DOKEZO Baadhi ya Trafiki wanaosimamisha Magari na kutaka wafuatwe pembeni ndio chanzo cha Rushwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kuna utaratibu umezoeleka kwa Askari wa Usalama Barabarani (Trafiki) kusimamisha Magari na kutaka Madereva au kama ni Daladala basi Kondakta amfuate alipo bila hata kukagua Gari.

Huu utaratibu unakera sana na ndio sababu kuu ya Rushwa kwa Askari. Hawa jamaa wamekuwa wakisimamisha Magari na kukaa mbali ilimradi tu Dereva ashuke akatoe chochote wakati hakuna hata sababu ya msingi ya kusimamisha Gari.

Kiutaratibu Dereva hapaswi kutoka nje ta Gari kama haijakaguliwa na kubainika na kosa na hata ikibainika kosa Trafiki anatakiwa kuongea na Dereva akiwa ndani ya Gari. Kama kosa litahusisha kuchukuliwa hatua kwa Dereva ndipo anatakiwa kushuka.

Lakini cha ajabu Trafiki wa Tanzania wao kazi yao kusimamisha Magari na kusubiri wapelekewa chochote.

Ifike wakati Jeshi la Polisi lifanye kazi kwa weledi.
 
Back
Top Bottom