TRA na kodi za kuagiza magari

TRA na kodi za kuagiza magari

unachangia ukuaji wa viwanda vya uganda.. ukisikia akili mbovu ndio hii!
Bora afanye hivyo tunachokitaka ni unafuu nikiwa Sirari huwa naenda kuweka mafuta Kenya sasa hivi ni 1600 kwa petroli huku Tanzania ni 2000 tunatafuta unafuu na kuweka uzalendo pembeni.
 
kweli mkuu....tatizo letu ni kushindwa kutanua wigo wa kodi
Mkuu mie nahusika vipi hapo wakati bunge letu ndiyo linapitisha haya bahati mbaya hata wabunge wa upinzani wapo kimya.
 
Tatizo ni kwamba wewe na wenzako hamjaelewa kwa nini kuna hizo kodi, lengo ndiyo msiagize magari chakavu hapa kwetu badala yake nenda CMC au toyota TZ kanunue hiyo gari! Dunia nzima hufanya hivi, hebu jaribu kutoa gari TZ kupeleka Japan hata gari hiyo hiyo uliyoinunua huko jaribu kuirudisha halafu uone watakuchaji kiasi gani!
Watanzania wengi ni wa kipato cha chini unamwambie ananue gari mpya ni sawa sawa kumtukana.

Kama kununua nguo mpya inakuwa mtihani sembuse gari jipya, gari mipya ya milioni 40 unatakiwa ulipe ushuru milioni 20 watanzania wangapi wataweza.

Nchi kama South Africa wameweka ushuru mkubwa mno wa magari kutoka nje sababu kubwa ni kulinda viwanda vyao vyao ndani na gari kwao ni bei rahisi kila mwananchi wa kipato cha chini anaweza kumiliki gari.

Tanzania ushuru wa magari upo juu sana mtu akimiliki gari unaonekana tajiri na jamaa zake wanamuangalia kama shujaa.

Haiwezekani gari kama Toyota IST unailipia milioni 8 mpaka 10.
 
TRA wanataka wapate mapato makubwa kwenye magari mitumba kuliko hata faida wajapani wanayopata kwenye magari mapya. Jamaa wanachekesha sana
 
Magari chakavu yanaharibu mazingira na ndiyo maana huko mnakoyanunua yanakuwa bei rahisi kwanza kuna wengine hata hupewa bure kwa maana huko hayaruhusiwi tena, hiyo ndiyo sababu!

Nyie hata kiwanda cha baiskeli mmeua halafu unatema upupu hapa. Unalaumu watz wasinunue magari chakavu kwa mishahara ipi mnayowalipa hadi wamudu kununu gari mpya? Kweli akutukanaye hakuchagulii tusi. Sera za ccm ndiyo zimetufikisha hapa mmevimbiwa sasa mmeamua kuwatusi masikini mliowatengeneza kwa miaka zaidi ya 50 sasa.
 
TRA wanajua vizuri sana haya mambo pengine hata kumzidi mleta mada. Lakini lengo lao kubwa ni kuidanganya jamii kuwa wanakusanya kodi kubwa ili wapate mianya ya kuiba fedha zetu. Hawa watu hawafai pamoja na waelekezaji wao(chichi-m).
 
Bila shaka malalamiko mengi yameandikwa kuhusiana na mada hii, sipendi ifikirike kwamba ni kitu kipya, ila kujaribu kukumbushia tena, pangine hawa wenzetu wanafikiria kwamba wannchi tumeridhika kwa kukaa kimya.

Kwanza nitoe mfano wa maheasabu nikizingatia kichakata chao TRA;

Used Motor Vehicles Valuation Calculator

Reference Number 1516307575
Make: BMW
Model: X5
Body Type: SUV
Year of Manufacture: 2002
Fuel Type: PETROL
Engine Capacity: 2001 - 2500 CC
Customs Value CIF (USD): 4805.46
Import Duty (USD): 1201.36
Excise Duty (USD): 600.68
Excise Duty due to Age (USD): 1802.05
VAT (USD): 1513.72
Custom Processing Fee (USD): 28.83
Railway Dev Levy (USD): 72.08
Total Import Taxes (USD): 5219
Total Import Taxes (TSHS): 11434829
Vehicle Registration Tax (TSHS): 380000.00

Hebu oneni mlolongo wa majina ya kodi kwa majina tofauti tofauti unzvyoongeza gharama ya uagizaji wa magari;

Ki-uchumi, kodi nyingi kama hizi huwa zina maana mbili kwa pamoja au pengine mojawapo;

1. Kuzuia/kupunguza bidhaa za nje zisifurike katika soko la ndani, ili kuimarisha viwanda vya ndani vinavyotengeneza kwa wingi na kwa ufanisi bidhaa hiyo hiyo au inayokikdhi mahitaji kama hiyo inayotakiwa kuagizwa nje, au kuzuia kabisa bidhaa mbovu zinazoweza kuharibu mazingira na afya ya wananchi na pia kuongeza ajira za ndani.

2. Kuongeza pato litokanalo na kodi; hii huwa ni kwa muda mfupi kwani ikiendelea kwa muda mrefu pato halitaongezeka, kwani watu wataacha kununua, na kushusha pato tegemewa.

Kwa hiyo TRA , wakiwa wanafanya kazi yao kwa maslahi ya wananchi ni lazima wafikirie namna ya kutoa huduma, kwa kuweka mifumo saidizi, itakayosaidia wananchi kupenda kulipa kodi, na kuilipa kwa hamasa.

Wanapashwa kuainisha malengo yao, kama yanafanana na la kwanza au la pili; kwangu mimi naona lile la pili haliwaungi mkono sana kwa sababu makato haya yamekuwa yanaongezeka tu kwa muda mrefu sana sasa, na kuondoa dhana ya makusanyo yapaswayo kuleta faida kwa muda mfupi.

Kwa lile la kwanza, pia haliwaungi mkono kwa sababu hatuna kiwanda cha ndani tunachokikinga na bidhaa za nje.

Napata fikra kwamba TRA hawapendi kufanya tathmini itakayosaidia wananchi, ili nao angalau wapendeke, wasionekane kama wanatoka sayari ingine (Aliens), kwa sababu wao kodi hizi haziwahusu; pamoja na wabunge.

Mawazo yangu ya kuhitimisha ni kwamba kitengo cha elimu kwa mlipa kodi wanapashwa kutoa elimu kwa ukamilifu, siyo kuishia tu kwenye matakwa yao kisheria tu. Utamsikia akisema ati kama maendeleo hayaonekani pamoja na utoaji kodi hil si swala lao, hawaoni kwamba wapo kwenye mnyororo wa maendeleo (development chain)? na kwamba wao kwa kuwa huenda kuonana na walipa kodi moja kwa moja, wanakumbana na vikwazo, na kutokuwa tayari kwa sababu hawakamilishi mnyororo huu?

Kwa mlolongo huo hapo juu, ni wazi kwamba wengi mno wataacha kuagiza bidhaa hizi, na hivo kupunguza pato ambalo TRA wangekusanya kidogo kidogo lakini kwa walipaji wazuri wengi; pia, inaongeza incentive ya watu kukwepa kodi.

Fikirieni na mufanyie kazi haya malalamiko.
Hiki ndio kilio kikubwa cha Wafanyabiashara na Watanzania na ni chanzo kikuu cha RUSWA Tanzania, na wanaosema tra sasa wanafuata invosi si kweli, hii ni sheria inatakiwa ibadilishwe sio swala la kuongea kwa mdomo, sheria iseme wazi kuwa afisa wa kodi atakokotoa kodi kutoka kwenye invoisi na risiti ya mteja tu, ila bidhaa isiyo na invosi na risiti ndio ataruhusiwa kukadiria na kama mwenye bidhaa hatarizika akakate rufaaa, hii iliwekwa kwa ajili ya kulinda wachangiaji na makada wa chama kwani hawawezi kushindana kwenye uwanja wa kibiashara.
 
Chakushangaza gari mpya inakodi kubwa kuliko kukuu
 
Mkuu mie nahusika vipi hapo wakati bunge letu ndiyo linapitisha haya bahati mbaya hata wabunge wa upinzani wapo kimya.
sijasema wewe unahusika mkuu...mbona uko tayari tayari sana kwa vita
 
unachangia ukuaji wa viwanda vya uganda.. ukisikia akili mbovu ndio hii!
Kweni Uganda wana viwanda vya kutengeneza hivyo vitu?
Hata Kama wanavyo huwezi nunua bidhaa chini ya kiwango Au bei kubwa kisa nikuze uchumi wetu.
Hapa matatizo ni KODI kodi Na makodi ya Ajabu.
 
A
Tukubali Tanzania hatuna uchumi imara. Tunategemea kodi za kukomoa ndio nchi ipate mishahara.
Tuna gesi haijulikani faida yake
Tuna dhahabu tunabaki na mashimo na fedha za kuuza pamoja na dhahabu zinabaki nje..Ujinga mkuu
Tuna serengeti ,kilimanjaro,ngorongoro nk watalii 750,000 kwa mwaka , dubai wanapokea 15,000,000...
Tuna mvua ya kutosha na ardhi safi...imebakia ya kufukuzana na wamasai
Tuna bahari na samaki kibao....tupo tu tunaikodolea macho tunadhani kazi ya ni kuvukia ferry

Tukirudi kwenye kodi ...hizi ni za kukomoa lakini sio kwa kukusudia bali hamna jinsi...
Kodi ya gari Tanzania ni Zaidi ya Faida Toyota pamoja kodi wapatayo serikali ya Japan kutoka Toyota !!!!and yet japan wanatusaidia !!
Nchi yenye madini ya kila aina lakini ikatemea kodi za magari, sigara, bia kuendesha nchi ni kuonesha tuna matatizo ya uelewa na elimu. Tuna matatizo makubwa
Ahsante Mkuu
 
Hii nchi kuna wakati unakaa na kutafakari, unajiuliza kama huko kwenye ngazi za maamuzi kuna angalao hata mtu mmoja mwenye akili, anayetumia muda wake kutafakari na kuja na chochote, hata watu wakasema, Mungu mkubwa, angalao tumempata huyu mmoja mwenye akili.

TRA mawazo yao wote wanaamini kuweka kodi nyingi na kubwa ni kuongeza mapato. Akili ndogo huenda kwenye mbinu zinazotumia akili ndogo kama hizo. Wajifunze kutoka Dubai au Hongkong ni kwa namna gani kodi ndogo imeweza kuhuisha uchumi na biashara, na kuongeza makusanyo ya kodi.

Mtu mwenye akili hujibana asile mbegu ili mbegu ikipandwa itoe mazao mengi zaidi, atakapouza atapata mapato zaidi. Mtu mpumbavu akipewa mbegu huiuza mbegu hiyo ili apate mapato siku hiyo hiyo. TRA wanauza mbegu badala ya kuipanda ili wavune kesho.
 
Watanzania wengi ni wa kipato cha chini unamwambie ananue gari mpya ni sawa sawa kumtukana.

Kama kununua nguo mpya inakuwa mtihani sembuse gari jipya, gari mipya ya milioni 40 unatakiwa ulipe ushuru milioni 20 watanzania wangapi wataweza.

Nchi kama South Africa wameweka ushuru mkubwa mno wa magari kutoka nje sababu kubwa ni kulinda viwanda vyao vyao ndani na gari kwao ni bei rahisi kila mwananchi wa kipato cha chini anaweza kumiliki gari.

Tanzania ushuru wa magari upo juu sana mtu akimiliki gari unaonekana tajiri na jamaa zake wanamuangalia kama shujaa.

Haiwezekani gari kama Toyota IST unailipia milioni 8 mpaka 10.

Uko sahihi kabisa. Ushuru ingekuwa ya kawaida hata kule vijijini Magari yangekuwepo na usafirishaji wa bidhaa ingekuwa rahisi zaidi. Ushuru iwekwe reasonable na zibandikwe zijulikane wazi ili unapoagiza gari unajipangia kabisa pesa yako ya kulipia ushuru. Na itasaidia kuondoa mianya ya rushwa kwani utakuwa unajua kabisa kodi ni kiasi gani kuliko sasa unaweza kuongezewa ushuru jinsi afisa anavyotaka
 
TRA nathubutu kusema kuwa tafakari ni zero, ubunifu ni zero, mipango ni zero, ni watu ambao upeo wao unaishia leo. hawana uwezo wa kuiona kesho, hawana uwezo wa kubuni wafanye nini ili kesho iwe bora kuliko leo. Hawa watu walistahili kuwa wabunifu na washauri wa serikali, walistahili kuiambia serikali ni kwa namna gani serikali ifanye ili walipa kodi wasione kodi ni mateso lakini wakati huo huo serikali ikizidi kupata zaidi na zaidi. Hapo ndiyo unaweza kumtofautisha mtu mwenye akili na mpumbavu. TRA walistahili kuchochea uwekezaji na uzalishaji lakini matendo yao yanaua uwekezaji na kuinuka kwa wajasiriamali.

Singapore walipoamua kulinda misitu yao, hawakuwazuia watu wao kukata miti ya kuchoma mkaa badala yake walitoa ruzuku kwenye majiko ya kupikia, umeme wa majumbani na gas ya kupikia. Ikafikia wakati ikaonekana kutumia mkaa wa kuni kupikia gharama yake ni mara mbili ya kupikia kwa kutumia gas au umeme. watu wakawa hawanunui mkaa, wachoma mkaa wakapotea kwa sababu hawakuwa na wateja.

Tanzania walipotaka kulinda misitu, kila mkuu wa wilaya aliwaambia watu kuwa kuanzia leo marufuku kukata miti. Wakuu wa Wilaya wakati wanatangaza hayo, wananchi maeneo mengi hawana misitu ya kupandwa, hawana umeme, hawana gas ya kupikia, na kulikokuwa na umeme na gas majiko bei juu, umeme bei juu, na kupikia mkaa ni gharama nafuu karibia ya mara nne ya kutumia umeme. Matamko kama hayo ni ya kuchochea rushwa maana yeyote mwenye akili anajua kabisa kuwa wananchi hawataweza kuacha kukata miti kwa sababu hawana nishati mbadala, na hakuna anayeweza kuishi bila ya kupika.
 
Tatizo ni kwamba wewe na wenzako hamjaelewa kwa nini kuna hizo kodi, lengo ndiyo msiagize magari chakavu hapa kwetu badala yake nenda CMC au toyota TZ kanunue hiyo gari! Dunia nzima hufanya hivi, hebu jaribu kutoa gari TZ kupeleka Japan hata gari hiyo hiyo uliyoinunua huko jaribu kuirudisha halafu uone watakuchaji kiasi gani!
Acha ujinga wewe ni watanzania wangapi wana uwezo wa kununua gari CMC ?na huko CMC unaweza kupata gari ya 2002 au 2005 usitupotoshe wewe mwenyewe umevaa mitumba nguo zote na kila kitu unachotumia ni used ki ukweli TRA wanatukomoa na kaa ujue kuwa gari siku hizi siyo anasa tena hizo bia na sigara ndiyo zimebaki kuwa anasa
 
Hii nchi kuna wakati unakaa na kutafakari, unajiuliza kama huko kwenye ngazi za maamuzi kuna angalao hata mtu mmoja mwenye akili, anayetumia muda wake kutafakari na kuja na chochote, hata watu wakasema, Mungu mkubwa, angalao tumempata huyu mmoja mwenye akili.

TRA mawazo yao wote wanaamini kuweka kodi nyingi na kubwa ni kuongeza mapato. Akili ndogo huenda kwenye mbinu zinazotumia akili ndogo kama hizo. Wajifunze kutoka Dubai au Hongkong ni kwa namna gani kodi ndogo imeweza kuhuisha uchumi na biashara, na kuongeza makusanyo ya kodi.

Mtu mwenye akili hujibana asile mbegu ili mbegu ikipandwa itoe mazao mengi zaidi, atakapouza atapata mapato zaidi. Mtu mpumbavu akipewa mbegu huiuza mbegu hiyo ili apate mapato siku hiyo hiyo. TRA wanauza mbegu badala ya kuipanda ili wavune kesho.

Nimewahi kuwaza kwanini serikali isilegeze kodi kwenye imports za magari ili yawe mengi sana nchini then yawe vyanzo vya kodi?
 
Bila shaka malalamiko mengi yameandikwa kuhusiana na mada hii, sipendi ifikirike kwamba ni kitu kipya, ila kujaribu kukumbushia tena, pangine hawa wenzetu wanafikiria kwamba wannchi tumeridhika kwa kukaa kimya.

Kwanza nitoe mfano wa maheasabu nikizingatia kichakata chao TRA;

Used Motor Vehicles Valuation Calculator

Reference Number 1516307575
Make: BMW
Model: X5
Body Type: SUV
Year of Manufacture: 2002
Fuel Type: PETROL
Engine Capacity: 2001 - 2500 CC
Customs Value CIF (USD): 4805.46
Import Duty (USD): 1201.36
Excise Duty (USD): 600.68
Excise Duty due to Age (USD): 1802.05
VAT (USD): 1513.72
Custom Processing Fee (USD): 28.83
Railway Dev Levy (USD): 72.08
Total Import Taxes (USD): 5219
Total Import Taxes (TSHS):
11434829
Vehicle Registration Tax (TSHS):
380000.00

Hebu oneni mlolongo wa majina ya kodi kwa majina tofauti tofauti unzvyoongeza gharama ya uagizaji wa magari;

Ki-uchumi, kodi nyingi kama hizi huwa zina maana mbili kwa pamoja au pengine mojawapo;

1. Kuzuia/kupunguza bidhaa za nje zisifurike katika soko la ndani, ili kuimarisha viwanda vya ndani vinavyotengeneza kwa wingi na kwa ufanisi bidhaa hiyo hiyo au inayokikdhi mahitaji kama hiyo inayotakiwa kuagizwa nje, au kuzuia kabisa bidhaa mbovu zinazoweza kuharibu mazingira na afya ya wananchi na pia kuongeza ajira za ndani.

2. Kuongeza pato litokanalo na kodi; hii huwa ni kwa muda mfupi kwani ikiendelea kwa muda mrefu pato halitaongezeka, kwani watu wataacha kununua, na kushusha pato tegemewa.

Kwa hiyo TRA , wakiwa wanafanya kazi yao kwa maslahi ya wananchi ni lazima wafikirie namna ya kutoa huduma, kwa kuweka mifumo saidizi, itakayosaidia wananchi kupenda kulipa kodi, na kuilipa kwa hamasa.

Wanapashwa kuainisha malengo yao, kama yanafanana na la kwanza au la pili; kwangu mimi naona lile la pili haliwaungi mkono sana kwa sababu makato haya yamekuwa yanaongezeka tu kwa muda mrefu sana sasa, na kuondoa dhana ya makusanyo yapaswayo kuleta faida kwa muda mfupi.

Kwa lile la kwanza, pia haliwaungi mkono kwa sababu hatuna kiwanda cha ndani tunachokikinga na bidhaa za nje.

Napata fikra kwamba TRA hawapendi kufanya tathmini itakayosaidia wananchi, ili nao angalau wapendeke, wasionekane kama wanatoka sayari ingine (Aliens), kwa sababu wao kodi hizi haziwahusu; pamoja na wabunge.

Mawazo yangu ya kuhitimisha ni kwamba kitengo cha elimu kwa mlipa kodi wanapashwa kutoa elimu kwa ukamilifu, siyo kuishia tu kwenye matakwa yao kisheria tu. Utamsikia akisema ati kama maendeleo hayaonekani pamoja na utoaji kodi hil si swala lao, hawaoni kwamba wapo kwenye mnyororo wa maendeleo (development chain)? na kwamba wao kwa kuwa huenda kuonana na walipa kodi moja kwa moja, wanakumbana na vikwazo, na kutokuwa tayari kwa sababu hawakamilishi mnyororo huu?

Kwa mlolongo huo hapo juu, ni wazi kwamba wengi mno wataacha kuagiza bidhaa hizi, na hivo kupunguza pato ambalo TRA wangekusanya kidogo kidogo lakini kwa walipaji wazuri wengi; pia, inaongeza incentive ya watu kukwepa kodi.

Fikirieni na mufanyie kazi haya malalamiko.

Mutanim umetiririka kwa takwimu. TRA hawana jipya, kodi maana yake ni win-win. Sisi walaji tunapunjwa sana. Mjapan yeye anacalculate profit margin anakuachia mzigo na nchi yako.
 
Nchi yetu imekuwa na kodi nyingi na kubwa lakini mafanikio yake kidogo. Kwa mfano mtu yupo Mwanza, anakwenda Uganda ananunua Laptop kwa bei nafuu kuliko hapa Tanzania. Mimi huwa najiuliza hivi hii inakuwa je sipati jibu. Uganda ni land locked country, bidhaa zao kama hawakupitisha hapa basi watapitisha Kenya inakuwa je wao bidhaa zao ziwe chini kwa bei kuliko hapa kwetu. Tatizo Kodi zisizokuwa na tija nyingi zinaingia kwenye mifuko ya watu.
Hata spare za magari, Uganda is very cheap, nadhani wanatumia ungo kuagiza toka japan, hivyo havipiti Dar wala mombasa
 
Tatizo ni kwamba wewe na wenzako hamjaelewa kwa nini kuna hizo kodi, lengo ndiyo msiagize magari chakavu hapa kwetu badala yake nenda CMC au toyota TZ kanunue hiyo gari! Dunia nzima hufanya hivi, hebu jaribu kutoa gari TZ kupeleka Japan hata gari hiyo hiyo uliyoinunua huko jaribu kuirudisha halafu uone watakuchaji kiasi gani!
GDP per capita ya mtanzania wastani ni US$ 981 kwa mwaka, hiyo inajumuisha nyumba, mtaji, nk. Toyota Tanzania gari mpya ni tsh ngapi wewe ngedere?
 
Back
Top Bottom