TRA ‘watibua nyongo’ za Wanzanzibari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA ‘watibua nyongo’ za Wanzanzibari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu wa Pwani, Oct 25, 2010.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  TRA ‘watibua nyongo’ za Wanzanzibari


  Monday, 25 October 2010 07:52
  0diggs
  digg
  Ally Mkoreha, Zanzibar
  IDARA ya Ushuru wa Forodha katika Bandari ya Dar es Salaam, imetajwa kuwa mmoja ya taasisi zinazochafua sura ya Muungano wa Tanzania baada ya baadhi ya maofisa wake kudaiwa kuwanyanyasa Wazanzibari.
  Tayari maofisa wa Wizara ya Fedha na Uchumi katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wamepanga kwenda Dar es Salaam mapema wiki hii kukutana na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuzungumzia suala hilo .
  Malalamiko kuhusu watu wa Zanzibar kunyanyaswa na maofisa wa Idara ya Ushuru wa Forodha kwa kutakiwa kulipia ushuru wa vifaa ambavyo si kwa ajili ya biashara, ulitolewa jana katika Mkutano Maalumu wa Baraza la Biashara la Zanzibar.
  Hali kadhalika na uamuzi wa maofisa wa Wizara ya Fedha na Uchumi kwenda Dar es Salaam kuonana na maofisa wa TRA.
  Mkutano huo, uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Zanzibar , Rais Amani Abeid Karume ulifanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, ulioko katika eneo la Mnazi Mmoja, mjini Unguja.
  Katika mkutano huo, mmoja wa wajumbe wa sekta binafsi Salum Hassan Turky, alisema maofisa wa Idara ya Ushuru wa Forodha katika Bandari ya Dar es Salaam, wanawanyanyasa na kuwadhalilisha Wazanzibari wanapopita katika bandari hiyo wakiwa na vifaa ambavyo ni vya matumizi ya kawaida kwa ndugu zao.
  “Maofisa wa TRA katika Bandari ya Dar es Salaam, wanaharibu sura ya Muungano wa Tanzania . Wazanzibari wanapopita katika bandari hiyo wakiwa na seti za televisheni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, wanasumbuliwa mno utafikiri wanatoka katika nchi nyingine,” alisema Turky.
  Alisema kero hiyo ni ya muda mrefu na kwamba haijapatiwa ufumbuzi licha ya wakuu wa TRA kuahidi kuishughulikia.
  Maelezo hayo yalimlazimisha Waziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Samia Suluhu Hassan kusimama na kujaribu kuitetea TRA.
  “Suala hili lilishughulikiwa na uongozi wa TRA na kama linaendelea basi halitokani na TRA kama mamlaka na badala yake, linatokana na wafanyakazi wachache watukutu na wala rushwa. Kama mtu anapita pale akiwa na bidhaa lakini hana risiti lazima atasumbuliwa, kinyume chake watu watoe taarifa kuhusu kunyanyaswa,” alisema waziri Suluhu.
  Hata hivyo maelezo hayo hayakuwaridhisha wajumbe na badala yake, yaliongeza chumvi katika vidonda vya wajumbe ambao walisema tatizo bado ni kubwa na kwamba hatua lazima zichukuliwe ili kuwawezesha Wazanzibari, kupita katika bandari hiyo kwa uhuru kama ilivyo kwa wenzao wa Tanzania bara wanapoingia Zanzibar.
  Hatua hiyo, ilimlazimisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Hamis Mussa, kusimama na kupndekeza kwa Rais Karume, haja ya kuridhia mpango wa maofisa wa wizara yake kwenda Dar es Salaam kukutana na maofisa wa TRA hiyo, kujadili kero hiyo.
  Kwa mujibu wa Mussa, safari hiyo itafanyika kati ya leo na kesho.
   
 2. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hebu nikusogezee wateja!

  Pengine hali inaweza kuwa mbaya zaidi iwapo vyama vyengine (ukiondowa CUF) vitaingia madarakani. Kwao wao CCM inaidekeza Zanzibar na inahitaji kubanwa zaidi.
   
 3. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mimi nilidhani kuwa Zanzibar NI nchi nyingine! Halafu kweli seti ZA televisheni kwa matumizi ya kawaida! Hivi kweli kila ukimtembelea jamaa unabeba televisheni? Kumbe sura ya Muungano nzuri inapowafaidia wao! Iko kazi.

  Amandla...........
   
 4. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tanzania hakuna kiwanda kinachotengeneza TV...kwa maana hiyo kila TV set inayopatikana Zanzibar au sehemu nyengine yeyote pale Tanzania huwa imeingizwa kutoka nje... na hao TRA wako katika kila sehemu za Tanzania. Kama TV set imeingizwa Zanzibar,kutoka nje basi hao TRA tayari wemeshachukua kipato chao hapo Zanzibar...Sasa kama wanataka tena pesa za ushuru wakiona kitu kinatoka Zanzibar,huu ni wizi ....kwasababu kama utatoa TV set Tanga kupeleka Arusha ,hakuna malipa ya ushuru utakao lipa....
   
 5. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Ninavyoelewa (inawezekana nimekosea) ni kuwa Zanziba waliwatoa nje TRA kwenye mpango wa kukusanya ushuru nchini kwao. Kwa hali hiyo kodi yeyote ambayo mtu analipia akiingiza kitu Zanziba haiingii katika mfuko wa serikali ya JMT bali ni kwa ajili ya nchi ya Zanziba. Hii ndiyo maana mtu akitoka nchi kamili ya Zanziba kuingia nchi kamili ya JMT anatakiwa kulipa ushuru bila kujali kuwa yeye ni mzanzibari, chogo au raia wa nchi nyingine. Njia pekee ya kukwepa hili tatizo ni kwa nchi kamili ya Zanziba kuwapa TRA mamlaka ya kukusanya ushuru nchini kwao, nje ya hii watakuwa treated kama raia wa nchi nyingine, ambavyo ndivyo walivyo. Ukitoa televisheni Tanga kupeleka Arusha hautozwi ushuru kwa sababu hiyo ni mikoa ndani ya nchi ya JMT. Au, Mkuu, unataka kutuambia Zanziba ni mkoa kama Tanga na Arusha? Wahenga waliisha tuasa kuwa waangalifu tunpoomba kitu maana tunaweza kukipata!

  Amandla......
   
 6. K

  Kizibao JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 742
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 80
  Fundi mchundo..
  Nina respect kubwa sana na michango yako unayoitoa mpaka niliposoma hii thread yako. inaonyesha hujui kabisa unachokiongea nataka ukasome upya nini majukumu ya TRA na ZRB zanzibar na kodi gami wanazozikusanya na yale makusanyo ya kodi huwa yanaenda wapi?imetokea kuwa nina family members wanafanya kazi katika intution tatu zifuatazo TRA,ZRB na BoT.kwa hivyo hayo maoni yako uliyoyatoa hapo uko totally wrong lakini it doesn't matter kwani hapa jamii forums.is the place of rumours and fabrication na watu hawaangalii facts....Halafu nataka ujiulize mbona TRA hawatozi kodi kwa bidhaa zinazotoka T.bara.Na vp ile sera iliyotumika ku kuanzisha sha VAT kwa ku harmonize kodi tanzania nzima? Pls usichanganye baina ya kunde na chooko na kuleta baseless points bila ya kuwa na understanding ya kile unachokizungumzia
   
 7. Masika

  Masika JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 731
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Yupi mkweli kati ya
  fundi mchundo na kizibao maana kwa wengine hatuna uzoefu na linalozungumzwa
   
 8. bona

  bona JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  e
  mzee unasikitisha unapojionyesha uelewa wako wa issues ni mdogo, ni kweli vinalipiwa ushuru lakini ukipitishia zenji unalipa ushuru kidogo sasa unaweza tumia mwanya huo kupitishia bidhaa huko na then kuja kuziuza uku na ukaweza kupata competitive advantage kulinganisha na aliyeagiza na kuipitishia direct bandari ya bara! kwni kwenda kumtembelea ndugu yako lazima ubebe TV? na kwa nini utoe bidhaa zenji uwaletee ndugu zako huku kwani najua hakuna bidhaa ambayo iko zenji huku hamna! msitake muungano uwape faida za kiuchumi unfairly! wanapenmda bure hawa!
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Tarehe 31/10 si mbali.

  Mchagueni SLAA na atakupeni SERIKALI yenu na kila mtu ajijue kivyake.

  Hii itasaidia watu kubebwa kama Wanawake. Watani zangu bana, kazi kwelikweli.

  Nyie mmekuwa kama MAJI, kila siku kufuata mteremko, ebo. Maisha ni Mlima ati, kuna kupanda na kushuka.
   
 10. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mkuu, kumbe heshima yako ni pale tu ninapokubaliana nawe! Halafu wewe unajiita expert kwa sababu ndugu zako wanafanya kazi TRA, ZRB na BOT! Hata kama ni matarishi, walinzi au madereva kule, kufanya kazi kwao huko kunakufanya wewe mwenye uhusiano nao kuwa mkali! Kwa mtaji huo hata mtoto wa miaka miwili wa bosi TRA ni mkali kuliko sisi wote!

  TRA hawana mamlaka ya kukusanya ushuru ( sio kodi) Zanzibar. Viwango vya ushuru Zanzibar vinapangwa na serikali ya mapinduzi Zanzibar na si JMT. Ndio maana ushuru unaotozwa ukiingiza mali Zanzibar ni chini kuliko ukiingiza JMT. Tofauti hii ndio inayochangia kwa kiasi kikubwa kufanya bei ya bidhaa za nje Zanzibar kuwa chini sana. Kutokana na hilo ndio maana dada zetu wengi walikuwa wakifanya biashara ya kwenda darajani kununua bidhaa na kuziingiza bara, ambako wakati ule walikuwa wakiingia bila kutozwa ushuru. JMT ilipogundua hilo ndio wakaanza kuwabana ili wazuie watu kutumia Zanzibar kama njia ya kuingiza bidhaa bara bila kulipa bidhaa. Mwanya huu ungeathiri sana biashara za wale ambao wanalipia ushuru bara. Hii haina tofauti na kuandikisha magari. Kuandikisha gari Zanzibar ni mchekea kuliko bara hivyo kuna watu walianza kuingizia magari yao Zanzibar, kuyaandikisha kule halafu kuyahamishia bara. Wajuao wakawastukia na kuanza kuwabana. Njia pekee ya kuepusha yote haya ni kuipa taasisi moja mamllaka ya kukusanya ushuru JMT na Zanzibar au kuhakikisha kuwa viwango vinakuwa sawa sehemu zote mbili. Nje ya hiyo, hauwezi kuwalaumu watu wa JMT wakijaribu kulinda soko lao. Zanzibar hawawezi kula keki yao halafu kubaki nayo.

  TRA wanatoza ushuru kwa bidhaa yeyote inayoingia au kutoka bara. Nenda long room ukaona watu wanavyobanwa mbavu! Jaribu kusafirisha nje vinyago hata viwili uone watakavyokusumbua! TRA hawawatozi kodi wazanzibari peke yao bali hata dada zetu kutoka bara. Wa kulalamika zaidi wangekuwa wao maana TRA iliwaharibia kabisa biashara yao bila kujali kuwa wao ni machogo wenzao!

  Amandla.....
   
 11. K

  Kizibao JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 742
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 80
  Hahahahahaaa
  Naona umejibu ki jamii forum way! sina nia ya kuwadharau matarishi au not lakini hao jamaa zangu siyo matarishi kama unvyosema wewe na wana position kubwa sana hapo. lakini kufanya kazi kwao katika tasisi hizo siyo kulonifanya nitoe maoni hayo hapo kwa sababu ninaongea vile ninavyofikiria mimi na hali halisi ilivyo na siyo kama wewe inaonyesha huna hata idea ya kile unachokizungumza. Hivi unajua kama ushuru wa forodha ni mamlaka ya serikali ya muungano? inakuwaje serikali ya ZNZ ndiyo yenye kuweka viwango vya kodi na siyo Muungano hata mtu mwenye mtindio wa ubongo anaweza kujua kama hilo siyo kweli?na nachelea kukuweka katika group hiyo.Wakati wa utawala wa Dr salmin ndiyo kweli hayo mabo yalikuwepo ya kuwa ushuru unaokusanywa na TRA ulikuwa mdogo T.bara na Zanzibar.lKINI alipoingia karume mambo yakawa sawa sawa inaonyesha hulijui hilo.na nakushauri fanya utafiti zaidi uone kwa nini zanzibar magari rahisi kuliko T.bara na siyo.hivi umesikia kauli ya waziri alivyosema na kwa nini aseme vile kama ushuru unaotzwa zanzibar ni mdogo?na kama uko nchi za nje fikiria harama za kuushusha mzigo ZNZ na T.bara wapi ziko juu na kitu gani kilichopelekea kuwa juu.jibu ni kuwa. Wafanyabiashara wengi sana wa Kizanzibar wanashusha mzigo Dar au Tanga kwa sababu ya ushuru wanaolipa uko sawa na zanzibar sasa ile faida ya kuushusha mzigo ZNZ haiko tena kwa hali hiyo inapelekea meli zinazopeleka mzigo ZNZ kuwa na Mzigo mdogo sana huku harama za kufunga gati ZNZ zikiwa zile zile kama za zamani matokeo yake huwa wana compasate gharama zile kwa ule mzigo mdogo wanaoupeleka na ndiyo maana kulishusha contena zanzibar ni ghali kuliko T.bara( inaonyesha hulijui hilo).na kwa mara nyengine tena fanya utafiti zaidi na siyo kutuletea pumba zako hapa ukatarajia kukuamini.
  Nilikuwa ninaziheshimu thread zako kwa sababu ulikuwa utatoa points kwa kile unachokiamini hata kama kitu kile cha uongo au kweli? lakini hapa leo naona blabbing tu.
   
 12. c

  chamajani JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Swadakta!
   
 13. c

  chamajani JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ndiyo, kwani si hata ukibeba mikate ya baressa kwenda nayo usukumani huwa unatozwa kodi-na kwa nini ubebe mikate toka ubungo pale au kule central, kwani huko uchagani hakuna
   
 14. c

  chamajani JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kizibao
   
 15. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mpaka dakika hii naandika kujibu maandiko yako, hao TRA bado wako Zanzibar na wanakusanya kodi kama kawaida... Malalamiko mengi zidi ya TRA ambayo waZanzibari wamekua wakilalamika ni kwamba ,wao (waZanzibari ) wanalipa kodi mara mbili, kwa TRA na ZRA. Ndio kumekuwa na tishio ka kuwafukuza TRA Zanzibar,kama utawala wa CCM ukimalizika...Lakini mpaka sasa TRA wako Zanzibar na wanakusanya kodi kama kwaida. Hao watu wanaolalamika sio vichaa, na hili ni moja ya mambo yanayo kereketa system nzima ya Muungano...Kama nia ya Tanganyika kuifanya Zanzibar kuwa ni mkoa ,basi bado haija fanikiwa, kwani waZanzibari wengi wamekua na muamko wa kudai nchi yao iwe katika mikono yao...Mimi ni mTanganyika ambae naishi Zanzibar...
   
 16. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Zanzibar kuna vyombo viwili vya ushuru TRA ambacho ni chombo cha mnyongano na ZRB Zanzibar Revenue Board ambacho ni chombo cha kukusanya ushuru wa forodha Zanzibar. Kwa maana hiyo wazanzibari wanalipa ushuru kwenye vyombo viwili vyenye mamlaka ya kukusanya ushuru yaani ZRB na TRA ndio maana wakati mwingine inakuwa wazimu kununua bidhaa zanzibar kwababu bei ya baadhi ya vitu ipo juu kwasababu inatozwa ushuru mara mbili na ukija nacho dar es salaam unatozwa tena.

  Utakuwa na risiti ya manunuzi umelipia mpaka VAT lakini ukitia show bandari ya Dar es Salaam unalazinika kulipa tena! Hili limekuwa ni kero si kwa wazanzibari peke yao hata sisi wabara pia maana hawakuangali wewe ni mzenji au ni mbara.
   
 17. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sasa tusubiri uchaguzi umalizike salama na kama CUF watashinda Zanzibar, basi hili tatizo litakwisha kwani serekali itakayoongozwa na CUF itawaondosha hawa TRA kule Zanzibar... sasa ile haki ya hawa TRA kukusanya kipato chao itakua hapo bandarini DAR, na sio pande zote mbili.
   
 18. c

  chamajani JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Will be so danger for Isles-Lakini hatimaye unafuu utakuja
   
 19. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hapa Jamii Forums huwa tunajibu hivi. Hatusemi tuna ankal mahali kwa hiyo tuamini bali tunaweka vielelezo. Soma hapa, ukurasa wa 7, ibara 11 inavyosema kuhusu VAT:
  http://www.tra.go.tz/documents/taxes%20and%20duties%20swahili.pdf

  Wameweka wazi kuwa kodi hizo zinahusu Tanzania Bara, na nikinukuu, " Kwa uagizaji na uingizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kuingia Tanzania BARA 18%". Kwa mtaji huu Zanziba ni nje ya Tanzania bara na yeyote atakayeingiza mali Tanzania Bara kutoka Zanzibar anawajibika kulipa 18% ya thamani ya huduma au bidhaa aliyoiingiza. Hakuna mahali waliposema kuwa mali au huduma kutoka Zanzibar zinakuwa exempted.

  Njia pekee ya kukwepa hili ni kwa Zanzibar kuomba kuwa sehemu ya Tanzania Bara kama Mwanza, Tanga na kwengine. Lakini ikibaki kuwa nchi basi kwenye hili itahesabiwa kama nchi nyingine.

  Amandla....
   
 20. K

  Kizibao JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 742
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 80
  Wowwww

  Kama interpretation yako ya kipengele hicho unaiweka ZNZ sawa na nchi ya kigeni huo ni uamuzi wako wewe haimaanishi TRA wanafanya hivyo na inaonyesha umepoteza wakati wako mwingi sana kuitafuta hiyo na ukaona ndiyo punching line.lakini kosa ni kutokuijua katiba yako inasemeje na ikakupelekea kusherehesha kipengele hicho kutoka na ufahamu wako mdogo au just umeeamuwa hivyo ili kufikia lengo lako ulilokusudia.Lakini nenda TRA kaulize ni ukitoa mzigo zanzibar kuuleta bongo unatozwa 18% kwani hata hao wanaolalamika bandarini wanahangaishwa na maofisa wa TRA basi hiyo pesa wanayoichukua basi ni asilimia ndogo sana na hata risiti unakuwa hupewi.sijui kama uko TZ au Nje lakini kwanza nenda bandarini jaribu kuuliza utapata ukweli halisi au nenda Ofisi za TRA kaulizie.
  PS: Pengine kwenye ndoto yako tu zanzibar itakuwa mkoa lakini in real world kitu hicho hakitotokea
   
Loading...