Transfer Window 2014/2015, Special thread

Kocha Wenger anamfuatilia mshambuliaji mkali wa Porto - Jackson Martinez, ambaye bei yake inakaribia £40m.
 
Kiungo Santi Cazorla (29) amesema anataka kuikacha Arsenal ili ajiunge na Atletico Madrid kwa msimu ujao.
 
Baada ya kumpata Fabregas kwa dau la £30m, Mourinho sasa ameanza kummendea ex-Arsenal mwingine - kiungo Alex Song (26) kwa dau la £10m. ManUtd nao wamo kwenye mawindo.
... Barcelona imesema Song hatoki bila £20m kuwekwa mezani.
 
Javier Hernandez CHICHARITO (26) ameweka wazi kwamba HANA MPANGO wa kubaki ManUtd na kuendelea kufanywa spare tyre wakati kipaji chake hakina utata ...Arsenal na Tottenham tayari washamtolea mimacho.
 
Karim Benzema (26) ameweka wazi kwamba anataka mshahara sawa na Gareth Bale - £135,000 kwa wiki, ama sivyo ataanza zake.
Gareth Bale ni mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi ndani ya LaLiga, akizidiwa na Christian Ronaldo pekee.
 
Kipa Pepe Reina anatakiwa kurudi Liverpool baada ya kuichezea Napoli kwa mkopo. Napoli imesema haina uwezo wa kulipa mishahara mikubwa kama ya EPL.
... Arsenal inajiandaa kumdaka juu kwa juu.
 
Mshambuliaji kinda wa Arsenal Joel Campbell (21) atarudi klabuni na kucheza ktk kikosi cha kwanza baada ya kung'ara ktk mechi dhidi ya Uruguay. Campbell alinunuliwa na Wenger mwaka 2011 kwa £1m tu, na amekuwa akicheza kwa mkopo nje ya Englanda kwa kunyimwa work permit. Ila sasa mambo yake yatanyooka baada ya kuonesha kiwango cha kutisha.
 
Arsenal imeandaa dau la £5m kumnunua kipa Pepe Reina wa Liverpool ambaye anatakiwa kurudi klabuni baada ya kuichezea Napoli kwa mkopo
 
Golikipa kinda wa Chelsea Thibaut Courtois (22) anarudi Darajani msimu ujao baada ya kuichezea Atletico Madrid kwa miaka 3 kwa mkopo, na kutwaa ubingwa wa LaLiga. Mkongwe Petr Cech anatafuta mlango wa kutokea.
 
ManUtd imetangaza rasmi inamtaka Thomas Varmaelen (28) wa Arsenal, kuziba pengo la Ferdinand na Vidic. Bei yake ni £15m
 
DIRISHA LA USAJILI LIPO WAZI HADI TAREHE 1 JULAI, 2014.

MANUTD
- Beki kinda Luke Shaw (19) ametua ManUtd kwa dau la £40m, kwa mkataba wa miaka 5 na mshahara wa £160,000 kwa wiki.
- Kocha van Gaal Louis anajipanga kumwaga kitita cha £20m kumnyakua kiungo wa Bayern, Bastian Schweinsteiger (29) baada ya kumkosa Thomas Muller (24).
- Kiungo Marouane Felaini (26) ametupwa sokoni, bei yake ni £12m. Hii ni baada ya kushindwa kung'ara tangu aliponunuliwa kwa £27.5m kutoka Everton.
- Kocha van Gaal ametua ManUtd kwa mkataba wa miaka 3, atasaidiwa na Ryan Giggs.
- Nemanja Vidic (32) atahamia InterMilan msimu ujao kwa uhamisho huru.
- Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani (27) anayechezea PSG amesema anatamani kutua Old Trafford msimu ujao. hii ni kutokana na kutoiva na kocha wake Laurent Blanc.
- Kinda Adnan Januzaj (19) anawindwa na PSG kwa ahadi ya mshahara mnono.

ARSENAL

- Mshambuliaji mtata Mario Balotelli (23) huenda akatua Arsenal kwa dau la £20m.
- Mshambuliaji Loic Remy (27) anasubiri ofa kutoka Arsenal, ingawa Tottenham wameshamwekea dau la £9m.
- Kocha Arsene Wenger (64) amesaini mkataba mpya wa kuifundisha Arsenal hadi mwaka 2017. Hii ni kufuatia mafanikio makubwa ya kuiwezesha Arsenal kucheza Champions League kwa misimu YOTE 17 aliyoifundisha Arsenal. Amepewa kitita cha £100m kwa usajili.
- Golikipa Lukasz Fabianski (29) anahamia Swansea kama mchezaji huru.
- Arsenal wanajipanga kumchukua kiungo Maraoune Fellaini (26) kutoka ManUtd kwa msimu ujao.
- Karim Benzema (26) anawindwa kwa dau la £40m.
- Beki Micah Richards (25) wa ManCity na mshambuliaji Wilfried Bony (25) wa Swansea wanawindwa kwa jumla ya £40m.

CHELSEA
- Beki anayepanda David Luiz (27) ametua PSG kwa kitita cha £40m, kwa mkataba wa miaka 5.
- Kiungo mshambuliaji Cesc Fabregas (27) ametua Chelsea kwa dau la £30m, kwa mkataba wa miaka 5! Atavaa jezi namba 4.
- Mshambuliaji anayetisha duniani kwa sasa Diego Costa (25) ametua Chelsea kwa dau la £32m.
- Frank Lampard (35) anaondoka Chelsea baada ya kunyimwa mkataba mpya.
- John Obi Mikel huenda akatua InterMilan msimu ujao.

LIVERPOOL
- Mshambuliaji wa England Rickie Lambert (32) ametua Liverpool kwa mkataba wa miaka 2 kwa dau la £4m.
- Kiungo anayetisha Adam Lallana (25) wa Southampton amepandishiwa dau hadi £25m.
- Real Madrid wametenga kitita cha £60m ili kumng'oa Luis Suarez (27).

MANCITY
- Full Beki JEMBE Bacary Sagna (31) amesaini mkataba wa miaka 3. Atalipwa £140,000 kwa wiki.
- Bei ya MKALI Lionel Messi (26) sasa ni £164m kwa mujibu wa dau lililotengwa na Mancity ili kumng'oa Barcelona.
- ManCity wametega dau la £53m kumng'oa kiungo kinda anayetisha duniani Paul Pogba (21) kutoka Juventus.

kuhusu messi kuna jarida nilisoma la ufaransa linasema psg wako tayari kutoa pound 250 million sasa cjajua kwa dau ilo kama city wanatakuwa na chao
 
Mshambuliaji kinda wa Arsenal Joel Campbell (21) atarudi klabuni na kucheza ktk kikosi cha kwanza baada ya kung'ara ktk mechi dhidi ya Uruguay. Campbell alinunuliwa na Wenger mwaka 2011 kwa £1m tu, na amekuwa akicheza kwa mkopo nje ya Englanda kwa kunyimwa work permit. Ila sasa mambo yake yatanyooka baada ya kuonesha kiwango cha kutisha.

waingereza washenzi sana na ndio maana hawafanyi vizuri world cup yani baada ya dogo kuperform ndio wanataka kumpa permit to hell with their permit
 
Karim Benzema (26) ameweka wazi kwamba anataka mshahara sawa na Gareth Bale - £135,000 kwa wiki, ama sivyo ataanza zake.
Gareth Bale ni mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi ndani ya LaLiga, akizidiwa na Christian Ronaldo pekee.

kaka ingia google upatye kusoma hii habari zaidi

Lionel Messi signed a new contract in May that will make him the highest-paid soccer player in the world at $27 million per year.
Going into the 2014 World Cup at age 26, Messi is already considered one of the best players ever and is already making more than $40 million with endorsements.
 
DIRISHA LA USAJILI LIPO WAZI HADI TAREHE 1 JULAI, 2014.

MANUTD
- Beki kinda Luke Shaw (19) ametua ManUtd kwa dau la £40m, kwa mkataba wa miaka 5 na mshahara wa £160,000 kwa wiki.
- Kocha van Gaal Louis anajipanga kumwaga kitita cha £20m kumnyakua kiungo wa Bayern, Bastian Schweinsteiger (29) baada ya kumkosa Thomas Muller (24).
- Kiungo Marouane Felaini (26) ametupwa sokoni, bei yake ni £12m. Hii ni baada ya kushindwa kung'ara tangu aliponunuliwa kwa £27.5m kutoka Everton.
- Kocha van Gaal ametua ManUtd kwa mkataba wa miaka 3, atasaidiwa na Ryan Giggs.
- Nemanja Vidic (32) atahamia InterMilan msimu ujao kwa uhamisho huru.
- Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani (27) anayechezea PSG amesema anatamani kutua Old Trafford msimu ujao. hii ni kutokana na kutoiva na kocha wake Laurent Blanc.
- Kinda Adnan Januzaj (19) anawindwa na PSG kwa ahadi ya mshahara mnono.

ARSENAL

- Mshambuliaji mtata Mario Balotelli (23) huenda akatua Arsenal kwa dau la £20m.
- Mshambuliaji Loic Remy (27) anasubiri ofa kutoka Arsenal, ingawa Tottenham wameshamwekea dau la £9m.
- Kocha Arsene Wenger (64) amesaini mkataba mpya wa kuifundisha Arsenal hadi mwaka 2017. Hii ni kufuatia mafanikio makubwa ya kuiwezesha Arsenal kucheza Champions League kwa misimu YOTE 17 aliyoifundisha Arsenal. Amepewa kitita cha £100m kwa usajili.
- Golikipa Lukasz Fabianski (29) anahamia Swansea kama mchezaji huru.
- Arsenal wanajipanga kumchukua kiungo Maraoune Fellaini (26) kutoka ManUtd kwa msimu ujao.
- Karim Benzema (26) anawindwa kwa dau la £40m.
- Beki Micah Richards (25) wa ManCity na mshambuliaji Wilfried Bony (25) wa Swansea wanawindwa kwa jumla ya £40m.

CHELSEA
- Beki anayepanda David Luiz (27) ametua PSG kwa kitita cha £40m, kwa mkataba wa miaka 5.
- Kiungo mshambuliaji Cesc Fabregas (27) ametua Chelsea kwa dau la £30m, kwa mkataba wa miaka 5! Atavaa jezi namba 4.
- Mshambuliaji anayetisha duniani kwa sasa Diego Costa (25) ametua Chelsea kwa dau la £32m.
- Frank Lampard (35) anaondoka Chelsea baada ya kunyimwa mkataba mpya.
- John Obi Mikel huenda akatua InterMilan msimu ujao.

LIVERPOOL
- Mshambuliaji wa England Rickie Lambert (32) ametua Liverpool kwa mkataba wa miaka 2 kwa dau la £4m.
- Kiungo anayetisha Adam Lallana (25) wa Southampton amepandishiwa dau hadi £25m.
- Real Madrid wametenga kitita cha £60m ili kumng'oa Luis Suarez (27).

MANCITY
- Full Beki JEMBE Bacary Sagna (31) amesaini mkataba wa miaka 3. Atalipwa £140,000 kwa wiki.
- Bei ya MKALI Lionel Messi (26) sasa ni £164m kwa mujibu wa dau lililotengwa na Mancity ili kumng'oa Barcelona.
- ManCity wametega dau la £53m kumng'oa kiungo kinda anayetisha duniani Paul Pogba (21) kutoka Juventus.

Na katika pita pita yangu nimekutana na hili
Messi is so valuable to Barcelona that if he ever leaves, the club that buys him will have to pay a $340 million buy out
that means kidogo PSG wanaelekea kumuwin kuliko man city
 
Huyo Messi ataozea hapo barca hakuna club inayoweza kutoa £340m labda kama angekuwa ana uwezo wa kucheza peke yake uwanjani dhidi ya wapinzani 11 na kushinda gemu!!
 
Rasmi: Arsenal imemwaga £25m mezani kumchukua Mario Balotelli (23)!
 
Tottenham inataka kumwaga mshambuliaji Emmanuel Adebayor (30) ili kupata fedha za kumnyakua Romelu Lukaku kutoka Chelsea, ambaye bei yake ni £32m.
 
Golikipa wa Mexico Guillermo Ochoa (28), ambaye aliizibia Brazil kwenye mechi ya kombe la dunia, ameingia kwenye rada za Arsenal na Liverpool. Ochoa hana mkataba kwa sasa baada ya kuichezea Ajaccio ya Ufaransa.
... Ajenti wa Ochoa amesema timu za EPL zilie tu, Ochoa yuko kwenye mazungumzo na Barcelona
Ochoa.PNG
 
Mshambuliaji wa PSG na Argentina Ezequiel Lavezzi (29) anawaniwa na Arsenal kwa dau la £12m. PSG imesema bei yake ni kuanzia £15m.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom