TRAFIKI ashindwa kuongea kiingereza

TRAFIKI ashindwa kuongea kiingereza

Mgengeli

Senior Member
Joined
Sep 23, 2011
Posts
193
Reaction score
13
Askari wa usalama barabarani wilaya ya kakonko anayejulikana kwa jina MBAYA ameshindwa kuwasiliana na Raia wa kigeni aliyekuwa anaendesha gari T7610BVV,mpaka akamuita askari mwenzake anaitwa Rudo,
 
Mbona hiyo ni kawaida mkuu, kuna nchi hata hicho kiingereza ni tabu kwelikweli.

Askari wa usalama barabarani wilaya ya kakonko anayejulikana kwa jina MBAYA ameshindwa kuwasiliana na Raia wa kigeni aliyekuwa anaendesha gari T7610BVV,mpaka akamuita askari mwenzake anaitwa Rudo,
 
Askari wa usalama barabarani wilaya ya kakonko anayejulikana kwa jina MBAYA ameshindwa kuwasiliana na Raia wa kigeni aliyekuwa anaendesha gari T7610BVV,mpaka akamuita askari mwenzake anaitwa Rudo,

Kaka wabongo lugha yetu kiswahili,kwa polisi kuongea kiingereza sio lazima,na hii sio kwetu tu,kuna nchi nyingi duniani ukienda na kiingereza chako unaweza kuchelewa kupata huduma.
 
mkuu hiyo namba ya gari umeiandika kwa usahihi kweli maana naona kama namba zimezidi three digits
 
Hiulo sio tatizo maana lugha yetu ni kiswahili, hata kwa wenzetu huko ASIa mfano China,Thailand,Japan wanaongea lugha yao
 
Kwanza hao wageni inabidi wajue lugha yetu na sio sisi tujifunze ya kwao kwani huo ni utumwa
 
Naam. Kuna nchi ukienda kusoma lazima usome lugha zao kabla ya kusomea kilichokupeleka!!

Sent from my Nokia 8310 using Tapatalk
 
Askari wa usalama barabarani wilaya ya kakonko anayejulikana kwa jina MBAYA ameshindwa kuwasiliana na Raia wa kigeni aliyekuwa anaendesha gari T7610BVV,mpaka akamuita askari mwenzake anaitwa Rudo,

Askari anayewahudumia watanzania ambao lugha yao mawasiliano ni kiswahili akishindwa kuwasiliana na mgeni anayetokeza mara moja kwa mwaka anayezungumza kingereza nini cha ajabu ! Mimi nilidhani cha ajabu hapo ingekuwa askari anamwongelesha kingereza halafu mgeni anamjibu kiswahili.
 
tuache kasumba kiingereza sicho ndicho kinachofanya kazi?
 
Sijaona tatizo, lugha yetu ni kiswahili hiki kiingereza tunababaisha tu...bora kamuita anayejua!
Na hii mbona iko kwingi tu duniani!
 
Mimi naona wachangiaji wengi hapa JF ni vilaza. Lugha ya kiingereza ndiyo inatumika kufundishia na mitihani yote inaandikwa kiingereza huyo askari alifaulu vipi hadi kupata ajira? Vyuoni kuanzia ukuruta hadi uafisa masomo ni kimombo sasa huyo askari wa wapi asijue kiingereza? Mimi naona tatizo labda mtasha mwenyewe alikuwa anaongea kiingereza cha kuchapia ndio mana jamaa akaona anampotezea wakati.
 
lakini ukiwa kwenye public service hasa traffic lugha kama kiingereza ni muhimu maana utakutana na binadamu wengi kutoka nje ya nchi.
 
"Shukrani kwa nyerere alicheza utazadhani pele kuendeleza kiswahili mikoani na mbelembele tunamfagilia mzungu wakati tuna shida tele kingereza bila hela ni sawa na kupiga kelele"-LANGA
 
Mimi naona wachangiaji wengi hapa JF ni vilaza. Lugha ya kiingereza ndiyo inatumika kufundishia na mitihani yote inaandikwa kiingereza huyo askari alifaulu vipi hadi kupata ajira? Vyuoni kuanzia ukuruta hadi uafisa masomo ni kimombo sasa huyo askari wa wapi asijue kiingereza? Mimi naona tatizo labda mtasha mwenyewe alikuwa anaongea kiingereza cha kuchapia ndio mana jamaa akaona anampotezea wakati.
Punguza kuongea usichojua kuhusu kuruta kufundishwa kwa kiingereza sio kweli kwani zamani Polisi walikuwa wanaajiri darasa la Saba, walikuwa wanafundishwa kwa Kiswahili, na depo ya mwisho kufundishwa kwa Kiswahili ni depo ya Michezo ya mwaka 2000, ambapo kulikuwa na mchanganyiko wasomi na darasa la Saba,
 
Back
Top Bottom