TRA 'wambana' Dk Slaa

TRA 'wambana' Dk Slaa

Nilitegemea TRA wangekuja na taarifa ikisema tofauti ikieleza kiundani kuhusu hii ishu sio kumtaka atoe ushahidi..au ndo hadithi ya kuku na yai..
 
TRA wakitaka evidence zipo nyingi sana kwani Hawa jamaa ni wezi hakuna mfano,makampuni ya ujenzi yanaibia nchi alot of money na Kitilya naye fisadi tuu zipu wazi muda wote hakika Rais wa Moyo wangu Dr Slaa hakuna kitakacho kugusa hawa vijimbwa vya Jakaya vinaiba tuu usiku na mchana vinapokea rushwa tuu,hata Mramba ametoa gari ya Million 150 kodi amelipa milion 5 huu wote wizi tuu.TRA WEZI
 
Waende Mahakamani,Ushahidi hautolewi Mitaani!!
Waende kama wana Ubavu huo!!
 
wapenda anasa wametajwa kinawauma sana,matanuzi mtaani hatunywi maji,watu hawana amani na ndoa zao kisa wafanyakazi wa TRA,maana hawa jamaa kama mke wa mtu ni mzuri wanakunyang'anya,dhambi ilioje
 
Sasa TRA wamembana vipi Dr Slaa?........au sioni vizuri labda

Kwa kusema kuwa maelezo aliyoyatoa ni ya UONGO, TRA kama taasisi ya umma haiwezi ikaenda mahakamani kumshitaki mwanasiasa kwa anayoyaongea jukwaani, walichofanya ni kuweka record sawa na kutoa alert kwa wananchi kuwa jamani eh mnalishwa kasa.
 
wapenda anasa wametajwa kinawauma sana,matanuzi mtaani hatunywi maji,watu hawana amani na ndoa zao kisa wafanyakazi wa TRA,maana hawa jamaa kamamke wa mtu ni mzuri wanakunyang'anya,dhambi ilioje

Hizo sasa ni chuki binafsi mkuu, haziendani na hoja iliyo mezani.
 
Basi watoe 'press release' ya kupinga kauli ya Dr. Slaa kama wana ubavu huo.
 
Basi watoe 'press release' ya kupinga kauli ya Dr. Slaa kama wana ubavu huo.

Unataka watoe mara ngapi?

TRA kupitia taarifa yake iliyotolewa na Idara ya Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, imekanusha madai hayo na kuyaita kuwa uzushi tu wa Dk Slaa na kumtaka atoe uthibitisho wa madai yake hadharani.

"Huu ni uzushi unaopaswa kulaaniwa vikali kwa sababu unapotosha wananchi na hasa wasomaji wa magazeti. Dk. Slaa atoe nakala ya hukumu hiyo ili wananchi wamwamini. Bila kufanya hivyo kutaonyesha kuwa ametoa habari za uongo kwa kusingizia mahakama," ilisema taarifa.

Taarifa hiyo ilimtaka Dk. Slaa kutoa vielelezo vya maelezo yake hadharani na kwenye mkutano ili awathibitishie wananchi kuwa alichosema ni cha kweli.

TRA ilisema kama Dk. Slaa atashindwa kufanya hivyo, ni dhahiri kuwa yeye si mtu makini na ni mtu mwenye nia ya kupotosha umma wa Watanzania na kuchafua heshima ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.

"Kudanganya watu kwa siri au hadharani ni aina mojawapo ya aina nyingi za kutokuwajibika. Kutokuwajibika kuna sura nyingi na uongo ni mojawapo. Dk. Slaa lazima ajisafishe na hili," ilisisitiza taarifa ya TRA. Taarifa hiyo ya TRA ilisema Luoga hajawahi kuzuia wala kukamata magari yanayodaiwa na Dk. Slaa.
.
 
Silaa alipotaja wezi hajapindisha maneno, Alitaja watu kwa majina. Sioni kwa nini TRA wanazungukazunguka. Wanachotakiwa kufanya ni kwenda mahakamani vinginevyo wanatafuta pa kuzuga tu
 
Kama wameshatoa basi tutamsubiri Dk. Slaa atoe uthibitisho wake.
 
Kwa kusema kuwa maelezo aliyoyatoa ni ya UONGO, TRA kama taasisi ya umma haiwezi ikaenda mahakamani kumshitaki mwanasiasa kwa anayoyaongea jukwaani, walichofanya ni kuweka record sawa na kutoa alert kwa wananchi kuwa jamani eh mnalishwa kasa.

Na wewe ni mmoja wao nini? Mpelekeni mahakamani kama kasema uongo na kuwachafua.
 
Silaa alipotaja wezi hajapindisha maneno, Alitaja watu kwa majina. Sioni kwa nini TRA wanazungukazunguka. Wanachotakiwa kufanya ni kwenda mahakamani vinginevyo wanatafuta pa kuzuga tu

Mkuu Rais aliyepo kwenye mioyo ya Watanzania anaitwa Dr Slaa,
Na huyu meya wa Ilala ndio anaitwa Silaa
 
ukweli unauma mara zote...sishangai nguvu kubwa isiyostahili kutumikia hapa kwa ajili ya kuficha madudu ambayo yapo wazi...TRA waende mahakamani km wameonewa
 
kwa mi ninavyojua kwenye ishu za kifisadi Dk Slaa hakurupuki na hana chembe hata moja ya kukurupuka kwenye kumwaga dataz za kifisadi...TRA inaingia mkenge sasahv..tm will come
 
Basi watoe 'press release' ya kupinga kauli ya Dr. Slaa kama wana ubavu huo.

Wametoa taarifa kwa umma nimeona hilo tangazo kwenye gazeti la mwananchi la leo ijumaa mei,6 2011
Nanukuu Hitimisho:
"Kwavile Dr.Slaa ametoa maelezo hayo hadharani na waziwazi kwenye mkutano,ni vema atoe vielelezo vya maelezo yake hadharani na kwenye mkutano pia ili awathibitishie wananchi kuwa alichosema ni kweli.
Akishindwa kufanya hivyo basi ni dhahiri kuwa yeye sio mtu makini na ni mtu mwenye nia ya kupotosha umma wa watanzania na kuchafua heshima ya maamlaka ya mapato Tanzania.Kdanganya watu kwa siri au hadharani ni aina mojawapo ya aina nyingi za kutowajibika.Kutokuwajibika kuna sura nyingi na uongo ni mojawapo.Dr slaa lazima ajisafishe na hili.
Mamlaka ya mapato ipo wazi kupokea mawazo,maoni hata kukosolewa na mtu binafsi au taasisi yoyote kaika maeneo yenye kuleta tija.Mamlaka pia ipo wazi katika utoaji wa taarifa mbalimbali za kiutendaji kwa mtu au taasisi kwa mujibu wa sheria za nchi"
Imetolewa na:
Idara ya elimu na huduma kwa mlipa kodi
Mamlaka ya mapato Tanzania
S.L.P 11491
Dar es salaam
Tarehe 5/5/2011
 
Back
Top Bottom