TRA wanakomoa wananchi, hii sio haki

TRA wanakomoa wananchi, hii sio haki

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,121
Reaction score
1,981
Mamlaka ya Mapato Tanzania,wanachokifanya kwa serikali ya awamu ya Tano ni unyanyasaji wa wananchi masikini wa nchi hii.

Mwananchi ambaye ameona ajiajiri mwenyewe ili ajiepushe na uhalifu kama vile ujambazi lakini kwa hali ilivyo sasa inatisha

TRA mwanza nimeshuhudia wakifunga visalooni ambavyo wateja wake hunyoa kwa sh 1000, kisa hajalipa kodi,fundi cherehani tena wanaorepair nguo nao wanafungiwa kisa hawajalipa kodi

Pia nikashuhudia wafanyabiashara wa ng'ombe kwenye minada wanapigwa faini kubwa kisa wanasafirisha ng'ombe bila kutumia malori,nimeshuhudia maafisa wa TRA wakiomba elfu 70 faini kwa kila ng'ombe,fikiria umenunua ng'ombe watatu kwa sh laki 6, unalipa sh laki 210 hii ni haki kweli

Chonde chonde serikali kupitia TRA wanajitathimini namna wanavyolipisha wananchi kodi za ajabu ajabu

Jamani salooni ya kunyoa sh 1000 ana mashine moja anatakiwa kulipa kodi,huu sio unyanyasaji,
Fundi cherehani masikini anayesubiria nguo ya mtu ichanike naye anambiwa alipie kodi
 
TRA TRA TRA hiki kimekua ni kilio kila kona,plz Mr President 2020 z coming tusiwe wepesi wakusahau yale mafuriko ya lowasa
 
TRA ya sasa haijapata kushuhudiwa hapa Tanzania. Ukadiriaji ni under presumptive regime tuu. Ukitaka ujaze return uwe mwasibu mwenye CPA (T). Awamu hii Sheria na taratibu nyingi sana zinakiukwa.
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania,wanachokifanya kwa serikali ya awamu ya Tano ni unyanyasaji wa wananchi masikini wa nchi hii.

Mwananchi ambaye ameona ajiajiri mwenyewe ili ajiepushe na uhalifu kama vile ujambazi lakini kwa hali ilivyo sasa inatisha

TRA mwanza nimeshuhudia wakifunga visalooni ambavyo wateja wake hunyoa kwa sh 1000, kisa hajalipa kodi,fundi cherehani tena wanaorepair nguo nao wanafungiwa kisa hawajalipa kodi

Pia nikashuhudia wafanyabiashara wa ng'ombe kwenye minada wanapigwa faini kubwa kisa wanasafirisha ng'ombe bila kutumia malori,nimeshuhudia maafisa wa TRA wakiomba elfu 70 faini kwa kila ng'ombe,fikiria umenunua ng'ombe watatu kwa sh laki 6, unalipa sh laki 210 hii ni haki kweli

Chonde chonde serikali kupitia TRA wanajitathimini namna wanavyolipisha wananchi kodi za ajabu ajabu

Jamani salooni ya kunyoa sh 1000 ana mashine moja anatakiwa kulipa kodi,huu sio unyanyasaji,
Fundi cherehani masikini anayesubiria nguo ya mtu ichanike naye anambiwa alipie kodi
Wapiga dili hao
 
daah ajira hakuna biashara ngumu kilimo hakuna suko zuri la mkulima shule za msingi walimu ni wachache mnoo gharama za maisha zimekuwa juu mishahara haiongezeki mikopo hailipiki Hawa mabeberu na mafisadi walio tufikisha hapa Mungu anawaona ngoja nitembee kifua mbele npo kwenye right track
 
Ukijua matawi wenzio wanajua mizizi. Tunduma mji wa mpakani na Zambia wafanyabiashara wote wa Tanzania wamehamia upande wa Zambia. Sasa TRA Tunduma hata hicho kidogo hawapati. Wanunuzi wa bidhaa zao ni watanzania waishio Tunduma kodi inalipwa Zambia kwenye mamlaka ya kodi ya kistaarabu
 
kila nilazima ilipwe hata muuza vitumbua # watanzania tunapenda burebure sana mbna hapa Argentina hata machinga mdogo analipa kodi tena yupo group D. nikiwa tanzania nimedhudia machinga wanafanya mauzo hadi ya lakini tano ila hawalipi kodi kisa ni machinga anamwaga bidhaa chini@
 
Kwa kweli TRA awamu hii wanatisha,kwa hali hii ccm wanajizika wenyewe
 
Back
Top Bottom