TRAFIKI ashindwa kuongea kiingereza

TRAFIKI ashindwa kuongea kiingereza

Mbona umekurupuka?Sasa sema basi nimedanganya nini?Au hutaki kuwa wabongo lugha yetu ni kiswahili?
Ulaya kwenyewe wazungu hawajui kiingereza,sasa ndo iwe aibu kwa polisi wa wilaya sijui ya Kankonko

Mkuu ni kweli kuwa Kiswahili ndio Lugha yetu ya Taifa, ila hilo halim-halalishii huyo Trafiki kutofahamu Kiingereza kwani amepata hiyo "ajira" kuwa kudhaniwa kuwa ana elimu stahiki itakayomwezesha kumudu majukumu yake! Na kwa hapa Tz kama nilivyodokeza mwanzo, ni kwamba Elimu bado inatolewa kwa Kiingereza! Kama ni kweli hajui hiyo lugha ina maana kwamba kachakachua vyeti ili apate ajira! Vinginevyo useme kapatia Elimu yake wasikotumia Kiingereza kufundishia!
 
wachangiaji wote mmeongea point, tusiwe watumwa kwa lugha za wenzetu, na ww mleta mada ................pia ......

Mkuu bado "utumwa wa lugha za watu" hatuwezi kuukwepa kwa maana bado Elimu yetu inatolewa kwa lugha za hao wenzetu! Tutakapoweza kutengeneza Mitaala kwa lugha yetu na kuwafundisha watoto wetu shuleni kwa lugha yetu,hapo ndio tutaweza kuwa na kiburi cha kutokupaswa kujua lugha za wenzetu! Lakini kama tunaendelea "kumbeba mtoto(Elimu) kwa mbeleko ya kuazima(Kiingereza)" tutaendelea bado kuwa watumwa wa mwenye mbeleko!
 
Askari wa usalama barabarani wilaya ya kakonko anayejulikana kwa jina MBAYA ameshindwa kuwasiliana na Raia wa kigeni aliyekuwa anaendesha gari T7610BVV,mpaka akamuita askari mwenzake anaitwa Rudo,

Mkuu, hebu naomba jambo la kwanza uweke huu uzi kiingereza..

Pili, elewa kwamba kiingereza sio lugha yetu, watu wengi tunaielewa kuandika na kusoma, lakini suala la kuongea ni tatizo kwa sababu hatufanyii mazoezi, nenda kenya au zimbabwe, hata kama mtu hajaenda shule yai anavunja kwa sababu wana nafasi ya kutumia kiingereza maeneo mbali mbali tofauti na sisi tunaotumia shuleni tu, Tanzania kujua kuongea kiingereza sio kigezo pekee cha kuonyesha uwezo wako kitaaluma japo inaumuhimu sana.

Weka kwanza huo uzi kiingereza tuone na wewe ukoje?
 
Mkuu ni kweli kuwa Kiswahili ndio Lugha yetu ya Taifa, ila hilo halim-halalishii huyo Trafiki kutofahamu Kiingereza kwani amepata hiyo "ajira" kuwa kudhaniwa kuwa ana elimu stahiki itakayomwezesha kumudu majukumu yake! Na kwa hapa Tz kama nilivyodokeza mwanzo, ni kwamba Elimu bado inatolewa kwa Kiingereza! Kama ni kweli hajui hiyo lugha ina maana kwamba kachakachua vyeti ili apate ajira! Vinginevyo useme kapatia Elimu yake wasikotumia Kiingereza kufundishia!

Eish! Panua mawanda ya mawazo mkuu, je angekuja mchina, au muitaliano au muhispaniola, nk bado ungeng'ang'aniza tu uache kushughulikia mambo kwa lugha yako ukomae kichwa kwa lugha za kigeni kwenye nchi yako yenye lugha yake?? Wewe tembelea nchi zao uone kama suala la kujua lugha yao ama kutoijua litawafanya wasikutie sheriani pale utakapoenda kinyume na utaratibu wa sheria zao!
 
sasa ndo kusema akija mfaransa nisipojua kifaransa nimechakachua vyeti,!wewe mwenyewe hujui kingereza acha hizo
 
Tatizo wabongo tunaona kiingereza kuongea eti ufahari wakati masomo yote shule ya msingi yanafundishwa kiswahili,ona fahari ya lugha yako,ndo maana hatuendelei,unanikumbusha mzee mmoja binti yake karudi toka uingereza na watoto wake mzee kuona wajukuu wanaongea kiingereza safi kaanza kumsifia binti yake "ehh mwanangu umesomesha yani vijukuu vinakata lugha kuliko hata rais"

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Mkuu kwa Tanzania ili uajiriwe na Jeshi la Polisi unadhaniwa kuwa na Elimu isiyopungua kidato cha Nne! Na Elimu hiyo inatolewa kwa Kiingereza! Tusiwe wepesi kumtetea huyo Trafiki kwani kama hilo ni kweli limetokea basi kuna walakini mahali fulani! Na kama "Forum ya Great Thinkers" tujiulize hii tabia ya "uchakachuaji" itadhibitiwa vipi! "Mwana-usalama" aliyechakachua Elimu/Vyeti ni hatari kuliko tunavyoweza kufikiri!!
 
Eish! Panua mawanda ya mawazo mkuu, je angekuja mchina, au muitaliano au muhispaniola, nk bado ungeng'ang'aniza tu uache kushughulikia mambo kwa lugha yako ukomae kichwa kwa lugha za kigeni kwenye nchi yako yenye lugha yake?? Wewe tembelea nchi zao uone kama suala la kujua lugha yao ama kutoijua litawafanya wasikutie sheriani pale utakapoenda kinyume na utaratibu wa sheria zao!

Mkuu huko kwa wenzetu wanatoa Elimu kwa lugha zao! Mtoa mada alitaja Kiingereza, na Kiingereza ndo lugha yetu ya kufundishia Sekondari na Vyuo! Na huyo Trafiki anadhaniwa awe amesoma walau Sekondari!
 
sasa ndo kusema akija mfaransa nisipojua kifaransa nimechakachua vyeti,!wewe mwenyewe hujui kingereza acha hizo

Angekuwa Mfaransa, au Mchina, au Italiano lingalikuwa swala tofauti! Mtoa mada kataja Kiingereza!!!
 
halafu watu wengi wanadhani kuwa polisi wanaelimu ya chini..wanadai kimbilio la waliofeli form four ni ualimu na upolisi sio kweli jeshini sasa kuna watu wamekwenda shule kwani jeshi la sasa ni tofauti na zamani jeshi la polisi la sasa nilaueledi.usasa.na polisi jamii.
 
Mkuu kwa Tanzania ili uajiriwe na Jeshi la Polisi unadhaniwa kuwa na Elimu isiyopungua kidato cha Nne! Na Elimu hiyo inatolewa kwa Kiingereza! Tusiwe wepesi kumtetea huyo Trafiki kwani kama hilo ni kweli limetokea basi kuna walakini mahali fulani! Na kama "Forum ya Great Thinkers" tujiulize hii tabia ya "uchakachuaji" itadhibitiwa vipi! "Mwana-usalama" aliyechakachua Elimu/Vyeti ni hatari kuliko tunavyoweza kufikiri!!

Kaka elewa kuna tofauti kubwa kati ya kufahamu lugha kwa kuiandika na kuijua lugha kwa kuongea.Pamoja na kwamba nipo upande wa traffik njoo hata huku vyuo vikuu wanazuoni kibao wenye vichwa vizuri tu katika taaluma ya lugha ya kuandika sio wazuri kabisa katika lugha ya kuongea na vyeti vyao ni genuine.
 
Nakubaliana na wewe,ila hicho bado sio kigezo cha kumtetea Trafiki! Kama GT tungalipaswa kukosoa mfumo wetu wa Elimu inayotolewa kwa Kiingereza ila bado wahitimu hawaimudu hiyo lugha!
 
Duuu mbona m cxhangai kuxkia huyo trafic kaxhndwa kuongea kiingereza coz mbona ronaldinho A.K.A mijino alikaa man u ila mpaka leo hajui ngel, xembuxe trafic wa tz bhana
 
halafu mbona waheshimiwa kule mjengonii wanashindwa kuongea kingereza kabisa kama unakumbuka kipindi wanawania wawakilishi wa bunge la east africa.walivyokuwa wanajiumauma ebu tujiulize tatizo ni nini! halafu mkumbuke kuwa kuna watu ni wazuri kwenye kingereza cha kuandika lakini kuongea tatizo.
 
Kwanini asimshangae huyo raia wa kigeni kutokujua Kiswahili??
kumbuka kuwa kuna wakati serikali ilikuwa na waajiriwa waliomaliza STD 7 hasa katika majeshi na hakuna taarifa inayoonesha kwamba walifukuzwa kazi wote kwa sababu hawajui Kiingereza!

Nyerere kumbe hakukamilisha shughuli za ukombozi...bado wengi wetu tunahitaji Ukombozi wa Kifikra, ili tuweze kuthamini vya kwetu! tusishabikie sana vya nje hata kama ni sumu!
Utumwa si kufungwa minyororo miguuni, bali hata kichwa kushindwa kutumika vizuri.

Mimi naona wachangiaji wengi hapa JF ni vilaza. Lugha ya kiingereza ndiyo inatumika kufundishia na mitihani yote inaandikwa kiingereza huyo askari alifaulu vipi hadi kupata ajira? Vyuoni kuanzia ukuruta hadi uafisa masomo ni kimombo sasa huyo askari wa wapi asijue kiingereza? Mimi naona tatizo labda mtasha mwenyewe alikuwa anaongea kiingereza cha kuchapia ndio mana jamaa akaona anampotezea wakati.
 
Askari wa usalama barabarani wilaya ya kakonko anayejulikana kwa jina MBAYA ameshindwa kuwasiliana na Raia wa kigeni aliyekuwa anaendesha gari T7610BVV,mpaka akamuita askari mwenzake anaitwa Rudo,

hivi huyu mtu anaitwa traffic polisi anatakiwa kuja lugha ngapi?
barabarani kuna wakongo, wazambia, wayunani, wachina tena ndo wengi sana.
nafikiri suala la kutojua king'eng'e sio issue. inawezekana akawa fit kwenye lugha zingine kama kisukuma, kihaya, kigiriki etc
 
Askari wa usalama barabarani wilaya ya kakonko anayejulikana kwa jina MBAYA ameshindwa kuwasiliana na Raia wa kigeni aliyekuwa anaendesha gari T7610BVV,mpaka akamuita askari mwenzake anaitwa Rudo,

Mkuu hebu vunja ung'eng'e wako hapa i.e. hii thread yako kwa kidhungu na chichi tujue kwamba wewe unakimanya haswa. Kama jamaa hapo juu alivyodai.

Ooops hata mimi chijui ati i.e. kwa kiswahili ni nini? Thread kwa Kiswahili ni nini? ooops i.e. mfano .... ..... .... Thread oh oh lala chijui kwa kweli ... ... khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Siwezi kupuuza umuhimu wa lugha ya Kiingereza lakini sioni ajabu kama huyo Polisi wa Kakonko ameshindwa kuwasiliana na huyo mzungu.
 
Duuu mbona m cxhangai kuxkia huyo trafic kaxhndwa kuongea kiingereza coz mbona ronaldinho A.K.A mijino alikaa man u ila mpaka leo hajui ngel, xembuxe trafic wa tz bhana

Mkuu hii ni lugha gani umeandika hapa?
 
Back
Top Bottom