Train badala ya kujenga kanisa

Nilufer

JF-Expert Member
May 10, 2012
9,565
13,540
Jamani hizi dini zinaconfirm kabisa kuwa ziko kibiashara na hao wachungaji wako kibiashara zaidi. Mi nilidhani kipaumbele kwa mchungaji kama mtumishi wa mungu ni kanisa.

Pale kwa Gwajima hamna kanisa yaani ni kama hana mpango kabisa maana anajua kikisanuka atabaki na asset zake kama train na helicopter.

Angalieni makanisa yanayohubiri katika roho au yaabuduyo Mungu kama Catholic na KKKT vipaumbele ni kuinua makanisa waumini wasali pazuri siyo unasali kwa wasiwasi jengo linaweza kukubomokea.

Pale kwa Gwajima unasali ukiwa unachungulia pakutokea maana linaweza dodoka muda wowote.

Jamani angalieni dini za kweli achaneni na dini za biashara.
Ni hayo tu
 
RC na KKKT yana bodi siyo mtu mmoja anamua anavyopenda, kanisa la Gwajima ni la mtu mmoja.
Kama hujui kitu nyamaza kimya [HASHTAG]#Babati[/HASHTAG] siyo kuonyesha ujinga mitandaoni.

Kwa taarifu yenu hakuna kanisa lisilo na bodi inayojulikana serikali kwa mujibu wa katiba iliyokubaliwa kabla kusajili kanisa pale kwa msajili wa serikali.

Kwa kanisa linaloongozwa na Askofu Gwajima lina bodi yake inachapakazi
 
Usilete hasira eti sababu tu Naibu Waziri wa Afya amesema mtafutwe mshitakiwe, wewe umeona uje kujificha humu ndani.
 
Nasikitika unaleta biashara yako ya ushoga kiaina kwenye bandiko hili.

Nimekuambia wazi kwamba acha kuropoka mambo usiyajua. Uliza kwanza kabla kuandika upumbavu mitandaoni.
 
Hiyo biashara yenu na baba yako ndiyo maana unamtetea mteja wenu.
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Lile eneo ambalo kuna kanisa la Gwajima i.e Ubungo Tanesco huwezi kujenga jengo la kudumu pale kutokana na eneo lile kuwa ni eneo linalopitiwa na nyanya za umeme wa gridi ya taifa.

Gwajima anajenga kanisa kubwa kabisa na lina eneo linalokaribia heka 200 huko Kiluvya Makurunge au Kwa Sumaye. Mwezi uliopita Gwajima alikuwa anakata viwanja huko kwa ajiri ya waumini wake, nikiwa kule niliona viwanja 1,000 vikigawiwa kwa waumini wake na kila kiwanja walikuwa wanalipia 550,000 (Hivyo ni vile nilivyohakikisha kwa macho yangu huenda alikata vingine Zaidi). Katika ilo kanisa kuna uwanja wa kutua chopa pia anataraji kujenga reli ambayo kutakuwa kuna treni ya kupeleka waumini wake (Ikumbukwe kule kuna reli ya kati imepita).

Gwajima amechonga barabara toka Kiluvya madukani unapoingilia kwenda Makurunge mpaka huko kwenye eneo lake ambapo panaitwa Mwanakondoo. Hata sisi wenye site maeneo karibu na huko tumenufaika sana kwa uwekezaji wa bwana Gwajima. Kwani tumepata barabara nzuri lakini pia amechimba visima virefu vya maji.

Sina uhakika wa ukweli/Uongo wa huduma yake ya kiroho ilo siliongelei sababu ni Mungu pekee ndiye ajuae, lakini upande wa kanisa tusimbeze huyu jamaa. Kama ni ujasiliamali wa dini huyu jamaa kajiimalisha tofauti na tunavyofikilia. Hii project anaifanya kimya kimya sana nafikiri anataka siku akiitangaza awe anahamia huko Makurunge iwe kama Surprise.
 
Jamani hizi dini zinaconfirm kabisa kuwa ziko kibiashara na hao wachungaji wako kibiashara zaidi. Mi nilidhani kipaumbele kwa mchungaji kama mtumishi wa mungu ni kanisa.

Pale kwa Gwajima hamna kanisa yaani ni kama hana mpango kabisa maana anajua kikisanuka atabaki na asset zake kama train na helicopter.

Angalieni makanisa yanayohubiri katika roho au yaabuduyo Mungu kama Catholic na KKKT vipaumbele ni kuinua makanisa waumini wasali pazuri siyo unasali kwa wasiwasi jengo linaweza kukubomokea.

Pale kwa Gwajima unasali ukiwa unachungulia pakutokea maana linaweza dodoka muda wowote.

Jamani angalieni dini za kweli achaneni na dini za biashara.
Ni hayo tu

Aliyepewa na Mungu simuonei wivu. Hiyo treni atapanda yeye au Watanzania?
Sijachangia na wala kutozwa kodi kwa ajili hiyo. Tena sijampigia kura kwa cheo au wadhifa alionao mtumishi wa Mungu.
Endeleza injili ya Bwana watu wamjue Mungu wa kweli wakaache dhambi, wivu na chuki. Aliyepewa kapewa hata mifereji na mito ikasirke itapeleka maji baharini maana mpango wa Mungu hauhojiwi.
 
Jamani hizi dini zinaconfirm kabisa kuwa ziko kibiashara na hao wachungaji wako kibiashara zaidi. Mi nilidhani kipaumbele kwa mchungaji kama mtumishi wa mungu ni kanisa.

Pale kwa Gwajima hamna kanisa yaani ni kama hana mpango kabisa maana anajua kikisanuka atabaki na asset zake kama train na helicopter.

Angalieni makanisa yanayohubiri katika roho au yaabuduyo Mungu kama Catholic na KKKT vipaumbele ni kuinua makanisa waumini wasali pazuri siyo unasali kwa wasiwasi jengo linaweza kukubomokea.

Pale kwa Gwajima unasali ukiwa unachungulia pakutokea maana linaweza dodoka muda wowote.

Jamani angalieni dini za kweli achaneni na dini za biashara.
Ni hayo tu
Umetumia kiasi tu cha akili yako kufikiri, lakini hukujiuliza maswali ya kutosha ilikujua kwanini hiyo reli na treni?, Maisha ni kupanga na kupanga ni vipao mbele, kama treni itaboresha zaidi maisha ya kanisa kuliko jengo basi hicho ndicho cha kuanza nacho.

lakini pia kumbuka kumwabudu Mungu sio kwenye jengo zuri, lakini nikatika uwepo wake. Jengo zuri halikuhikishii uwepo wa Mungu japo ni jambo zuri kuwa na jengo zuri lenye uwepo wa MUNGU, na watu wengi wameenda kwenye majengo mazuri lakini hawakuenda kwenye madhabahu zenye moto wa MUNGU. Vitabu vitakatifu vinatuonyesha MUNGU aliwatokea watu katika sehemu hata siziso pendeza, lakini ndivyo alivyochagua yeye, na cha ajabu watumishi waliofanya sana kazi ya MUNGU kwenye vitabu ni wale ambao maisha yao yalikuwa ya mapangoni, nyikani na sehemu sizizopendeza kama akina Yohana, Samsoni, Paulo nk.

Tunacho cha kijifunza hapo, kila ulipo hakikisha roho yako inakushuhudiwa kuwa hapo ulipo pana nguvu ya Mungu na sio mashairi ya waandishi na ujuzi wa Mwanadamu katika kusema maneno ya MUNGU.

Ili kukidhi idadi ya waaumini wanaokuja ufufuo na uzima upo mpango wa kujenga kanisa nje ya mji, ambako huko eneo lakutosha kanisa la mita 300 kwa 100 na huduma nyingine limepatikana, hivyo kurahisisha usafiri wa waamini, ndipo wazo la kuwa nausafiri wa treni linakuja. Hata kama litatoa huduma kwa jamii lakini pia lengo kuu ni hilo.

Na katika swala la maendeleo, wazo huja kwanza, ndipo resources zinaanza kutafutwa, hivyo wakati mwingine mawazo yasizue watu kufikiri na kujaribu kusonga mbele, wengi tunataka tupate hela kwaanza ndo tuwaze cha kufanya, nadhani ndiyo maana tunakuwa masikini sana, kwa sababu muda ukiwa na hela bila wazo ni rahisi kuharibu hiyo pesa au kuipeleka kusiko. Hata kama hunapesa usiache kuwaza mbali na kuja na fikra zitazokusukuma kupata pesa na mambo kutokea. nadhani ndiyo falsafa ufufuo na uzima wnaijenga na ndivyo pia MUNGu anatamani tufanye na ndiyo haswaa maana ya imani katika kristo.
 
Jamani hizi dini zinaconfirm kabisa kuwa ziko kibiashara na hao wachungaji wako kibiashara zaidi. Mi nilidhani kipaumbele kwa mchungaji kama mtumishi wa mungu ni kanisa.

Pale kwa Gwajima hamna kanisa yaani ni kama hana mpango kabisa maana anajua kikisanuka atabaki na asset zake kama train na helicopter.

Angalieni makanisa yanayohubiri katika roho au yaabuduyo Mungu kama Catholic na KKKT vipaumbele ni kuinua makanisa waumini wasali pazuri siyo unasali kwa wasiwasi jengo linaweza kukubomokea.

Pale kwa Gwajima unasali ukiwa unachungulia pakutokea maana linaweza dodoka muda wowote.

Jamani angalieni dini za kweli achaneni na dini za biashara.
Ni hayo tu
Siku utakaposoma na kuelewa vizuri vitabu vya Danieli na Ufunuo wa Yohana ndipo utakapoelewa malengo ya dini kongwe unayosifu!
 
Back
Top Bottom