TRAFIKI ashindwa kuongea kiingereza

TRAFIKI ashindwa kuongea kiingereza

kaka mleta uzi jaribu kufanya kitu kimoja. jaribu kuongea kiswahili hata kwa mabosi wako wa kizungu ili kukipa hadhi kiswahili. na kwa taarifa yako nimezunguka nchi nyingi dunian na maofisa weng wa airpot wa nchi hasa zinazoongea kiport, kireno au france hawajui kiingereza unachoona wewe dili. sasa ijekuwa huyo askari wa mwanamtoti!?
 
Hebu tembeleeni Home mjiridhishe kama kweli naongea nisichokijua wakati ni zaidi ya mkuu wa chuo cha mafunzo
 
Askari wa usalama
barabarani wilaya ya kakonko anayejulikana kwa jina MBAYA ameshindwa
kuwasiliana na Raia wa kigeni aliyekuwa anaendesha gari T7610BVV,mpaka
akamuita askari mwenzake anaitwa Rudo,

kawaida sana ungemshangaa mtasha kushindwa kuongea kiswahili, mbona tunao wasomi wa vyuo vikuu kingereza kinawapa tabu mpaka mawaziri, acha hizo wewe lugha yetu kiswahili acha mawazo mgando
 
Kaka wabongo lugha yetu kiswahili,kwa polisi kuongea kiingereza sio lazima,na hii sio kwetu tu,kuna nchi nyingi duniani ukienda na kiingereza chako unaweza kuchelewa kupata huduma.

Mkuu acha kutudanganya bana! Tanzania bado hatujavua "mbeleko ya mkoloni katika Elimu"!!! Huyo Polisi anadhaniwa kuwa na kiwango cha Elimu ya chini kabisa-Kidato cha 4, na masomo yote ya "Vidato" yanatolewa kwa "Lugha ya Malkia"!!! Kwamba kashindwa sio swala la kutetea kirahisi rahisi hivyo!!!
 
Hao binadamu wengi kutoka nje ya nchi unaongelea nchi gani mkuu??..kama wapo, wao ndo wajifunze kiswahili!
Hebu kuwa serious hivi nani anaongea kiingereza hapa bongo bwana?..hata huko vyuoni ubabaishaji tu!

lakini ukiwa kwenye public service hasa traffic lugha kama kiingereza ni muhimu maana utakutana na binadamu wengi kutoka nje ya nchi.
 
Inaonekana watanzania tunasoma kwa ajili ya kuhudumia wageni na si watanzania wenzetu...."Mtanzania ukimwambia jambo la kipumbavu kwa kiingereza anaona la maana"JK Nyerere.!
 
Tatizo wabongo tunaona kiingereza kuongea eti ufahari wakati masomo yote shule ya msingi yanafundishwa kiswahili,ona fahari ya lugha yako,ndo maana hatuendelei,unanikumbusha mzee mmoja binti yake karudi toka uingereza na watoto wake mzee kuona wajukuu wanaongea kiingereza safi kaanza kumsifia binti yake "ehh mwanangu umesomesha yani vijukuu vinakata lugha kuliko hata rais"

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
soldier yuko sawa,ila wachangiaji kama salimkabor ndio hawatakiwi kwani wao hawayajui maisha ya watanzania maana kama angekuwa anayajua angejua kuwa wala si askari huyo tu ndiye mwenye tatizo la hiyo english,kwani hata maprof. wanachemka na ikiwezekana hata yeye mwenyewe inazwezekana ni wale wale waliokula uji wa mgon......
 
Askari wa usalama barabarani wilaya ya kakonko anayejulikana kwa jina MBAYA ameshindwa kuwasiliana na Raia wa kigeni aliyekuwa anaendesha gari T7610BVV,mpaka akamuita askari mwenzake anaitwa Rudo,

Huyo mzungu akikutana na ma traffic wa aina hiyo watatu lazima ajifunze kiswahili.
 
Askari wa usalama
barabarani wilaya ya kakonko anayejulikana kwa jina MBAYA ameshindwa
kuwasiliana na Raia wa kigeni aliyekuwa anaendesha gari T7610BVV,mpaka
akamuita askari mwenzake anaitwa Rudo,

ulitakaje ndg yangu mbona mambo za kawaida huenda ata wewe kwenu anaefahamu kingereza ni wewe 2, ongeza ubunifu acha kuwa mtumwa nchini mwako.
 
huyo askari alikuwa sahihi9,sio lugha yake.sema alitakiwa kujiongeza mwenyewe juu ya kumuongoza.
 
Mkuu acha kutudanganya bana! Tanzania bado hatujavua "mbeleko ya mkoloni katika Elimu"!!! Huyo Polisi anadhaniwa kuwa na kiwango cha Elimu ya chini kabisa-Kidato cha 4, na masomo yote ya "Vidato" yanatolewa kwa "Lugha ya Malkia"!!! Kwamba kashindwa sio swala la kutetea kirahisi rahisi hivyo!!!

Mbona umekurupuka?Sasa sema basi nimedanganya nini?Au hutaki kuwa wabongo lugha yetu ni kiswahili?
Ulaya kwenyewe wazungu hawajui kiingereza,sasa ndo iwe aibu kwa polisi wa wilaya sijui ya Kankonko
 
wachangiaji wote mmeongea point, tusiwe watumwa kwa lugha za wenzetu, na ww mleta mada ................pia ......
 
nimewapenda saana wachangiaji wa uzi huu, mmeandika ukweli, ukimfuatilia kwa undani mleta uzi alitaka kebehi zimwagwe kwa traffic huyu. zingatia hata yy kwa kutumia uzalendo wake ,angeweza kuingilia kati na kuwa mfasiri.ili sheria ichukue mkondo wake ipasavyo.
 
kwanza hao wageni inabidi wajue lugha yetu na sio sisi tujifunze ya kwao kwani huo ni utumwa
ukienda kusoma nje unapigwa miaka 2 dry kwanza ya kujifunza lugha yao ndio uanze masomo
 
Askari wa usalama barabarani wilaya ya kakonko anayejulikana kwa jina MBAYA ameshindwa kuwasiliana na Raia wa kigeni aliyekuwa anaendesha gari T7610BVV,mpaka akamuita askari mwenzake anaitwa Rudo,

Ulithibitisha kuwa huyo raia wa kigeni alikuwa anaongea kiingilishi!!! unadhani raia wa kigeni wote wanaongea hiyo lugha ya BBC?!!!
:majani7:
Yote kwa yote, kiingilishi ni vizuri kukifahamu kamailivyo kwa lugha nyingine mathalani kichina na kijeremani. na ni wakati sasa wa kuimarisha mitalaa yetu ili lugha ya kiingilishi itiliwe mkazo kama ilivyo kwa kiswahili
 
Back
Top Bottom