Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,962
- 6,906
Wowwww
Kama interpretation yako ya kipengele hicho unaiweka ZNZ sawa na nchi ya kigeni huo ni uamuzi wako wewe haimaanishi TRA wanafanya hivyo na inaonyesha umepoteza wakati wako mwingi sana kuitafuta hiyo na ukaona ndiyo punching line.lakini kosa ni kutokuijua katiba yako inasemeje na ikakupelekea kusherehesha kipengele hicho kutoka na ufahamu wako mdogo au just umeeamuwa hivyo ili kufikia lengo lako ulilokusudia.Lakini nenda TRA kaulize ni ukitoa mzigo zanzibar kuuleta bongo unatozwa 18% kwani hata hao wanaolalamika bandarini wanahangaishwa na maofisa wa TRA basi hiyo pesa wanayoichukua basi ni asilimia ndogo sana na hata risiti unakuwa hupewi.sijui kama uko TZ au Nje lakini kwanza nenda bandarini jaribu kuuliza utapata ukweli halisi au nenda Ofisi za TRA kaulizie.
PS: Pengine kwenye ndoto yako tu zanzibar itakuwa mkoa lakini in real world kitu hicho hakitotokea
Kama uelewa wako ndio huu basi sina cha kukusaidia. Hapa nimekuwekea pdf kutoka kwenye website ya TRA lakini wewe unaniambia niende bandarini au ofisi za TRA nikaulizie. Hii pdf imetayarishwa na hao hao TRA kutuondelea wewe na mimi usumbufu wa kuwafuata kuwauliza kuhusu masuala kama haya. Katika kifungu cha VAT, TRA wameeleza bayana kuwa bidhaa yeyote itakayoingia kutoka nje ya Tanzania BARA itatozwa kiasi hicho cha kodi. Kama bidhaa kutoka Zanzibar zisingehusika wangesema bidhaa yeyote itakayoingia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itatozwa kiasi hicho cha VAT. Kwa kukazania kuwa mizigo kutoka Zanzibar isamehewa chini ya sheria hii ni sawa na kusema kuwa Zanzibar iko ndani ya Tanzania BARA. Kama afisa wa TRA anamhangaisha mtu na anakataa kutoa risiti kwa pesa anayopewa huyo ni wa kumpeleka kwa Pilato akashikishwe adabu. Lakini kama umemkatia kitu kidogo ili asikutoze hiyo asilimia, sidhani kama utakuwa na ubavu wa kudai risiti ya rushwa au kumpeleka kwa Pilato.
Mimi binafsi wala sina haja ya Zanzibar kugeuzwa mkoa wa Tanzania Bara. Ninachosema ni kuwa kwa vile imejitangaza nchi kamili nje ya Tanzania BARA basi haya ni baadhi ya majukumu yake. Katiba inaingiaje hapa wakati ni Zanzibar wenyewe wanaodai kuwa katiba yao inasema kuwa wao ni nchi kamili yenye mipaka yake na sehemu ya mipaka hiyo ni kati yake na Tanzania Bara. Kwa mtaji huo, basi Zanzibar ni nchi ya kigeni kama Kenya na wengine. Kama ilivyo kwenye masuala ya mafuta, ndivyo ilivyo kwenye VAT.
Amandla.......