Trend Reading: Salum Mwalimu, Mb. Mtarajiwa, Kinondoni!. Hata Wana CCM Wasioendekeza Ujinga, Watamchagua!.

Wanabodi,

Declaration of Interest
Naomba nianze kwanza kwa kudeclare interest, kuwa mimi Pascal Mayalla ni kaazi wa Wilaya wa Kinondoni, ambako ni Mwananchi wa kawaida, sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa chama chochote cha siasa, na hili bandiko, sio la kumpigia debe mgombea yeyote, bali as good citizen of this nation, ukiona mtu yoyote au chama chochote, kinatuleta ujinga Watanzania, sisi ambao sio wajinga, we have a duty of care, kuwaelimisha wengine, na kuwahamasisha, wasikubali kuletewa ujinga na chama chochote, na kukubali kuuchagua huo ujinga, hivyo kuwa waliochagua ujinga, ndia wajinga Zaidi, kuliko hata aliyewaletea ujinga!, ila ukiletewa ujinga, ukaelimishwa kuwa huu ni ujinga, na bado ukachagua ujinga, then, utakuwa umefanya informed decision ya kuukubali ujinga huo, swali linabaki Jee Wana Kinondoni ni Wajinga?.

Jee Watanzania ni Mazuzu?. Tunaweza Kuletewa Ujinga na Kuuchagua Ujinga Huo?.
Bandiko hili ni muendelezo wa ile hoja yangu kuwa Watanzania kwa muda mrefu tumekuwa tukifanywa mazuzu na baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kwa kutuletea ujinga, na wanasiasa wajinga, just to take us for granted kuwa kwa vile ni chama kikubwa, kinapesa sana, kinapendwa sana, na kinakubalika sana, hata wakisimamisa jiwe, jiwe litachaguliwa!.

Ujinga huu ndio CCM imewafanyia wana Kinondoni kwa kuwaletea mgombea aliyewafanyia ujinga fulani kinondoni.

Ujinga wa CCM Kinondoni ni Upi?, Jee ni Ujinga Kweli?, Jee Wana Kinondoni ni Wajinga Kuchagua Ujinga?.
Ili kuielewa hoja yangu hii kwa kina, inakubidi ujipe muda kupitia bandiko hili
Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law!, Kuendelea Kuitumia ni Ujinga?, Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!.


CCM na Ujinga Uliopitiliza, Jee wana Kinondini ni Wajinga?. Ni Mazuzu?. Wanafanyiwa Ujinga, Jee Wataukubali Ujinga Huu?.

Kiukweli kitendo kilichofanywa na CCM kuwasimamisha wabunge wale wale waliotufanyia ujinga wa kujiuzulu, na kutuingiza ghara za uchaguzi wa mazudio kwa sababu za kijinga, ni ujinga uliopitiliza!.

Hii inaamisha CCM inawaona wana Kinondoni na wana Siha kuwa ni wajinga!, yaani mtu aliyeaminiwa na wananchi, na kuchaguliwa kuwa mwakilishi wao, halafu anajiuzulu kwa sababu za kijinga, kisha kugombea tena kupitia cha kingine, akitaraji atachaguliwa tena!, ikitokea ni kweli akachaguliwa, wananchi wa maeneo hayo, watakuwa ni wajinga wa kutupwa, kwa kufanywa wajinga na kuukubali ujinga huu!. Kwa sasa siwezi kuwasemea wananchi wa Siha, ila kwa vile mimi ni mkazi wa Kinondoni, na ni mpiga kura wa Kinondoni, kamwe siwezi kuukubali ujinga huu, hivyo nitawahamasisha wana Kinondoni, wanaojielewa ma kujitambua, wasiukubali ujinga huu wa CCM, kutaka kutufanya mazuzu!, hivyo kutoa wito kwa wana Kinondoni wote, wakiwemo wana CCM, kuutumia uchaguzi huu wa marudio, kutuma ujumbe Mzito kwa Chama cha Mapinduzi, kuwa Wana Kinondoni sio wajinga, sio mazuzu, na hawakubali kuletewa ujinga!, hivyo watamchagua mhombea yoyote, kutoka chama kingine chochote but not CCM!.

Namfahamu Mgombea wa Chadema Kinondoni, Salum Mwalimu!, Ni Jembe la Ukweli!.
Hivyo baada ya Chadema kumtangaza Salum Mwalimu, kugombea jimbo la Kinondoni katika uchaguzi wa marudio, naomba kwanza kukiri, mimi Pascal Mayalla, namfahamu Kijana huyu kwa karibu, alikuwa ni Mwandishi wa Habari na Mwenzangu wa Channel Ten, alipoajiriwa Channel Ten, alinikuta na nilimpokea, ni mchapa kazi hodari, hivyo kwa ujinga ambao CCM imewafanyia wana Kinondoni, naamini kabisa, hata wana CCM wanaojitambua, na wasiokubali ujinga, watamchagua Salum Mwalimu!.

Kinondoni, Msikubali, Kuwachagua Mala.. wa Kisiasa, Wanaohongwa Kuhama Vyama Vyao, ni Mala.. tuu kama Wale Wanawake Mala.. Wengine Wote!.
Kitendo cha mwanasiasa kukubali kuhama chama kwa kuahidiwa chochote, maana yake ni kukubali kuhongwa, na kuhongwa, kuko kwa aina nyingi, sio lazima kuhongwa pesa!, kuna waliohongwa ajira, kuna waliohongwa kugombea tena, juhongwa ni kuhongwa tuu, na kiyendo cha mtu yoyote kuhongwa chochote na kukubali hongo hiyo, huu ni umala.. wa kisiasa, hivyo kuna wanasiasa, wanaohama vyama vyao na kuhamia vingine, kwa ridhaa zao wenyewe, hawa hawana kosa lolote kwa sababu hii ndio demokrasia yenyewe.

Lakini wanaohama vyama kwa kuhongwa au kushawishiwa kwa namna yoyote, na kuukubali ushawishi huo, hawa ni wanasiasa mala.. wa kisiasa!. Na kuhongwa sio lazima pesa tuu, hata kuitwa Ikulu na kuombwa kuhama chama chako. huku ni kutongozwa, ukibali ni hongo!. Thank God, Mwamba wa Kaskazini, uliitwa Ikulu na kutongozwa uhame, kwa vile sio mala.., mwamba huu uligoma, ila ndio ulitifungua macho kuwa kumbe kuna hongo, watu wanatongozwa, na kuhongwa, uthibitisho wa kuhongwa huku ni kupokea hongo hizo wazi wazi na kila mwenye macho, anaziona!.

Kwa kufuata kanuni ya aliyekutwa na ngozi, ndiye aliyekula nyama, huu ni uthibitisho jinsi viongozi wetu wenye dhamana, wanavyofanya mambo ya kujinga ya kutongoza wanasiasa na kuwahonga!.
Kama Hiki Ndicho Lowassa Alichoitiwa Ikulu!, Then Tuna Rais wa Ajabu!, Kama ni Uongo, Lowassa Ashitakiwe Kwa Uchochezi!.
Kwa vile tuhuma hii haijakanushwa!, then huu ndio uthibitisho wa baadhi ya wanaohama kuhongwa!.

Jee Mtulia wa CUF Kinondoni, na Moleli wa Chadema Siha, Wamehongwa?. Hivyo ni Mala.. wa Kisiasa!.

Jibu ni yes!, hawa wote wawili, wametongozwa!, wakahongwa na kuhongeka!, hivyo wote wawili ni mala.. wa kisiasa!. Uthibitisho kuwa wamehongwa na kuhongeka, ni kiyendo cha kujitoa vyao vyao, na kujiunga CCM, na hapo hapo kuteuliwa kuwa wagombea wa CCM. Ugombea wa CCM, unapitia mchakato Fulani, kitendo cha wajiuzulu hawa kujinga CCM leo, na kuteuliwa bila mchakato wa kura za maoni, ni uthibitisho tosha, walikubali kujiengua vyama vyao kwa ahadi za kuteuliwa tena!. Hii I hongo na huu ni umala.. wa kisiasa!. Wana Kinondoni na Wana Siha, wasiukubali ujinga huu!.

Paskali
Wakati unaiponda na kuhoji haki ya kuhama chama, kimantiki una tetea haki ya raia kugombea popote katika nchi hii. Kua makini na swala la haki ya mtu.
 
Salum Mwalim anaweza kuja kushinda endapo tu Cuf wangekubali kumtoa mgombea wao na kumsupport Mwalim but otherwise chadema kushinda kinondoni hiyo ni ndoto..Cuf ndio chama pekee cha upinzani kikubwa sana maeneo ya kinondoni...nimekulia huko so ninauwakika na hichi ninachokisema.
Cuf ipi? Cuf lipumba aka cufccm au cuf original?
 
Unge declare interest kwamba we ni Ccm na umeshindwa kukubali kua utatakiwa uchague Cdm kwa ujinga mliofanyian uko ndani ya chama

Wewe ni nani mpaka unipangie cha kufanya?

Mpumbavu nini? Jikite kwenye maoni siyo assumptions kuhusu mtoa maoni.

Who's Mwalimu mpaka tulazimishane kumchagua?
 
Wakati unaiponda na kuhoji haki ya kuhama chama, kimantiki una tetea haki ya raia kugombea popote katika nchi hii. Kua makini na swala la haki ya mtu.
Nadhani panapo tumika pesa au aina ingine ya kishawishi cha kumfanya mtu aamue basi neno haki huwa alitumiki, haki ni pale tu penye free will decision
 
Kwa style ile ya uchaguzi tuliona kwenye udiwani,tusitegeme ushindi kwenye ubunge kuna mambo mengi bado hayako sawa kwenye utaratibu wa chaguzi

Ova
 
Binafsi huwa ninakukubali sana Paskali

Bila shaka wana-Siha na wana-Kino wamekusoma na nnavyowajua hawawezi kuukubali ujinga huo wa mchana kweupe.
 
Paskali umepiga chini ya mkanda.....

Naelewa hiyo hasira na dissatisfaction....lkn kumwita mtu mala..... wa kisiasa...haijatulia...

Wewe ni muungwana, naamini utanielewa....
 
Hawa jamaa, tayari walikuwa wabunge, kwanini walijiuzuru, kisha, wanarudi kwa watu wale wale, kuwaomba wawape tena nafasi ile ile, walioikataa, tena kwa gharama kubwa, kutoka kwa watu wale wale,waliomuheshimu, wkamkubali, akawakataa! ! Sasa, anarudi kwa wale wale, na kuwatia gharama mpya na kubwa! (Chaguzi mpya,kwa kodi yao! Uzalendo upo wapi hapo ?
MASIKINI MAMA TZ. WANAO TUMEAMUA KUKUHUJUMU NA KUJIMALZA KIASI HIKI?
 
Kwahiyo kuna mtu kajimililisha mkoa sio? Kwa huu ujinga wako tu ilioandika hapo ndugu zako wangetakiwa waanze mchakato wa kupata kitanda milembe
Ww hujijui kuwa tayari ni mwendawazim?najua unapenda pesa za kupewa ili uwe msaliti wa taifa lkn ngoja nikwambie iko siku utakuja jua nn maana ya haki 2akati huo utakuwa ushachelewa,pole na ujinga wako mwanakwenda ww.
 
Ukweli Kinondoni ubunge huu Ukawa tayari wameshachukua. Hakuna wa kuwazuia.Ushindi uko wazi

Kinondoni ni jimbo la wasomi. Watu wenye uelewa na ni katika majimbo ambayo hayatakagi ujinga.
Ccm wamefanya utoto kwa kudhani watanzania bado ni wajinga na wapumbavu hata wakimleta mwizi au kibaraka wa lipumba wata mchagua hapana.
Nina uhakika ccm wenyewe wa kinondoni nao hawatakubali ujinga huu wa kumteua mbunge ali acha mwenyewe kwa sababu za kijinga.
Ccm nina amini hawa kubali kumpa kura mtu ambaye amesababisha 300m zitumike kurudia uchaguzi.

ONYO au TAHADHARI
Kinondoni ni eneo la Bashite....mastermind wa hila hivyo mjiandae kugombana naye Polisi wana muogopa kuliko Wanavo muogopa Magu. Kazi haitakuwa rahisi , ushindi sio kura tu....na mkitaka kupima ubabe wake kabla ya 2020 basi ni huu uchaguzi wa kinondoni...muwe tayari kwa vipigo, kesi za kugushi,na kutekwa
 
Siyo tu hasiruhusiwe kugombea kwenye uchaguzi wa marudio bali iwe mwisho kwake kugombea kwenye nafasi husika, mathalani mbunge akijiuzulu hasigombee tena ubunge katika ardhi ya Tanzania.
 
179 Reactions
Reply
Back
Top Bottom