TRA na Maafisa Biashara wa Wilaya ya Songwe acheni kuwaibia wananchi

Njaa kali30

Member
Jul 18, 2021
47
28
TRA wakishirikiana na maafisa wa wilaya ya Songwe wamekuwa wakiwahuhujumu wafanya biashara wadogo wa wilaya ya Songwe wamekuwa wakiwafungia biashara zao hasa mama na kuwalazimisha walipie sh 50,000 ya kufuli na kuwapiga faini ya 50000, ya usumbufu, 50000 kupata TIN namba na Sh 50000 kwa ajili ya leseni ya biashara, 30000 kwa ajili ya kuhuisha TIN namba iliopotea.

Wameweka kambi katika vijiji vya muheza, manda, mamile, songambele kambarage, khanga ifwekenya na wako huko wakiendesha kuwafungia wafanyabiashara maduka.Ikumbukwe wakati wa magufuli watu waliambiwa kukata vitambulisho vya ujasiliamali.

Sasa nashindwa kuelewa sasa hivi inashindikana nini mama ntilie na mama lishe wanasumbuliwa hivi katika Nchi yao.Wizara ya fedha iseme kama imwatuma hawa maafisa biashara wa halmashauri kukusanya mapato wakishirikiana na maafisa TRA.

Wamekuwa ni kuja na mgari usiku na kufanya msako. Mhe Rais chonde chonde wanakukosanisha na wapiga kura wako kuwa makini wananchi wa wilaya ya Songwe wanaumia.

Kama mwigulu ndo kaagiza anakugombanisha na watu wako naomba usiturudishe kwenye mambo ya kodi ya kichwa.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom