TRA-KUBORESHA TAARIFA mnataka Acc.# yangu ya Benki iweje?

joshua_ok

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
12,803
2,000
Wakuu nimepitia tovuti ya TRA nikakuta fomu ya Kuboresha Taarifa za Mlipa Kodi, sasa humo ndani wantaka utoe details zako kama UMEOA ama bado, una akaunti wapi (benki gani, Jina la benki, tawi, namba ya akaunti, jina la akaunti na kama akaunti ni Local/ Foreign Currency!!.
MASWALI:
1. Hizi details mnataka kuzipeleka wapi kwa mtu (binafsi) ambaye anaboresha taarifa zake?
na wala hafanyi biashara?
2. Nina uhakika gani nikitoa taarifa hizi kuwa zitakuwa salama, na hazitadukuliwa na wahalifu?
3. Hali yangu ya NDOA (Married/Single/Divorced) inahusiana vipi na mambo ya KODI?

** Ningeshauri hebu pitieni upya hiyo fomu kuondoa baadhi ya maswali ya kutaka details nyiingi za mlipa kodi, maana kwa namna hii ama watu watadanganya kwa kuweka taarifa za uongo au hawataboresha kabisa hizo taarifa hivyo mtakosa mapato.

NB: Nimeambatanisha na fomu husika.
 

Attachments

franktemu123

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
1,144
2,000
Daah yaani mtu akifanikiwa kuingia/kuipata hiyo fomu yako ya.TRA Anapata information zako karibia zote kasoro HIV status tu.
 

joshua_ok

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
12,803
2,000
Mimi nimeshauri tu wandugu ili kuboresha zoezi, tunajenga nyumba moja ya nn kugombea fito?
 

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
5,055
2,000
Tembelea ofisi ya TRA ya karibu nawe kamuone Officer elimu kwa mlipakodi akuelezee kwa nini muundo wa hiyo form uko hivyo na umuhimu wa hizo taarifa kuhusiana na kazi za kikodi.

Inamaana wewe hujui umuhimu wa taarifa za bank account kwenye maswala ya kikodi?

Inamaana hujui uhusiano wa mwenza au familia kwenye maswala ya kikodi?

Zingatia ushauri wa hapo juu hutakuwa yule yule !
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom