Changamoto zinazoikabili Taasisi ya Teknolojia ya Dar (DIT) zinazopelekea ishindwe kuchangia kikamilifu Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii Tanzania

w0rM

Member
May 3, 2011
51
145
UTANGULIZI

Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam almaarufu kama DIT ni moja ya vyuo vikongwe sana hapa nchini, chuo hiki kimetoa wataalamu mbalimbali kuanzia mafundi mchundo mpaka wahandisi katika kada mbalimbali. Ni ngumu kumkosa mtaalam kutoka DIT katika Taasisi yoyote ya Serikali na ya binafsi ndani ya Tanzania. Hii ni kutokana kwamba siku za nyuma elimu iliyotolewa katika taasisi hii ilikuwa ya vitendo zaidi. Kauli mbiu ya Serikali yetu ambayo pia imekuwa kauli ya nchi nzima ni kufikia Uchumi wa kati unaochochewa na Viwanda.

Ili kuwezesha maendeleo endelevu katika taifa letu ni lazima taasisi kama hii iwe na mchango mkubwa siyo tu katika kupika wataalamu wa Tanzania ya viwanda lakini pia kuibua bunifu zenye tija na zenye kuweza kutatua changamoto mbali mbali zinazolikabili taifa letu. Kwa sasa zipo changamoto nyingi zinazohafifisha uwezo wa Taasisi hii katika kuchangia maendeleo ya Taifa, changamoto hizi zimechambuliwa kwa kina na kutolewa maelezo na ushahidi wa kutosha lengo ikiwa ni kuifungua Serikali macho iweze kusimamia mabadiliko yanayohitajika na hatimaye Taasisi hii iweze kuleta mchango chanya kwa kizazi cha sasa na kwa vizazi vijavyo.

Hivi karibuni DIT imepata mkopo wa Bilioni 74 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kuanzisha vituo viwili vya umahiri wa Tehama pamoja na uchakataji wa mazao ya ngozi. Hili ni deni kubwa sana kwa Taifa letu na kwa walipakodi wa Tanzania. Endapo hatua za haraka hazitachukuliwa kubadili hali ya mambo, pesa hizi zitapotea na hazitaleta tija stahiki kwa Taifa.

Ripoti hii inaanza kwa kuainisha matatizo mbali mbali sugu yaliyopo DIT kwa ushahidi. Baada ya kuonyesha changamoto zilizopo pia inatoa historia ya matatizo sugu ya DIT, namna ambavyo uongozi wa sasa umeendelea kuchangia katika hayo matatizo, na inaainisha kuhusu uhitaji na umuhimu wa kuchukuliwa hatua za dhati kuinusuru DIT, na mwisho kabisa inatoa mapendekezo ya hatua stahiki zinazopaswa kuchukuliwa katika hatua ya awali ili kuinusuru DIT.


Changamoto za DIT​

DIT inakabiliwa na changamoto kadhaa zinazohafifisha ubora na zinazoathiri upatikanaji wa elimu inayojikita zaidi katika vitendo (competence based). Hatuwezi kuzungumzia Tanzania ya viwanda bila kutilia maanani na mkazo elimu ya vitendo na elimu yenye kutatua changamoto za jamii yetu. Kwa muda mrefu huko nyuma DIT imekuwa ndiyo kiinua mgongo au alama ya elimu ya ufundi kwa vitendo katika taifa letu, alama hii kwa sasa iko taabani na inafifia kutokana na changamoto kadhaa. Baadhi ya changamoto sugu zinazoikabili DIT zimeainishwa hapa chini:

i. Ucheleweshwaji wa vifaa vya kufundishia (Teaching materials)

Kwa Taasisi kama DIT, suala la vifaa vya kufundishia ni suala la msingi na la kipaumbele pengine kushinda suala lolote lile. Hapa DIT suala la vifaa vya kufundishia limeendelea kuwa tatizo kwa muda mrefu na bajeti inayotengwa kwa ajili ya suala hili kilamwaka haiendani na uhalisia. Mfano, kitendo cha Taasisi kukosa vifaa vya kufundishia kwa muhula ulioanza 1/6/2020 mpaka 14/9/2020 siyo kitendo kizuri, waalimu wamelazimika kufundisha katika mazingira magumu sana vitu kama chaki, karatasi na marker pen hazikupatikana, hata kalamu za kusahihishia wafanyakazi wamelazimika kutafuta mabaki ya siku za nyuma na wengine kujinunulia kwa pesa zao mifukoni. Kwa upande wa vifaa vya maabara katika muhula huu vimechelewa sana kufika na vifaa vilivyostahili kuanza kutumika wakati wa mazoezi kwa vitendo vimeletwa mwishoni kabisa mwa muhula wakati wanafunzi wanakaribia kuanza mitihani hali iliyopelekea wanafunzi kukosa mazoezi ya vitendo ya kutosha.

ii. Ukosefu wa mtandao (Internet) kwa wanafunzi​

Katika karne ya 21 inastaajabisha kwa taasisi tena ya teknolojia kukosa kuwapatia wanafunzi wake huduma ya mtandao, teknolojia kwa sasa inapiga hatua kwa kasi sana, hivyo ili wanafunzi wetu waendane na kasi hiyo ni lazima wapate nafasi na uwezo wa kuangalia yanayoendelea duniani. Rais Magufuli wakati wa Uzinduzi wa Bunge la 12 jijini Dodoma alisikika akisisitiza DIT itakuwa Kitovu cha tehama Tanzania; hili linahitaji taasisi hii kuwa connected vema. Wakati mwingine elimu inyotolewa kwenye mitandao ina ubora kuzidi vitini wanavyotoa walimu wetu ambavyo wakati mwingine vimepitwa na wakati na haviendani na uhalisia wala mahitaji ya soko la ajira. Kitendo cha wanafunzi wa DIT kukosa Mtandao si kizuri, wataalamu wanaoandaliwa lazima wawe na uwezo wa kulinganisha na kujifunza yanayofanywa na wenzao duniani. Kinyume cha hapo itakuwa teknolojia ya makaratasi ambayo haitakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na kutatua changamoto za kwenye jamii.

iii. Ukosefu wa mtandao kwa waalimu

Tatizo la mtandao DIT siyo tu kwa wanafunzi, pia kwa waalimu wa DIT suala la mtandao limekuwa kama anasa kwa walimu, mtandao umekuwa wa kusuasua mara kadhaa na wakati mwingine waalimu wamekaa bila mtandao hata kwa wiki mbili kutokana na shida ndogo ndogo kama za AC kwenye vyumba vya kuhifadhia mitambo ya mtandao (server room). Pia kumekuwa na matatizo endelevu mfano katika jengo la mnara wa ufundishaji (teaching tower) hakuna mfumo wa kompyuta katika jengo lote, hii inamaanisha hakuna mtandao jengo zima. Inashangaza kwamba iliwezekanaje jengo kubwa kama hilo kujengwa DIT bila kuwekewa mifumo ya mawasiliano na yawezekana Serikali inayajua haya yote. Maswali yakiulizwa kuhusu maswala hayo majibu yake ni 'Mradi mkubwa wa Benki ya Dunia', eti mradi huo ndio utakuwa suluhisho la matatizo yote ya DIT. Wahadhiri na waalimu wanalazimika kutumia fedha zao za mifukoni ili kuwezesha upatikananji wa mtandao kwa ajili ya shughuli za taasisi, huku uongozi ukiwa kimya.

iv. Ubovu na uchache wa madarasa ya kufundishia​

Madarasa mengi ya DIT ni mabovu sana yaani hakuna maintenance, yamechakaa utadhani hayapo katika taasisi ya teknolojia, unaweza ukafikiri ni magofu yaliyositishwa kutumika miaka kadhaa iliyopita, awali vijana wengi wa kitanzania wanajisikia ufahari wanapochaguliwa kujiunga na DIT lakini wanapofika mazingira yanawakatisha tamaa na kuwafanya wajione hawawezi kufanya kitu kizuri wala kikubwa. Wanashindwa kuelewa umuhimu wa kusoma uhandisi ambao hauwezi kutumika kutatua changamoto zinazowakabili katika mazingira yao ya DIT. Hii ni moja ya sababu inayopelekea wanafunzi wengi kusoma kwa ajili ya maksi tu na wanashindwa kuthubutu kufanya vitu vikubwa maana hawana imani kama inawezekana kufanya vitu vikubwa.

Screenshot 2020-11-17 at 06.19.15.png


Katika jengo jipya la mnara wa ufundishaji (teaching tower) yapo madarasa hayana samani wala ubao jengo hilo lilizinduliwa rasmi mnamo 18/4/2018, lakini hadi leo tarehe 24/9/2020 hakuna kilichofanyika kubadili hali hiyo. Baadhi ya madarasa yasiyokuwa na samani angalia Picha 2 chini. Masuala ya kutafakari ni kuwa garama za kuweka samani katika baadhi ya vyumba inagharimu fedha kubwa kiasi gani na gharama kiasi gani zinahitajika kufanya marekebisho ya madarasa ya zamani ili kufanya mazingira ya usomaji yawe rafiki kwa wanafunzi wetu. Hapa ikumbukwe kuwa DIT ni taasisi inayopika na inayotoa mafundi na wahandisi katika maeneo yote hayo yenye changamoto.

Screenshot 2020-11-17 at 06.21.02.png


v. Uchakavu na upungufu wa mashine na vifaa vya maabara vya kuwezesha mazoezi ya vitendo

Maabara za kufanyia mazoezi kwa vitendo DIT zimechoka kupita maelezo, vifaa vingi katika maabara hizo ni vifaa vya kizamani sana vifaa vipya ni kama havipo. Tukichukulia idara ya mitambo (Mechanical Engineering) kama mfano, mashine nyingi sana katika idara hiyo ni za kizamani sana, pamoja na uchakavu wa vifaa hivyo pia ripea za mara kwa mara ambazo ni muhimu ili kurefusha muda wa mashine kutumika imekosekana kwa muda mrefu sana. Mfano ukitembelea maabara ya uchomeleaji vyuma (welding), maabara ya mashine (machine shop), maabara ya magari (automobile workshop), maabara ya majokofu (refregeration ), maabara ya nishati (power plant), na maabara ya kufua chuma (foundry) katika idara ya ufundimitambo, utagundua kuwa hizi maabara zote ziko katika hali mbaya sana mashine nyingi zimepitwa na wakati na mashine nyingi zimekufa, au ziko karibu kufa. Baadhi ya mitambo iliyochoka angalia Picha 3 chini.

Screenshot 2020-11-17 at 06.22.58.png

Screenshot 2020-11-17 at 06.23.14.png


Idara ya mitambo ni moja ya idara ambazo wakati DIT inaanzishwa zilikuwa zinaibeba DIT hasa kutokana na mchango mkubwa katika jamii, lakini kwa sasa karibia inakufa kutokana na uchakavu wa maabara na upungufu mkubwa wa rasilimali watu wenye weledi na wabobezi. Kimsingi maabara hizi zimekuwa kama madampo ya vyuma chakavu. Wahusika wamejaribu kuelezea ukweli huu kwa viongozi wakuu wa taasisi lakini hakuna hatua zimechukuliwa ili kubadili hali hii.

vi. Ukosefu wa vitendea kazi kama kompyuta kwa wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa Taasisi​

Moja kati ya changamoto kubwa sana kwa wafanyakazi wa DIT hasa walioajiriwa ndani ya miaka kama sita iliyopita ni ukosefu wa vitendea kazi. Moja ya kitendea kazi kikubwa sana kwa mwalimu hasa kwa karne hii ni kompyuta ambayo humuwezesha mwalimu kuandaa mada za kufundisha, kuandaa mitihani, pamoja na kupandishia matokeo kwenye mtandao baada ya kusahihisha. Kuna wafanyakazi ambao wamekaa DIT kwa takriban miaka sita sasa bila kuwa na kompyuta, uongozi wa juu wa taasisi unafahamu uhalisia wa jambo hili lakini hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa kutatua changamoto za waalimu.

Uongozi unawaagiza waalimu kutunga, kusahihisha na kupandisha matokeo ya wanafunzi huku wakijua uhalisia kuwa waalimu hawana vitendea kazi. Nalo hili suluhisho lake ni mradi wa benki ya dunia, yaani kwa sasa kila kitu DIT kinasubiri mradi wa benki ya dunia. Hapa pia tunaona ukosefu wa Vipaumbele.

Kwa upande wa wanafunzi hali ya mambo ni mbaya zaidi. Maabara karibia zote za kompyuta DIT zimekufa, tukianza na maabara ya Idara ya Mawasiliano ya anga ambayo ilikuwa imejaa kompyuta kipindi cha nyuma, hizo kompyuta zote zimekufa na hadi sasa hakuna hata kompyuta moja kwa ajili ya wanafunzi kutumia kufanyia mazoezi, ama za kutumika wakati wa kufundishia hasa kwa yale masomo yanayohitaji kompyuta. Vivyo hivyo maabara ya kompyuta iliyokuwa Idara ya Umeme, Idara ya Ujenzi, Idara ya Kompyuta pamoja na maeneo mengine ya Taasisi nyingi zimekufa. Baadhi ya maabara hizo zimeonyeshwa katika Picha 4,5,6 chini.

Sote tunafahamu uhalisia kuwa familia nyingi za kitanzania ambazo wanafunzi wengi wa DIT wanatoka ni masikini na hazina uwezo wa kuwanunulia watoto wao kompyuta, hivyo ufanisi wa wanafunzi kusoma teknolojia hasa kwa vitendo ni hafifu.

Screenshot 2020-11-17 at 06.27.14.png
Screenshot 2020-11-17 at 06.27.27.png
Screenshot 2020-11-17 at 06.28.59.png


vii. Ubovu, uchakavu, na ufinyu wa nafasi katika ofisi ya mitihani

Moja ya vitu vya msingi sana katika Taasisi yoyote ya elimu ni mitihani maana ndiyo njia ya moja kwa moja ambayo imetumika kupima uwezo wa wanafunzi kwa miaka mingi, hivyo kwa taasisi ambayo ina viongozi makini na wanaotoa kipaumbele katika ubora wa elimu lazima ofisi ya mitihani iwe na ubora unaostahili. Hapa DIT mambo ni tofauti, ofisi ndogo ambayo ilitumika tangu enzi za DTC wakati wanafunzi walipokuwa wachache ndiyo inayotumika mpaka sasa, ofisi ni finyu sana na imechakaa sana haina hadhi hata ya kuitwa ofisi ya mitihani, ukiingia unaweza kudhani ni stoo. Hapa karibuni takriban mwezi kabla ya mitihani ya muhula wa pili 2019/2020 kuanza, mvua iliharibu baadhi ya nyaraka maana paa lilichakaa mpaka likawa linapitisha maji na kupelekea kuloa kwa baadhi ya nyaraka hizo. Baada ya nyaraka kuloa ndipo ofisi ya mitihani imefanyiwa marekebisho ya paa. Hii inaonyesha moja kwa moja ukosefu wa vipaumbele katika taasisi. Masuala ya msingi kama hayo hayashughulikiwi mpaka madhara yatokee. Mpaka tunavyoongea tofauti na suala la paa bado ofisi imechakaa sana na ni finyu, ni aibu hata kukiita kile chumba ofisi ya mitihani ya DIT, taasisi inayoandaa wataalamu kwa ajili ya kutumika nchini lakini inashindwa kuwatumia wataalamu wake hao hao kutatua changamoto zake yenyewe.

viii. Changamoto katika kusimamia uthibiti wa ubora wa elimu(Quality assurance and Quality control)​

Ubora wa elimu limeendelea kuzorota sana DIT, uongozi unadhani kuwa ubora wa elimu unaangaliwa tu wakati wa usimamizi wa mitihani. Hii ndiyo maana vifaa vya kufundishia vinaweza kuchelewa na hakuna anayejali. Sote tunafahamu kuwa ubora unachangiwa na mambo mengi mojawapo ikiwa ni suala la mazingira elimu inapotolewa, suala zima la ufundishaji hasa uwepo wa elimu kwa vitendo na mwisho ndipo suala la mitihani linafuata. Changamoto za DIT zinavuruga ubora kwa kuwa maeneo yote matatu ya msingi yaliyotajwa yana shida.

Nitoe mfano mdogo tu wa namna ambavyo mazingira yanaweza kuharibu ubora wa elimu hasa katika kipengele cha mitihani ambacho ndicho uongozi uliopo wa DIT unatilia maanani kama kigezo pekee cha ubora. Muhula wa kwanza 2019/2020 kabla ya janga la Korona wanafunzi wetu walifanya majaribio endelevu (continuous assessment) pamoja na baadhi ya mitihani ya mwisho katika bwalo kubwa la chakula, wakati huo feni katika bwalo hilo zilikuwa zimeharibika. Kutokana na ubovu wa feni hizo wanafunzi walilazimika kutoka nje mara kwa mara wengine hata kujimwagia maji vichwani ili kurudisha bongo zao katika utulivu kabla ya kuendelea na mitihani. Kwa upande wa wasimamizi walijikuta wanakaa karibu tu na milango au madirisha ili walau kupata hewa safi kutoka nje. Maana yake ni kwamba wasimamizi walikuwa hawasimamii kama ilivyostahili lakini haikuwa kutokana na utashi wao bali mazingira yaliwalazimisha.

Feni hizo zilikaa katika ubovu huo kwa kipindi cha zaidi ya mwaka bila kufanyiwa matengenezo stahiki, ikumbukwe kuwa DIT ni taasisi ya teknolojia ambayo inatoa wataalamu wa umeme kwenda kutataua matatizo ya jamii maeneo mbalimbali Tanzania, hivyo inashangaza kuona taasisi inashindwa kutataua matataizo yake madogo kama swala la feni kwa zaidi ya mwaka mzima.

ix. Kudorora kwa maswala ya utafiti na ushauri wa kiufundi​

Moja ya majukumu muhimu sana kwa wahadhiri wa taasisi za elimu ya juu katika taifa letu ni kushiriki kufanya tafiti zenye tija na zenye kuleta suluhisho la matatizo mbali mbali tuliyonayo katika jamii. Ili haya yawezekane ni lazima mazingira ya kufanyia kazi yawe rafiki kuwezesha utafiti kufanyika, ni dhahiri kwamba kama mhadhiri mwenye (PhD) anakosa japo compyuta ya kufanyia kazi za kawaida ofisini basi siyo rahisi akapata uwezeshaji mwingine unaostahili ili aweze kufanya utafiti wenye tija na manufaa kwa taifa. Kwa namna nyingine ni dhahiri kwamba kama mazingira ya kawaida tu ya kufundishia na uwezeshaji wa kawaida tu ili kumuwezesha mwalimu kufundisha kwa weledi haiwezekani, basi ni ndoto kwa utafiti wenye tija kufanyika.

Bajeti inayotengwa kwa ajili ya kazi za utafiti ni karibia na hakuna, na ikitoke kikatengwa hata kiasi ch asilimia 1 hakitolewi kwa ajili ya shughuli hizo, hivyo ni dhahiri kuwa hakuna dhamira ya kweli ya kuwezesha utafiti. Pia kutokana na uchache wa wafanyakazi DIT mhadhiri anajikuta anafanya kazi hata za msaidizi wa maabara wakatimwingine na kazi za msaidizi wa mhadhiri pia anafanya yeye hivyo kunakosekana muda wa kutosha wa wahadhiri kujihusisha na utafiti.

Kwa upande wa ushauri wa kiufundi kumekuwa na changamoto nyingi sana. Changamoto kubwa kuliko zote ni mtazamo hasi wa mkuu wa taasisi juu ya ushauri wa kiufundi (consultancy) mkuu aliyepo DIT kwa sasa anabeza majukumu ya ushauri wa kiufundi anasema kazi za ushauri wa kiufundi ni pesa nyepesi (cheap money) anasahau kuwa taasisi kubwa sana ya utaalamu wa kiufundi kwa vitendo katika Tanzania ni DIT na ina utofauti ukilinganisha na chuo kikuu cha dar es salaam ambacho ni mrengo wa nadharia zaidi. Hivyo DIT ipo katika nafasi nzuri sana ya kutoa ushauri wa kiufundi unaotokana na uzoefu wa kazi za vitendo na hilo ni jukumu tanzu kabisa la DIT. Hivyo mazingira ya wahadhiri wa DIT kushiriki katika kazi za ushauri wa kiufundi yameendelea kuwa magumu, hili linazorotesha hata uwezo wa wahadhiri kutoa elimu yenye ubora kwa weledi, maana sote tunafahamu kuwa ili kuwa na elimu bora ya vitendo ni lazima mhadhiri awe na mahusiano mazuri na endelevu na viwanda, hii itamuwezesha kujua teknolojia mpya na kuweza kujua mambo gani yamebadilika na namna tofauti ya kufanya vitu kwa umahiri. Kimsingi ukimchukua mhadhiri ambaye anahusika kufanya kazi za mtaani ukamlinganisha na yule ambaye anaishia kufundisha chuoni pekee, utakuta kuna tofauti kubwa sana hasa kwenye ubora wa elimu ambayo wanaitoa na hiyo iko wazi hata kwa wanafunzi. Walau kipindi hiki kuna baadhi ya wahadhiri wameenda viwandani kwa ajili ya mazoezi kwa vitendo (Industrial attachment) lakini ni kutokana na mradi wa Benki ya Dunia.

x. Upungufu wa rasilimali watu (Human resource) na manyanyaso kwa wafanyakazi​

Moja ya changamoto kubwa sana zinazoikabili DIT ni upungufu mkubwa wa rasilimali watu, Wakufunzi wengi sana wamestaafu bila kuwepo na mpango wa urithishwaji ujuzi mzuri, changamoto hii imekuwepo kwa muda mrefu sana katika idara nyeti za DIT kama Umeme, Mitambo, Ujenzi na idara zingine. Kwa upande mwingine wafanyakazi wengi sana wamehama DIT katika miaka ya hivi karibuni (2016-2020) kutokana na mazingira magumu ya kufanya kazi, kimsingi wafanyakazi wengine waliopo DIT wameomba kuhama lakini wamekataliwa na wizara kwa madai kwamba DIT haina wafanyakazi wa kutosha. Takriban wafanyakazi wanne kutoka katika ofisi ya idara ya rasilimali watu wamehama DIT, kimsingi idara hiyo ndiyo inapaswa kuleta chachu na kuwezesha wafanyakazi wengine watamani kuendelea kufanya kazi DIT lakini wao wenyewe hawana matumaini na wanahama. Unapoona wanaopaswa kuhamasisha wafanyakazi kuendelea kufanya kazi wanahama unagundua kuna tatizo kubwa sana DIT. Kwa sasa asilimia kubwa ya wafanyakazi wa DIT wangeulizwa kama wanatamani kuendelea kubaki au waondoke DIT zaidi ya asilimia tisini wangechagua kuondoka.

Tatizo lingine kubwa katika idara ya rasilimali watu ni ucheleweshwaji wa kupandisha watu madaraja hasa wafanyakazi wanapotoka masomoni. Kwa DIT kuna changamoto kubwa sana inayokatisha tamaa wafanyakazi, zipo hatua kadhaa za ndani ya DIT ambazo maranyingi huchelewesha mchakato wa kumpandisha daraja mtumishi. Mtumishi anpotoka shule anaweza akakaa hata Zaidi ya mwaka bila kupata barua ya uthibitisho wa ndani ya taasisi hata kama tayari ametimiza vigezo vyote vya uthibitisho kutoka TCU, tangu uongozi wa sasa wa DIT uingie madarakani tatizo hili limekuwa sugu sana na hii imepelekea watumishi wengi kukata tamaa kabisa.

Kuna wakati mtumishi anakuwa amepewa majukumu yanayoendana na cheo kipya ilhali hata barua ya ndani ya taasisi hajapatiwa ya kuthibitisha cheo hicho. Yaani kwa DIT watumishi wanateseka sana baada ya kutoka masomoni kana kwamba hawana haki katika taifa lao. Ikumbukwe kuwa wafanyakazi wa DIT wanapokwenda masomoni wanakutana na wenzao wanaotoka katika taasisi nyingine za Elimu ya Juu na taasisi nyingine za Serikali, cha ajabu ni kuwa wanaporudi wote kwa vipindi karibia vinavyofanana wale wafanyakazi wa taasisi nyingine kama UDSM, MUST na maeneo mengine wanakuwa wameshapata stahiki zao na hata mishahara yao inakuwa imeshapanda lakini kwa watumishi wa DIT inakuja kuchukua takriban miaka miwili na zaidi kwa hilo kutokea.

Mfano, mmoja kati ya watumishi alikabidhi vyeti baada ya kutoka masomoni na kuthibitishwa na TCU Disemba 2018 lakini mpaka sasa takriban mwaka na miezi minane hajapandishwa mshahara, yote ni kutokana na uzembe wa wahusika wa DIT maana hata barua ya ndani ya taasisi ya kumkubali kuwa Mhadhiri ameipata mwaka huu mwezi wa nne. Cha kustaajabisha zaidi ni kuwa wapo wafanyakazi kutoka taasisi nyingine ambao wamerudi mwaka jana katikati na wengine mwishoni lakini tayari kumekuwa na mabadiliko kwenye mishahara yao. Uzembe wa ndani ya taasisi unasababisha serikali ilaumiwe kwa kutopandisha madaraja na hivyo inabebeshwa mzigo isiyostahili.

Viongozi wa idara ya rasilimali watu wamekuwa wakilalamika kuwa Mkuu wa Taasisi hatoi ruhusa na wala haidhinishi fedha za kuiwezesha Idara kufuatilia masuala ya wafanyakazi kwa ukaribu Dodoma. Idara ikitaka kufanya ufuatiliaji na linapokuja suala la pesa mkuu wa taasisi anasema ataenda kushughulikia masuala ya wafanyakazi yeye mwenyewe akiwa Dodoma lakini mara zote hafuatilii wala kuyashughulikia akiwa Dodoma. Kimsingi ni kama anataka maisha ya watu wote DIT yawe magumu ili aendelee kuabudiwa maana yeye amejiweka kama Mungu wa DIT.

INAENDELEA...
 

w0rM

Member
May 3, 2011
51
145

xi. Upungufu wa ofisi kwa ajili ya wafanyakazi

Kuna upungufu mkubwa sana wa Ofisi kwa ajili ya wafanyakazi wa DIT, hata kwa hizo ofisi chache zilizopo mazingira yake ni mabovu na samazi zilizopo zimechoka. Kimsingi kwenye ofisi nyingi kuna mrundikano mkubwa wa watu hali inayopelekea ukosefu wa utulivu unaostahili ili kuwawezesha wahadhiri kufanya kazi zao kwa weledi na utulivu wa akili unaostahili. Ikumbukwe kuwa tofauti na majukumu ya kufundisha mhadhiri ana majukumu ya kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kiufundi. Haya yote ni majukumu makubwa yanayohitaji eneo lenye utulivu ili kufanya kazi kwa weledi.

xii. Ubovu wa vyoo kwa waalimu na wanafunzi​

Pamoja na kuwafundisha wanafunzi wetu umahiri wa teknolojia ni lazima pia kuwafundisha ustawi na ustaarabu wa kijamii ili waweze kuleta mchango chanya katika nyanja zote za maendeleo katika taifa letu. Tunapozungumzia ustawi na ustaarabu wa jamii mazingira yetu ni sehemu ya kwanza muhimu ya kutufundisha na kuwafundisha vijana wetu. Suala la choo ni suala muhimu sana katika sehemu yoyote ambayo binadamu wanaishi na nimuhimu vyoo viwe katika hali nzuri kila wakati. Kwa DIT mazingira ya vyoo yamekuwa mabaya kwa muda mrefu sana, ni kana kwamba kupata huduma nzuri za vyoo ni anasa. Ukipita kwenye vyoo wanavyotumia wanafunzi wetu ndiyo aibu kabisa, vyoo vya DIT vinadhohofisha na kutweza utu wa waalimu Pamoja na wanafunzi wetu. Baadhi ya vyoo vya wanafunzi DIT vimeonyeshwa kwenye Picha 7,8 chini.

Screenshot 2020-11-17 at 06.40.41.png

Screenshot 2020-11-17 at 06.41.50.png


Mwanafunzi wa kitanzania anapochaguliwa kujiunga na DIT anajisikia ufahari sana lakini akifika katika mazingira ya DIT anakatishwa tamaa maana anafundishwa kwenda kutatua changamoto za jamii ilhali mazingira anayofundishiwa yana changamoto nyingi sana ambazo hazitatuliwi kutumia ujuzi huo huo.

Katika jengo jipya la mnara wa ufundishaji kumekuwa na matatizo mengi sana yanayohusu vyoo, ikumbukwe kuwa jengo lilianza kutumika April 2018 lakini kutokana na kukaa kwa muda mrefu bila kukamilika vipo vifaa vilivyokuwa vimekwisha chakaa wakati jengo linazinduliwa. Mfumo wa maji wa kusukuma uchafu katika takriban asilimia 80 ya vyoo katika jengo hilo vilikuwa tayri ni chakavu wakati jengo linazinduliwa, hii ilipelekea vyoo vingi sana kufungwa. Hata vile ambavyo havikufungwa iliwalazimu watu kutumia makopo ya kawaida na doo za kawaida katika kujihudumia. Pia vyoo katika jengo hilo vimekuwa na shida kubwa sana ya maji mara kwa mara hali inayohatarisha afya ya watumiaji wa jengo.

Kutokana na kusuasua kwa upatikanaji wa maji katika jengo pamoja na ubovu wa mifumo ya kusafisha taka, wanafunzi wetu wamezuiwa mara zote kupata huduma katika vyoo hivyo. Wahusika huakikisha wakati wa mitiani na wakati wa kusoma vyoo vinafungwa ili wanafunzi wasitumie kwa kigezo kwamba wanafunzi watachafua vyoo. Hivyo haijalishi mtihani unafanyika ghorofa ya tisa au kumi, mwanafunzi akipata shida ya choo hulazimika kushuka mpaka kwenda kwenye jengo la pembeni ili kupata huduma ya choo na hatimaye ndipo arudi kuendelea na mtihani au masomo. Huu ni unyanyasaji na ukatili uliopindukia, na uongozi wa taasisi kimsingi ni kama umeridhika na haya yanayoendelea katika taasisi na hii imekuwa kama ndiyo maisha ya kawaida ya wanafunzi wetu wasioweza kujitetea. Ikumbukwe hii ni taasisi ya teknolojia ambayo inajinasibu kutoa wataalam mahiri katika fani takriban zote za uhandisi, ila haiwezi kuwatumia wataalamu wake hao katika kutatua changamoto zake yenyewe.

xiii. Ubovu wa lifti katika jengo la mnara wa ufundishaji​

Moja kati ya changamoto kubwa zilizopo katika jengo hilo jipya ni ubovu wa lifti. Mara kwa mara lifti zinaharibika na kushindwa kufanya kazi, mara kadhaa imepita miezi hata mitatu bila hizo lifti kufanya kazi. Katika kufuatilia chanzo cha adha hiyo yakagundulika mambo mawili makubwa. Jambo la kwanza ni kuwa wakati mvua zinaponyesha maji hujaa katika sehemu ya chini ya jengo ambapo kuna mitambo hivyo kupelekea mashine na mitambo ya lifti kuharibika kutokana na kuingiliwa na maji. Jambo la pili ni kuwa mara nyingi lifti zingine zinafungwa na kuachwa moja tu kufanya kazi, hii inapelekea lifti hiyo kuchoka sana maana wanafunzi wanaotumia jengo hilo ni wengi kupindukia. Wapo waliohusika wakati jengo linajengwa na kuruhusu ujenzi kufanyika ulivyofanyika bila weledi hali iliyopelekea matatizo ya lifti ya sasa. Mfano wa lifti moja pekee ikifanya kazi umeonyeshwa kwenye Picha 9.

Suala la lifti limekuwa ni adha kubwa kwa wanafunzi na waalimu maana zipo ofisi na madarasa katika ghorofa za juu, tutafakari mtu mwenye ofisi ghorofa ya saba, nane, na tisa kama kilasiku mtu anakuja ofisini anakwenda madarasani nje ya jengo mara kadhaa na kwedha kushiriki katika majukumu mengine ya DIT na adha anayoipata namna ambavyo inaweza kuathiri ufanisi na utendaji kazi wa mwalimu Pamoja na athari za afya kwa wahusika.

Screenshot 2020-11-17 at 06.44.36.png


xiv. Uchakavu wa mabweni ya wanafunzi​

Katika karne hii na hasa katika taasisi kama DIT ni aibu kuona mazingira ya mabweni wanayoishi wanafunzi wetu, kimsingi mazingira wnayoishi wanafunzi wa DIT yanatweza utu wa wanafunzi wetu. Ikumbukwe kuwa hawa ndio watalamu ambo wanapaswa kuiendeleza Tanzania katika nyanja zote muhimu, hivyo kuna uhitaji na ulazima wa kuwafanya waone kuwa inawezekana kufanya mambo ya tofauti, mambo makubwa, na mambo mazuri. Hilo siyo rahisi kulifanikisha iwapo tunawaweka katika mazingira yanayotweza utu wao.

Katika eneo la Chang’ombe mkabala na chou cha DUCE lipo jengo linalotumiwa na wanafunzi wa shahada ya kwanza DIT kama makazi, toka miaka ya 2010 jengo lilikuwa chakavu na uchakavu huo umeendelea mpaka sasa. Kimsingi mazingira kama haya hayawezi kuleta utulivu wa fikra kwa vijana wetu ili wawaze kufanya vitu vikubwa kwa ajili ya Taifa hili. Uchakavu wa mabweni ya wanafunzi changombe Pamoja na kampasi kuu zimeonyeshwa kwenye Picha 10.

Screenshot 2020-11-17 at 06.46.37.png

Screenshot 2020-11-17 at 06.47.19.png


xv. Mtatizo ya kunguni katika mabweni ya wanafunzi​

Kumekuwa na matatizo makubwa ya kunguni kwa wanafunzi wetu kwa muda mrefu sana. Tatizo hilo limeshughulikiwa kiasi lakini halijapewa uzito unaostahili. Haiwezekani baada ya wanafunzi wetu kukesha wanasoma wakienda kulala waumwe na kunguni. Kwa yeyote aliyewahi kuwa katika mazingira ya namna hiyo mnajua adha yake inakosesha utulivu wa akili. Inashangaza kuona kuwa katika karne hii bado taasisi kama hii yenye watalamu wa teknolojia ya maabara inashindwa kuja na suluhisho la wadudu kama kunguni. Zipo familia nyingi ambazo zimeathirika kutokana na watotoa wa familia hizo wanaosoma DIT kupeleka kunguni majumbani, mara kwa mara wanafunzi wamelazimika kuanika magodoro nje ili walau kupunguza kunguni. Takriban 60% ya wanafunzi wa DIT wanaokaa hostel wamekuwa wakitoa magodoro kwenye vitanda na kuvitandika sakafuni ili walau wapunguze makali ya kuumwa na kunguni.

Tatizo hili limekuwapo kwa muda mrefu sana na mara kadhaa dawa zisizo na ubora zimekuwa zikipigwa ili kuwaangamiza kunguni lakini hakukuwa na mabadiliko. Mwanzoni mwa mwaka huu wakati wanafunzi wetu walipoondoka kurudi nyumbani wakati wa janga la CORONA bado tatizo hili lilikuwa sugu. Hivi karibuni kumetokea kitu ambacho kimewastaajabisha sana wanafunzi wetu, ikumbukwe kwamba serikali yetu iliichagua DIT kuwa moja ya vituo vya KARANTINI kwa ajili ya kutoa hifadhi ya muda kwa wasafiri waliotoka nje kuja nchini. Mara baada ya kutangazwa kuwa moja ya vituo ilifanyika furmigation kwa ajili ya kuteketeza kunguni na mara hii inaonekana kuwa dawa zenye ubora zilitumika kuwaua kunguni, wanafunzi wetu waliporudi kuendelea na masomo mara bada ya serikali kuruhusu maisha kuendelea, walishangaa kuona kunguni wamedhibitiwa kwa kiasi kikubwa sana. Mpaka muhula wa masomo unaisha mwaka huu wa 2020 tatizo la kunguni lilikuwa limedhibitiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Hii imepelekea wanafunzi wetu kujiuliza maswali mengi sana na kushangaa, mpaka serikali kuu itoe maagizo ya kufanywa DIT kituo ndipo watu waone aibu na kutatua tatizo la kunguni japo kwa muhula unaoisha. Hii Ina maana wao thamani yao ni ndogo sana kuliko hao binadamu wengine ambao walikuwa waletwe kukaa katika hostel za DIT. Hii inadhihirisha Kwa ukweli kuwa utu wa wanafunzi wetu umeendelea kutwezwa kwa muda mrefu sana.

HISTORIA YA MATATIZO SUGU YA DIT

Wakati wa uandishi wa ripoti hii ilibidi kutafakari kuhusu matatizo ya DIT na ililazimu kutafuta chanzo, na hiyo ikapelekea kurudi katika historia ya DIT pamoja na kufanya majadiliano kadhaa na wazee wakongwe ambao wamekuwepo katika vipindi tofauti tofauti na wale wanaojua historia kuanzia kipindi cha Dar es Salaam Technical Institute (DTI), Dar es Salaam Technical College (DTC), na sasa Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) miaka ya 1957, 1962, na 1997. Pia tulifanya mazungumzo na wanafunzi wa zamani wa DIT yaani DIT-Alumni waliokuwepo kipindi cha DTC ili kupata uelewa mpana wa changamoto za DIT.

Ikumbukwe kuwa umahiri wa wanafunzi wa DIT kipindi ikiitwa DTC unashuhudiwa katika Taifa hili kwa namna mbali mbali. Mfano, kwa maelezo ya wakongwe waliofundisha vipindi vya nyuma DIT, na kwa ushuhuda ambao unapatikana katika viwanda vyote vya Tanzania Pamoja na sekta mbali mbali za serikali na binafsi ambazo zina watumishi waliosoma DIT katika kipindi hicho cha nyuma. Imeshuhudiwa kwamba wakati wa DTC, zikiwa zinatolewa Full Technician Certificate (FTC) na Advanced Diploma in Engineering (ADE) kiwango cha ubora wa elimu ya ufundi kilichotolewa kilikuwa ni cha hali ya juu sana. Hii ilitokana na hatua Madhubuti zilizochukuliwa na chuo pamoja na Serikali kupitia Wizara husika kuweka mkazo katika mazoezi kwa vitendo. Sehemu ya mitihani ilitokana na mazoezi kwa vitendo na haya yote yalisimamiwa na Braza la Mitihani la Taifa.

Baraza kama chombo kilichokuwa kinasimamia ubora wa elimu pamoja na kuratibu na kusimamia mitihani, kilihakikisha kuwa maabara zote za ufundi zinakuwa na vifaa stahiki ili kuwezesha ufundishaji pamoja na kuwatahini wanafunzi. Hili liliwezekana kwa sababu bila kuwa na vifaa vya mazoezi kwa vitendo isingewezekana mitihani kufanyika. Kutokana na umuhimu wa mazoezi kwa vitendo baraza la mitihani lilisimamia kuhakikisha upatikanaji wa bajeti kwa ajili ya ku-repair vifaa vya maabara na kununua vifaa vipya ilipohitajika. Pia Baraza na Wizara walihakikisha uwepo wa rasilimali watu ya kutosha ili kuwezesha ufundishaji pamoja na mazoezi kwa vitendo kufanyika katika idara zote za taasisi.

Mara baada ya chuo kurasimishwa mwaka 1996 na kupata mamlaka kamili ya kujitegemea ikiwa ni pamoja na kubadilishwa kutoka DTC kwenda DIT ndipo mlolongo wa matatizo ulipoanza. Mkuu wa kwanza wa DIT Prof. John Wanjaga Kondoro (mtaalamu wa fizikia ya nuclear) aliletwa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ili kuiongoza DIT.

Ikumbukwe kuwa pamoja na umahiri mkubwa uliopo UDSM kuna tofauti ya msingi sana kati ya DIT na UDSM. Elimu iliyokuwa ikitolewa DIT wakati wa DTC ilikuwa imeegemea zaidi kwenye vitendo zaidi (Competence based-CBET) ilhali elimu ya UDSM ni kwa nadharia zaidi (Knowledge based-KBET) hivyo kwa ndugu zetu wa UDSM suala la umahiri katika kazi za mikono si kipaumbele, na hata pale ambapo hakuna mazoezi ya vitendo ya kutosha bado malengo ya elimu yanafikiwa UDSM.

Baada ya taasisi kupewa mamlaka kamili na uongozi kubadilishwa hakukua na chombo kingine kilichosimamia ubora wa elimu iliyokuwa ikitolewa. Ikumbukwe kwamba taasisi ilianza kutoa mitihani yake yenyewe tofauti na h apo mwanzo ambapo NECTA ndiyo ilisimamia suala hilo, na hapa ndipo ubora wa elimu ulipoanza kushuka maana hata pale ambapo hakukuwa na vifaa vya kutosha vya kuwezesha elimu kwa vitendo bado mambo yaliendelea tu bila shida yoyote, pia ikumbukwe kuwa taasisi iliyokuja kuundwa kusimamia elimu ya ufundi NACTE pia ni kama ilizaliwa na DIT hivyo unaweza ukaona namna ambavyo ilikuwa ngumu kwa NACTE kuiwajibisha DIT hasa pale ambapo ubora wa elimu ya ufundi hasa kwa mikono ilipoanza kushuka, hii ilipelekea ubora wa elimu kuendelea kuzorota mwaka hadi mwaka tangu 1997.

Matatizo ya DIT hayakuishia tu katika kuzorota kwa ubora wa elimu kwa vitendo, yalisambaa katika maeneo mengine kama miundombinu hafifu, upungufu wa majengo ya kufundishia, upungufu wa maabara, uchakavu wa vifaa vya maabara, uchakavu wa mashine nk. Ikumbukwe kuwa idadi ya wanafunzi imeendelea kuongezeka maradufu kwa miaka ya karibuni lakini ongezeko hili halikuendana na uboreshaji wa miundombinu ya taasisi. Mfano, ujenzi wa jengo la mnara wa ufundishaji (Teaching tower) ulianza mwaka 2009 lakini jengo hilo limekuja kuzinduliwa mwaka 2018 hivyo limechukua takriban miaka tisa. Kwa kipindi hicho chote taasisi imeendelea kuzorota na hata jingo lilipofunguliwa lilikuwa na matatizo mengi sana utadhani ni jengo la zamani. Hatufahmu ni hatua zipi zilizochukuliwa kuwawajibisha wahusika hilo tunaiachia Serikali. Kiufupi taasisi imeendelea kuzorota kila kukicha na tatizo la rasilimali watu nalo limeendelea kuongezeka.

Uongozi wa sasa kwenye taasisi nao unatoka kwenye mrengo ule ule wa KBET, kama ilivyokuwa kwa uongozi wa kwanza ambapo taasisi ilianza kuzorota na kupungua ubora, na hii imepelekea taasisi kuendelea kuwa na hali mbaya. Uongozi wa sasa wa taasisi umekosa uelewa wa juu ya umuhimu wa DIT katika taifa hili na umuhimu wa kuhakikisha kuwa brand ya DIT inabaki katika uhalisia wake, bila kuchanganywa na brand ya chuokikuu cha UDSM au kubadilishwa kufanana nayo.

UONGOZI ULIOPO WA TAASISI ULIVYOENDELEA KUCHOCHEA KUDORORA NA KUZOROTA KWA DIT​

Badala ya kuwa sehemu ya suluhisho la matatizo ya DIT uongozi uliopo sasahivi hasa mkuu wa taasisi amechukua hatua kadhaa ambazo zimeendelea kuvuruga na kuizorotesha DIT. Hapa chini tumegusia tu sehemu ndogo ya matatizo yanayotokana na uongozi wa sasa wa DIT, yapo mengi sana na tunaamini serikali yetu inayatambua hayo yote. Kama itahitajika kutoa maelezo ya ziada ili kuthibitisha tuyasemayo tupo tayari kufanya hivyo...

1. Anafanya maamuzi ya kibabe hata kwa masuala nyeti yanayohusu wafanyakazi wa DIT​

Moja ya vitu ambavyo mkuu wa sasa wa taasisi alivifanya alipoingia DIT ni kitu kinaitwa ringfencing, mwaka wa masomo 2015/2016 alikuja na lengo la kununua basi, changamoto ni kwamba katika kununua basi hilo alichukua pesa za walimu waliokuwa wamefundisha muda wa ziada zikawa sehemu ya pesa zilizonunua basi. Kuanzia kipindi hicho waalimu wameendelea kuminywa stahiki zao za kisheri na miongozo zinazotokana na kazi za ziada, mfano mtu anadai 2,000,000 anaishia kulipwa 500, 000 kwa miaka kadhaa mfululizo. Hii imepelekea morali ya wafanyakazi wa DIT kushuka sana na wengi wanafanya kazi kwa uoga tu ili waendelee kulisha familia zao, kimsingi wengi ni waoga tu na wameamua wengine kutumia muda mwingi kufanya mambo binafsi nje ya Taasisi ili kusukuma Maisha.

2. Hatoi vipaumbele kwa mambo makini na ya msingi kwa mustakabali wa Taasisi​

Anatoa vipaumbele katika vitu vinavyoonekana huku masuala ya ndani na ya msingi akiyafumbia macho. Mfano ni kipaumbele cha kununua basi kubwa sana lenye nembo ya TEACHING FACTORY ilhali maabara za DIT zikiwa zimechoka kiasi cha kukosekana hata compyuta kwa ajili ya wanafunzi wetu kujifunzia. Anazipangia Idara bajeti zisizokuwa na uhalisia na zisizokidhi haja, ikumbukwe kuwa katika maabara nyingi mashine nyingi zimekufa na kuchakaa na hilo ameelezwa mara nyingi na viongozi wa maidara hayo waliopita lakini hakutilia maanani. Vya msingi kwake ilikuwa ni kununua basi, kutengeneza pavements za barabara za ndani, na kumalizia library. Isipokuwa kwa swala la library, mengine yote aliyofanya ni kwa ajili ya maonyesho hasa kwa watu wanaotoka DIT. Hivi karibuni alimwalika waziri wa elimu kuja kuzindua bodi ya kampuni ya DIT na pesa nyingi tu zimetumika, pia ameitisha conference ya ma CEO hivi karibuni, hizi zote ni jitihada za kujaribu kuiaminisha serikali kwamba anafanya kazi sana na anafanya makubwa sana hapa DIT.

Unawezaje kufanya haya ya nje na kusahau masuala ya msingi kama vyoo kwa wanafunzi na waalimu wa DIT, ofisi kwaajili ya waalimu, uchakavu wa madarasa ya kufundishia, uchakavu wa vifaa vya maabara, ukosefu wa vitendea kazi na fanicha za maofisini kwa waalimu na hata kwa wanafunzi, tatizo la kunguni kwa wanafunzi na mengine mengi. Hii inadhihirisha kukosekana kwa utu dhidi ya wanafunzi, wafanyakazi, na taifa.

3. Anarudisha gawio serilakini ilhali taasisi inaelekea kufa kwa kukosa vifaa​

Ikumbukwe kuwa mwaka wa fedha 2018/2019 DIT ilitoa gawio la zaidi ya fedha taslimu za kitanzania zaidi ya milioni miamoja (100,000,000/=) kwa serikali. Sasa kama tukiyaangalia haya maswala yote yaliyozungumziwa katika taarifa hii, kiongozi mwenye mapenzi mema na DIT na taifa anawezaje kurudisha pesa serikalini na kufumbia macho matatizo haya sugu katika taasisi yake?

Jibu la moja kwa moja ni kuwa anataka kutoa taswira fulani kwa viongozi wa serikali kinyume na uhalisia wa mambo hapa DIT. Hii bila shaka ni kwa maslahi yake binafsi na siyo kwa maslahi ya taasisi, watu wake, au kwa taifa letu.

4. Anawadharau sana watu aliowakuta DIT​

Kuanzia kwa naibu wake aliyetokea DIT, wakuu wa maidara, pamoja na waalimu na wafanya kazi wengine aliowakuta. Hana huruma kama mzazi wala mlezi wa DIT, amekuwa akitawala DIT kwa vitisho na hata kukaripia baadhi ya wafanyakazi wanaoonekana kutokubaliana na mambo yake wala mipango yake. Pia tunajua kuhusu shida iliyotokea kutokana na dharau aliyoionyesha kwa mmoja wa viongozi wa wizara hili hatutalizungumza humu.

5. Hatoi ruhusa kwa mawazo huru ya watu wengine​

Yaani hapa DIT sasahivi mawazo yanayofanya kazi ni ya mtu mmoja tu ambaye ni principal, anajua kila kitu na haruhusu hata ushauri wala mawazo ya watu wengine. Ikumbukwe kuwa principal wa sasa wa DIT amebobe kwenye masuala ya maji lakini huko pia amebobea zaidi kwenye utafiti wa nadharia na siyo ya vitendo vinavyoendana na mrengo wa CBET, hivyo ana uelewa mfinyu sana wa mambo yanayohusu umahiri wa kufanya mambo kwa mikono. Kama angekuwa msikivu na anayekaribisha mawazo ya watu aliowakuta angepata msaada wa kutosha na tunaamini hali ingebadilika na DIT ingepiga japo hatua kidogo.

6. Anadhalilisha wafanyakazi​

Anawafokea na kuwadhalilisha wafanyakazi wakiwemo hata wasaidizi wake Ikiwa ni pamoja na kuwafokea hata wasaidizi wake mbele ya wafanyakazi wengine, kuwaamurisha wafanyakazi, wakiwemo wakuu ma maidara, kukaa chini hata kama wanatoa hoja za msingi kwenye vikao.

7. Anamdharau kila mtu ndani ya DIT na kila mara anasema 'DIT hamna watu'

Huu ni upotoshwaji mkubwa maana hata sasa miradi yote mikubwa iliyokuja DIT ambayo imeanza kutekelezwa kama ESTRIP, TELMS na mingine mingi imeandikwa na kusimamiwa na watu wa DIT hakuna hata mradi mmoja ambao kimsingi umetokana na juhudi zozote binafsi za Principal. Kimsingi kuna wakati ambapo amekuwa moja ya vizingiti vikubwa sana kwa maendeleo ya DIT kutokana na kujisikia kwake na kujiona anajua kila kitu.

Mfano mmoja wa suala hili ni katika mradi wa DIT Design Studio ulioletwa kwa mashirikiano na chuo kikuu cha RICE cha Marekani na ambao umefadhiliwa na Lemelson Foundation. Mradi huu unasua sua sana kutokana na ujuaji na utashi binafsi wa Principal, kuna mambo mengi sana anayoyakwamisha.

Uchunguzi wa kina ukifanyika bila kupitia kwenye uongozi wa Taasisi na bila kupitia kwa kiongozi wa mradi kutoka DIT ukweli utabainika. Mfano wa pili ni pale alipokataa kusaini barua ya makubaliano madogo tu ya awali kuwezesha kuanza kwa mashirikiano kati ya DIT na Chuo kikuu cha mashariki ya finland (UEF) mashirikiano yaliyoletwa na mmoja wa wahadhiri vijana hapa DIT. Mhadhiri huyo aliwezesha mashirikiano kam hayo kwa chuo cha taifa cha zanzibar (SUZA) kitengo cha Physics na chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Kitengo cha Physics.

8. Anatoa taarifa zisizo na usahihi kuhusu dhana ya 'Teaching Factory'​

Ikumbukwe kuwa katika siku za hivi karibuni mkuu wa Taasisi amekuwa akijinasibu na suala liitwalo teaching factory, kimsingi kwa yeyote ambaye amewahi kuliona basi jipya la taasisi liilonunuliwa kwa kutumia fedha ambazo zilikuwa stahiki za baadhi ya walimu, nembo kubwa katika basi hilo ni teaching factory. Uhalisia ni kwamba miradi iliyotekelezwa DIT kipindi cha karibuni kimsingi haijawahusisha wanafunzi kwa kiasi kikubwa, sehemu kubwa imefanywa na wanafunzi wa VETA Pamoja na wafanyakazi kutoka mtaani. Hii ilitokana na uhalisia kuwa katika miongozo ya masomo kwa wanafunzi wa DIT hakuna sehemu yoyote inayosisitiza ushiriki katika hiyo dhana na pia uwingi wa wanafunzi na changamoto ya ratiba za ufundishaji hazikuwa rafiki kuwawezesha waalimu na wanafunzi kushiriki katika dhana hiyo.

Kimsingi dhana hiyo ilikuwepo vichwani mwa wana DIT kwa muda mrefu, yeye alivyokuja akaidandia na bila kushirikisha watu akajiamulia namna anavyotaka mambo yafanyike. Kama kawaida yake yeye anajua kila kitu na wengine wote waliopo DIT ni ma mbumbumbu, hivyo mawazo yao hayana maana. Kimsingi ni usanii mtupu uliopo kwenye dhana ya teaching factory.

Siku za hivi karibuni baada ya taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa jamii forum , aliibuka na suala la kuwataka wanafunzi waandike proposal kwa ajili ya kutatua changamoto za DIT hii ilikuwa ni mbinu ya kimkakati kwasababu katika ripoti ya jamii forum ilisemekana kwamba anadanganya viongozi wa serikali kuhusu dhana ya teaching factory. Kama kawaida yake kila kitu ni order, top-down approach anatoa oda na anataka watu watekeleze bila kuruhusu mawazo mbadala ya kushauri nini kifanyike. Muandishi wa ripoti hii ndiye katibu wa kinachoitwa teaching factory steering commettee, hivyo anaelewa kwa undani uhalisia w namna oda ilivyoletwa na mkuu wa taasisi. Matokeo ya kazi hiyo ni kwamba fungu limetolewa kufanya mambo yafuatayo, kufanya repair ya system ya umeme kwenye moja ya mabweni, kujenga vimbweta vya kusomea wanafunzi nje, na kujenga viwanja cha mpira wa kikapu. Mambo haya ni mazuri lakini bado ukiangalia unaona shida ya vipaumbele, unawezaje kujenga uwanja wa basketball au vimbweta na kusahau suala la msingi kama madarasa ya kusomea, huduma ya vyoo, vifaa kama kompyuta vya maabara, mashine za maabara na mengine ya msingi ambayo yanahusu elimu ya vijana wetu?

Hapa pia utagundua kuwa kumekuwa na kukurupuka, lengo lake ni kutaka kuonyesha kuwa sasahivi DIT imekuja na miradi inayofanywa na wanafunzi, kwa lengo la kujisafisha. Hili linafanyika bila kufanya uchunguzi na upembuzi yakinifu ili kuwezesha matokeo mazuri. Kimsingi ni kiongozi anayefanya mambo kwa utashi wake na kwa namna anavyoona na kujisikia.

9. Anateua viongozi wote kwa utashi binafsi​

Kudhihirisha uhalisia wa fikra zake kwa wana DIT hivi karibuni ameteua wakuu wa maidara wapya bila kuwashirikisha wala kuwahusisha wafanyakazi katika hizo idara. Amehakikisha kuwa wakuu wa idara wote waliokuwa katika awamu ya kwanza ya uongozi wake ambao hakukubaliana nao hawapati tena nafsi, yaani anataka watu ambao anaweza kuwaendesha kama tairi bovu, wasioweza kuhoji chochote, wanopokea kila wanachoambiwa na kukitekeleza kama kilivyo. Tunashindwa kuelewa mkuu wa taasisi anawezaje kuwateua viongozi wa maidara bila kujaribu kupata japo mawazo ya wanaidara wenyewe, ikumbuka hapa tunazungumzia wasomi siyo ma mbumbumbu, hivyo ni lazima mawazo yao yachukuliwe ili kusaidia kuziendesha idara vizuri pamoja na kusaidia kuipereka taasisi mbele.

10. Anazorotesha hata miradi midogo ambayo tayari ipo DIT​

Katika kuelezea uhalisia huu tutatumia mradi wa DIT DESIGN STUDIO ulioletwa kwa ushirikiano na chou kikuu cha RICE nchini Marekani na kufadhiliwa na Lemelson Foundation. Mradi huu umekuwa msaada mkubwa sana kwa wanafunzi wetu katika siku za hivi karibuni kuwasaidia walau waweze kufanya uhandisi kwa kutumia vifaa vya kisasa. Kwa sasa mradi huu una changamoto nyingi sana na changamoto zote zinaletwa na principal wa DIT, changamoto hizo ni kama ifuatavyo:

Amekatalia mtanzania kuajiriwa katika maabara hiyo, kimsingi maabara hiyo kwa sasa inasimamiwa na mwanamama kutoka Zimbabwe na kipindi chake kitakapoisha atatakiwa awepo mtanzania ambaye atakuwa amehamishiwa ujuzi ili ujuzi huo uendelee kusambazwa kwa vijana wetu. Kwa utaratibu wa mradi alitakiwa aajiriwe kijana wa kitanzania kuwa msaidizi na baadae aweze kuendesha mwenyewe maabara, pesa zote za kulipwa mtanzania huyo zingetokana na mradi na DIT wala serikali ya Tanzania isingelipa chochote kwa kipindi chote cha mradi. Mpaka leo principal amekataa kuruhusu mtanzania mwingine kupata ajira hapo. Mwanzo wakati mradi unaanza alikuwepo kijana mahiri sana wa kitanzania ambaye alistahili kuajiriwa lakini mkuu alikataa na mwishowe kijana huyo amepata ajira BOT na kuondoka hapo. Hadi sasa hakuna mtanzania anayeendelezwa vizuri kurithi na kuendeleza mradi bila sababu zozote za msingi, yaani mkuu wa taasisi anataka anachotaka na anachoamua yeye kimsingi yeye ni Mungu wa DIT.

Toka mwaka jana maabara hiyo ilisaidia kurekebisha vifaa vingi sana vya hospitali ya Amana na pia ilikuwa inaanza kutaka kusaidia hospitali zingine, kutokana na matokeo chanya hospitali ya Amana ilitaka kuanzisha mahusiano rasmi na DIT na iliandaliwa MOU kati ya amana na DIT toka mwaka jana mwezi wa tisa lakini mkuu wa taasisi amekataa kuisaini toka kipindi hicho mpaka sasa na hivyo kuzorotesha michango ambayo ingeendelea kutolewa katika hospitali hiyo michango ambayo inakwenda kusaidia familia masikini za kitanzania zinazopata tiba Amana.

Wakati wa janga la CORONA maabara hiyo ilitumika kutengeneza vifaa vya kuwakinga madaktari sehemu ya uso pua na mdomo, vifaa vya plastiki sawa na kioo cha mbele cha helmet ya bodaboda na vifaa hivyo vilisambazwa katika baadhi ya hospitali zetu. Baada ya baadhi ya wadau kama UNDP waliziona jitihada zile na wakaahidi kuisaidia maabara kwa kuipatia vifaa vya ziada vya kielektroniki ili wanafunzi wetu wapate nafasi ya kufanya mambo makubwa zaidi ya viwango vya dunia ya kwanza, lakini mpaka tunavyozungumza hayo yote yamekwamia kwa mkuu wa taasisi na hakuna chochote kilichoendelea. Wapo wadau wengi tu ndani ya nchi ambao wametaka kusaidia maabara hiyo lakini juhudi zao zote zimegonga mwamba kwasababu ya mkuu wa taasisi.

Maabara hii inafanya kazi katika mazingira magumu sana na mkuu wa taasisi ni kama inaifanya isifanye kazi kwa ufasaha ki makusudi, kutokana na hili watu wa DIT tunajiuliza na tunahisi hataki DIT kuchangia maendeleo makubwa ya Taifa hili, maana juhudi zote kubwa nazikwamisha mkuu wa taasisi. Kwa vitendo hivi mkuu wa taasisi ameendelea kuwashusha morali watanzania wa DIT wenye mapenzi mema na wanaotaka kuona maendeleo ya DIT.

Swali la kujiuliza ni je kama kimradi kidogo namna hii mkuu wa taasisi ameki paralyze, je mradi mkubwa wa Bilioni 72 utaweza kustawi katika mikono yake? Bilashaka kila mmoja wetu anaweza kujijibu swali hilo.


KWANINI NI MUHIMU KUCHUKUA HATUA ZA HARAKA KUBADILISHA HALI YA DIT

1. KUZUIA NCHI KUPATA HASARA​

Kuna umuhimu wa kuchuku hatua za makusudi kubadilisha hali iliyopo ili kuinusuru DIT. Taarifa za hapo juu zinaonyesha ni kwa kiasi gani kiongozi aliyepo DIT asivyoelewa maana ya DIT wala umuhimu wake katika mandeleo ya Taifa hasa tukizungumzia Tanzania ya viwanda. Hivi karibuni DIT imepata nafasi ya kuwa sehemu ya Mradi wa Kujenga Ujuzi kwa Maendeleo na Uingiliano wa Kikanda katika Afrika Mashariki, ujulikanao kama “East Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP)” ni mradi wa kimkakati wenye lengo la kuboresha Elimu ya Ufundi na Mafunzo katika ukanda wa Afrika Mashariki. Mradi huu unashirikisha nchi tatu ambazo ni Ethiopia, Kenya na Tanzania. Ni mradi wa miaka mitano (5) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na ulianza rasmi tarehe 31 Mei 2019 na unatarajia kukamilika mwezi wa sita 2024. Kwa upande wake DIT imepata fedha kwajili ya miradi miwili:

Kituo cha Umahiri wa TEHAMA Afrika Mashariki “Regional Flagship ICT Centre (RAFIC)” kitakachoanzishwa katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam - Kampasi Kuu ya Dar es Salaam, “Dar es Salaam Institute of Technology Main Campus”.

Kituo cha Umahiri wa Uchakati wa Mazao ya Ngozi, “Centre of Excellence in Leather Products and

Allied Technology (CELPAT)” kitakachoanzishwa katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam - Kampasi ya Mwanza, “Dar es Salaam Institute of Technology Mwanza Campus”.

Katika miradi hii miwili DIT imepewa mkopo wa jumla ya shilingi za kitanzania Bilioni 74 ambayo walipakodi wa Tanzania tukiwemo na sisi wafanyakazi tunawajibika kuilipa kwa jasho letu. Hiki ni kiasi kikubwa sana cha pesa ambacho taifa limekopa. Hivyo basi kuna umuhimu mkubwa wa kupata usimamizi mzuri na uongozi mzuri na mahiri ili kuwezesha taifa kupata faida inayolingana na thamani ya pesa tuliyokopa na zaidi (value for money).

Kwa mazingira ya sasa ya DIT na hasa kutokana na uongozi uliopo kuna uwezekano mkubwa sana wa mradi huu kutokufanikiwa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mafanikio ya mradi siyo suala tu la kujenga majengo na kuweka vifaa vya kisasa. Ili mradi huu uwe na tija kwa taifa na kwa wananchi walipa kodi yapo mambo makuu matatu ya msingi tunayoweza kutumia kupima mafanikio:

Uwezo wa kuwafanya wana DIT wauchukulie mradi kama wa kwao binafsi (sense of ownership) ili kuweza kutumia muda wao, akili zao, na nguvu zao zote katika kuhakikisha mradi unafanikiwa.

Uwezo wa kujenga umahiri kwa wahadhiri, wakufunzi, na wafanyakazi wengine wa taasisi ili kuufanya mradi uwe na tija. Wahadhiri na wakufunzi wa DIT wanapaswa kuhakikisha kuwa ujuzi unaoambatana na mradi huu unabaki miongoni mwao ili uweze kusaidia katika kuwaandaa watalamu mahiri kwa manufaa ya Tanzania ya sasa na vizazi vijavyo.

Uwezo wa mradi kuwa stahimilivu (sustainability) hii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa vifaa, mashine, maabara pamoja na majengo yote yatakayopatikana kutokana na mradi yanaendelea kuwa hai na kutoa huduma hata pale mradi unapofikia mwisho. Hapa ndipo tutapata faida kutokana na uwekezaji tulioufanya kama Taifa na ikiwezekana faida zitakazotokana na mradi huu zitumike kuanzisha miradi mingine.

Kama tukiangalia vigezo hivyo vitatu vya msingi tutagundua kuwa uwezekano wa kukosa tija katika mradi huu ni zaidi ya asilimia 60, hii ni kutokana na historia ya miradi iliyopita huko nyuma. Mfano mradi wa TELMS uliofadhiliwa na waitaliano, Mradi ulioanzisha ITCoICT uliofadhiliwa na India uliokuwa na supercomputer na telemedicine (PARAM-SERENGETI), msaada wa supercomputer kutoka marekani. Msaada wa Vitabu kutoka IBM, msaada au mradi wa kompyuta katika maktaba ya wanafunzi, mradi wa KOICA ulio weka kompyuta katika idara ya ETE.

Matokeo makubwa na chanya yaliyotokana na mradi wa TELMS mpaka sasa hayaonekani. supercomputer mpaka sasa zipo kwenye basement ya jengo la mnara wa ufundishaji la DIT, hii imeambatanishwa kwenye Picha 11 mwisho wa ripoti, yeyote anayeweza kufika DIT anaweza kushuhudia. Vitabu kutoka IBM vingi vilichakaa kwenye makontena nje ya chuo mpaka sasa lipo kontena lililojaa vitabu vilivyochakaa baada ya kukaa muda mrefu bila kutumika, hii imeonyeshwa katika Picha 12 mwisho wa ripoti. Kompyuta katika maktaba ya wanafunzi zilitumika kwa siku chache sana baadae zikawa zinafungiwa tu na mwishowe zikachakaa, kompyuta zote zilizoletwa na KOIKA zimeharibika na kwisha kabisha hakuna hata moja inayofanya kazi mfano ni kwenye maabara ya komputa ya idara ya ETE.

Screenshot 2020-11-17 at 07.04.02.png

Screenshot 2020-11-17 at 07.04.39.png


Ili maendeleo yapatikane ni lazima matokeo ya miradi yawe endelevu, hilo kwa DIT limekuwa ndoto hasa kuanzia mwaka 1997, kila mara ni kama tunaanza upya mfano wa mtoto ambaye kila siku anatambaa, akianza kusimama anadondoka na kurudi kutambaa. Bila maamuzi magumu na ya dhati ni ukweli usiopingika kuwa DIT itaendelea kutambaa.

Kutokana na ukweli huu ambao uko dhahiri shahiri moja kwa moja utaona kuwa siyo rahisi mradi huu wa sasa wa EASTRIP kufanikiwa vizuri , hii ni kutokana na ukweli kuwa uongozi wa taasisi haujafanya tathmini ya miradi iliyopita, kubaini sababu za kushindwa kwa hiyo miradi, na kutafuta namna bora ya kuhakikisha mkopo huu mkubwa wa walipakodi unaleta matunda stahiki. Uongozi uliopo hausikilizi maoni na wala hautoi nafasi kwa wasomi wa DIT kutoa mawazo ya kusaidia kuleta suluhu ya matatizo ya DIT.

Mkuu w taasisi anajua kila kitu na anawachukulia wengine wote poa na anawaamrisha tu kufanya anachojisikia yeye. Pia ameshusha sana morali ya wafanyakazi wa DIT, kimsingi asilimia 99 ya watu wa DIT hawana morali ya kufanya kazi na hivyo hawana utulivu wa akili na wa maisha wa kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha mradi huu unakuwa na tija. Ikumbukwe pia kuwa mkuu huyu wa Taasisi amewatengenezea uoga wa kupindukia wafanya kazi wa DIT na anatumia uoga alioutengeneza kutawala DIT. Kimsingi DIT hakuna kiongozi bali kuna mtawala ambaye anatumia DIT kutimiza ndoto zake binafsi ambazo haziendani na ndoto za Taifa letu na kasi ya serikali yetu. Kwa sasa wafanyakazi wa DIT wanafanya kazi ili wasifukuzwe lakini hawana ile morali inayostahili ili kuleta na kuwezesha matokeo chanya na makubwa hasa katika elimu ya Ufundi nchini.

2. KUINUSURU DIT ISIFE KATIKA MIKONO YETU KIZAZI CHA SASA​

Kwa uhalisia uhai wa DIT unategemeana na mchango ambao DIT inautoa katika jamii, iwapo DIT ikikosa uwezo wa kuendelea kutoa elimu yenye tija kwa vijana wetu wa Tanzaia ni hakika kwamba DIT itakuwa imekufa hata kama kutakuwa na magofu yamesimama na maskrepa yamejaa katika maabara zetu.

Katika sehemu hii nitatumia uhalisia ulio wazi wa idara ya mitambo (Mechanical Engineering) ambayo ndiyo idara kubwa kuliko zote DIT. Kimsingi mashine zilizopo katika maabara za idara hii nyingi zimekufa, kwa uhalisia kabisa nizungumzie maabara ya maligafi (Materials Laboratory), amabayo kimsingi ni muhimu sana katika masuala ya uhandisi kokote duniani. katika maabara hii mashine zote zimekufa, hakuna hata mashine moja inayofanya kazi angalia Picha 13. Mfano wa pili ni katika maabara ya kupooza vitu (Refregeration laboratory) ambapo baadhi ya mashine zimekufa na chumba cha kupoozea vitu (Cooling room) nacho kimekufa Picha 14, katika mabara ya joto na nguvu (Heat and power laboratory) ambapo mashine takriban zote zimekufa Picha 15, katika maabara ya ufuaji vyuma chumba cha kuzalisha joto (Heat treatment chamber) kimekufa Picha 16, compressor katika eneo la kubadilishia magari kwenye mfumo wa gesi imekufa Picha 17, na katika maabara zingine nyingi zipo mashine zilizokufa, nyingine zimekufa vipuri, na mashine nyingine hazijafanyiwa service kwa miaka mingi sana Picha 18.

Screenshot 2020-11-17 at 07.07.50.png

Screenshot 2020-11-17 at 07.08.04.png

Screenshot 2020-11-17 at 07.08.18.png
Screenshot 2020-11-17 at 07.08.44.png
Screenshot 2020-11-17 at 07.09.06.png
Screenshot 2020-11-17 at 07.09.19.png
Screenshot 2020-11-17 at 07.09.33.png


Kwa mfano huu wa idara ya mitambo na mifano tuliyoiona katika idara zingine huko nyuma ni dhahiri kwamba DIT inaelekea kufa. Kila mwaka mkuu wa taasisi anatenga takriban shilingi milioni ishirini pekee kwa mahitaji ya idara nzima katika vifaa, kwa uchakavu unaoonekana kwenye picha ni dhahiri kwamba hicho kiasi ni kidogo sana na hakiwezi kukidhi mahitaji ya pengine hata kufufua mashine japo moja kwenye idara ya mitambo. Ni dhahiri kwamba kama hatua za makusudi hazitochukuliwa DIT inakufa.


NINI KIFANYIKE KUINUSURU DIT?​

1. Mabadiliko yanahitajika katika uongozi wa taasisi​

Hivi karibuni baada ya andiko la JamiiForums, Wizara iliteua Tume kuja kuchunguza changamoto za DIT, cha kusikitisha ni kuwa takriban asilimia 80 ya wajumbe katika Tume hiyo ni watu ambao Mkuu wa Taasisi wa sasa amewahi kufanya nao kazi kwa vipindi tofauti akiwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM). Ni wazi Tume hii lazima itaegemea mrengo fulani (biased) katika ripoti yao na kwa namna ya kibinadamu lazima kufahamiana kwao kutapata nafasi katika ripoti. Pia katika Tume hii hakukuwa na nafasi sawa kwa wajumbe wa DIT kwenda kutoa maoni. Kimsingi wajumbe ambao hawaridhishwi na uendeshwaji wa taasisi hawakupewa nafasi ya kuonana na Tume, sehemu kubwa ya watu waliokwenda ni wakuu wapya wa Idara ambao ni watu aliowazawadia nafasi za uongozi, hakika hawa watamtetea maana watakuwa wanatetea vitumbua vyao.

Baada ya Tume kufanya kazi yake na japo kuonyesha mapungufu machache ya Mkuu wa Taasisi wana DIT tulipata taarifa kuwa aliwekwa katika kipindi cha matazamio ili kuangalia mienendo yake kama kutakuwa na mabadiliko, hali hii ilitufanya wana DIT tuamue kutulia kuona kama kuna mabadiliko chanya yatatokea. Kikao cha kwanza alichokiita baada ya kurudi likizo fupi kiliwashangaza wengi kwa mabadiliko ya ghafla yaliyotokea maana walau alianza hata kutoa nafasi ya kusikiliza maoni ya watu hata kama mwisho hakuyachukua lakini walau alisikiliza, hivyo wengi wakapata japo matumaini kidogo. Baada ya hapo mambo yalianza kurudi taratibu katika utaratibu wa awali na asili yake iliendelea kujirudia katika vikao kimoja baada ya kingine kadri siku zilivyosonga, mwisho tukatambua kuwa huyu ni mjasiri ambaye hawezi kuiacha asili yake.

Hivi karibuni amefanya matukio makubwa mawili katika kujaribu kuionyesha serikali kwamba uongozi wake unatija DIT, ikumbukwe kuwa matukio haya yamefanyika kimkakati (strategically) mwisho wa kipindi chake cha uangalizo (Probation period) ili kutoa taswira isiyo sahihi kwa serikali kuhusu taasisi. Moja ya vitu alivyovifanya ni kutumia garama kubwa takraban zaidi ya shilingi milioni 30 katika kuzindua bodi ya Kampuni ya DIT, katika uzinduzi huo waziri wa elimu alialikwa na viongozi wengine wengi. Jambo la pili ni kuwa ametoa maelekezo kwa watendaji DIT kuandaa conference inayosema "Mchango wa Taasisi za Elimu ya juu katika kuendeleza ajenda ya Taifa ya viwanda (fourth industrial revolution)"; hii ilikuwa ifanyike mwaka huu lakini kutokana na changamoto za hapa na pale imepangwa kufanyika mwakani. Hili nalo ukiliangalia kwa upana wake unagundua lengo hapa ni kujitangaza na kujionyesha kwa viongozi kwamba kuna makubwa yanafanyika katika ajenda ya Taifa. Kiukweli kama sote tumefuatilia hii ripoti vizuri tutakuwa tayari tunaujua ukweli.

Kiongozi anayejitambua na ambaye anaitakia mema DIT hawezi kutumia pesa nyingi kufanya vitu vya maonyesho na kusahau majukumu ya msingi ya DIT. Vifaa kwenye maabara vimechoka, kompyuta zote zimekufa, morali ya wafanyakazi ipo chini kupitiliza, madarasa na vyoo vimechakaa kupita maelezo lakini kipaumbele chake ni kuzindua bodi kwa kutumia pesa ambazo zingetumika kurekebisha vitu vya msingi DIT. Hii ndiyo sababu tunasema kwamba Principal wa DIT wa sasa anaitumia DIT kama stepping stone kwa ajili ya mahitaji yake binafsi ya kisiasa au ya kiuongozi na hana malengo ya dhati ya kuitoa DIT kwenye matope.

Tunaamini kuwa maamuzi magumu yanahitajika kuchukuliwa ili kuinusuru DIT. Kwanza kabisa, kubadilisha mitizamo ya watu wa DIT, kutambua na kuratibu changamoto zilizopo ili hatimaye kuweza kuja na suluhisho sahihi litakalowezesha taasisi hii kukua na kufanya nafasi yake katika kuinua uchumi na maendeleo ya kijamii ya Tanzania. Hilo halitowezekana kama uongozi uliopo hasa mkuu wa taasisi aliyepo ambaye kwa kiasi kikubwa sana ametweza utu wa wafanyakazi na kuwaonyesha kiwango cha dharau cha hali ya juu sana akiendelea kubaki DIT. Moja kati ya hatua zinazostahili kuchukuliwa ili kubadili mambo DIT ni kuubadilisha uongozi wa juu wa DIT ili kurudisha amani ya mioyo ya wana DIT ambayo imenyongonyea na kusononeka kwa miaka yote ya uongozi wa mkuu wa taasisi aliyepo.

2. KUSHIRIKISHA WADAU WAKUBWA WA DIT KATIKA UTATUZI WA MATATIZO​

Ikumbukwe kuwa DIT imetoa viongozi mbalimbali ambao wanaongoza na wameongoza kwa umahiri kabisa katika vyuo vingi vya ufundi na vyenye mrengo wa CBET hapa nchini: Mfano Prof Mganilwa (Rector NIT), Dr Mgaya (Deputy Rector Academic, NIT), Dr Masika (Aliyekuwa Mkuu wa Chuo Arusha Tech), Deputy Rector wa sasa hivi wa Arusha Tech, Aliyekuwa mkuu wa Chuo cha Maji, Makamu wa mkuu wa sasa wa chuo cha maji, Mkuu wa chuo wa sasa wa DMI, nk. Hii inadhihirisha pasiposhaka uwezo wa baadhi ya mazao ya DIT katika uongozi. Pia wapo viongozi kama Prof. John W. Kondoro ambao wanyatambua na kuyafahamu kwa undani matatizo ya DIT. Nadhani wadau wote waliotajwa hapo juu pamoja na wadau wengine wa taifa hili ambao wapo DIT na katika viwanda mbalimbali hapa nchini wanaweza kusaidia kutafuta namna sahihi ya kuipeleka mbele DIT.

3. KUHAKIKISHA WATU WALIOPO DIT NI WATU SAHIHI​

Jambo la pili ni muhimu kuhamisha baadhi ya watumishi kutoka DIT, hii ni kutokana na ukweli kuwa vipindi tofauti vya uongozi vya DIT vimejitengenezea makundi yanayozorotesha ukuaji wa DIT na ambao wana mawazo mgando. Wengi wa watuhao wanafanya kazi kwa mazoea katika ofisi zao na wamekuwa kama miungu watu, hali hii inaleta ukiritimba na ucheleweshwaji usiyokuwa na misingi yoyote kwa maendeleo na mustakabali wa DIT na Taifa. Tunaamini Taifa letu lina watu mahiri hasa wanaotoka katika mrengo wa ufundi au katika mrengo wa viwanda vilivyofanikiwa katika taifa hili. Kwa maoni yetu hawa ndiyo watu wanaopaswa kuwa waalimu DIT, kuiongoza DIT, na kuirudisha katika ubora wake, bila kujali kama hao watu wanatokana na DIT au la, maana Tanzania ina hazina kubwa sana ya watu mahiri katika masual ya ufundi na uhandisi.

DIT kwa sehemu kubwa inapaswa kubaki na waalimu ambao wamebobea katika kufanya kazi kwa vitendo zaidi, wale ambao ni wa nadharia waperekwe katika vyuo ambavyo vinafundisha nadharia. Katika suala hili lazima serikali yetu iwe makini na ifanye maamuzi magumu kwa maslahi mapana ya taifa letu kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo, kinyume na hapo nyota maridhawa ya DIT iliyowekwa na marehemu Baba wa Taifa pamoja na viongozi wengine waliotangulia mbele ya haki itazimika na kulirudisha nyuma taifa letu.

4. KUONGEZA RASILIMALI WATU DIT​

Kwa muda mrefu sana kumekuwa na upungufu mkubwa sana wa wahadhiri, waalimu, pamoja na wanataaluma wengine DIT, hivyo baada ya kufanyika mabadiliko thabiti katika nguvu kazi ya DIT ni muhimu serikali yetu ikaongeza wafanyakazi wapya watakaosaidiana na wafanyakazi waliosalia DIT kufanya kazi ngumu kuirudisha DIT katika ubora wake ili iweze kuwanoa baraabara watalamu waleo na wakesho wa Tanzania.

5. KUREKEBISHA MIUNDOMBINU NA VIFAA VYA KUFUNDISHIA DIT​

Baada ya mambo ya msingi yaliyoainishwa hapo juu kufanyika ni muhimu kuiwezesha DIT iendane na dunia ya leo kwa vifaa, ujuzi, na ufundishaji wenye tija na wenye kulenga matokeo chanya kwa taifa letu. Ni lazima tujiulize kama taifa tunataka kuitumia DIT kufika wapi, na tuiwezeshe DIT ili iweze kufanya sehemu yake katika kuwezesha maendeleo na maslahi mapana ya Tanzania.

Hitimisho​

Katika ripoti hii tumeainisha matatizo makubwa yanayoikabili DIT na pia kuona namna ambavyo uongozi wa sasa unapwaya na kushindwa kuleta mabadiliko chanya katika kuwezesha maendeleo endelevu ya DIT na taifa kwa ujumla. Ni ukweli usiopingika kuwa matatizo ya DIT kwa sehemu kubwa yametokana na mabadiliko ya kimfumo kutoka kusimamiwa na Baraza la mitihani hasa katika suala la ubora wa elimu hadi kusjisimamia yenyewe na kupewa kiongozi anayetokea mrengo wa KBET kuja kuongoza katika mfumo wa CBET. Pia ni dhahiri kuwa sehemu kubwa ya matatizo ya DIT yanatokana na kutojielewa na kutokujitambua kwa wafanyakazi wengi wa DIT hali iliyopelekea wao kushindwa kusimamia mambo ya msingi kwa mustakabali wa DIT na taifa. Tunasikitika kushuhudia kwamba jambo kubwa alilofanikiwa kulifanya mkuu wa sasa wa taasisi ni kuchochea uoga kwa wahadhiri na wafanyakazi wengine wa taasisi ili aweze kuendesha taasisi kwa utashi wake binafsi.

Sote tunatambua kuwa serikali ya awamu ya tano imefanya mambo makubwa ya kustaajabisha katika taifa hili ndani ya miaka mitano inayomalizika. Moja kati ya maeneo makubwa yaliyofanyiwa kazi ni eneo la elimu, tumeshuhudia shule zote kongwe nchi hii zikikarabatiwa na kurudishwa katika hadhi yake, pia tumeshuhudia marekebisho makubwa kaatika baadhi ya vyuo kama UDSM, MUST, CBE na vingine. Lakini kwa upande wa DIT tumekwama na tumegota, tunajiuliza kama changamoto kama hizi za DIT zinaweza kuendelea katika serikali hii ya kizalendo, inayochapa kazi, na inayotanguliza maslahi mapana ya taifa, tunashindwa kuelewa ni serikali ipi itakayosaidia au kusimamia DIT ipate maendeleo. Hili ni swala linalotupa shida sana wana DIT, lakini tuna matumaini kuwa serikali yetu ni sikivu, makini, na yenye weledi na itachukua maamuzi sahihi kwa wakati sahihi.

Ni dhahiri shahiri kuwa mradi wa EASTRIP wa bilioni 74 utafanyika majengo yatajengwa, mashine zitanunuliwa, na wafanyakazi kadhaa watajengewa uwezo kutokana na mradi, lakini matokeo chanya na makubwa (Value for money + multiplying effect) ya mradi huu hayatafikiwa kwa uongozi uliopo. Serikali yetu ina vyombo mahiri vinavyoweza kufanya uchunguzi wa kina na wa usiri DIT ili kubaini ukweli wa ripoti hii, kama hili litafanyika lisipitie katika mkondo wa utawala wa taasisi, lipitie katika mkondo mwingine na hasa kuwahoji wafanyakazi wa kawaida pamoja na viongozi wa maidara waliomaliza vipindi vyao.

Changamoto zilizoainishwa katika ripoti hii zimeiperekea DIT kutoa elimu ya nadharia zaidi ya vitendo na haina tofauti na vyuo vingine vya nadharia hapa nchini. Pia kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi hasa kwa miaka ya karibuni, lakini ongezeko hili halijaenda sambamba na upanuzi wa miundombinu wala ongezeko sawia la wahadhiri na wana taaluma wengine. Hii imepelekea ubora wa elimu inayotolewa kuendelea kushuka kwasababu vifaa na miundombinu haviendani na idadi ya wanafunzi. Mfano madarasa ambayo zamani yalibeba watu 24 kwa sasa yanalazimika kubeba wanafunzi takriban 50 na zaidi kwasababu madarasa ni machache, hali hii inazorotesha ubora wa elimu na ufanisi wa DIT katika kuchangia maendeleo endelevu ya Tanzania.

Kwa upande mwingine miradi mingi iliyofanyika huko nyuma hasa kuanzia 1997 haijaleta tija ya kutosha na haikupata usimamizi thabiti hasa kuiwezesha iwe endelevu na hii ndiyo sababu leo hii miundombinu takriban yote ya DIT imechakaa na kuharibika kwa kiwango cha kustaajabisha. DIT imeendelea kuwa kama mtoto anayetambaa ambaye hawezi kusimama, kupiga hatua, na kusonga mbele kulisaidia taifa. Itakuwa ni kosa kubwa sana kuruhusu hali hii kuendelea hasa wakati huu ambapo kuna mradi mkubwa unaotokana na mkopo wa benki ya dunia wa bilioni 74. Kama hatua stahiki hazitachukuliwa kubadilisha hali ya mambo taifa litapata hasara kubwa na DIT itaendelea kuzorota, na hatuko tayari kuona hili linatokea maana tutakuwa wanafiki. Tunaiomba serikali yetu pendwa na sikivu ichukue hatua stahiki ili kubadilisha hali ya mambo.

Wazalendo tulioshiriki kuandaa ripoti hii hawana matatizo binafsi na principal wala uongozi wa juu wa DIT, matamanio yetu ni kuona taasisi hii inabadilishwa na kurudishwa katika umahiri wake kwa maslahi ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo. Tunaamini yapo majukumu mengi katika taifa letu ambayo yanaweza kufaa kutekeleza kwa weledi na kiongozi wa sasa wa DIT, ila kwa hapa DIT tunaomba apumzishwe. Tunatanguliza maslahi mapana ya DIT na taifa letu ndiyo maana tumezungumza vitu hivi kwa uwazi na pia muandishi na mratibu mkuu amejitambulisha, maana tuliyoyaandika siyo majungu. Tutakuwa tayari kushirikiana na serikali yetu kutafuta suhuhisho la kudumu ili DIT iweze kurudi kwenye ubora unaostahili, iweze kutoa wataalamu mahiri, na pia iweze kuchangia kuwezesha ukuaji wa uchumi wa taifa letu.
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
14,045
15,299
Dar es Salaam Technical College kwa sasa DIT ni chuo cha kwanza kikubwa nchini Tanganyika kabla ya uhuru, chuo hiki kimo kwenye historia ya Tanganyika, lakini bahati mbaya kimezidiwa na vyuo vya watu binsfsi! Ni nini kilichkikumba mpaka serikali ikipe mgongo mizimu pekee inajua. Kutokana na umri wake chuo hiki kingeweza kuwa chuo kikuu cha tekinolojia, lakini wapi!
 

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,618
8,378
Huu uzi umesimama sana, ni wakati sasa kwa wahusika kuchukua hatua stahiki ili kukinusuru chuo hiki
 

Vege

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
329
348
Hongera sana mwandishi
umetufungulia mlango na mawazo yetu kupitia makala hii yatafika sehemu sahihi
 

Chunda

Senior Member
Apr 7, 2016
188
251
Serikali ya Tanzania haifanyii kazi habari kama hizi.
Prof mama angekuambia ni umbea na majungu baada ya kuchukua bahasha za kaki.
 

East Wind

JF-Expert Member
Jun 17, 2020
2,812
5,321
Elimu ya bongo ni janjajanja.. nimesoma DIT kitambo.. hayo matatizo yalikuwepo na tukatusua tu mzee baba.. pambana na hali yako. Walio katika nafasi za kutatua hayo hawajali maana wanaona mambo yao yaenda.. Kunguni nao ni uchafu wa wawanafunzi hasa wa OD kunguni huanzia block 1 kwenda block 3 block kwa videmu pale visafi kidogo.. ila hawa block 1 na 3 ndio husambaza kungunk chuo chote😀😀😀😀😀
 

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,047
10,709
Ni jambo la kushangaza sana kuwa vyuo vinarudisha gawio serikalini, je vinafanya biashara gani?
 
11 Reactions
Reply
Top Bottom