TRA yaichunguza CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA yaichunguza CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 18, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wednesday, 18 May 2011 11:55 newsroom


  Na Mwandishi Wetu Gazeti la Uhuru

  MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza uchunguzi wa ukwepaji kodi unaodaiwa kufanywa na CHADEMA, imebainika. TRA imeanza uchunguzi baada ya kuwepo madai kuwa chama hicho kimekwepa kodi katika ununuzi na uingizaji vifaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana na mishahara ya wafanyakazi wake. Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Placidus Luoga, juzi alikiri kuwepo ufuatiliaji huo na kuwa tayari uchunguzi wa suala hilo umeanza.

  "TRA inafuatilia suala hili kwa umakini na endapo itathibitika kodi haikulipwa, lazima sheria itafuata mkondo wake. "Uchunguzi wetu hautakuwa wa kumuonea mtu au chama, bali utasimamia maadili na sheria zinazotuongoza ili kuhakikisha haki inapatikana,'' alisema. Luoga alisema lengo la kufanya uchunguzi ni kuhakikisha kila mtu, chama au taasisi inayopaswa kulipa kodi inafanya hivyo kwa mujibu wa sheria. Alisema baada ya ufuatiliaji itajulikana endapo CHADEMA ilikwepa kulipa kodi ilipoingiza nchini vifaa vya uenezi kutoka China. Vifaa hivyo ni kofia, fulana na bendera. Vifaa hivyo vilinunuliwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana na ilidaiwa vilipitishwa njia za panya katika eneo la Holili mkoani Kilimanjaro, baada ya kupata sh. milioni 100 kutoka kwa mfanyabiashara Mustapha Sabodo.


  [​IMG]


  Ununuzi wa vifaa hivyo unadaiwa kugubikwa na ufisadi kutokana na uamuzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, kudai aliongeza sh. milioni 188 katika ununuzi, hivyo kufanya kiasi cha fedha kilichotumika kuwa sh. milioni 288. Utata kuhusu ununuzi huo unathibitishwa na habari za kuaminika kutoka ndani ya CHADEMA, pale Mbowe aliposema anakidai chama hicho sh. milioni 188 ambazo aliongeza ili kununua vifaa, lakini ameshindwa kuonyesha risiti aliyotumia kulipa wakati wa kuviingiza nchini ili kuthibitisha madai yake. Akizungumzia mishahara ya wafanyakazi wa chama hicho kutokatwa kodi, Luoga alisema sheria ipo wazi kuwa mishahara yote ya wafanyakazi lazima ikatwe kodi. "Mwajiri atawajibika kumlipia kodi mtumishi wake ikiwa TRA itaona mfanyakazi anastahili kulipa kodi, hivyo CHADEMA wakibainika kwenye hilo basi itabidi walipe kodi,'' alisema.

  Gazeti hili lilifichua kuwa mshahara wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa ni zaidi ya sh. milioni saba ambazo ni nyingi kuliko za wabunge alizowahi kuzipigia kelele. Pia mshahara huo haukatwi kodi na TRA. Siku moja baada ya taarifa hizo kuvuja, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa CHADEMA, Anthony Komu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mabere Marando, waliitisha mkutano na waandishi wa habari kukanusha taarifa hizo, jambo ambalo baadhi ya viongozi wa CHADEMA wamefichua kwamba ufafanuzi uliotolewa na viongozi hao ni wa uongo. "Komu kudai Dk. Slaa analipwa mshahara wa sh. 1,725,000 na lita 1,000 za mafuta kila mwezi ni uongo wenye lengo la kutaka kuficha jinsi baadhi ya viongozi waandamizi walivyounda mtandao wa kutumbua fedha za CHADEMA," chanzo cha habari kilisema.

  UHURU ilipata waraka unaoonyesha mapendekezo ya posho ya Dk. Slaa kama Azimio la Kamati Kuu iliyokaa Januari 29 hadi 30 mwaka huu, Dar es Salaam ni tofauti na maelezo waliyotoa Komu na Marando.

  Kwa mujibu wa waraka huo, ambao hauonyeshi kiwango kinachokatwa kodi, posho ya Dk. Slaa imegawanywa katika sehemu sita za posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi.

  Wakati Komu katika ufafanuzi wake alisema Dk. Slaa analipwa mshahara (basic) wa sh. 1,725,000 waraka unaonyesha analipwa sh. 2,300,000. Mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi.

  Kwa upande wa posho, Dk. Slaa analipwa fedha za mafuta sh. 1,387,500 kwa lita 750 kwa mwezi, huku fedha za majukumu zikiwa sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. 1,000,000.

  Posho nyingine ni kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa hivyo.

  Dk. Slaa akiungwa mkono na Mbowe anadaiwa kujipatia posho ya nyumba mara mbili, kwani ilishapendekezwa alipwe sh. milioni 40 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba yake eneo la Mbweni, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam anakoishi.

  Licha ya kupewa fedha hizo, Dk. Slaa ameendelea kupewa posho ya nyumba ya sh. 1,000,000 kila mwezi.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,474
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Naona wako kazini.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,837
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hapa TRA ndipo watakapo sema wanafanya kazi . Mara nyingi wametumika sana kuwaumiza wapinzani waa CCM naona sasa wameanza . Hope Chadema watakua wako sahihi na kulipa kodi zote then wakose la kusema .HIvi kule Holili si kuna TRA au kupo wazi hadi kuitwe njia za panya ?
   
 4. d

  dotto JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,714
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Victimised LUOGA. Yaani CCM aliwakagua lini??? Na walitumia kiasi gani kwenye chaguzi zote?? Vijisenti vya jamaa vililipwa kodi kiasi gani!! Anataka madaraka makubwa atayapata!! Expectations huwa ni mbaya pale panapotibuka!
   
 5. p

  profkobayashi JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 224
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nadhani kuna umuhimu wa kuanzisha thread ya kuijadili hii TRA ya Kitilya
   
 6. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #6
  May 18, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 15,645
  Likes Received: 2,562
  Trophy Points: 280
  Magari ya rz1 yalilipiwa kodi?
   
 7. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,740
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  luoga anafanya kile alichofanya hosea wa PCCb, baada ya wabubge kumtaka ajiuzulu kwa kuhusika ktk kashfa ya richmond yeye aliamua kuchunguza posho za wabunge , sasa huyu luoga ametajwa na Dr slaa kuhusika katika ufisad wa 800bn, wiki haijaisha anaanza mchakacho wa kuwachunguza chadema, kuna dhamira safi hapa? je asingetajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi angewachunguza?
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,602
  Likes Received: 349
  Trophy Points: 180
  Hahahahaa!
  Uenezi na itikadi. CRAP
   
 9. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 5,919
  Likes Received: 1,700
  Trophy Points: 280
  Nahisi TRA sasa wameanza kupoteza dira, hivi kweli mamlaka ya mapato ina mda kiasai hicho kutumwa kazi na CCM? nimepita kariakoo mchana watu wanauziana bidhaa bila risiti kisa TRA wapo kuwachunguza CHADEMA,

  POLE TANZANIA
   
 10. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,404
  Likes Received: 591
  Trophy Points: 280
  Kila mwenye kipato na alipe kodi kwa maendeleo ya nchi. Wakati wa kampeni kulikuwepo malalamiko ya CCM kuingiza picha za kampeni toka CANADA bila kulipia kodi, hili nalo vipi TRA wanalifanyia kazi? Ingependeza kama ukaguzi huu ungehusu vyama vyote vya SIASA na NGOs zote kama WAMA kwa maana kuna malipo mengi yanayostahili kulipiwa kodi Mfano Utafiti uliofanywa na Mkama kuhusu CCM kuanguka uchaguzi mkuu kama alilipwa Consultancy fee, CCM walimkata Withholding tax na kuiwasilisha TRA? Kadhalika kazi aliyofanya Mkumbo ya kupendekeza namna ya kuwapata wabunge wa viti maalum nayo kama alilipwa pale kuna kodi. Tusichukulie kila kitu KISIASA maana huwezi lipwa 6 million, ukasema unalipia kodi 1.7 million tuu, hakuna sheria kama hiyo hapa Tanzania LABDA enzi zile za Serikali ya Mwinyi ambapo posho zote zilikuwa hazilipiwi kodi. TRA wanavyoibana Sekta binafsi ni wakati sasa kuhamishia majeshi huko kwenye vyama vya SIASA, Serikalini na NGOs ili wafanyakazi wote hapa nchini watendewe sawa na Sheria ya Kodi ya mwaka 2004.
   
 11. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nilipokutana na maandishi haya "Na Mwandishi Wetu Gazeti la Uhuru" nikashindwa kuendelea kusoma thread hii!
  Am sorry bandugu!
   
 12. z

  zamlock JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,850
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  waende zao uko awana maana hata kidogo
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,090
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Luoga & co kama hawakuwa makini huu uchunguzi unaweza kula kwao. Unless kama wanatishia mtu nyau lakini kama ni uchunguzi mimi naona ni vita ya mawe wakati uko ndani ya nyumba ya vioo. Ask Nape!
   
 14. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,125
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Wacha wachunguze, TRA yenyewe wana sheria ambazo wao wenyewe wanashindwa kuzifafanua.
  Nime export maua na mauzo yake nikanunlia mzigo wa pikipiki toka China.
  Kwenye returns zangu za VAT kila mwezi nahakikisha naidai TRA no matter I imported one container only.
  Sheria zetu za kodi zina mianya mingi ya kuikwepa.
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Jamani tusiwe biased, imeandikwa na Mwandishi wa habari na kuna Ukweli kwanini uogope kujadili sababu ni Gazeti la CCM - UHURU?
  Sio kila siku tutasikia Mazuri ya CHADEMA, this is a Democracy, we as viewers we should be involved in giving out our critics and not just brush it off as not a good news. LINI TUTAENDELEA???

  ~ The secret of successful journalism is to make your readers so angry they will write half your paper for you. ~

   
 16. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Bravo TRA kwa kutekeleza sheria , kwani nijuavyo kwa hili cdm hawaruki , kuna ukwepaji mkubwa sana wa kodi pale. Sasa andaeni maandamano ya kukataa kulipa kodi
   
 17. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,681
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  CCM ina kazi kwelikweli
  hizo zote ni harakati za kujivua gamba au?
   
 18. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,124
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Kodi inalipwa,hata kama cdm wamekwepa,basi watailipa hata kwa kuongeza penalty. Hamna cha ajabu hapo. Ila kama kazi inafanywa na yule Luoga,ambaye cdm inamjua kuwa ni 'jambaz' la uchumi wetu,mi sina amani tena. Hapo zamani nliposomea uhasibu nlikutana na kitu kama lack of independence, na substantial interest, Luoga hana hadhi ya kuichunguza cdm kwani cdm ilishamtuhumu,mjinga kweli hata hajui kuigiza.
   
 19. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,586
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Umenifumbua macho nilitaka kuanza kuwachana kwa kutumia vifungu vya ITA 2004 ila itakuwa ni wastage of my precious time kujadili gazeti la Uhuru, TRA wamuulize Shimbo kaishia wapi mbona hasikiki tena. Ngoma ya siasa ina wenyewe na hawana budi kuachiwa, wajue kuwa hukohuko ndani ya TRA kuna makada wa vyama vya upinzani watamwaga data zote kuhusu CCM na matumizi ya ruzuku kuanzia mwaka 1996.
   
 20. LOOOK

  LOOOK JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,385
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Wameanza kumchezea simba mkia ngoja wafike kwenye sharubu wayaone makali yake...
   
Loading...