TRA wanavyofunga biashara za wazalendo

Nashauri; TRA wachunguzwe juu ya uhalali wa kodi zao. Kesi zimekuwa nyingi siku za hivi karibuni.
Wachunguzwe na nani kama anaewatuma ndo last say wa state.
Hii inchi imewekea malengo ya ukusanyaji hadi Traffic police na Hospital sasa sielewi wamelenga makosa ya barabarani yaongezeke na watu wazidi kuumwa ?
 
Ushauri: Mtu yeyote asifanye biashara yenye mkono/uhusiano wa TRA wala kusajiliwa na TRA.

Inabidi pawe na uzi wa orodha ya biashara mbalimbali ambazo hazihusiani na TRA wala ukiifanya hiyo biashara hauhitajiki kusajiliwa na TRA.
Biashara zote zenye mtaji usiozidi mil 4 zinatozwa na kitamburisho cha mjasiriamali so ficha stock zako store nunua kitamburisho weka dukani
 
Wizi mtupu. Wamejazana maofisini kurudia kazi zile zile. Sio wabunifu.

Kodi zimeacha makampuni mengi yakiwa na madeni yasiyolipika. Wengi wanatumia assessment kama sehemu ya kuchukua rushwa tena bila aibu.

TRA wanaua biashara zetu kwa kubambikia kodi zisizolipika.

Hivi kwenye hizi biashara zetu, Kuna kampuni ngapi zinazopata faida zaidi ya asilimia 30 kwa mwaka? Mbona wao wanakuwa kama sio wasomi. Kila hela kampuni inayoingiza wanaichukulia kama ni faida.

Yes TRA sio mbali sana mtakuwa hamna mtu wa kukusanya tena kodi. Yatabaki madeni yasiyolipika
 
Wachunguzwe na nani kama anaewatuma ndo last say wa state.
Hii inchi imewekea malengo ya ukusanyaji hadi Traffic police na Hospital sasa sielewi wamelenga makosa ya barabarani yaongezeke na watu wazidi kuumwa ?
Kwani ni mara yako ya kwanza kuona wafanyakazi wanalipa kodi?? Au unamaana gani hapa 🤔🤔??
 
Hujasomeka kabisaaaaa mkuu.yan sijui umeandika kitu gan!!
 
T.R.A ni tatizo kubwa kwa sasa ustawi wa nchi. Wafanyabiashara wengi wanakimbilia nje ya nchi. Ukitaka kujionea hili,nenda mpaka wa tunduma. Mamlaka za Zambia baada ya kuona wafanyabiashara wananyanyaswa sana upande wa Tanzania wakakaaa nao wamewatengea eneo upande wa zambia,kwa hiyo wengi wanahamia upande wa zambia kujenga maduka. Soon Tunduma upande wa Tz itakufa kabisaaa. Ona kariakoo inavyotia huruma kwa sasa.

Kipindi miaka 6 tu nyuma kariakoo ilikuwa ni kitivo cha biashara kwa nchi za DRC,Malawi,Zambia,Mozambique n.k,kariakoo ndio ilikuwa dubai yao.

Baada ya kuona bidhaa ziko juu kariakoo sbb ya T.R.A wafanyabiashara hizo nchi nao wamejiongeza wanaenda nao mbele. Lakini T.R.A wakijisahihisha bado tuna nafasi ya kuzikamata hizo nchi
 
Kama unadaiwa kalipe tu siyo unalia lia JF.
Easier say than do. Unalipa na nini? Wala sio kulia. TRA iko kwa mujibu wa sheria. Na hawako juu ya sheria. Msijidanganye. Mwenzako akinyolewa, wewe tia maji
 
Kodi zinalipwa na wakaguzi wanapita lakini wapo baadhi hukataa ukaguzi wa awali wanaamua kufunga A/C kienyeji kwa njia haramu za kishetani ili kutengeneza mazingira ya Rushwa au kumkomoa watu.

TRA walio wengi ni wala rushwa wakubwa
 
TRA vinara wa kuwafungia A/C wafanyabiashara wanajulikana vizuri ni vye Serikali ikaitisha mkutano wa wafanyabiashara wote walionja Adha ya kufungiwa A/€ zao ili waelezee kero zao na kuwataja kwa majina maofisa wa TRA wanaoshiriki vitendo haramu vya kuwabambikia kodi kubwa kisha kupata kisingizio haramu cha kuwafungia A/C
 
Inatia uchungu kuona ni mtanzania anayefanya haya.Inaumiza sana.Kwann Mungu asimchukue tu!!??
 
Mtamlaumu tu TRA huku kuna mtu anaharibu masoko ya nje kwa kushindwa kucheza vizuri na uwanja wa diplomasia anaropokea wahisani na nchi rafiki kauli za kuwa yeye anahadhina nyingi na pesa nyingi za kuendeshea nchi ONA SASA wamemchunia ameanza kutoa malengo magumu ya makusanyo kwenye taasisi za kiserikali bila kujari anaua biashara na maisha ya watu
 
Hapo utapigizana sana kelele na wamachinga,ili waone maumivu ni mpaka wawe walipa kodi,hakuna mmachinga anaeona maumivu haya kwa hiyo usijichoshe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…