Transfer Window 2014/2015, Special thread

Transfer Window 2014/2015, Special thread

Duh huyu jamaa kila nikimwona nabaki nacheka tu.

Kwa nini mkuu? Huyu ni si kazaliwa 1997? Kifaa kwa Wenger hiki!!

meenala.jpeg


 
Mshambuliaji kinda wa Chelsea Romelu Lukaku (21) huenda akatua Atletico Madrid kuchukua nafasi ya Diego Costa anayehamia Stamford Bridge.
 
Chelsea na ManUtd wamo kwenye vita kali kumwania Cesc Fabregas (27). Barcelona wanataka aende kwa vibonde ManUtd ambao hawatacheza Champions League msimu ujao, huku Chelsea wakitangaza mshahara wa £200,000 kwa wiki.
 
barcelona wanamtaka kiungo anaechezea fc sevile ivan rakitic ni raia wa crotia hapo hapo na real madrid wameshatangaaza dau la 25m euro kumwania kioungo huyo
 
Mshambuliaji Loic Remy (27) amesema chaguo lake ni kwenda Arsenal kuliko timu nyingine yoyote.
 
Kiungo Marouane Felaini (26) wa ManUted amewekwa sokoni, bei yake ni £12m. Hii ni baada ya kushindwa kung'ara tangu aliponunuliwa kwa £27.5m kutoka Everton. ManUtd wapo tayari kupokea ofa yoyote.
 
Van Gaal huenda akaachana na beki kinda Luke Shaw (19) wa Southampton na kumfuatilia Jordi Alba (25) wa Barcelona.
 
Kocha van Gaal Louis anajipanga kumwaga kitita cha £20m kumnyakua kiungo wa Bayern, Bastian Schweinsteiger (29) baada ya kumkosa Thomas Muller (24).
 
Chelsea imeipiga bao MauUtd kwa kumsajili Cesc Fabregas (27) kwa dau la £30m, kwa mkataba wa miaka 5! Atavaa jezi namba 4.
(Arsenal itanufaika kwa kupata mgao wa £5m kutokana na dili hilo).
 
ManUtd imejibu mapigo ya Chelsea kwa kukamilisha usajili wa Luke Shaw kwa dau la £40m, kwa mkataba wa miaka 5 na mshahara wa £160,000 kwa wiki.
 
Kocha anayetisha EPL Roberto Martinez (40) amesaini mkataba mpya wa miaka 5 kuifundisha Everton.
 
ManUtd imewaweka sokoni akina Nani, Javier Hernandez na Anderson. Ofa zinakaribishwa.
 
PSG wamekamilisha usajili wa beki anayepanda David Luiz (27) kutoka Chelsea kwa kitita cha 40m, kwa mkataba wa miaka 5. Atajiunga na timu yake mpya baada ya Kombe la Dunia.
 
PSG wamekamilisha usajili wa beki anayepanda David Luiz (27) kutoka Chelsea kwa kitita cha £40m, kwa mkataba wa miaka 5. Atajiunga na timu yake mpya baada ya Kombe la Dunia.
 
ManCity imekamilisha usajili wa beki Bacary Sagna (31) kutoka Arsenal kwa mkataba wa miaka 3.
Sagna atatua Etihad baada ya Kombe la Dunia.
Sagna alisajiliwa na Arsenal mwaka 2007 akitokea Auxerre kwa dau la £7m.
 
Mshambuliaji mtata Mario Balotelli (23) huenda akatua Arsenal msimu ujao. Wenger yumo kwenye mchakato MKALI wa kuhakikisha anainyakua mashine hiyo kutoka AC Milan.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom