Transfer Window 2014/2015, Special thread

Transfer Window 2014/2015, Special thread

Mshambuliaji anayetisha duniani Diego Costa (25) huenda akatua Chelsea msimu ujao.
 
Kocha Arsene Wenger (64) amesaini mkataba mpya wa kuifundisha The Gunners hadi mwaka 2017. Hii ni kufuatia mafanikio makubwa ya kuiwezesha Arsenal kucheza Champions League kwa misimu YOTE 17 aliyoifundisha Arsenal. Wenger atalipwa £8m kwa mwaka. na amehakikishiwa kitita cha £100m kwa ajili ya usajili.
wenger_FA.jpg
 
Liverpool wamepandisha dau kumchukua kiungo anayetisha EPL Adam Lallana (25) wa Southampton hadi £25m.
 
Barcelona imetangaza kwamba Cesc Fabregas (27) HAUZWI. Arsenal na ManUtd wameambiwa wasipoteze muda wao kumfuatilia.
 
Frank Lampard (35) anaondoka Chelsea baada ya kunyimwa mkataba mpya.
 
Kocha Louis van Gaal ametengewa kitita cha £220m kwa ajili ya usajili ManUtd. Wachezaji wanaotarajiwa kuja ni pamoja na kiungo Kevin Strootman (24), Luke Shaw, Cesc Fabregas, Koke, Mats Hummels na Miranda.
 
Mshambuliaji wa England Rickie Lambert (32) ametua Liverpool kwa mkataba wa miaka 2 kwa dau la £4m kutoka Southampton.
 
Mi namshangaa huyu mzee wenger sijaona dalili ya kuoneshq kwamba anataka mchezaji mwenye uchu na magoli kama suarez
 
Manchester City wanakaribia kumsajili Fernando kutoka Porto kwa pauni milioni 15 (Daily Mirror),

kiungo wa Arsenal Santi Cazorla amemtaka Mspanish mwenzake Cesc Fabregas kurejea Emirates (Metro), Edin Hazard amepewa jezi namba 10 msimu ujao. PSG wanamtaka kwa pauni milioni 61, lakini mwenyewe amesema hatoondoka baada ya kupewa namba 10 (Daily Mail),



Diego Costa yuko karibu sana kusaini Chelsea kwa pauni milioni 32, kilichosalia tu ni vipimo vya afya (Telegraph), Louis van Gaal anaamini Uholanzi haina budi kumshukuru David Moyes kwa kumfanya Robin van Persie kuwa hatari zaidi katika Kombe la Dunia (Daily Mirror),

Cesc Fabregas amekubali kusaini mkataba na Chelsea.
Kilichosalia ni makubaliano ya ada ya uhamisho, Barcelona wakiwa wanataka Euro milioni 36 (Mundo Deportivo), Koke, Fabregas na Paul Pogba wa Juventus, wote wapo kwenye 'rada' za Chelsea ili kuchukua nafasi ya Frank Lampard (Evening Standard).
 
Ila hii ya Fabregas mda mfupi Jose The special one kazungumza kuhusu hii ili swala lakini ukweli ni kwamba huwenda akatua Chelsea.
 
Mshambuliaji anayetisha duniani kwa sasa Diego Costa (25) amehamia Chelsea baada ya kukamilisha vipimo vya afya kwa dau la £32m.
 
ManUtd na Chelsea zipo kwenye vita kali ya kumnyakua Cesc Fabregas (27) kutoka Barcelona. Barcelona wanataka aende ManUtd kwa sababu haitacheza Champions League na hivyo sio tishio kwao. Lakini Chelsea wametangaza mshahara wa £200,000 kwa wiki.
 
Ila hii ya Fabregas mda mfupi Jose The special one kazungumza kuhusu hii ili swala lakini ukweli ni kwamba huwenda akatua Chelsea.

Unamuuza Matta unamleta Fabr?Hii akili au matope itakuwa kama kweli!Hawa wote uchezaji wao ni play maker hawakabi wala hawana nguvu ila ni wazuri kwenye kuanzisha move!

Kama unamkataa Matta huwezi mkubali Fabr!
 
Unamuuza Matta unamleta Fabr?Hii akili au matope itakuwa kama kweli!Hawa wote uchezaji wao ni play maker hawakabi wala hawana nguvu ila ni wazuri kwenye kuanzisha move!

Kama unamkataa Matta huwezi mkubali Fabr!

Yeye ndo kocha atajua njisi ya kufanya wakati amemleta Eto nae waliona kachanganyikiwa lakini tuliona alivyomsaidia kiasi chake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom