TRA wanavyofunga biashara za wazalendo

TRA wanavyofunga biashara za wazalendo

Pumbav wewe
We ni mmoja wao? Je kweli kwa akili ya kawaida watu mil hamsin waende somea kapato,nini mgawanyo wa majukum,wao wako pale kwa kazi iyo ya kodi ,kutoa elim na si kuonea watu KWA bambikia makodi.na kila fani inaumuhim wake,Sasa ukisema kila mtu akasomee Mambo ya kodi, hivyo hivyo ipo siku utasema Kila mmoja akasomee ualim,police,bwanashamba n.k ,hoja ya maajabu Sana hii,na ya funga mwaka
 
Ngoja nikueleweshe kidogo tofauti ya withholding tax, provisional tax na corporate tax.
Withholding tax ni kodi ya mapato ya awali(advance payment) inayokatwa na kuwasilishwa TRA na mlipaji kwa niaba ya mlipwaji.
Mfano mimi kama tax consultant nikaja kukusaidia kazi za kiuhasibu kwa makubaliano wa kunilipa TZS 10,000,000.
Unatakiwa ku-withhold 5% ya contract price, ambayo ni 500,000 na badala yake unanilipa net ya TZS.9,500,000.
Assume mwaka mzima nilipata kazi hiyo moja tu.
Lakini niliingia gharama za operating cost may be 8,000,000 kwa mwaka mzima.hivyo faida ni 10,000,000 minus 6,000,000= hivyo faida ni 4,000,000.
Sasa corporate tax ni 30% ya faida ,hivyo natakiwa nilipe 1,200,000.
Sasa before sijalipa
(i) natakiwa ni-deduct advance payment ya withholding tax ambayo ni laki 5.hivyo tax payable inapungua kutoka 1200,000 to 700,000
(ii) natakiwa ni-deduct provisional taxes nilizolipa kwenye all 4 installments, let say nililipa 150,000 for each installment, hivyo nimeashalipa total of 600,000
Hivyo basi tax liability inapungua kutoka 700,000 to 100,000.
In summary corporate tax of 1200,000 umeilipa kama ifuatavyo
● 500,000 by way of withholding tax
● 600,000 by way of installment
● 100,000 by way of final tax.
Nadhani hakuna double taxation hapo
Hii ndio JF yenye manufaa hasa, hata sisi tusiokuwa na ABC ya haya mambo ya kodi tunafaidika vizuri kabisa.

Ahsante sana mkuu 'IFRS' kwa kuongeza thamani ya JF.
 
Shule ya st.Jude ni wapumbavu kama wafanyabiashara wengine, hawataki ku-comply na sheria za kodi, wanaishia kuleta mambo yao mitandaoni ili wapate public sympathy. Court of appeal imewaruhusu TRA wakombe hela kwenye akaunti baada ya rufaa kushindikana wanasema wanaonewa.TRA wamesimamia hukumu ya Court kwamba wachukue hela.
Sasa wewe kwepa kodi kwa kisingizio chochote kama hujaja kuanzisha uzi humu.fuata sheria kaka
Unajua, kelele nyingi zinazosikika sasa, baadhi yake ni sababu za ujinga (kutojua) kwa walipakodi. Duniani kote, mkusanya kodi huwa ni mtu wa kuogopwa.Hata kwenye biblia wameelezwa, kwa kutopendwa na wafanya biashara.
 
Ingependeza Kama mkuu watahalam wa wambo ya kodi wengeanzisha uzi mahalum kuhusu elimu ya kodi ,maana kweli wenda watu wanapigwa na TRA kutoka a na uelewa ndogo,
Kodi zinatokana na sheria ambazo accountants inabidi wazitumie ila siyo kitu constant maana kodi zenyewe zinabadilika kila mwaka wa fedha na mara nyingine kubadilika kwake zinabadilisha treatment of certain items in the final accounts.

Jinsi wenzetu wanavyo update practice wataalamu wa sheria za kodi (ambao na wenyewe lazima walikuwa accountants in their past life) wanatafsiri application za sheria kwa kutoa vitabu ambavyo accountants wote wasiobobea kwenye tafsiri za sheria wanatumia, that’s how things work.

Vinginevyo bila ya watu kama hao kila mwaka all accountants will need to get the entire budget manuscript and start to interpret the law, utaratibu utakuwa ni majanga sio wote watasoma kwanza na kwa watakaosoma chances are kutakuwa na variation of interpretation.

Kurahisisha mambo ndio maana wataalamu wa tax law ambao ni accountants waliojiongeza wanatafsiri kodi zilizobadikika kwenye budget na application zake pamoja na mambo mengine allowed or disallowed expenditures and so for forth to do with VAT taxes as well final accounts.

Na hao ndio wataalamu the likes of international accounting firms such as PWC or KPMG hire, watu kama hao sheria zetu za copy and paste wanazijua applicability yake kushinda accountants tia maji tia maji wa TRA.

Ndio maana unaona makampuni makubwa ya kigeni wanatumia hizo large accounting firms kuwafanyia hesabu zao matokeo yake tunabaki tunalia hawalipi kodi wakati sheria wanazotumia tumepitisha wenye bungeni.

Kwa ivyo kusema utaanzisha mjadala wa kodi wakati mambo yanabadilika kila mwaka sio tu kwamba watu wanaweza pishana interpretations (kama ulivyoona baadhi ya wachangiaji humu kwenye treatment za withholding tax) bali unaweza kuwa mjadala usio jenga.

Ni muda wa kuchapisha kitabu cha kutumiwa na proffesionals (ambacho kinakuwa updated kila mwaka) kama nchi nyingine wanavyofanya mambo, iwapo ili jambo alifanyiki kwa sasa.
 
Tuzidishe spana habari zinawafikia
IMG_20201216_183602.jpeg
 
TRA wametumwa kodi , wamepewa kazi ya kusimamia sheria za kodi ,kama hau-comply ni ujinga wako sio kosa Lao.
Chuo cha kodi kinatoa kozi za kodi hata kwa form 4 failure ,hamtaki kwenda.
Mimi nashangaa mtu anaposema TRA wanaonea wafanyabiashara, wewe na TRA mnaongozwa na sheria za kodi, mkishindwana kuna tribunals mpaka court of appeal.
Upande wangu TRA ya Tz haipo serious sana kukusanya kodi ,imekuwa inawalea sana wafanyabiashara wazembe sababu ya kujuana
Thats the crux of the matter.
Mkuu hujijui kuwa hujui.
Mfano uliotoa umejionyesha kuwa licha ya kuwa "Tax Consultant" hujui hata kukokotoa With Holding tax kwa kukosa uelewa.
Chuo cha kodi kama threshold ni form four failures na kinapokea watu kama wewe, then you know what to expect.
 
Kuna uzi umeletwa humu maafisa wa tra wasimamishwa kazi na waziri mpango
Makosa yao moja yapo ni kubambikia watu mikodi

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Mkuu kuna watu wajinga wajinga wanafikiri hatujui wanachokifanya .
Hii ni trela maana sasa tutanza kutoa zile transactions ambazo huwa wanazifanya kukomoa mfanya biashara ili wavute michuzi.
Tnashukuru Waziri Mpango ameanza kufungua macho sasa.
 
Kama vipi na viongozi wachunguzwe tokea enzi za nyerere sehemu aliposaini mktaba pia utajiri wake na Hela aliyokuwa analipwa kama na tax return TRA Iko proportion hata kama ana biashara je alikuwa anazilipia kodi.
Yaani lisisalie jiwe juu ya jiwe.

Ila hawa majamaa tokea nilivyowanaga mwaka 95 wanampiga dingi mdogo kama 10M niliwaogopa sana.
Mpaka wamenifanya nilitaka kufanya biashara nawaza TRA mana kama ni kovu na nilivyokuwa mdogo jamani
 
Thats the crux of the matter.
Mkuu hujijui kuwa hujui.
Mfano uliotoa umejionyesha kuwa licha ya kuwa "Tax Consultant" hujui hata kukokotoa With Holding tax kwa kukosa uelewa.
Chuo cha kodi kama threshold ni form four failures na kinapokea watu kama wewe, then you know what to expect.
Bahati mbaya hujui kama hujui, hivi unashindwa kuwa na uelewa wa kodi rahisi kama withholding tax payments halafu unashinda humu kuwalalamikia TRA. TRA kazi yao ni kusimamia na kutafsiri sheria za kodi na sio kufundisha watu sheria.kama hujui angaika kutoa huo ujinga
 
Shule ya st.Jude ni wapumbavu kama wafanyabiashara wengine, hawataki ku-comply na sheria za kodi, wanaishia kuleta mambo yao mitandaoni ili wapate public sympathy. Court of appeal imewaruhusu TRA wakombe hela kwenye akaunti baada ya rufaa kushindikana wanasema wanaonewa.TRA wamesimamia hukumu ya Court kwamba wachukue hela.
Sasa wewe kwepa kodi kwa kisingizio chochote kama hujaja kuanzisha uzi humu.fuata sheria kaka
Wafanyabiashara wengi wanafuata Sheria pasipo kukwepa kodi, lakini TRA wakiamua kusaka Rushwa ama kumkomoa mtu humbambikia VAT hewa kodi bandia kwa njia haramu za kishetani, maofisa vinara wa kupora pesa za wafanyabiashara hawakosagi sababu hata kama mfanyabiashara analipa kodi zote bila Tatizo, wakidhamilia kutaka Rushwa hulazimisha chochote mpaka wafanikishe malengo yao
 
TRA wametumwa kodi , wamepewa kazi ya kusimamia sheria za kodi ,kama hau-comply ni ujinga wako sio kosa Lao.
Chuo cha kodi kinatoa kozi za kodi hata kwa form 4 failure ,hamtaki kwenda.
Mimi nashangaa mtu anaposema TRA wanaonea wafanyabiashara, wewe na TRA mnaongozwa na sheria za kodi, mkishindwana kuna tribunals mpaka court of appeal.
Upande wangu TRA ya Tz haipo serious sana kukusanya kodi ,imekuwa inawalea sana wafanyabiashara wazembe sababu ya kujuana
Hizi kazi inabidi wapewe watu waliowiva.
Mfano uliotoa kweli ni kilaza.
 
Bahati mbaya hujui kama hujui, hivi unashindwa kuwa na uelewa wa kodi rahisi kama withholding tax payments halafu unashinda humu kuwalalamikia TRA. TRA kazi yao ni kusimamia na kutafsiri sheria za kodi na sio kufundisha watu sheria.kama hujui angaika kutoa huo ujinga
Nikupe swali jingine rahisi ili kuku expose dunia nzima ijue aina ya watuwetu wa kodi tulio nao.

Je katika biashara yako uliyoieleza , profit yako ni kiasi gani?
 
Tunalazimika kueleza jinsi TRA wanavyofunga biashara za wafanyabiashara.

TRA wamepangiwa malengo ya ukusanyaji fedha, kinyume cha hivyo mtu anafukuzwa kazi na ajira inakoma.

TRA kama ilivyo ada kwao, hawafuati weledi wa kibiashara au kuona jinsi ya kupata mapato endelevu, wao ni kutimiza amri ya mkubwa wao, iwe isiwe.

Mfano:
Wafanyakazi wawili wawili au watatu wanapewa kampuni mbili au tatu na wanatakiwa watazame makosa ya kiuhasibu ndani ya returns za mfanyabiashara zilizowasilishwa TRA hata miaka 10 iliyopita.

Haijalishi kama kuna wenzao walipita mwaka jana na mwaka juzi. Ni kama mtu anaamrishwa kuvuna shamba lililokwisha kuvunwa.

UKWELI hapo ni kwamba hakuna kodi ya mapato inayotafutwa, ni hela tu, basi. Uwe nazo usiwe nazo unalijua Jiji.

Hivyo makosa ya kiuhasibu yanatafutwa kwa nguvu. Tunajua fika level ya wahasibu wetu, ambao hata serikalini wapo, na makosa yanayoweza kufanywa.

Hiyo timu ya wakaguzi wa TRA wanapata makosa ya kulazimisha kama kumi hivi, na huo ndio mtaji wa “kodi”, na si kutokana na mapato.

Kwanza, makosa hayo yajengewa uhalali wa kupigwa kodi
Pili, yanapigwa fine
Tatu, yanapigwa interest-riba

Yakijumlishwa ndiyo eti unaletewa assessment ya kodi unayodaiwa-wizi mtupu, maana hizi ni kodi za kupikwa.

Ukiwa na Tax Consultant ataweza kupangua baadhi ya hizo “kodi”, kama huna TRA wanakimbilia akaunti yako benki na kukomba chochote kilichomo.

Sasa hii ni State Robbery.
Na haya yanafanyika kila leo.

Matokeo yake:
Sasa hivi kuna misururu ya wafanyabiashara kule matawi ya TRA, wanafunga biashara.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kodi iliyokokotolewa haitokani na mapato, bali makosa ya kiuhasibu.
Kodi iliyokokotolewa na TRA hao haiwezi kulipika kutokana na mapato ya kibiashara, hivyo mtu kulazimika kufunga biashara.

Makampuni tunayoyaona mitaani yametembelewa mara tatu au nne kwa mwaka, TRA wanataka kodi za kupikwa.

USHAURI
TRA inatakiwa ifanye kazi kwa madhumuni iliyo anzishwa, yaani kukokotoa kodi kutokana na MAPATO YA BIASHARA na si vinginevyo.
Sasa hivi kodi zinachukiliwa kutokana na punitive measures na si mapato, hivyo kula mtaji wa biashara.
Kiuchumi hili kosa linaua biashara nchini.
Nekwenda kwenye moja Kati ya maduka maarufu ya nguo na viatu vya kiume hapa Dar lililopo kariakoo nikanunua kiatu kwa TZS 90,000/- namdai risiti ananiletea stori kwamba mashine imeharibika. Nilipokuuliza kuhusu barua toka TRA hana nikamwambia anirudishie hela siwezi kutoka bila Risiti.

Akainama chini ya counter akaniprintia Risiti fasta.

Kesho mkisikia maduka hayo yamefungwa kama kawaida yenu mtaanza kuimba mapambio ya TRA wanaonea wafanya biashara.

Nyambafu kabisa...
 
Rais Hussein Mwinyi akiapishwa Mawaziri wa Serikali yake alisema kuwa Kodi kubwa kwa walipa kodi haihakikishi mapato makubwa ya Serikali bali Kodi rafiki walipa kodi wengi. Huyu ni Rais wa wananchi wake milioni 1.5, inashangaza Rais wa watu milioni 60 pamoja na wale haelewi ukweli huu badala yake anatoa maagizo na malengo makubwa ofmagumu kufikiwa. Hii inawafanya wakusanyaji Kodi kutumia nguvu na ubabe kufikia viwango walivyoagizwa wakiongeza cha juu chao na kufanya viwango kuwa vikubwa zaidi kutolipika. TRA ni moja ya Taasisi chache wafanyakazi wao wanalipwa vizuri sana na rushwa njenje kuwa hiyo vilaza wa wakubwa wamekaa huko. Idara ya Polisi hapo zamani ilikuwa inapata shida sana kupata wafanyakazi hata wasio na kazi yoyote ya kuwaletea kipato hawakutaka upolisi lakini leo ni vigumu sana kwa mtoto wa mwananchi wa kawaida kupata kazi ya upolisi ni watoto wa wakubwa na wa Polisi wenyewe ndo wamejaa huko kwa sababu ya fursa ya rushwa. Kuhusu ukusanyaji Kodi, TRA ndo iandae malengo yao kila mwaka bila cha juu kulingana na hali halisi kiuchumi kwenye maeneo yao ya kazi na kupeleka malengo hayo Serikalini ili iandae bajeti zake. Lengo la ukusanyaji lisipofikiwa ni TRA wa kulaumiwa.
Hali halisi iko wazi. Kinyume cha hapo ni wizi. Na wanatumia nafasi kama hizo kujipatia rushes.
 
Nekwenda kwenye moja Kati ya maduka maarufu ya nguo na viatu vya kiume hapa Dar lililopo kariakoo nikanunua kiatu kwa TZS 90,000/- namdai risiti ananiletea stori kwamba mashine imeharibika. Nilipokuuliza kuhusu barua toka TRA hana nikamwambia anirudishie hela siwezi kutoka bila Risiti.

Akainama chini ya counter akaniprintia Risiti fasta.

Kesho mkisikia maduka hayo yamefungwa kama kawaida yenu mtaanza kuimba mapambio ya TRA wanaonea wafanya biashara.

Nyambafu kabisa...
Mbona nyambafu wengi zaidi mnao majumbani kwenu wakijenga mahekalu huko Kimara, Kinsudi, Bonyokwa na kwingineko.
Semeni tu !
Tulianzishe kuleta picha humu mtandaoni?
Na uzuri siku hizi unaweza weka hata google location.
 
Tuzidishe spana habari zinawafikiaView attachment 1651677
Safi sana waziri sasa umeanza vizuri, tunaomba wana JF waje na List ya maofisa wa TRA vinara wa kufunga Account kuwabambikia kodi kubwa hasa wilaya ya ilala kule long room makao makuu ya TRA, TRM mkoa wa Dsm Kinondoni na Temeke ndipo kuna vinara wa kuwabambikia kodi na kufunga Account za wafanyabiashara kienyeji kwa njia haramu za kishetani.
 
Back
Top Bottom