TRA, Road licence mnazodai zinakwamisha ulipaji kodi

Mkuu hawa watu wanalazimisha MAITI kulipa kodi.... kuna jamaa yangu anadaiwa 50m..... unakuta mtu alikuwa na malori anayauza kama vyuma chakavu na leo anadaiwa magari ya tangia 2009..... hapa bila kuonea, hamna mtu anaweza sema gari lake limekuwa scraped kama liko barabarani, hivo kama wanavo update TIN, wange update namba za magari... kama mtu amescrape
gari, aende na barua awaeleze hilo na wao walitoe kwenye system ili wabaki na magari yanayo temebea au amabayo mmiliki anaona yatatembea.... kwa hili wametuumiza sana na
watatuumiza sana.... kwa hili wanalazimisha
MAITI kulipa kodi. ... hata kwenye vitabu takatifu, mmeambiwa mkusanye kodi ya haki.... la sivo mnatenda zambi.....

Nakubaliana na wewe. Ilipaswa kuwe na sheria kama gari hailipiwi leseni miaka mitatu mfululizo basi usajili wake unafutwa. Mwenye gari akitaka kusajili upya ndio apewe huo msala.
 
Hii ya kulipia kwenye mafuta ingesaidia sana both sisi kama wananchi na TRA wenyewe. TRA wangeweza kuongeza hata hayo mapatao. Wananchi wanaomiliki vyombo vya moto. Kulingana sheria ya road license, gharama ya kulipia hutegemeana na ukubwa wa engine ya chombo chako regardless wether kinatumia barabara au la. Sasa najiuliza inawezekanikaje mtu anayemiliki mende anayepaki pale Bunju kusubira order za mchanga alinganishwa sawa na mabasi yaendayo mikoani kila siku kwenye swala zima la ulipiaji wa matumizi ya barabara. Lakini kwenye kulipia indirectly kwenye mafuta ingekuwa fair, jinsi mileage inavyosoma ndo jinsi unavyolipa.
Wazo zuri.sema wabunge wetu wamelala na kusubiria misimamo ya vyama na mamlaka za juu.
 
Mkuu kutoa taarifa ni muhumi tatizo rekodi za gari lako hazikuwa zimefutwa TRA na wewe hukufanya busara baada ya kuliuza kama skepa na haukutoa taarifa huko kwa wazee wa mapato!
 
Mkuu kutoa taarifa ni muhumi tatizo rekodi za gari lako hazikuwa zimefutwa TRA na wewe hukufanya busara baada ya kuliuza kama skepa na haukutoa taarifa huko kwa wazee wa mapato!
wee hiyo sheria unaijua? ipo kwenye kadi ya gari unapotaka ukitaka kuuza gari/kuweka juu mawe/kuuza scraper utoe taarifa? sheria ipo chumbani haijawekwa wazi.kwangu naijuaje?!
 
Halafu hiyo road license fee zamani iliitwa road toll. Sina uhakika kama hiyo kodi iliondolewa kwenye mafuta. Inawezekana kabisa tunalipa hii kodi mara mbili.
Na wabunge wetu wapo kimya kabisa. Siyo wa CCM au UKAWA, wote wako kimya, hawahoji ili kuona namna bora ya kuliendea jambo hili tofauti na sasa ambapo jambo hili halijawekwa sawa. Halafu hii road license kww nini isiwe kama luku? Kwamba ukiwa na gari barabarani unakatwa road toll kupitia mafuta.
Ila kuna mdau alichallenge kuwa kwa kupitia mafuta inakua siyo sawa kwa sababu kuna wafanyabiashara wanamiliki mabasi na malori mengi na wao hununua mafuta IN BULK, je itakuaje? Sikuwa na jibu la moja kwa moja.
 
Niliwahi kusema humu kuna kitu UK kinaitwa SORN yaani statutory off road notification. DVLA (drivers and vehicles licensing agency) kila mara road license yako ikikaribia kuisha wanakutumia form ya ku renew ambapo kuna kifungu cha SORN ambapo unajaza kama gari haitumiki.

Sasa hawa ndugu zetu TRA lazima uwafuate wao kuwalipa kodi na ukitaka chochote lazima uwafuate. Kwanini wasiwaandikie reminder wamiliki? Wana address za kila mmiliki wa gari.

Hizi TIN tutaziacha tutaagiza magari kwa TIN za wengine na biashara zitafanywa kwa majina ya wengine.
 
Binafsi,napenda kushauri wizara husika kuwa karibu na wateja wao yaani walipa kodi Ili marekebisho yafanywe na uwekwe utaratibu wa elimu kwa wananchi ili ulipaji wa kodi kwa mwananchi isiwe kama ni vita baina ya mtoza kodi na mlipa kodi.
 
Kabra ya kuliuza kama Chama chakavu ulipaswa kumwita mkaguzi wa magari toka polisi athibitishe kwamba hiyo gari ni right off na haifai tena kwa matumizi. Baada ya hapo angekujazia form maalum ambayo ungeipeleka TRA,wao wangeifuta kwenye mfumo.
Kwanza elimu juu ya jambo hilo iliwahi kutolewa lini na wapi!?
Pili hata kama hiyo njia ingefuatwa sidhan kama ungepata ushirikiano unaotakiwa, mtu unazungushwa weeee hadi unakasirika kwa kupotezewa muda. Kuna jambo kama Taifa linatakiwa kufanyika ili kuondoa kadhia hii. Na njia ya pekee ni ku start afresh! Yaani kuanza era mpya, mambo ya zamani yawe waived. Litolewe tangazo kuwa wote waliouza magari au kufanya scraper huko nyuma waende wakafute kwenye mfumo, na pia kwa wanunuzi ambao hawajabadili umiliki wafanye hivyo labda ndani ya miezi miwili tu.
Ila hii ya kufukua MAKABURI kwa mambo yaliyopita na kukosewa zamani sidhan kama yana tija.
 
Kodi inaitwa Road License. Sasa kama gari imeharibika na haiko barabarani inadaiwa kodi kivipi? Magari yote yanayotembea lazima yanaonekana barabarani, na kama hayajalipa kodi TRA wana wajibu wa kuyakamata na kuwapiga faini kubwa wanaoyatumia. Tatizo hapa hapa ni hawa watu kung'ang'ania kukaa kwenye mabox. Hawatoki na kufikiria mbinu mpya za kukusanya kodi. Kuwa na gari katika nchi hii imeshakuwa kama dhambi, unatozwa kila aina ya kodi. Kuna kodi hata zinaitwa "fire inspection" lakini wenye magari wanalipa na hawaelewi maana yake nini kwani huwa hawapewi kitu chochote cha tahadhali ya moto. Na ukikamatwa barabarani matraffic wanakupiga faini kwa kuwa na vifaa vya kuzimia moto! Sasa sijui hiyo kodi inakwenda wapi? Ni ujinga mtupu..
 
Tatizo lipo upande wako, hukutoa taarifa TRA
Hii kauli siipendi hata kidogo, kulipa kodi sio mchezo wa kuviziana, TRA wanazo namba za simu za mlipa kodi, anuani ya posta, anuani ya makazi, wamewajibikaje kwa maana "two way traffic of communication" kumwelekeza mlipa kodi kukamilisha miamala.

Hizi anuani huwa wanachukua kama mapambo?

Ni bora wayatoze kodi mawasiliano hayo angalau kwa wale waliopitisha kidogo (mwzi mmoja au 2) muda wa kukamilisha muamala.

Maana kwa kufanya hivyo itakuwa chachu ya wale waliojisahau, itasaidia kuwa na good will kwa mlipa kodi, na inaweza kuongeza mapato kwa tozo ya mawasiliano.
 
Nilinunua gari mwaka 2004 saloon car, kabla ya hapo mmiliki wake wa kwanza alinunua mwaka 1993 Japan gari mpya ilikuwa imetengenezwa mwaka 1992. Niliitumia mpaka 2010 nikauza kama scraper ilikuwa imekwisha thamani.sikutoa taarifa popote.

Wiki iliyopita nilienda TRA kufanyiwa makadirio ya biashara yangu mpya.Nimeambiwa nadaiwa road licence toka ile gari nilivyouza scraper! 2010! Pia hawawezi kukubali makadirio ya biashara yangu mpya mpaka nilipe malipo ya leseni ya barabara hata kama gari iliuzwa kama chuma chakavu!

Mana yake niendelee kufanya biashara bila kukadiriwa mapato mpaka nipate hela za kulipia hizo road licence ambayo gari haikutumia,iliuzwa kama chuma chakavu!

Naomba Rais/waziri wa fedha/commissioner wa TRA Na wizara ya mambo ya ndani waone njia bora ya kupata ufumbuzi wa haya malipo ya uonevu yanayokwamisha mfanyabiashara kukadiriwa na kulipa mapato kwa biashara mpya pia kupunguza mapato ya leseni za biashara kwakuwa TRA hawatoi Business licence Tax clearance certificate/kibali bila kulipa hayo malipo ya uonevu ya road licence hewa!.

Kama hujawahi kutana na hiyo hali TRA hapa pita tu.kwakuwa hutanielewa.

Kila mara tunashauriwa tutoe taarifa mara gari au chombo cha usafiri kilichosajiliwa kinapoondoka barabarani kwa uchakavu au kwa matengenezo na TRA watakifuta kwenye kumbukumbu zao mpaka kurudi barabarani. Ila nawashauri TRA wafanye utaratibu wa kuweka gharama za motor vehicle licence kwenye mafuta ili kuondoa kero hii. Kwa sasa bila shaka wanazo takwimu za mapato yatokanayo na hizi leseni na pia wanazo takwimu za lita za mafuta yanayoingia nchini kwa mwaka. Wanaweza kurekebisha kila mwaka kutegemea na idadi ya vyombo vya usafiri vinavyoendelea kusajiliwa. Wasije wakatuambia kuwa hawawezi hizi hesabu!
 
Niliwahi kusema humu kuna kitu UK kinaitwa SORN yaani statutory off road notification. DVLA (drivers and vehicles licensing agency) kila mara road license yako ikikaribia kuisha wanakutumia form ya ku renew ambapo kuna kifungu cha SORN ambapo unajaza kama gari haitumiki.

Sasa hawa ndugu zetu TRA lazima uwafuate wao kuwalipa kodi na ukitaka chochote lazima uwafuate. Kwanini wasiwaandikie reminder wamiliki? Wana address za kila mmiliki wa gari.

Hizi TIN tutaziacha tutaagiza magari kwa TIN za wengine na biashara zitafanywa kwa majina ya wengine.
mkuu.kweli ni changamoto kubwa.kodi haipaswi iwe regressive pia kumpa taarifa mlipakodi ni muhimu kuliko kusubiri umvizie mpaka aje kwa ishu nyingine umgonge na hiyo.
Kila mara tunashauriwa tutoe taarifa mara gari au chombo cha usafiri kilichosajiliwa kinapoondoka barabarani kwa uchakavu au kwa matengenezo na TRA watakifuta kwenye kumbukumbu zao mpaka kurudi barabarani. Ila nawashauri TRA wafanye utaratibu wa kuweka gharama za motor vehicle licence kwenye mafuta ili kuondoa kero hii. Kwa sasa bila shaka wanazo takwimu za mapato yatokanayo na hizi leseni na pia wanazo takwimu za lita za mafuta yanayoingia nchini kwa mwaka. Wanaweza kurekebisha kila mwaka kutegemea na idadi ya vyombo vya usafiri vinavyoendelea kusajiliwa. Wasije wakatuambia kuwa hawawezi hizi hesabu!
 
Kila mara tunashauriwa tutoe taarifa mara gari au chombo cha usafiri kilichosajiliwa kinapoondoka barabarani kwa uchakavu au kwa matengenezo na TRA watakifuta kwenye kumbukumbu zao mpaka kurudi barabarani. Ila nawashauri TRA wafanye utaratibu wa kuweka gharama za motor vehicle licence kwenye mafuta ili kuondoa kero hii. Kwa sasa bila shaka wanazo takwimu za mapato yatokanayo na hizi leseni na pia wanazo takwimu za lita za mafuta yanayoingia nchini kwa mwaka. Wanaweza kurekebisha kila mwaka kutegemea na idadi ya vyombo vya usafiri vinavyoendelea kusajiliwa. Wasije wakatuambia kuwa hawawezi hizi hesabu!
mkuu hiyo taarifa kuwa kila mara tunaambiwa sio kweli.natumia magari kwa kipindi kisichopungua miaka 20.mwezi uliopita ndio nimejua hayo.nimeenda TRA hata wafanyakazi wanalalamika kukumbwa na hiyo hali.nani alikuwa anaelimisha hilo darasa ambalo hata wafanyakazi TRA wanalia pia?!
 
hivi unaelewa ninavyokwambia hata wafanyakazi wa TRA ni Victim wanakiri ni janga la kitaifa.ina maana hawakuwa wanainforce hayo malipo awali.mpaka walivyopewa muongozo juzi hapo
Mi sipinganii NA mwongozoo hats kidogoo ..we lalamikia awakuwapa somo ama elimu non cha kufanya huko nyuma bytheway Mpwa ..so ubadilishe tin ama tumia tin ya mkeooo unapata safi Leseni.......
 
Njia bora ya kulipia MV Licence ni kuiweka hii kodi kwenye mafuta ili gari zinazotembea zilipe kodi kupitia ununuzi wa mafuta.
Hakunachamafuta pelekeni kodi serikaliin badaaaaa elimuu bureee wanasaidiaje shule sikodizenu banaa tukalipe tu atuna jinsi
 
Back
Top Bottom