Trafiki ni mradi wa mapato Serikalini na wakubwa fulani

Jana nimesafiri safari ya zaidi ya km 300 lakini sijaulizwa chochote na traffic, kuna mmoja nilimpita kasimama karibu na centreline nilivyokaribia akawahi kunipisha nikabaki na shangaa leo na kismati gani

Kuna haja ya kufanya survey na kuleta mrejesho. Jamaa hawa walitesa sana watu. Kuwa na gari ikawa kero!

Sasa hivi Kitimoto na wenzako mwagilieni mioyo bwawa limeingiwa luba!
 
Polisi akikagua vyote hivyo huchomoki usipokamatwa hapo atacheki taa akikukosa atacheki condition ya gari kama kuna mikwaruzo au michubuko hakuachi, katika watu100 wanaoweza kupona ni wawili au watatu. Polisi wa bongo ni wa hovyo sana.
Kuna ndugu yangu aliambiwa gari lina mikwaruzo, mwingine akaambiwa gari ni chafu, dakika kidogo ukapita msafara wa RC wa Njombe umetoka vijijini magari hayajulikani yana rangi gani, akawauliza hayo magari yamechafuliwa na nani? Akaona ujinga akaunga kwenye msafara wa RC.
 
Askari akitaka kukugea kosa hashindwi. Hata gari utoke nayo show room sahizi akikudaka labda awr hana nia ya hongo ila hela utatoa tu huwezi kuwa salama nyakati zote
 
Askari akitaka kukugea kosa hashindwi. Hata gari utoke nayo show room sahizi akikudaka labda awr hana nia ya hongo ila hela utatoa tu huwezi kuwa salama nyakati zote
Ukiwa umekamolika kila kitu na unafuata sheria za barabarani ni ngumi kukuta na kosa
 
Kuna haja ya kufanya survey na kuleta mrejesho. Jamaa hawa walitesa sana watu. Kuwa na gari ikawa kero!

Sasa hivi Kitimoto na wenzako mwagilieni mioyo bwawa limeingiwa luba!
Mimi siendeshi gari ni mwezi wa 3 sasa nakwea daladala tu. Siwezi ku deal na gharama za mafuta na gharama za trafiki tena. Ni ngumu
 
Polisi akikagua vyote hivyo huchomoki usipokamatwa hapo atacheki taa akikukosa atacheki condition ya gari kama kuna mikwaruzo au michubuko hakuachi, katika watu100 wanaoweza kupona ni wawili au watatu. Polisi wa bongo ni wa hovyo sana.
Unaweza ukajizatiti kweli kumbe tairi ime expire mds wake na gari imetoka show room lazma akulime 3OK
 
Na huwezi kuwa umekamilika siku zote 3O za mwezi wewe kama mmiliki wa gari. Utaotewa
tu aidha hujafunga mkanda. Umeruka zebra ama umeruka taa. Hayo maeneo lazma utadakwa tu.
Utakuwa siyo dereva makini.

Mimi nikiingia kwenye gari kabla sijawasha gari nafunga kwanza mkanda, kwa kifupi siwezi kuendesha gari bila kufunga mkanda. Hata abiria atakayekaa mbele namwambia funga mkanda ndio naondoa gari. Hata nikipewa lifti nikikaa mbele lazima nifunge mkanda.

Uzuri gari lenyewe kama sijafunga mkanda inapiga alarm na pia abiria kama hajafunga mkanda alarm inapiga
 
Mkuu unaishi nchi gani?
 
Mbona una hasira kama mwendakuzimu?
 
Nilitegemea nione wananchi wenye magari wakiandamana kuunga mkono kauli ya Kinana!
Ni ukweli kuwa nchi yetu imefikia hatua mbaya ya kuwa na wezi ndani ya sare maarufu kama polisi. Na hasa traffic... ni wanyanganyi wakubwa sana!
Serikali inapaswa kuwapunguza hawa wezi barabarani... Yaani ni too much... Askari anaomba omba hela utafikiri wewe ndo ulimpangia kazi barabarani!
Enyi wenye magari amkeni amkeni... msiendekeze kulalamimia pembeni! Muda ndo huu!
 
Hawa jamaa ni kama vile wamepewa target ya kukusanya ela.
Hamna siku nimekereka kama kupigwa Tochi saa moja na dakika hamsini asubuhi maeneo ya Tegeta Scansa nikiwa na speed ya 65 km/hr.
Yaani asubuhi asubuhi watu tunapigana Tochi mjini kweli.!!?
Ifike mahali hizi Sheria za makazi na speed tuziangalie. Maana jinsi raia wanavyozidi kujenga karibu na barabara kuna uwezekano huko mbeleni ikawa Dar Moro inabidi mtu utembee na speed ya 50km/Hr.
 
PCCB wanashughulikia minor issues ambazo pengine impacts zake ni kiduchu sana, mfano ile ya mwenyeki wa kitongoji X kapokea rushwa ya elfu ishirini ili kumruhusu mfugaji kunyweshea ng'ombe kwenye kisima cha kitongoji.......hapo watatafuta hadi vyombo vya habari ili kumbana mwenyekiti.....lakini Rushwa ya Trafiki barabara wala aihitaji uchunguzi wala maswali mengi maana rushwa wamegeuza ni seheme ya kazi na haki yao kufanya hivyo lakini PCCB huwezi waona
 
Ila mkiendelea kufa kwa maajali msije kuloloma humu.
 
Kwa taarifa yako askari akikumata hajawahi kukosa kosa la kukupa ili tu apate ela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…