TRA ni taasisi ya kukosa network kweli?

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
4,271
2,401
Nimekuwa nafuatilia masuala yangu TRA (sisemi ni wapi) hapa Dar. Wakati wahudumu wakiendelea na huduma unasikia wanasema subiri network irudi. Hapo majukumu inabidi yasimame hadi network ikae tena sawa. Ikifika hapo baadhi ya wateja huamua muahirisha kilichowapeleka pale.

Hili nimekumbana nalo siku mbili mfululizo. Ina maana ndio kawaida kwa mtandao kusumbua TRA.

Katika ulimwengu huu wa leo kweli taasisi kama TRA wanasumbuliwa na network? Wanakwamisha huduma kisa mtandao uko chini au umekata? Kweli? Na hela zote mnazokusanya hata kama zinaenda serikali kuu, hamna fungu la kutatua hiyo kero? Mnatia aibu kwa kweli.

Mtu anafika TRA kwa hofu kama anaingia kituo cha polisi. Basi mfanyieni huduma yake kwa ufanisi mkizingatia muda. Hakuna anayetaka kushinda humo ndani maana si sehemu rafiki sana.

Ukiwatazama hata wakadiriaji wenyewe wamekaa kivitisho vitisho tu. Hadi uongee na ndio ujue ni rafiki au la, ila wengi wanaogofya. Mamlaka husika fanyieni kazi hilo suala la mtandao ASAP!
 
Kuna mfanyakazi mmoja wa TRA niliwahi kumtishia balaa, yaani nimepewa control number ya kufanya malipo ndani ya miezi 6...yeye kutwa simu mbona ujafanya malipo.
Siku ya kwanza nilimsikiliza ..siku ya pili nikamsikiliza ...siku ya tatu alipopiga simu nilimkomesha na ndo ikawa mwisho wa kunipigia simu Tena.
 
Binafsi suala la Network problem kule TRA nimeshalizoea kiasi kwamba nikifika Ofisi ya TRA nikakuta Network iko sawa ndiyo napigwa na Butwaa.

Mpaka kuna nyakati nikajawa na hisia huenda ni mchezo wao kutusubirisha ili waweze Kuchat na wapendwa wao kwenye Simu..
Hata mimi nilihisi ni mpango wao kuzubaisha wateja na kusababisha urasimu usio na tija
 
Nimekuwa nafuatilia masuala yangu TRA (sisemi ni wapi) hapa Dar. Wakati wahudumu wakiendelea na huduma unasikia wanasema subiri network irudi. Hapo majukumu inabidi yasimame hadi network ikae tena sawa. Ikifika hapo baadhi ya wateja huamua muahirisha kilichowapeleka pale.

Hili nimekumbana nalo siku mbili mfululizo. Ina maana ndio kawaida kwa mtandao kusumbua TRA.

Katika ulimwengu huu wa leo kweli taasisi kama TRA wanasumbuliwa na network? Wanakwamisha huduma kisa mtandao uko chini au umekata? Kweli? Na hela zote mnazokusanya hata kama zinaenda serikali kuu, hamna fungu la kutatua hiyo kero? Mnatia aibu kwa kweli.

Mtu anafika TRA kwa hofu kama anaingia kituo cha polisi. Basi mfanyieni huduma yake kwa ufanisi mkizingatia muda. Hakuna anayetaka kushinda humo ndani maana si sehemu rafiki sana.

Ukiwatazama hata wakadiriaji wenyewe wamekaa kivitisho vitisho tu. Hadi uongee na ndio ujue ni rafiki au la, ila wengi wanaogofya. Mamlaka husika fanyieni kazi hilo suala la mtandao ASAP!
Nilipoteza vyeti vyangu vyote, nikaambiwa niende polisi . Nilikwenda mara tatu bila mafanikio kwani internet haiko. ( kituo cha polisi oysterbay)
 
Back
Top Bottom