Posts 29,697,436