TRA wanakomoa wananchi, hii sio haki

TRA wanakomoa wananchi, hii sio haki

Vp kuhusu biashara, ongelea biashara
Kuhusu biashara ili upate leseni ni lazima ulipe kodi kwanza (hapa haujaanza biashara).
*Je, kodi inalipwa kutoka kwenye mtaji wa biashara au faida ya biashara?
*Vipi kuhusu makadirio ya kodi? Utanikadiriaje kodi wakati haujaja kuiona?
 
Hata Rwanda machinga wanalipa Lodi# Burundi hadi baiskeli inalipia kodi @ kodi ni lazima kwa maendeleo
Kule wanalipa kwasbb hakuna makadirio ya kodi. Ww ushaona wapi kabla ya kuanza biashara unatakiwa kulipa kodi. Kodi inalipwa kutoka kwenye mtaji au faida?
 
Mambo kama haya yanajenga sana chuki ktk jamii, serikali isipokuwa makini watu watakuja zinguana mchana kweupe
 
Du ndugu ungekaa chini kwanza uandike vizuri.TRA sijawahi sikia ati sheria zao zinakutaka upakize ng'ombe kwenye Lori. Halafu kama unatunza kumbukumbu zako za biashara kwa nn ufunge duka? Mbona mm nipo Tunduma ndiyo kwanza napiga biashara yangu sababu sioni kwa nn niwaogopevTRA hali ya kuwa najua kiwango nachopata nastahili lipia 150,000 kwa mwaka. Tatizo tukiwa hatujitambui ndiyo tunatafuta sababu.Hakuna sheria TRA inataka ubebe ng'ombe kwenye Lori, hao jamaa wao ni watu wa kukusanya Kodi tu.Kama unaona vipi kuja jamaa mm huwa wananisaidia sana kama nakuwa na utata 0800780078 au 0800750075
Hivi vitu sio vya kubumba Mzee
Nimeshuhudia kwa macho yangu,TRA wanazuia na kuwakamata ng'ombe kisa wanaswagwa bila kubakizwa kwenye Lori
Sijui unakaa nchi gani bro
 
Hakuna namna kipaumbele chetu ni kodi ukiuza toa risiti ukinunua dai risiti
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania,wanachokifanya kwa serikali ya awamu ya Tano ni unyanyasaji wa wananchi masikini wa nchi hii.

Mwananchi ambaye ameona ajiajiri mwenyewe ili ajiepushe na uhalifu kama vile ujambazi lakini kwa hali ilivyo sasa inatisha

TRA mwanza nimeshuhudia wakifunga visalooni ambavyo wateja wake hunyoa kwa sh 1000, kisa hajalipa kodi,fundi cherehani tena wanaorepair nguo nao wanafungiwa kisa hawajalipa kodi

Pia nikashuhudia wafanyabiashara wa ng'ombe kwenye minada wanapigwa faini kubwa kisa wanasafirisha ng'ombe bila kutumia malori,nimeshuhudia maafisa wa TRA wakiomba elfu 70 faini kwa kila ng'ombe,fikiria umenunua ng'ombe watatu kwa sh laki 6, unalipa sh laki 210 hii ni haki kweli

Chonde chonde serikali kupitia TRA wanajitathimini namna wanavyolipisha wananchi kodi za ajabu ajabu

Jamani salooni ya kunyoa sh 1000 ana mashine moja anatakiwa kulipa kodi,huu sio unyanyasaji,
Fundi cherehani masikini anayesubiria nguo ya mtu ichanike naye anambiwa alipie kodi
Ulimpigia kura Nani? Ulipopiga kura si uliambiwa kuwa usifanye makosa na ukaelimishwa madhara yatakayotokea katika nchi ikiwa utampigia kura Yule aliekuwa akikanywa na jk na pinda Lakini haukusikia sasa usilie lie tulia hivyo hivyo sindano ikuuingie vizuri
 
Ulimpigia kura Nani? Ulipopiga kura si uliambiwa kuwa usifanye makosa na ukaelimishwa madhara yatakayotokea katika nchi ikiwa utampigia kura Yule aliekuwa akikanywa na jk na pinda Lakini haukusikia sasa usilie lie tulia hivyo hivyo sindano ikuuingie vizuri
Sindano hii ni chungu sana
 
Back
Top Bottom