TRA 'wambana' Dk Slaa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), 'imemkaba kooni' Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Dk. Willibrod Slaa, kufuatia tuhuma alizozitoa dhidi ya ofisa wa mamlaka hiyo kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha.

Hivi karibu, gazeti moja lilimkariri Dk. Slaa akitaja majina ya watu mbalimbali wanaotuhumiwa kuwa ni mafisadi. Pia wakati akihutubia katika mkutano wake wa hadhara mkoani Tabora, alitaja orodha ya watuhumiwa hao akiwamo oafisa wa TRA, Placidus Luoga. Gazeti hilo lilimkariri Dk. Slaa akidai kuwa Luoga aliingizia serikali hasara ya Sh800 bilioni kwa kuzuia magari ya Kampuni ya Tango, Transport ya jijini Dar es Salaam kwa miaka 10 kwa kisingizio cha kutolipa kodi.

Alidai kuwa kitendo hicho, kiliilazimisha kampuni hiyo, kufungua kesi mahakamani ambako ilishinda na serikali kuamriwa kuilipa kiasi hicho cha fedha.Gazeti hilo lilimkariri kiongozi huyo wa Chadema akidai kuwa tayari serikali imeshailipa kampuni hiyo Sh500 milioni.

Hata hivyo jana TRA kupitia taarifa yake iliyotolewa na Idara ya Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, imekanusha madai hayo na kuyaita kuwa uzushi tu wa Dk Slaa na kumtaka atoe uthibitisho wa madai yake hadharani.

"Huu ni uzushi unaopaswa kulaaniwa vikali kwa sababu unapotosha wananchi na hasa wasomaji wa magazeti. Dk. Slaa atoe nakala ya hukumu hiyo ili wananchi wamwamini. Bila kufanya hivyo kutaonyesha kuwa ametoa habari za uongo kwa kusingizia mahakama," ilisema taarifa.

Taarifa hiyo ilimtaka Dk. Slaa kutoa vielelezo vya maelezo yake hadharani na kwenye mkutano ili awathibitishie wananchi kuwa alichosema ni cha kweli.

TRA ilisema kama Dk. Slaa atashindwa kufanya hivyo, ni dhahiri kuwa yeye si mtu makini na ni mtu mwenye nia ya kupotosha umma wa Watanzania na kuchafua heshima ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.

"Kudanganya watu kwa siri au hadharani ni aina mojawapo ya aina nyingi za kutokuwajibika. Kutokuwajibika kuna sura nyingi na uongo ni mojawapo. Dk. Slaa lazima ajisafishe na hili," ilisisitiza taarifa ya TRA. Taarifa hiyo ya TRA ilisema Luoga hajawahi kuzuia wala kukamata magari yanayodaiwa na Dk. Slaa.

"Hakuna ofisa wa TRA mwenye akili timamu anayeweza kukaa na mali ya mtu anayedaiwa kodi kwa miaka 10 huku akijua kuwa anatakiwa kukomboa kodi hiyo. Anatakiwa kuuza mali hiyo ili serikali ipate kodi; Kwa afisa yoyote aliye kwenda shule hawezi kufanya hivyo akishuhudia mlipa kodi anapeleka kesi Mahakamani ambako atapata fidia ya sh.800 bilioni," ilisema sehemu ya taarifa.

Ilisema hata kama ofisa huyu hajaenda shule, lakini hawezi kuhusika na mpango kama huo.

Ilisemwa mujibu wa maelezo ya Dk. Slaa,mahakama iliona kuwa Tango Trasport ya Dar es Salaam ilipata hasara ya wastani wa Sh80 bilioni kwa mwaka."Kwa biashara ya kawaida Tanzania, mahesabu kama haya hayawezi kuingia vyema kichwani kwa yeyote mwenye busara," imesisitiza TRA.

Hata hivyo TRA katika taarifa yake ilisisitiza kuwa Luoga haifahamu Kampuni ya Tango Transport ya jijini Dar es Salaam ambayo magari yake yamewahi kuzuiwa kwa muda wa miaka 10.

Imefafanua kuwa kumbukumbu zilizoko TRA zinaonyesha kuwa kampuni ya Tango Transport ni ya Arusha na kusisitiza kwamba hakuna taarifa zinazoeleza kuwa TRA imewahi kukamata magari ya kampuni hiyo kwa miaka 10.

Juhudi za gazeti hili kumpata Dk. Slaa kuzungumzia taarifa ya TRA hazikufanikiwa kwa kuwa simu yake ya mkononi haikuwa hewani.
 
Vitu vingine vipi TRA inaficha au mbona issue ya Tango Transport inawauma hivyo? Tuonyesheni data zote na mnakusanya kodi vipi na kwanini mishahara yenu wote haiendani na maisha mnayoishi? Sisi ni majirani zenu mtaani na tunajua ndugu zetu wanaishi maisha ya juu sana wakifanya kazi TRA, mnapata wapi hizo pesa na bosi mbona anaishi kama CEO, hivi TRA mna CEO?
 
Washaona Dr Slaa anaingia TRA, wanaogopa maovu yao mengi yatajulikana ndio maana wanakuwa defensive kiasi hicho. Nendeni mahakamani kama mmesingiziwa
 
Duh! Dr. Slaa umeingia TRA? Sasa unatafuta balaa..Maana hao ni MIUNGU WATU!!!!

Luoga - No Longer AT EASE!!
 
Washaona Dr Slaa anaingia TRA, wanaogopa maovu yao mengi yatajulikana ndio maana wanakuwa defensive kiasi hicho. Nendeni mahakamani kama mmesingiziwa

Hapo hawatathubutu...! watapiga kelele magazetini tu.
 
TRA ni vibaka tu hawana lolote.
  • Kwanini watu wanapitishia magari yao Bandari ya Mombasa badala ya Dar na Tanga?
  • Ni mabilioni mangapi yanapotea kwa kwa watu kupitishia magari yao Mombasa?
  • Nani hajui kuhusu TAX Holiday kwa wawekezaji?
  • CAG report imebainisha madudu ya misamaha ya mabilioni ya Kodi,Je, hiyo nayo TRA hamkubali?
  • Nani hajui kuwa mtu ukiagiza gari toka Japan likifika hapa nchini TRA wanaongeza bei(uplift) kwa madai kuwa bei inayokuwa claimed kwenye docs siyo ya kweli??
  • Nani hajui mgogoro uliopo kati ya TRA Zanzibar na TRA Bara? Kwamba gari ikiingia kupitia Zenj you pay less lakini the same vehicle ikija Bara you pay more???
  • TRA ndiyo the highest payed employees hapa nchini lakini ndiyo the most corrupt people(wala rushwa wakubwa)?
TRA acheni longolongo kusanyeni KODI ili pato la serikali liongezeke na nchi isonge mbele.Pambaf!
 
Hapa lazima kuna jambo. Katika hiyo taarifa ya TRA sijaona mahali palipomtaka Dr. kuthibitisha la sivyo watamshitaki. TRA hawaja thubuti kabisa kuingiza issue ya kumshitaki kabisa ... kama vile hizo tuhuma ni za kweli vile ...
 
Kwa sasa hakuna mwanasiasa anayeaminiwa na kukubalika kwa wananchi kama Dk Slaa,watu wanajua mwizi ni nani
 
TRA hawajambana Dr Slaa bali wemevuma kama debe tupu. Aliyeandika kichwa cha habari cha gazeti hili amevuma pia. Ni mtu mjinga tu ndiye anaweza kuseme TRA wamembana Dr Slaa. Wamagamba mmeshindwa, chama ndo hicho, kinakufa.
 
Hatua zaidi tunataka zichukuliwe. Kutajataja majina hakutusaidii sana. Dr Slaa, tunakutarajia ufanye zaidi.
 
TRA ni vibaka tu hawana lolote.
  • Kwanini watu wanapitishia magari yao Bandari ya Mombasa badala ya Dar na Tanga?
  • Ni mabilioni mangapi yanapotea kwa kwa watu kupitishia magari yao Mombasa?
  • Nani hajui kuhusu TAX Holiday kwa wawekezaji?
  • CAG report imebainisha madudu ya misamaha ya mabilioni ya Kodi,Je, hiyo nayo TRA hamkubali?
  • Nani hajui kuwa mtu ukiagiza gari toka Japan likifika hapa nchini TRA wanaongeza bei(uplift) kwa madai kuwa bei inayokuwa claimed kwenye docs siyo ya kweli??
  • Nani hajui mgogoro uliopo kati ya TRA Zanzibar na TRA Bara? Kwamba gari ikiingia kupitia Zenj you pay less lakini the same vehicle ikija Bara you pay more???
  • TRA ndiyo the highest payed employees hapa nchini lakini ndiyo the most corrupt people(wala rushwa wakubwa)?
TRA acheni longolongo kusanyeni KODI ili pato la serikali liongezeke na nchi isonge mbele.Pambaf!

Makoye upo sahihi kabisa ni mauzauza hapo !
 
Sasa huyo Luoga si ndio iliwahi kusemekana anatarajia kuchukua mikoba ya Kitillya? Kama naye ni fisadi itakuwa balaa...!
 
Si waende mahakamani waone kama hatatoa data za uhakika? Huyu wa ukweli dr ni kama wikileaks atawachemsha hadi basi!
 
Si waende mahakamani waone kama hatatoa data za uhakika? Huyu wa ukweli dr ni kama wikileaks atawachemsha hadi basi!
Hawawezi kuthubutu kwenda mahakamani! Ni wachache sana hapo TRA wenye 'usafi' wa kuthubutu kwenda mahakamani.
 
Back
Top Bottom