TRA 'wambana' Dk Slaa

Dkt Willbrod Slaa huwa hakurupuki bila ushahidi wa uhakika lazima hapo pana ufisadi ndani yake pengine ktk hizo bilioni 80 huyu Luoga anazo zake 40.Pili ktk habari hii mwandishi kakurupuka maana kichwa cha habari hakiendani na habari sambamba maana sioni mahali TRA wamembana Dkt wa ukweli Willbrod Slaa.
Nimelipa kodi TRA kwa miaka 4 ktk biashara yangu na cha kushangaza mwaka wa tano wameniambia nilikuwa nnaiibia Serikali pesa sbb ikiwa aliekuwa akikadiria alikosea.Sasa Kama ni kweli nilikuwa nikiibia Serikali mapato nnahusika vp hapo kwani kodi zote nimezilipa ktk ofisi zao?
 
Issue ya uplifting ukiagiza kijigari chako japan is disgusting. I used to respect tra but since such horrible thing happened to me naona km genge tu la wakusanya ushuru tena unfairly. Hata ukiwapa documents za email how u negotiated with the vendor na invoice hawakuelewi. sanasana wakishaup lift wanakaa kimya na documents hazi move tena utajijua kwenye storage/demurrage charges. Since then najiuliza hawa ma assessors/ valuers wa tra wamesoma vyuo gani au ndo wale wanagraduate na gentlemen gpas. Next time nikipata vijisent napitishia gari yangu Mombasa and am not being unpatriotic!
 
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), 'imemkaba kooni' Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Dk. Willibrod Slaa, kufuatia tuhuma alizozitoa dhidi ya ofisa wa mamlaka hiyo kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha.

Hivi karibu, gazeti moja lilimkariri Dk. Slaa akitaja majina ya watu mbalimbali wanaotuhumiwa kuwa ni mafisadi. Pia wakati akihutubia katika mkutano wake wa hadhara mkoani Tabora, alitaja orodha ya watuhumiwa hao akiwamo oafisa wa TRA, Placidus Luoga. Gazeti hilo lilimkariri Dk. Slaa akidai kuwa Luoga aliingizia serikali hasara ya Sh800 bilioni kwa kuzuia magari ya Kampuni ya Tango, Transport ya jijini Dar es Salaam kwa miaka 10 kwa kisingizio cha kutolipa kodi.

Alidai kuwa kitendo hicho, kiliilazimisha kampuni hiyo, kufungua kesi mahakamani ambako ilishinda na serikali kuamriwa kuilipa kiasi hicho cha fedha.Gazeti hilo lilimkariri kiongozi huyo wa Chadema akidai kuwa tayari serikali imeshailipa kampuni hiyo Sh500 milioni.

Hata hivyo jana TRA kupitia taarifa yake iliyotolewa na Idara ya Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, imekanusha madai hayo na kuyaita kuwa uzushi tu wa Dk Slaa na kumtaka atoe uthibitisho wa madai yake hadharani.

"Huu ni uzushi unaopaswa kulaaniwa vikali kwa sababu unapotosha wananchi na hasa wasomaji wa magazeti. Dk. Slaa atoe nakala ya hukumu hiyo ili wananchi wamwamini. Bila kufanya hivyo kutaonyesha kuwa ametoa habari za uongo kwa kusingizia mahakama," ilisema taarifa.

Taarifa hiyo ilimtaka Dk. Slaa kutoa vielelezo vya maelezo yake hadharani na kwenye mkutano ili awathibitishie wananchi kuwa alichosema ni cha kweli.

TRA ilisema kama Dk. Slaa atashindwa kufanya hivyo, ni dhahiri kuwa yeye si mtu makini na ni mtu mwenye nia ya kupotosha umma wa Watanzania na kuchafua heshima ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.

"Kudanganya watu kwa siri au hadharani ni aina mojawapo ya aina nyingi za kutokuwajibika. Kutokuwajibika kuna sura nyingi na uongo ni mojawapo. Dk. Slaa lazima ajisafishe na hili," ilisisitiza taarifa ya TRA. Taarifa hiyo ya TRA ilisema Luoga hajawahi kuzuia wala kukamata magari yanayodaiwa na Dk. Slaa.

"Hakuna ofisa wa TRA mwenye akili timamu anayeweza kukaa na mali ya mtu anayedaiwa kodi kwa miaka 10 huku akijua kuwa anatakiwa kukomboa kodi hiyo. Anatakiwa kuuza mali hiyo ili serikali ipate kodi; Kwa afisa yoyote aliye kwenda shule hawezi kufanya hivyo akishuhudia mlipa kodi anapeleka kesi Mahakamani ambako atapata fidia ya sh.800 bilioni," ilisema sehemu ya taarifa.

Ilisema hata kama ofisa huyu hajaenda shule, lakini hawezi kuhusika na mpango kama huo.

Ilisemwa mujibu wa maelezo ya Dk. Slaa,mahakama iliona kuwa Tango Trasport ya Dar es Salaam ilipata hasara ya wastani wa Sh80 bilioni kwa mwaka."Kwa biashara ya kawaida Tanzania, mahesabu kama haya hayawezi kuingia vyema kichwani kwa yeyote mwenye busara," imesisitiza TRA.

Hata hivyo TRA katika taarifa yake ilisisitiza kuwa Luoga haifahamu Kampuni ya Tango Transport ya jijini Dar es Salaam ambayo magari yake yamewahi kuzuiwa kwa muda wa miaka 10.

Imefafanua kuwa kumbukumbu zilizoko TRA zinaonyesha kuwa kampuni ya Tango Transport ni ya Arusha na kusisitiza kwamba hakuna taarifa zinazoeleza kuwa TRA imewahi kukamata magari ya kampuni hiyo kwa miaka 10.

Juhudi za gazeti hili kumpata Dk. Slaa kuzungumzia taarifa ya TRA hazikufanikiwa kwa kuwa simu yake ya mkononi haikuwa hewani.

Ha ha ha haaaa mzee wa watu Slaa amelishwa kasa tena na wajanja wa mjini , sijui lini ataacha kujiabisha namna hii
 
TRA ni vibaka tu hawana lolote.
  • Kwanini watu wanapitishia magari yao Bandari ya Mombasa badala ya Dar na Tanga?
  • Ni mabilioni mangapi yanapotea kwa kwa watu kupitishia magari yao Mombasa?
  • Nani hajui kuhusu TAX Holiday kwa wawekezaji?
  • CAG report imebainisha madudu ya misamaha ya mabilioni ya Kodi,Je, hiyo nayo TRA hamkubali?
  • Nani hajui kuwa mtu ukiagiza gari toka Japan likifika hapa nchini TRA wanaongeza bei(uplift) kwa madai kuwa bei inayokuwa claimed kwenye docs siyo ya kweli??
  • Nani hajui mgogoro uliopo kati ya TRA Zanzibar na TRA Bara? Kwamba gari ikiingia kupitia Zenj you pay less lakini the same vehicle ikija Bara you pay more???
  • TRA ndiyo the highest payed employees hapa nchini lakini ndiyo the most corrupt people(wala rushwa wakubwa)?
TRA acheni longolongo kusanyeni KODI ili pato la serikali liongezeke na nchi isonge mbele.Pambaf!

Naunga mkono.
 
wapenda anasa wametajwa kinawauma sana,matanuzi mtaani hatunywi maji,watu hawana amani na ndoa zao kisa wafanyakazi wa TRA,maana hawa jamaa kama mke wa mtu ni mzuri wanakunyang'anya,dhambi ilioje

Kwa hilo mie sina tatizo nalo kwani popote pale nikisikia tu huyu au yule ni mke wa mfanyakazi wa TRA basi kwishney, kwa gharama zozote zile na alhamdulilah wengi wao si wabaya kama waume zao wanavyotufanyia pale long room
 
hilo tamko limetolewa na nani? na ni vyombo vingapi vya habari vilihusishwa?
I mean hii habari inaelea elea tuu!!
huu ni usanii mtupu toka kwa taasisi nyeti kama tra..
binafsi nawaelewa sana hawa: ni mafisadi waliokubuhu!!
 
Eti 'kuchafua heshima ya mamlaka ya mapata'.
Hii imenichekesha sana, heshima ipi? Misamaha holela ya kodi kwa wageni au heshima ipi- chukua chako mapema au heshima ipi?
Najisikia kuweweseka na hii heshima ambayo inadaiwa kuchafuliwa.
 
akitoa ushahidi wao watawajibika vipi? watajiudhuru na kukubali kufilisiwa?
kwa nini wao hawataki kujisafisha kwa kusema nini hasa kilitokea,
hii nayo ni aina ya upuuzi hapa TANZANIA ndio kichaka chao cha kujificha siku hizi
sisi wananchi Dr Slaa tunamsoma
MIMI NINA HAKIKA SIKU DR SLAA akiongopa kama wao wanavyodai na wakajua kadanganya kesi itafunguliwa haraka sana
na hivi vyombo vya serikali, maana mtu wanayetaka kumuona JELA kwa sasa ni Dr Slaa (most wanted )



Wametoa taarifa kwa umma nimeona hilo tangazo kwenye gazeti la mwananchi la leo ijumaa mei,6 2011
Nanukuu Hitimisho:
"Kwavile Dr.Slaa ametoa maelezo hayo hadharani na waziwazi kwenye mkutano,ni vema atoe vielelezo vya maelezo yake hadharani na kwenye mkutano pia ili awathibitishie wananchi kuwa alichosema ni kweli.
Akishindwa kufanya hivyo basi ni dhahiri kuwa yeye sio mtu makini na ni mtu mwenye nia ya kupotosha umma wa watanzania na kuchafua heshima ya maamlaka ya mapato Tanzania.Kdanganya watu kwa siri au hadharani ni aina mojawapo ya aina nyingi za kutowajibika.Kutokuwajibika kuna sura nyingi na uongo ni mojawapo.Dr slaa lazima ajisafishe na hili.
Mamlaka ya mapato ipo wazi kupokea mawazo,maoni hata kukosolewa na mtu binafsi au taasisi yoyote kaika maeneo yenye kuleta tija.Mamlaka pia ipo wazi katika utoaji wa taarifa mbalimbali za kiutendaji kwa mtu au taasisi kwa mujibu wa sheria za nchi"
Imetolewa na:
Idara ya elimu na huduma kwa mlipa kodi
Mamlaka ya mapato Tanzania
S.L.P 11491
Dar es salaam
Tarehe 5/5/2011
 
hilo tamko limetolewa na nani? na ni vyombo vingapi vya habari vilihusishwa?
I mean hii habari inaelea elea tuu!!
huu ni usanii mtupu toka kwa taasisi nyeti kama tra..
binafsi nawaelewa sana hawa: ni mafisadi waliokubuhu!!

ndo maana asubui nkasema sasa TRA imekuwa chama kipya cha siasa,uksoma wananchi utaona upeo mdogo wa mleta habari!
 
TRA Ni waongo na wazushi wakubwa tena kutumia kodi za watanzania kuandika uongo ni ufisadi mwingine.

N a wana JF hebu tujenge utamaduni wa kusoma ripoti mbalimbali zinazowekwa hapa , kuhusu ufisadi wa Luoga na TRA CAG ALISEMA HIVI;

RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA
HESABU ZA SERIKALI KUHUSU TAARIFA ZA
FEDHA ZA SERIKALI KUU KWA MWAKA​
ULIOISHIA TAREHE 30 JUNI, 2010

•​
Malipo ya fidia isiyostahili kwa kampuni ya TANGO
Limited Sh.554,464,133

Kiasi cha Shs.554,464,133.60 kililipwa kwa M/S Tango
Transport Limited (Verani Tango) kama fidia kwa
mujibu wa hati za Magari yake zilizodaiwa
kuchukuliwa na maafisa wa TRA mwaka 1997 kwa
muda wa siku tisini (90). Hata hivyo, mapungufu
yafuatayo yalibainishwa:
i. Mrejesho ya Shs.53,650,151 yaliambatanishwa na
hati ya kukiri mapokezi ambayo uhalisi wake
haukuthibitishwa. Aidha, kiasi hiki kililipwa mara
mbili, wakati awamu ya kwanza malipo yalifanywa
kwa amri ya mahakama.
ii. Malipo ya Sh.6,788,840 hayakuhusiana na madai ya
msingi
iii. Malipo ya riba ya Shs.554,464,133.60 yalifanyika​
kwa ‘compound interest” badala “simple interest”.

SASA WANAPOSEMA HAWAJAWAHI KULIPA KIASI HICHO NA HAWANA KUMBUKUMBU KAMA KUNA KESI YA TANGO TRANSPOTERS WANAMAANISHA NINI?

NTAREJEA.
 
Kifupi nawaambia kuwa hii itakuwa aibu kubwa sana kwa TRA kwani wameingia kwenye mtego wenyewe, nalifahamu hili suala niliwahi kushirikishwa na Dr.Slaa.

Ni aibu ya mwaka na nawaambia kuna hukumu inaonyesha kuwa Veran alipwe fidia ya 800 bilioni ,na hata malipo yaliyofanywa najua effort za Dr.Slaa akiwa mbunge aliandika barua nyingi sana na nyingi zilijibiwa na Luoga mwenyewe na hata mwanasheria mkuu wa serikali wakati huo Mwanyika amewahi kujibu na hata waziri mkuu pinda amejibu kwa maandishi sasa TRA wamenasa, wait u shall see.
 
Imefafanua kuwa kumbukumbu zilizoko TRA zinaonyesha kuwa kampuni ya Tango Transport ni ya Arusha na kusisitiza kwamba hakuna taarifa zinazoeleza kuwa TRA imewahi kukamata magari ya kampuni hiyo kwa miaka 10.

Nawaambia magari yalikamatwa , kama hawajakamata waseme milioni 554 zilizohojiwa na CAG ni za kazi gani?

wanapaswa kujipanga upya na hapa nafikiri kuna kesi ya Dr.Slaa kukashifiwa na TRA na kwa sababu hawa wana pesa za kumlipa fidia sio vibaya akafa nao kwa mara ya kwanza mahakamani.
 
mamlaka ya mapato tanzania (tra), 'imemkaba kooni' katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo(chadema) dk. Willibrod slaa, kufuatia tuhuma alizozitoa dhidi ya ofisa wa mamlaka hiyo kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha.

hivi karibu, gazeti moja lilimkariri dk. Slaa akitaja majina ya watu mbalimbali wanaotuhumiwa kuwa ni mafisadi. Pia wakati akihutubia katika mkutano wake wa hadhara mkoani tabora, alitaja orodha ya watuhumiwa hao akiwamo oafisa wa tra, placidus luoga. Gazeti hilo lilimkariri dk. Slaa akidai kuwa luoga aliingizia serikali hasara ya sh800 bilioni kwa kuzuia magari ya kampuni ya tango, transport ya jijini dar es salaam kwa miaka 10 kwa kisingizio cha kutolipa kodi.

alidai kuwa kitendo hicho, kiliilazimisha kampuni hiyo, kufungua kesi mahakamani ambako ilishinda na serikali kuamriwa kuilipa kiasi hicho cha fedha.gazeti hilo lilimkariri kiongozi huyo wa chadema akidai kuwa tayari serikali imeshailipa kampuni hiyo sh500 milioni.

hata hivyo jana tra kupitia taarifa yake iliyotolewa na idara ya elimu na huduma kwa mlipa kodi, imekanusha madai hayo na kuyaita kuwa uzushi tu wa dk slaa na kumtaka atoe uthibitisho wa madai yake hadharani.

"huu ni uzushi unaopaswa kulaaniwa vikali kwa sababu unapotosha wananchi na hasa wasomaji wa magazeti. Dk. Slaa atoe nakala ya hukumu hiyo ili wananchi wamwamini. Bila kufanya hivyo kutaonyesha kuwa ametoa habari za uongo kwa kusingizia mahakama," ilisema taarifa.

taarifa hiyo ilimtaka dk. Slaa kutoa vielelezo vya maelezo yake hadharani na kwenye mkutano ili awathibitishie wananchi kuwa alichosema ni cha kweli.

tra ilisema kama dk. Slaa atashindwa kufanya hivyo, ni dhahiri kuwa yeye si mtu makini na ni mtu mwenye nia ya kupotosha umma wa watanzania na kuchafua heshima ya mamlaka ya mapato tanzania.

"kudanganya watu kwa siri au hadharani ni aina mojawapo ya aina nyingi za kutokuwajibika. Kutokuwajibika kuna sura nyingi na uongo ni mojawapo. Dk. Slaa lazima ajisafishe na hili," ilisisitiza taarifa ya tra. Taarifa hiyo ya tra ilisema luoga hajawahi kuzuia wala kukamata magari yanayodaiwa na dk. Slaa.

"hakuna ofisa wa tra mwenye akili timamu anayeweza kukaa na mali ya mtu anayedaiwa kodi kwa miaka 10 huku akijua kuwa anatakiwa kukomboa kodi hiyo. Anatakiwa kuuza mali hiyo ili serikali ipate kodi; kwa afisa yoyote aliye kwenda shule hawezi kufanya hivyo akishuhudia mlipa kodi anapeleka kesi mahakamani ambako atapata fidia ya sh.800 bilioni," ilisema sehemu ya taarifa.

ilisema hata kama ofisa huyu hajaenda shule, lakini hawezi kuhusika na mpango kama huo.

ilisemwa mujibu wa maelezo ya dk. Slaa,mahakama iliona kuwa tango trasport ya dar es salaam ilipata hasara ya wastani wa sh80 bilioni kwa mwaka."kwa biashara ya kawaida tanzania, mahesabu kama haya hayawezi kuingia vyema kichwani kwa yeyote mwenye busara," imesisitiza tra.

hata hivyo tra katika taarifa yake ilisisitiza kuwa luoga haifahamu kampuni ya tango transport ya jijini dar es salaam ambayo magari yake yamewahi kuzuiwa kwa muda wa miaka 10.

imefafanua kuwa kumbukumbu zilizoko tra zinaonyesha kuwa kampuni ya tango transport ni ya arusha na kusisitiza kwamba hakuna taarifa zinazoeleza kuwa tra imewahi kukamata magari ya kampuni hiyo kwa miaka 10.

juhudi za gazeti hili kumpata dk. Slaa kuzungumzia taarifa ya tra hazikufanikiwa kwa kuwa simu yake ya mkononi haikuwa hewani.

mimi binafsi sioni kazi zenu zinaendaje watoza ushuru nyie mnashibisha matumbo yenu
 
TRA ni taasisi kubwa nchini na ina wanasheria wazuri. Kama inaona imechafuliwa, kwa nini wasifungue mashitaka dhidi ya Dr. Slaa?
Jamani yaani siku hizi Bongo ukikashifiwa suluhu ni kumuomba aliyekuchafua aweke mambo wazi kwa wananchi na si kwenda mahakamani. Sasa aeleze umma mara ngapi kuwa kuna ufisadi?

Kwa mtazamo wangu: Kama umechafuliwa na ukashindwa kwenda mahakamani wakati una haki ya kwenda mahakamani kutoa malalamiko yako, basi nina-assume kuwa uko GUILTY.
 
Back
Top Bottom