TRA wanavyofunga biashara za wazalendo

Ni matumaini yangu kuwa Waziri Dr Mpango anapitia humu ili kuona taasisi yake ya TRA , ilivyobadilika kuwa a business terrorist instrument.
TRA inatega bomu la kibiashara litakalotengua nchi kiuchumi.
 
Wengine Ni Brela sijui serikali haioni ule upuuzi wao ? Mtu unafungua kampuni ila wanakuzungusha Hadi unachoka.


Yule Mtendaji mkuu wa Brela ni wa kufukuzwa kabisa hajawahi kufanya mabadiriko yoyote. Rushwa zimekithiri Brela.


Jamii forum anzisheni Uzi maalumu wa kutoa kero ya hizi taasisi za umma tuisaidie serikali na wao wawe wanapita humu kuona uozo.
 
Mkuu hicho ndicho wafanyabiashara wengi kwa sasa wanafanya.
Funga biashara kula mtaji uliomao taratibu.
Hii si nzuri kwa afya ya uchumi wa nchi.
Bora hivyo kuliko kufa kwa pressure aisee jamaa wana force kila siku kutuma barua tunataka kuja kukukagua hesabu zako za 2016 na 17 na 19 🙆
 
Nashauri; TRA wachunguzwe juu ya uhalali wa kodi zao. Kesi zimekuwa nyingi siku za hivi karibuni.
Mkuu tatizo ni malengo wanayo pewa, wanapewa malengo makubwa sana.
Na manager wa mkoa asipo fikisha inabidi ajieleze kwann?
Sasa hapa ndio kwenye shida
 
Acha tu aisee una fanya kazi kwa nguvu kubwa sana watu wanakuja kukuumiza kwa hesabu za uwongo!🙆
 
Usihangaike mkuu kuna watu humu wanafrahia wengine wakipata shida
 
Ungekuja na takwimu walau ungetushawishi tukuamini. Tuletee walau takwimu kidogo ya wafanyabiashara waliofungiwa.
 
Umelimbikiza madeni nenda kalipe na TRA wanakubali malipo kwa awamu.
Wewe hujui unalosema,nyie ndio amabo hamjui kitu kwa sababu hujawahi fanya biashara na kulipa kodi.na hujui mchango wa biashara za kati kwenye mchango wa pato la serikali. Yaani serikali zinazoendelea dunia ninkwa kuwa na mfumo mzuri wa kodi.serikali haitakiwi kuingia kufanya biashara,inatakiwa kuwezesha watu wafanye biashara ili walipe kodi.

Ni hivi mtu ulifanyiwa tax assesment miaka mingi iliyopita na hao hao maafisa tra na kulipa chao baadaye wanakuja hawa tena wanafanya upya na kusema uli underfile,so unakokotolewa kodi nyingine na ile tofauti unapigwa fine na interest.kwa nini wasianze na hao maofisa wa nyuma waliosema kila kitu kiko cleani. yaani hapa kwa nini warudi miaka ya nyuma ambayo tayari walishaicheki wenyewe. Hii nadhani inawezekana kwa some instances siyo kila assesment.yaani wanaweza pia baadaye wakarudi pia na kusema kiasi hicho kipya nacho kilikuwa wrong.

Tunazungumzia "unpridictabe enveronment" watu wanakuwa waoga kuendelea na biashara kwa sababu TRA wenyewe kwa wenyewe kila ofisa na tafsiri kivyake sheria ya kodi.

Labda tushauri yafuatayo.


1.Kuwe na TIC,kituo cha uwekezaji kwa wafanyabiashara wadowadogo wenye mitaji midogo na ya kati,mathlani mtu anataka kufungua hardware,duka la jumla,phamacy,biashara ya usafirishaji,gereji,shule,Hotel,bar,guesthouse,lodge,uchimbaji wa madini n.k kuwe kuna kitengo mahali flani serikalini (kila wilaya) cha kwenda kuomba ushauri na kusaidiwa kukamilisha vitu mhimu na kupewa elimu muhimu ya maswala ya kodi na vibali mbalimbali na kufafanuliwa kwa sheria mbali mbali kulingana na sekta ambayo biashara husika iko

2.Lile dawati la ushauri la TRA lingekuwa linafikika na wafanyabiashara wa kawaida

3.Kuwe kuna kitengo kingine cha kuhakiki ukokotoaji kodi kabla mtu hajapewa bili yake ya kodi

3.Kuwe na idara huru(Obusman).Ili wafanyabiashara wenye malalamiko wawe wanaenda kupeleka malalamiko ya unfair tax assesment.kiwe huru na kiwezeshwe kufanya kazi.na kiwe nje ya wizara ya fedha.(kiwe kina dhibiti ubabe wa TRA).yale mabalaza (tribunal) yalishashashindwa kazi zamani

4.TRA wawe na kitengo cha kumentor biashara ndogo ili ziweze kukua.Kila oficer anayekusanya kodi,biashara anayokusanya kodi ikifa naye kazi iishe.Ila ikiweza kukua na kuongeza mapato aweze kupata promotion.kwa mfano wakati wana asses performance ya mkoa wa kikodi waangalie pia idadi ya wafanyabiashara wapya waliojisajiri.ikitokea waliojisajiri ni wengi kulikowalifunga biashara basi wapewe bonas.ila biashara zilizofungwa zikiwa nyingi kuliko mpya then wapunguziwe points za performance. so in short inatakiwa biashara zikifungwa kuwe na direct negative impact kwa TRA region ofice.yaani wafike mahali wahusike kulinda biashara kufa.so zile fine na riba wanazokokotoa wazire-flect juu ya uhai wa biashara husika

Sasa hivi TRA wanaonekana miungu watu,na kituo cha uwekezaji (TIC) wanaonekana wajinga tuu.kumbe ndiyo kitengo mhimu na kilipaswa pengine kiwe ndani ya Wizara ya fedha na mipango.Chini ya waziri mmoja.aulizwe biashara kufungwa na upande wa pili aulizwe juu ya mapato toka kwa hizo biashara
 
Unaona kama watu wanachosema ni siasa?[emoji41],huyu mdudu anaeitwa TRA ni kiboko
Wafanya biashara ndio tunajua uchungu.. binafsi wamenikarisha... nafikiri kurudi kijijini nijipange upya 🥲🥲
 
Mkuu tatizo ni malengo wanayo pewa, wanapewa malengo makubwa sana.
Na manager wa mkoa asipo fikisha inabidi ajieleze kwann?
Sasa hapa ndio kwenye shida
sasa ndio kuamua kuziua biashara ambazo hawakuchangia mitaji? Yao si kodi tu?
 
Bank sasa siyo mahala salama kwa pesa za wafanyabiashara kwani TRA huenda kufunga A/C kienyeji na kupora pesa za wafanyabiashara kwa njia haramu za kishetani
Upo sahihi, kuna mtu wame piga kienyeji kabisa..
 
Tatizo ni kubwa sana Mungu awasaidie mlio baki kwenye ligi ya biashara
 
Ifike mahali, wananchi tutangaze kuwa TRA ni adui wa mwananchi, ni adui wa maendeleo, na adui mkuu wa Taifa.

Kiundwe chombo kingine kipya. TRA kwa ujumla ni genge la wevi wanaotumia mgongo wa Serikali.

Kuanzishwe jumuia ya walipa kodi. Jumuia hiyo ikiwa na nguvu ya kutosha, hakuna mlipa kodi atakayeonewa na hawa wahuni TRA. Kuwe na ada ya wanachama. Itakuwa jukumu la jumuia hii kutetea wanachama wake.

Chama hiki kitakuwa na uwezo wa kuunganisha nguvu za wanachama, ikibidi hata kuitisha mgomo wa walipa kodi. Wanachama wanaweza kugomea kufungua viwanda vyao na biashara zao hata kwa mwezi mmoja ikilazimu ili kuishinikiza Serikali kuisimamia TRA .
 
Ushauri: Mtu yeyote asifanye biashara yenye mkono/uhusiano wa TRA wala kusajiliwa na TRA.

Inabidi pawe na uzi wa orodha ya biashara mbalimbali ambazo hazihusiani na TRA wala ukiifanya hiyo biashara hauhitajiki kusajiliwa na TRA.
Unawajua municipal wewe? Hawa ndiyo shida kabisa hata kama una biashara ya mamantilie wakija wa naondoka na masufuria na vijiko

yaani hii nchi hakuna pa kukimbilia, ujanja ni kuhamisha tu mtaji unapeleka nchi jirani maana hakuna namna
 
,=
Ungekuja na takwimu walau ungetushawishi tukuamini. Tuletee walau takwimu kidogo ya wafanyabiashara waliofungiwa.
Sijui kama uko nchini.
Nenda kariakoo uone biashara zilizofubgwa.
Nenda mitaa ya Sinza, Temeke, Ilala uone frame zilizofungwa.Nenda au uliza ofisa yeyote TRA uone watu wakirudisha form za kufunga biashara.

Tunayoongea ni ya kuisaidia serikali ijinusuru kiuchumi.
Hata Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amegusia hili, tusiwapige wafanyabiashara kodi za kulemaza biashara.
 
Nchi Haina pesa,
Hao nao,wanaogopa kupoteza vibarua vyao,sasa ni mwendo wa mbwa kala mbwa,
Tumefika kwenye Dog eat dog society,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…