DOKEZO Mfumo wa kupata TIN Namba (TRA) una shida, unatengeneza mazingira ya kutoa rushwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Juni 2023 (sikumbuki tarehe rasmi) Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitoa taarifa kuwa hadi kufikia Desemba 31, 2023 kila mtu mzima Nchini Tanzania anatakiwa kuwa na Namba ya Mlipa Kodi (TIN), hayo yote walinukuliwa wakiyasema kupitia vyombo vya habari.

Lakini Juni 8, 2023, TRA ilitoa taarifa ya ufafanuzi zaidi kuwa usajili wa TIN kwa Wananchi wote wenye umri wa kuanzia miaka 18 sio kwa ajili ya biashara bali kwa utambuzi kama ilivyo katika usajili wa Kitambulisho cha Taifa (NIDA).

Baada ya maelezo hayo nije kwenye hoja yangu ya msingi: Kama TRA wanaweza kuwa na mipango yao hiyo, kwa hiki kinachoendelea ninachotaka kukisema ni wazi kuwa hawa watu ama hawapo ‘serious’ au hawajui wanachokifanya au kuna watu wachache ambao nia yao ni kuendelea kuirudisha nyuma mamlaka hiyo.

Mimi ni mmoja wa Wafanyabiashara wa muda mrefu, nimefanya uchunguzi kwa watu kadhaa pia kwa hiki kilichonitokea nao kimewatokea.

Kila mtu anajua kupata TIN namba ni bure lakini imekuwa mtihani mkubwa kuipata kwa miezi ya hivi karibuni.

Wanasema unaweza kupata TIN mtandaoni (online), nimefanya hivyo lakini mfumo (system) wao ukawa unagoma, una-load tu ikifika mwisho.

TIN Namba ninayotaka kuifunguwa ni ya Biashara inagoma, nikajaribu TIN ya binafsi napo sikufanikiwa.

Nikajaribu kuuliza kwa wenzangu ambao wanajishughulisha na TRA kila siku, nikajibiwa kuwa huko online ngoma haiwezekani kukubali imewekwa kama geresha tu, mpaka niende pale ofisini na nikifika kama ni TIN binafsi basi Wafanyakazi wanaweza kunisaidia nikafanikiwa kupata, kwa kuwa wanajua hiyo haina mpunga.

Kwa wanaotaka TIN za biashara niwanajibiwa vilevile kama ambavyo wanajibiwa mtandaoni kuwa iko pending au ina load tu.

Nikajulishwa kuwa nikitaka kufanikiwa basi lazima niwatafute staff wanao-deal na hiyo kitu pembeni kisha niwashike mkono watanifanikisha zoezi langu fasta tu.

Nikafanya kama nilivyoambiwa, nikaenda pale ofisini kwao Mwenge (Dar es Salaam), nikapata majibu yaleyale kama nilivyoambiwa na watu kuwa niendelee kusubiri.

Inauma sana, hivi kweli TIN ya biashara ni ya kusubiri zaidi ya mwezi mmoja kisa system?

Hapa ninavyoandika nina zaidi ya mwezi sijafanikiwa kupata TIN ya biashara na ninachoona bora niende tu nikawashike mkono hao watu nilioambiwa lakini moyoni naumia, tutaendelea na hali kama hii mpaka lini?

Ndio maana kuna watu wengi wanaamua kufanya biashara kimagendo kwa mambo ya usumbufu kama haya, mazingira yanatengenezwa ili upate ugumu na ulazimike kutoa chochote.

Serikali Kuu na TAKUKURU saidieni Wafanyabiashara wanalazimishwa kutoa rushwa huku.
 
Kwanza kabisa tunawapa pole wale wote ambao wamepata changamoto ya kutopata TIN. Kumekuwepo na changamoto kwa baadhi ya waombaji kupata TIN, tatizo halikuwa kubwa na tumeshachukua hatua.Endapo bado utapata changamoto yoyote katika kupata TIN tunaomba uwasiliane nasi kwa namba za bure 0800780078, 0800110016 kuanzia saa 2 kamili asubuhi mpaka saa 1 kamili jioni siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa au barua pepe ; huduma@tra.go.tz au whatsApp 0744233333 tuweze kukusaidia.
 
sipo nchini website yenu inaload tu
 
Acheni saundi
Fafanua vizuri jinsi ya kupata TIN online nina miezi minne sijafanikisha
Ni ina load tu
 
Acheni saundi
Fafanua vizuri jinsi ya kupata TIN online nina miezi minne sijafanikisha
Ni ina load tu
Mlipakodi wetu. Tafadhali tunaomba tupigie simu 0800780078 au tutumie whatsApp 0744233333 ili tukusaidie. Tunashukuru kwa mrejesho wako kuhusu kupata TIN online tutaendelea elimisha eneo hilo.
 
Back
Top Bottom