Bila shaka malalamiko mengi yameandikwa kuhusiana na mada hii, sipendi ifikirike kwamba ni kitu kipya, ila kujaribu kukumbushia tena, pangine hawa wenzetu wanafikiria kwamba wannchi tumeridhika kwa kukaa kimya.
Kwanza nitoe mfano wa maheasabu nikizingatia kichakata chao TRA;
Used Motor Vehicles Valuation Calculator
Reference Number 1516307575
Make: BMW
Model: X5
Body Type: SUV
Year of Manufacture: 2002
Fuel Type: PETROL
Engine Capacity: 2001 - 2500 CC
Customs Value CIF (USD): 4805.46
Import Duty (USD): 1201.36
Excise Duty (USD): 600.68
Excise Duty due to Age (USD): 1802.05
VAT (USD): 1513.72
Custom Processing Fee (USD): 28.83
Railway Dev Levy (USD): 72.08
Total Import Taxes (USD): 5219
Total Import Taxes (TSHS): 11434829
Vehicle Registration Tax (TSHS): 380000.00
Hebu oneni mlolongo wa majina ya kodi kwa majina tofauti tofauti unzvyoongeza gharama ya uagizaji wa magari;
Ki-uchumi, kodi nyingi kama hizi huwa zina maana mbili kwa pamoja au pengine mojawapo;
1. Kuzuia/kupunguza bidhaa za nje zisifurike katika soko la ndani, ili kuimarisha viwanda vya ndani vinavyotengeneza kwa wingi na kwa ufanisi bidhaa hiyo hiyo au inayokikdhi mahitaji kama hiyo inayotakiwa kuagizwa nje, au kuzuia kabisa bidhaa mbovu zinazoweza kuharibu mazingira na afya ya wananchi na pia kuongeza ajira za ndani.
2. Kuongeza pato litokanalo na kodi; hii huwa ni kwa muda mfupi kwani ikiendelea kwa muda mrefu pato halitaongezeka, kwani watu wataacha kununua, na kushusha pato tegemewa.
Kwa hiyo TRA , wakiwa wanafanya kazi yao kwa maslahi ya wananchi ni lazima wafikirie namna ya kutoa huduma, kwa kuweka mifumo saidizi, itakayosaidia wananchi kupenda kulipa kodi, na kuilipa kwa hamasa.
Wanapashwa kuainisha malengo yao, kama yanafanana na la kwanza au la pili; kwangu mimi naona lile la pili haliwaungi mkono sana kwa sababu makato haya yamekuwa yanaongezeka tu kwa muda mrefu sana sasa, na kuondoa dhana ya makusanyo yapaswayo kuleta faida kwa muda mfupi.
Kwa lile la kwanza, pia haliwaungi mkono kwa sababu hatuna kiwanda cha ndani tunachokikinga na bidhaa za nje.
Napata fikra kwamba TRA hawapendi kufanya tathmini itakayosaidia wananchi, ili nao angalau wapendeke, wasionekane kama wanatoka sayari ingine (Aliens), kwa sababu wao kodi hizi haziwahusu; pamoja na wabunge.
Mawazo yangu ya kuhitimisha ni kwamba kitengo cha elimu kwa mlipa kodi wanapashwa kutoa elimu kwa ukamilifu, siyo kuishia tu kwenye matakwa yao kisheria tu. Utamsikia akisema ati kama maendeleo hayaonekani pamoja na utoaji kodi hil si swala lao, hawaoni kwamba wapo kwenye mnyororo wa maendeleo (development chain)? na kwamba wao kwa kuwa huenda kuonana na walipa kodi moja kwa moja, wanakumbana na vikwazo, na kutokuwa tayari kwa sababu hawakamilishi mnyororo huu?
Kwa mlolongo huo hapo juu, ni wazi kwamba wengi mno wataacha kuagiza bidhaa hizi, na hivo kupunguza pato ambalo TRA wangekusanya kidogo kidogo lakini kwa walipaji wazuri wengi; pia, inaongeza incentive ya watu kukwepa kodi.
Fikirieni na mufanyie kazi haya malalamiko.