TRA yaichunguza CHADEMA

TRA yaichunguza CHADEMA

Nilicheka kidogo niliposoma tangazo la TRA kukanusha madai ya Dr Slaa kwamba iliihujumu kampuni ya Tango transport kwa kusimamisha magari yake bila kufuata sheria,tangazo lilisema kwamba Slaa inabidi akanushe tuhuma zake hadharani vinginevyo jamii haitamwamini au atapoteza umaarufu,hawajasema watamshitaki kwa kusema uwongo

Nadhani hlili la Luoga litakuwa kujibu mapigo,kama walikuwa wanajua wamekwepa kodi kwa nini hawakuchukua hatua mapema?huo nao ni udhaifu mkubwa
Ila najua ngoma hawataiweza
 
Wednesday, 18 May 2011 11:55 newsroom


Na Mwandishi Wetu Gazeti la Uhuru

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza uchunguzi wa ukwepaji kodi unaodaiwa kufanywa na CHADEMA, imebainika. TRA imeanza uchunguzi baada ya kuwepo madai kuwa chama hicho kimekwepa kodi katika ununuzi na uingizaji vifaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana na mishahara ya wafanyakazi wake. Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Placidus Luoga, juzi alikiri kuwepo ufuatiliaji huo na kuwa tayari uchunguzi wa suala hilo umeanza.

“TRA inafuatilia suala hili kwa umakini na endapo itathibitika kodi haikulipwa, lazima sheria itafuata mkondo wake. “Uchunguzi wetu hautakuwa wa kumuonea mtu au chama, bali utasimamia maadili na sheria zinazotuongoza ili kuhakikisha haki inapatikana,’’ alisema. Luoga alisema lengo la kufanya uchunguzi ni kuhakikisha kila mtu, chama au taasisi inayopaswa kulipa kodi inafanya hivyo kwa mujibu wa sheria. Alisema baada ya ufuatiliaji itajulikana endapo CHADEMA ilikwepa kulipa kodi ilipoingiza nchini vifaa vya uenezi kutoka China. Vifaa hivyo ni kofia, fulana na bendera. Vifaa hivyo vilinunuliwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana na ilidaiwa vilipitishwa njia za panya katika eneo la Holili mkoani Kilimanjaro, baada ya kupata sh. milioni 100 kutoka kwa mfanyabiashara Mustapha Sabodo.


tra_tanzania.jpg



Ununuzi wa vifaa hivyo unadaiwa kugubikwa na ufisadi kutokana na uamuzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, kudai aliongeza sh. milioni 188 katika ununuzi, hivyo kufanya kiasi cha fedha kilichotumika kuwa sh. milioni 288. Utata kuhusu ununuzi huo unathibitishwa na habari za kuaminika kutoka ndani ya CHADEMA, pale Mbowe aliposema anakidai chama hicho sh. milioni 188 ambazo aliongeza ili kununua vifaa, lakini ameshindwa kuonyesha risiti aliyotumia kulipa wakati wa kuviingiza nchini ili kuthibitisha madai yake. Akizungumzia mishahara ya wafanyakazi wa chama hicho kutokatwa kodi, Luoga alisema sheria ipo wazi kuwa mishahara yote ya wafanyakazi lazima ikatwe kodi. “Mwajiri atawajibika kumlipia kodi mtumishi wake ikiwa TRA itaona mfanyakazi anastahili kulipa kodi, hivyo CHADEMA wakibainika kwenye hilo basi itabidi walipe kodi,’’ alisema.

Gazeti hili lilifichua kuwa mshahara wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa ni zaidi ya sh. milioni saba ambazo ni nyingi kuliko za wabunge alizowahi kuzipigia kelele. Pia mshahara huo haukatwi kodi na TRA. Siku moja baada ya taarifa hizo kuvuja, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa CHADEMA, Anthony Komu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mabere Marando, waliitisha mkutano na waandishi wa habari kukanusha taarifa hizo, jambo ambalo baadhi ya viongozi wa CHADEMA wamefichua kwamba ufafanuzi uliotolewa na viongozi hao ni wa uongo. “Komu kudai Dk. Slaa analipwa mshahara wa sh. 1,725,000 na lita 1,000 za mafuta kila mwezi ni uongo wenye lengo la kutaka kuficha jinsi baadhi ya viongozi waandamizi walivyounda mtandao wa kutumbua fedha za CHADEMA,” chanzo cha habari kilisema.

UHURU ilipata waraka unaoonyesha mapendekezo ya posho ya Dk. Slaa kama Azimio la Kamati Kuu iliyokaa Januari 29 hadi 30 mwaka huu, Dar es Salaam ni tofauti na maelezo waliyotoa Komu na Marando.

Kwa mujibu wa waraka huo, ambao hauonyeshi kiwango kinachokatwa kodi, posho ya Dk. Slaa imegawanywa katika sehemu sita za posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi.

Wakati Komu katika ufafanuzi wake alisema Dk. Slaa analipwa mshahara (basic) wa sh. 1,725,000 waraka unaonyesha analipwa sh. 2,300,000. Mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi.

Kwa upande wa posho, Dk. Slaa analipwa fedha za mafuta sh. 1,387,500 kwa lita 750 kwa mwezi, huku fedha za majukumu zikiwa sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. 1,000,000.

Posho nyingine ni kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa hivyo.

Dk. Slaa akiungwa mkono na Mbowe anadaiwa kujipatia posho ya nyumba mara mbili, kwani ilishapendekezwa alipwe sh. milioni 40 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba yake eneo la Mbweni, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam anakoishi.

Licha ya kupewa fedha hizo, Dk. Slaa ameendelea kupewa posho ya nyumba ya sh. 1,000,000 kila mwezi.

Hii imetulia nyongeza kwa TRA:-
Chunguzeni na mishahara wa yafanyakazi wa secta ya ujenzi kama inakatwa kodi! Msikimbilie CDM pekee kwa kuwa imemshikia bango mmoja wa mabosi wenu.
Pia tuambieni transaction za Voda M-Pesa zimeingiza kiasi gani?
Baadaye tuambieni Transcation za CCM kumlipa mmiliki wa mabango ya outdoors na free media ili kuweka zile posta zenye picha za JK akiwa amevaa mabangili ya dhahabu mlipata kodi kiasi gani?

MAMBO HAYA YOOOTE YAAMBATANE NA HUO UFUATILIAJI WA CDM KUKWEPA KODI!!
 
Jamani tusiwe biased, imeandikwa na Mwandishi wa habari na kuna Ukweli kwanini uogope kujadili sababu ni Gazeti la CCM - UHURU?
Sio kila siku tutasikia Mazuri ya CHADEMA, this is a Democracy, we as viewers we should be involved in giving out our critics and not just brush it off as not a good news. LINI TUTAENDELEA???

~ The secret of successful journalism is to make your readers so angry they will write half your paper for you. ~

​
Nadhani hujaelewa msingi wa hoja hii!!hapa ni siasa zimetawala!unajua mgawo wa umeme unaokuja unasababishwa na nini??japo wenyewe wanakwambia ni gas ya songosongo je umeshawahi kujiuliza kabla ya gas ya songosongo je kulikuwa na mgao wa aina hii ya masaa ha di kumi na ushee??
kama swala ni chadema kukwepa kodi je hao TRA kama kweli wako makini na kazi zao imekuwaje wakashindwa kugundua ubadhirifu uliofanywa na CCM wa kuchapisha mabango,vipeperushi na tisheti ,kanga na mengineyo mengi ambayo hadi leo yana i cost serikali??pliz zungusha kichwa chako kwa maendeleo ya taifa kama unavyosema and dont be biased!!pole yako na na familia yako
 
mh hii ni kali sasa when there done na CHADEMA They should go to RZ na EL office to collect kodi za maedeleo ya wa Tanzania......!
 
Dk. Slaa akiungwa mkono na Mbowe anadaiwa kujipatia posho ya nyumba mara mbili, kwani ilishapendekezwa alipwe sh. milioni 40 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba yake eneo la Mbweni, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam anakoishi.

Licha ya kupewa fedha hizo, Dk. Slaa ameendelea kupewa posho ya nyumba ya sh. 1,000,000 kila mwezi.
Kashfa.

Inawezekana ni mwanachama wa kutembea na kadi wa CHADEMA, na unatetea na kuunga mkono mabadiliko ya kweli nchini, lakini kama una uzalendo wa dhati kabisa, na unachukia ufisadi na ubadhilifu katika taasisi zozote za umma, ni lazima ushtuke ukisikia Dr. Slaa, Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani, amekomba milioni 40 za chama kumalizia nyumba yake binafsi, halafu anaendelea kupokea milioni kila mwezi kama posho ya nyumba.

Na ni shutuma mbaya kuliko wabadhilifu wanaoiba wazi wazi kwa sababu Rostam Aziz hajawahi kusema yeye ni mtakatifu anaepambana na ufisadi.
Andrew Chenge hajawahi kusema mshahara wa wabunge ni mkubwa sana. Edward Lowassa hajawahi kutamka kwamba Jakaya Kikwete yupo kwenye orodha ya wabadhilifu.

Mwanaharakati Malcolm X aliwahi kusema "I have more respect for a man who lets me know where he stands, even if he is wrong, than one who comes up like an angel, when he is nothing but a devil."
 
Victimised LUOGA. Yaani CCM aliwakagua lini??? Na walitumia kiasi gani kwenye chaguzi zote?? Vijisenti vya jamaa vililipwa kodi kiasi gani!! Anataka madaraka makubwa atayapata!! Expectations huwa ni mbaya pale panapotibuka!
WAANZIE HAPA
​

Nape: "Nikwambie ukweli, hali ilivyo ndani ya Chama watendaji wanafanya kazi kwa mazoea. Hali ya uchumi katika Chama ni mbaya. Huwezi kuamini kwamba kwamba katika mazingira ambayo tuna mali zenye thamani takriban Sh bilioni 50, kinachoingia kwa maana ya mapato ni takriban Sh. bilioni moja hivi. Ni lazima sasa tujiimarishe katika sehemu zote; sio tu kimaadili na kisiasa lakini pia kiuchumi."Nape Mnauye mahojiano Raiamwema Toleo la Aprili 20 - 26, 2011 NAPE: Kujivua gamba CCM kumezingatia utafiti, si vinginevyo
 
Kama Chadema wasafi wanaogopa nini si wapeleke vielelezo TRA badala ya kubwabwaja hapa JF?
 
Headless chickens on the move! hang on a minute!!! Kama TRA wanasema hii ni fair game ngoja wakimaliza kuchunguza CDM tu raise questions against CCMs dodging taxes and stuff. THEN if they have got balls and because they are playing what they call it a fair game and not intentional, they can also turn their empty heads to CCM for further investigations. Camon TRA!!!!
 
Wameanza kumchezea simba mkia ngoja wafike kwenye sharubu wayaone makali yake...

Una maana gani? Kodi ni mali ya serikali. Haiwezekani mtu, kampuni, chama n. k. yoyote yenye kipato lazima ilipe kodi! Hakuna cha mswalie mtume hapa.
 
Nilicheka kidogo niliposoma tangazo la TRA kukanusha madai ya Dr Slaa kwamba iliihujumu kampuni ya Tango transport kwa kusimamisha magari yake bila kufuata sheria,tangazo lilisema kwamba Slaa inabidi akanushe tuhuma zake hadharani vinginevyo jamii haitamwamini au atapoteza umaarufu,hawajasema watamshitaki kwa kusema uwongo

Nadhani hlili la Luoga litakuwa kujibu mapigo,kama walikuwa wanajua wamekwepa kodi kwa nini hawakuchukua hatua mapema?huo nao ni udhaifu mkubwa
Ila najua ngoma hawataiweza

MwanaHalisi la wiki iliyopita lilikuja na maelezo marefu ambayo kwa nchi yenye uwajibikaji ingebidi TRA ijichunguze na kujiwajibisha..
 
Nadhani kuna umuhimu wa kuanzisha thread ya kuijadili hii TRA ya Kitilya

ni kweli tujadili suala hili kwa ukweli maana watanzania tumefanywa mazuzu sana. Mbona kitilya na hajasema mshahara na posho za watendaji wa ccm? Unafiki, uzandiki, pumba tupu
 
Wakiichunguza ccm haitakuwa na tofauti na lile suala la risiti za kukodi ndege za serikali. Ni suala gumu kwa idara ya serikali kama TRA kuishutumu au kuichunguza CCM inayounda serikali yao
 
Wednesday, 18 May 2011 11:55 newsroom


Na Mwandishi Wetu Gazeti la Uhuru

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza uchunguzi wa ukwepaji kodi unaodaiwa kufanywa na CHADEMA, imebainika. TRA imeanza uchunguzi baada ya kuwepo madai kuwa chama hicho kimekwepa kodi katika ununuzi na uingizaji vifaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana na mishahara ya wafanyakazi wake. Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Placidus Luoga, juzi alikiri kuwepo ufuatiliaji huo na kuwa tayari uchunguzi wa suala hilo umeanza.

“TRA inafuatilia suala hili kwa umakini na endapo itathibitika kodi haikulipwa, lazima sheria itafuata mkondo wake. “Uchunguzi wetu hautakuwa wa kumuonea mtu au chama, bali utasimamia maadili na sheria zinazotuongoza ili kuhakikisha haki inapatikana,’’ alisema. Luoga alisema lengo la kufanya uchunguzi ni kuhakikisha kila mtu, chama au taasisi inayopaswa kulipa kodi inafanya hivyo kwa mujibu wa sheria. Alisema baada ya ufuatiliaji itajulikana endapo CHADEMA ilikwepa kulipa kodi ilipoingiza nchini vifaa vya uenezi kutoka China. Vifaa hivyo ni kofia, fulana na bendera. Vifaa hivyo vilinunuliwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana na ilidaiwa vilipitishwa njia za panya katika eneo la Holili mkoani Kilimanjaro, baada ya kupata sh. milioni 100 kutoka kwa mfanyabiashara Mustapha Sabodo.


tra_tanzania.jpg



Ununuzi wa vifaa hivyo unadaiwa kugubikwa na ufisadi kutokana na uamuzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, kudai aliongeza sh. milioni 188 katika ununuzi, hivyo kufanya kiasi cha fedha kilichotumika kuwa sh. milioni 288. Utata kuhusu ununuzi huo unathibitishwa na habari za kuaminika kutoka ndani ya CHADEMA, pale Mbowe aliposema anakidai chama hicho sh. milioni 188 ambazo aliongeza ili kununua vifaa, lakini ameshindwa kuonyesha risiti aliyotumia kulipa wakati wa kuviingiza nchini ili kuthibitisha madai yake. Akizungumzia mishahara ya wafanyakazi wa chama hicho kutokatwa kodi, Luoga alisema sheria ipo wazi kuwa mishahara yote ya wafanyakazi lazima ikatwe kodi. “Mwajiri atawajibika kumlipia kodi mtumishi wake ikiwa TRA itaona mfanyakazi anastahili kulipa kodi, hivyo CHADEMA wakibainika kwenye hilo basi itabidi walipe kodi,’’ alisema.

Gazeti hili lilifichua kuwa mshahara wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa ni zaidi ya sh. milioni saba ambazo ni nyingi kuliko za wabunge alizowahi kuzipigia kelele. Pia mshahara huo haukatwi kodi na TRA. Siku moja baada ya taarifa hizo kuvuja, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa CHADEMA, Anthony Komu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mabere Marando, waliitisha mkutano na waandishi wa habari kukanusha taarifa hizo, jambo ambalo baadhi ya viongozi wa CHADEMA wamefichua kwamba ufafanuzi uliotolewa na viongozi hao ni wa uongo. “Komu kudai Dk. Slaa analipwa mshahara wa sh. 1,725,000 na lita 1,000 za mafuta kila mwezi ni uongo wenye lengo la kutaka kuficha jinsi baadhi ya viongozi waandamizi walivyounda mtandao wa kutumbua fedha za CHADEMA,” chanzo cha habari kilisema.

UHURU ilipata waraka unaoonyesha mapendekezo ya posho ya Dk. Slaa kama Azimio la Kamati Kuu iliyokaa Januari 29 hadi 30 mwaka huu, Dar es Salaam ni tofauti na maelezo waliyotoa Komu na Marando.

Kwa mujibu wa waraka huo, ambao hauonyeshi kiwango kinachokatwa kodi, posho ya Dk. Slaa imegawanywa katika sehemu sita za posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi.

Wakati Komu katika ufafanuzi wake alisema Dk. Slaa analipwa mshahara (basic) wa sh. 1,725,000 waraka unaonyesha analipwa sh. 2,300,000. Mbunge analipwa sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi.

Kwa upande wa posho, Dk. Slaa analipwa fedha za mafuta sh. 1,387,500 kwa lita 750 kwa mwezi, huku fedha za majukumu zikiwa sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. 1,000,000.

Posho nyingine ni kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa hivyo.

Dk. Slaa akiungwa mkono na Mbowe anadaiwa kujipatia posho ya nyumba mara mbili, kwani ilishapendekezwa alipwe sh. milioni 40 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa nyumba yake eneo la Mbweni, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam anakoishi.

Licha ya kupewa fedha hizo, Dk. Slaa ameendelea kupewa posho ya nyumba ya sh. 1,000,000 kila mwezi.

Kwa nini ukaguzi haufanyiki continuously? Je, wamekwisha kagua Caspian?
 
Kama kweli wamekwapa kodi, ukweli utaonekana, walipe kwa kupigwa faini kwa nini wao wapinge wakwepaji wa kodi ilihali wao wanakwepa. Na kwa ikibainika hawakukwepa, itabidi waombwe radhi kwa kuchafuliwa jina.
 
TRA wangeanza na CCM ndio waende chadema, kisha kwa wafanyabiashara wanaichangia CCM, waone kama hawatavunya rekodi yao ya ukusanyanji mapato kwa mwezi!
 
Tanzania ni nchi ya ajabu sana. Yaani CDM waliokuwa wanalia na CCM kwa kukwepa ushuru leo Luoga unasema walikwepa? Hivi kweli CCM wangesubiri mpaka leo hawajasema kuhusu hilo? hivi kweli mafisadi waliojaa nchi nzima wangekaa kimya? Sasa kama zilipishwa njia za panya na tayari zimetumika Luoga utajua vipi? ulikuwapi siku zote, kwanini hazikukamatwa mpakani?

Kama najua vizuri mali zinazoingia bila kulipiwa ushuru huwa zinakamata kilomita chahce mara baada ya kutoka holili, kuna road block au kuna TRA wana-patrol kwa ajili ya kusimamisha magari wanayohisi yameingiza mali bila ushuru? Je Luoga atakuja na santuri gani? Kama wametengeneza kofia kariakoo je ?

Halafu kichefu chefu kikubwa ni pale anaposema eti Mbowe aliongezea 188m . Come on TRA.
Ila dawa ni kumpeleka yeye kisutu kwa kuisbabishia hasara serikali. Na nina amini CDM walilipa ushuru unaostahili kama kweli waliingiza mali zozote. na naamini mishahara inayohitajika kodi , nssf, nk ilikatwa na fedha kupelekwa kunkohusika.

Inatia kinyaa TRA kufanya kazi kisiasa.
 
Luoga as he was mentioned katika orodha ya ufisadi he shouldn't have been a spokesman for this issue. Now the whole issue is tainted politics.
 
Jamani tusiwe biased, imeandikwa na Mwandishi wa habari na kuna Ukweli kwanini uogope kujadili sababu ni Gazeti la CCM - UHURU?
Sio kila siku tutasikia Mazuri ya CHADEMA, this is a Democracy, we as viewers we should be involved in giving out our critics and not just brush it off as not a good news. LINI TUTAENDELEA???

~ The secret of successful journalism is to make your readers so angry they will write half your paper for you. ~

​

Ila hii habari haina uzuri wowote. Ukijaribu kuifanyia analysis hata huyo mhariri unakuwa na mashaka naye. sema kwa sababu wanataka kuonyesha Luoga sio fisadi lilosababishia hasara, sasa wanataka kupima oil nguvu ya umma.

Hivi kama mishahara ya wafanyakazi wa CDM haikatwi kodi, hilo ni swala la Luoga na uhuru au lingekuwa swala la TRA. halafu kama hawakatwi ushuru kwanini wasipelekwe mahakamani?

Swala la kofia tangia mwaka jana walikuwa wapi? Ni vyema kutumia akili badala ya tumbo kufikiri. jamaa anapagwa na sasa anadandia treni kwa mbele. Haya kanyaga twende wengi watakufa na CCM
 
Back
Top Bottom