TRA na kodi za kuagiza magari

TRA na kodi za kuagiza magari

Tatizo ni kwamba wewe na wenzako hamjaelewa kwa nini kuna hizo kodi, lengo ndiyo msiagize magari chakavu hapa kwetu badala yake nenda CMC au toyota TZ kanunue hiyo gari! Dunia nzima hufanya hivi, hebu jaribu kutoa gari TZ kupeleka Japan hata gari hiyo hiyo uliyoinunua huko jaribu kuirudisha halafu uone watakuchaji kiasi gani!
Ikiwa mpya haitoi unafuu bado kwasababu wanafanyia mahesabu customs value kubwa kwasababu ya upya wa gari. sana sana ule ushuru wa uchakavu ndo utaondolewa na bado ushuru mwingine uko palepale.
 
Magari chakavu yanaharibu mazingira na ndiyo maana huko mnakoyanunua yanakuwa bei rahisi kwanza kuna wengine hata hupewa bure kwa maana huko hayaruhusiwi tena, hiyo ndiyo sababu!

Acha uongo fikiria kabla ya kuandika katika dunia ya sasa nani atakupa gari bure kutoka Marekani au UK. UK gari ambayo hairuhusiwi kutembea utalipitisha wapi kuipeleka Tanzania. Kwa akili yako unafikiria naweza kununua gari mbovu kutoka UK kuleta Tanzania???. Ninunue gari pound £2000 unajua £2000 ni pesa ngapi ya TZ. £2000x3500= this 7m ongeza £1000 ya kuisafirisha jumla ni tshs 10,500,000 niambie hapo nani mwenye akili mbovu wa kuweza kupoteza 10m kwa kununua gari mbovu ya kuja kukaa nalo miaka miwili au mitatu. Na hapo hajalipa ushuru.

Kama mnaongelea Magari mabovu na yanayochafua mazingira ni hayo Magari yenu na malori ya tangu miaka ya sabin ndio yanayochafua mazingira. Kwanza mngeyasafisha Magari yenu mabovu. Wanaoagiza Magari kutoka nje wanasaidia nchi angalau kuwa na magari yenye ubora kuliko mengi yaliyopo hapo.

Kinachochangia kodi kuwa kubwa kwa Wanaoagiza Magari nje ni baadhi ya vigogo serikalini ambao hawataki watu wa chini wawe na Magari mazuri. Wanachotaka wao viongozi ndio wawe na Magari mazuri kwasababu hawalipi kodi na Magari mengi ni za serikali na wanauziana baada ya muda fulani. Pia viongozi wengi hawalipi ushuru kama kulipia wanalipa ushuru kidogo baada ya kupewa punguzo. Wangeweka kodi inayoeleweka wengi tungeweza kununua hata Magari za mwaka huu na nchi yetu lisingekuwa na Magari mabovu mengi.
 
Naona na Railway Dev levy imo.... Tusishangae wakiweka na kodi ya maendeleo ya kilimo humo maana ndio tunakoelekea
 
Ndugu Barbarosa, huwa unatetea sana tra kwenye maada za kodi za magari tena kwa hoja hiyo moja tu ya uchakavu kitu ambacho ni kizuri. Kama ubishi wako ni wa logiki hebu fanya kitu hiki :ingia kwenye calculator ya tra tumia gari hili la meta mada kwa kubadili tu mwaka wa kutengeneza gari hilo kwenda 2010. Jumla ya kodi itaongezeka zaidi Kuliko gari la 2002!!!!, ukiangalia contribution ya kila kipengele cha kodi kwenye jumla kuu, gari la 2002 lina kodi kubwa ya uchakavu lakini jumla ya kodi zoote ni ndogo ukilinganisha na gari jipya. Hebu angalia hapo kama kweli kuna encouragement ya kuagiza magari mapya kama unavyo dai uzingatie pia kuwa mlipaji ni mmoja hivyo atazingatia jumla ya kodi atayo lipa.
 
Tatizo ni kwamba wewe na wenzako hamjaelewa kwa nini kuna hizo kodi, lengo ndiyo msiagize magari chakavu hapa kwetu badala yake nenda CMC au toyota TZ kanunue hiyo gari! Dunia nzima hufanya hivi, hebu jaribu kutoa gari TZ kupeleka Japan hata gari hiyo hiyo uliyoinunua huko jaribu kuirudisha halafu uone watakuchaji kiasi gani!

Sina uhakika kama ni kweli kauli yako! kwa sababu hayo mapya pia yanaagizwa toka yalipotengenezwa, ujumbe najaribu kusema hapa ni mlolongo wa kodi uliokithiri, jaribu uagize gari ya 2013, utaona kodi ya uchakavu ni 0, yaani hamna kodi! Lakini kodi zingine zinapandana mpaka mara mbili ya bei ya gari. Tuongee kiuchumi na kufafanua kwa details tafadhali!
 
Hili nakuunga mkono hata kodi ya mapato ya biashara ni kubwa sana inayopelekea kuua biashara au kutafuta njia ya kukwepa
 
TRA, tai nyingi shingoni, wezi wa kodi tangu mkurugenzi mkuu hadi mfagiaji! Ni taasisi yenye watumishi wenye sifa za chini kabisa kielimu. Utawasikia eti nilisoma chuo cha kodi. Kwa ujumla watu wenye tabia na elimu ya aina hii, hawana ubunifu maana hawajawahi kulazimika kubuni mambo.

Kamishna wa tra anapoambiwa kuongeza mapato, anakimbilia bia na magari. Tofauti na bia, gari ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Ukikosa utatafuta baiskeli au tukutuku. TRA wanasababisha gari ionekane ni utajili wa aina fulani. Ukichanganya na ulimbukeni wa maskini wenzetu wanaotaka kujionyesha wanazo, tra wanaona ni sawa tu. Je, wamejiuliza kwa nini sasa tuna vigari vidogo viiingi mijini? Wanaelewa mahitaji ya lazima ya mafuta kuhudumia kigari cha watu wawili?

Nashauri ajira za TRA zifanyike upya. Wanaojiita graduate wa chuo cha kodi, watafute ajira mpya au wakasome wapate uelewa.
Wanaweza kubadilika wakibadilishwa
 
TRA haipangi viwango vya kodi. Wao kazi ni kukusanya kodi kwa mujibu wa sheria zilizotungwa na bunge na kanuni toka wizara ya fedha.
Lawama hizi zielekezwe kwenye serikali iliyopo madarakani na bunge lililopitisha viwango hivyo .
Tatizo kubwa la serikali yetu ni ufinyu wa vyanzo vya kodi. Kuna vyanzo havijatumiwa hadi leo. Mfano mzuri ni kodi ya nyumba.
Tatizo lingine ni rushwa inayochochewa na misamaha kibao isiyo na tija.
 
sibonoke Tra kuna kitengo cha utafiti wa kodi zoote na kinatumia gharama nyingi pia na wao ndio wanashauri kwa kupitia wizara ya fedha.
 
Wewe na we KILAKA, kwa kipato kipi uzuie wananchi kuagiza magari chakavu? Nchi hii ya ajabu kweli badala ya kuexempt kodi wananchi wenye kipato cha chini na watumishi wenye kipato kidogo, tunaexempt wabunge... Pathetic isn't it

Very right, halafu tunategemea watasimamia kwa uchungu upi mapato ambayo hawachangii! Na wanaendelea kuomba waongezewe posho za vikao, pia wanaomba rushwa kwa nguvu zote!
 
Bila shaka malalamiko mengi yameandikwa kuhusiana na mada hii, sipendi ifikirike kwamba ni kitu kipya, ila kujaribu kukumbushia tena, pangine hawa wenzetu wanafikiria kwamba wannchi tumeridhika kwa kukaa kimya.

Kwanza nitoe mfano wa maheasabu nikizingatia kichakata chao TRA;

Used Motor Vehicles Valuation Calculator

Reference Number 1516307575
Make: BMW
Model: X5
Body Type: SUV
Year of Manufacture: 2002
Fuel Type: PETROL
Engine Capacity: 2001 - 2500 CC
Customs Value CIF (USD): 4805.46
Import Duty (USD): 1201.36
Excise Duty (USD): 600.68
Excise Duty due to Age (USD): 1802.05
VAT (USD): 1513.72
Custom Processing Fee (USD): 28.83
Railway Dev Levy (USD): 72.08
Total Import Taxes (USD): 5219
Total Import Taxes (TSHS):
11434829
Vehicle Registration Tax (TSHS):
380000.00

Hebu oneni mlolongo wa majina ya kodi kwa majina tofauti tofauti unzvyoongeza gharama ya uagizaji wa magari;

Ki-uchumi, kodi nyingi kama hizi huwa zina maana mbili kwa pamoja au pengine mojawapo;

1. Kuzuia/kupunguza bidhaa za nje zisifurike katika soko la ndani, ili kuimarisha viwanda vya ndani vinavyotengeneza kwa wingi na kwa ufanisi bidhaa hiyo hiyo au inayokikdhi mahitaji kama hiyo inayotakiwa kuagizwa nje, au kuzuia kabisa bidhaa mbovu zinazoweza kuharibu mazingira na afya ya wananchi na pia kuongeza ajira za ndani.

2. Kuongeza pato litokanalo na kodi; hii huwa ni kwa muda mfupi kwani ikiendelea kwa muda mrefu pato halitaongezeka, kwani watu wataacha kununua, na kushusha pato tegemewa.

Kwa hiyo TRA , wakiwa wanafanya kazi yao kwa maslahi ya wananchi ni lazima wafikirie namna ya kutoa huduma, kwa kuweka mifumo saidizi, itakayosaidia wananchi kupenda kulipa kodi, na kuilipa kwa hamasa.

Wanapashwa kuainisha malengo yao, kama yanafanana na la kwanza au la pili; kwangu mimi naona lile la pili haliwaungi mkono sana kwa sababu makato haya yamekuwa yanaongezeka tu kwa muda mrefu sana sasa, na kuondoa dhana ya makusanyo yapaswayo kuleta faida kwa muda mfupi.

Kwa lile la kwanza, pia haliwaungi mkono kwa sababu hatuna kiwanda cha ndani tunachokikinga na bidhaa za nje.

Napata fikra kwamba TRA hawapendi kufanya tathmini itakayosaidia wananchi, ili nao angalau wapendeke, wasionekane kama wanatoka sayari ingine (Aliens), kwa sababu wao kodi hizi haziwahusu; pamoja na wabunge.

Mawazo yangu ya kuhitimisha ni kwamba kitengo cha elimu kwa mlipa kodi wanapashwa kutoa elimu kwa ukamilifu, siyo kuishia tu kwenye matakwa yao kisheria tu. Utamsikia akisema ati kama maendeleo hayaonekani pamoja na utoaji kodi hil si swala lao, hawaoni kwamba wapo kwenye mnyororo wa maendeleo (development chain)? na kwamba wao kwa kuwa huenda kuonana na walipa kodi moja kwa moja, wanakumbana na vikwazo, na kutokuwa tayari kwa sababu hawakamilishi mnyororo huu?

Kwa mlolongo huo hapo juu, ni wazi kwamba wengi mno wataacha kuagiza bidhaa hizi, na hivo kupunguza pato ambalo TRA wangekusanya kidogo kidogo lakini kwa walipaji wazuri wengi; pia, inaongeza incentive ya watu kukwepa kodi.

Fikirieni na mufanyie kazi haya malalamiko.

Ni suala la sheria, mapato yote yapo kwenye sheria yang kodi ya mwaka iliyopitishwa na bunge 2015 unapaswa kuwaambia akina mawaziri hususan msando ni mtaalamu wa kodi atalishughulikia,
Pia unapaswa kufikiria kuwa magari ya zaman au used ni uchafu na ndio maana nchi nyingine haziuzwi unalipia tu pesa ya kadi unachukua gar kwenye madampo ila shart litoke nchini mwao
 
Tatizo ni kwamba wewe na wenzako hamjaelewa kwa nini kuna hizo kodi, lengo ndiyo msiagize magari chakavu hapa kwetu badala yake nenda CMC au toyota TZ kanunue hiyo gari! Dunia nzima hufanya hivi, hebu jaribu kutoa gari TZ kupeleka Japan hata gari hiyo hiyo uliyoinunua huko jaribu kuirudisha halafu uone watakuchaji kiasi gani!
unajua kodi ya gari jipya...usiongee bila research
 
Ndugu Barbarosa, huwa unatetea sana tra kwenye maada za kodi za magari tena kwa hoja hiyo moja tu ya uchakavu kitu ambacho ni kizuri. Kama ubishi wako ni wa logiki hebu fanya kitu hiki :ingia kwenye calculator ya tra tumia gari hili la meta mada kwa kubadili tu mwaka wa kutengeneza gari hilo kwenda 2010. Jumla ya kodi itaongezeka zaidi Kuliko gari la 2002!!!!, ukiangalia contribution ya kila kipengele cha kodi kwenye jumla kuu, gari la 2002 lina kodi kubwa ya uchakavu lakini jumla ya kodi zoote ni ndogo ukilinganisha na gari jipya. Hebu angalia hapo kama kweli kuna encouragement ya kuagiza magari mapya kama unavyo dai uzingatie pia kuwa mlipaji ni mmoja hivyo atazingatia jumla ya kodi atayo lipa.
hafanyi research anaongea tuuu
 
Gari mpya ushuru wake 50% wangapi wataweza mkuu gari used nazo ushuru wake balaa utadhani Tanzania kuna kiwanda cha magari wanalinda soko la ndani.
kweli mkuu....tatizo letu ni kushindwa kutanua wigo wa kodi
 
Tatizo ni sheria zetu za kodi, TRA wanatekeleza sheria, ukiwalaumu nadhani si sahihi tulifanya makosa kuruhusu uchumi utumikie siasa badala ya siasa kutumikia uchumi. Ila mawazo yako ni mazuri
 
Ukiwa mkoani Kagera ni bora kununua vitu toka Uganda, kwanza vina ubora ukilinganisha na vya hapa Tz mfano nguo, viatu, hata vifaa vya kutumia umeme.

unachangia ukuaji wa viwanda vya uganda.. ukisikia akili mbovu ndio hii!
 
Tatizo ni kwamba wewe na wenzako hamjaelewa kwa nini kuna hizo kodi, lengo ndiyo msiagize magari chakavu hapa kwetu badala yake nenda CMC au toyota TZ kanunue hiyo gari! Dunia nzima hufanya hivi, hebu jaribu kutoa gari TZ kupeleka Japan hata gari hiyo hiyo uliyoinunua huko jaribu kuirudisha halafu uone watakuchaji kiasi gani!
Mbona sasa kodi ya Gari chakavu haina utofauti na mpya?
 
Ukipigiwa hesabu hiyo wewe mwenyewe utaomba upunguziwe.Hapo ndipo utakapoambiwa utoe ulaji ili upunguziwe gharama!
 
Back
Top Bottom