TRA kichaka kilichokubuhu kwa Ufisadi,Hatimaye Rais Magufuli ameliona hilo

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
584
1,000
Mimi ni muumini wa kuamini Matokeo ya Jambo flani lililofanyika ,hivyo nnasubiria Matokeo ya hatua alizo chukua huyu Mkuu wa Nchi kama nilivyo kwisha kuyaona ya kina Bade/ Mpango/Kidata/Kichere na sasa Edwin..

Nikukumbushe tu kuwa ,Mfumo ulioshindwa kutoa Matokeo flani haufai kuendelea kuwepo au kutumika.
Swala sio mfumo bali watendaji wanafanya kazi kwa mazoea sana ndo maana Rais anakuwa mkali. Sheria za kodi mbona zipo wazi iweje mtu amkadarie pasipo kufuata sheria inavyoelekeza
 
Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
584
1,000
Hizi ni Yasisi
Rais mwenyewe ni kama anatuzunguka tu na kujifanya mzalendo ina mana alikuwa haoni au hasikii habari kila siku zinatangazwa kuwa biashara zinafungwa yeye yupo kimya mpaka mapato sasa yanashuk ndo anachukua hatua ili kuendelea kudumisha dhana ya uzalendo
Mpaka sasa hatuoni rais akitoa tamko lolote kuhusu CAG pesa inapigwa watanzania tuamke
Hizi ni Taasisi nyeti sio za kukurupa ukiona Rais anafanya maamuzi ujue kajiridhisha vya kutosha
 
Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,477
2,000
Naunga mkono kwa 100%, mchango wako, uliyouasema ni kweli kabisa. Thanks mkuu
Mku ktk teuzi zote Rais bado hajapata bahati nisema kama sio Waziri Mkuu ,Jafo,Makamba ,Lukuvi hawa wanambeba sana la sivyo serikali ingezidi kupwaya.

Mfano mzuri ni pale Waziri wa mambo ya nje anapomshukuru Rais kwa kwenda kutafuta solo la mahindi na biashara nyingine Zimbabwe na Namibia sasa sijui kazi yake Waziri nini zaidi kwenda kutafuta fursa huko nje.
 
mwantui

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
1,624
2,000
Kodi ni process. ..kwa sheria hizi zilizopo zikifuatwa vilivyo hakuna duka au biashara yeyote itaendelea kuwepo
 
Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
584
1,000
Kodi ni process. ..kwa sheria hizi zilizopo zikifuatwa vilivyo hakuna duka au biashara yeyote itaendelea kuwepo
Ulimsikiliza vizuri jana Waziri wa Fedha mapendekezo aliyoyatoa jana?nini Tafsiri ya Rais kuitisha kikao na wadau wote wa biashara jana?Waziri alisema pamoja na kero zote hizo walizotoa wafanyabiashara lakini pia inabidi wazipitie upya sheria zote za kodi Nchini ili kuleta tija kwa pande zote
 
Ngisibara

JF-Expert Member
Jan 2, 2009
3,091
2,000
Rushwa kwa wafanya kazi TRA ni janga. Na kumtafuta asie kula rushwa ndani ya TRA ni sawa na kutafuta bikira wodi ya wazazi. Vijana wana taka utajiri wa haraka. Sheria ya kodi itoe jedwali la kodi la kueleweka kwa kila biashara.
Mkuu umeeleza kilio Cha watanzania ambacho wahusika hawaoni umuhimu wake wakati wanataka rushwa ikome
 
mwantui

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
1,624
2,000
Ulimsikiliza vizuri jana Waziri wa Fedha mapendekezo aliyoyatoa jana?nini Tafsiri ya Rais kuitisha kikao na wadau wote wa biashara jana?Waziri alisema pamoja na kero zote hizo walizotoa wafanyabiashara lakini pia inabidi wazipitie upya sheria zote za kodi Nchini ili kuleta tija kwa pande zote
Sheria za kodi zifanyiwe marekebisho na elimu ya kodi itolewe kwa kila ngazi ya elimu.mfanyabiashara yeye yupo kwa ajili ya profit maximization hata kama akaambiwa alipe elfu tano kwake itakua bado ni kubwa.
 
Mkwaruu

JF-Expert Member
Mar 13, 2017
2,937
2,000
Mku Mkirindi haya yafichiki kwani kila ukiangalia mambo hayaendi vizuri ninaamini hawa wateuliwa kujitahidi kujituma ili mambo yaonekana .
Ebu niambie mambo yalivyo kwa sasa na huu uchaguzi Mkuu tutawambia nini Watanzania kwani imefika mahali viongozi wakuu wa chama Bashitu na Polepole wameamua kukaa kimya baada mambo yalivyo kwani RAIA ndio wanaolia hali ya Nchi ilivyo kwa sasa.
Japo ni muda mfupi uliobakia Rais ajitahidi kujishusha kwa watendaji wake ili kuwa nao karibu kwa kuwaambia nini anataka kifanyike ili tuondoke hapa tulipo na maisha yaendelee kwani ukali sana utamkosesha mengi mazuri kutoka kwa hao watendaji wake.
Naunga mkono kwa 100%, mchango wako, uliyouasema ni kweli kabisa. Thanks mkuu
 
Mfiaukweli

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
5,630
2,000
Toka hii Taasisi ilipovunjwa na kuundwa upya kuwa Malmaka ya Mapato Tanzania tumeona mazuri yake lakini pia tumeona tatizo kubwa.

Pamoja na kwamba wamekuwa wakikusanya mapato vizuri lakini TRA imekuwa ikilalamikiwa sana wafanya biashara Nchini

Karibu asilimia kubwa ya wafanyakazi wa hii Mamlaka wamekuwa sio waaminifu kabisa,Wamekuwa wakiomba rushwa kwa wafanya biashara au kuwakadiria mapato makubwa pindi wasipopewa rushwa

Tumeona baadhi ya wafanya biashara wakifunga maduka au biashara zao kisa hawa wafanyakazi ambao sio waaminifu

Kwa mara ya kwanza tunaona Rais Magufuli akiifumua zaidi ya mara mbili pindi kunako bainika jambo au utendaji mbovu na Serikali kukosa mapato stahiki

Natumai sasa wafanyabiashara wote watakuwa wanatoa ushirikiano kwa Serikali ili hawa wafanyakazi wanaochafua taswira ya hii Taasisi waondoke

Rais Magufuli watanzania na hasa wafanya biashara wanaimani kubwa nawe pia hatujafanya makosa kukuchagua wewe na zaidi 2020 hatutafanya makosa tena.

#JPM KIOO TUELEKEACHO 2020
Alex Fredrick
afredrick59@gmail.comView attachment 1121530

Kumbe kuna biashara zinafungwa, si mlituambia zinazofunguliwa ni nyingi kuliko zinazofungwa? Imekuaje tena?
 
Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,477
2,000
Mku Mkirindi haya yafichiki kwani kila ukiangalia mambo hayaendi vizuri ninaamini hawa wateuliwa kujitahidi kujituma ili mambo yaonekana .
Ebu niambie mambo yalivyo kwa sasa na huu uchaguzi Mkuu tutawambia nini Watanzania kwani imefika mahali viongozi wakuu wa chama Bashitu na Polepole wameamua kukaa kimya baada mambo yalivyo kwani RAIA ndio wanaolia hali ya Nchi ilivyo kwa sasa.
Japo ni muda mfupi uliobakia Rais ajitahidi kujishusha kwa watendaji wake ili kuwa nao karibu kwa kuwaambia nini anataka kifanyike ili tuondoke hapa tulipo na maisha yaendelee kwani ukali sana utamkosesha mengi mazuri kutoka kwa hao watendaji wake.
Ndugu yangu Mkwaruu, kuna wakati tunafanya siasa kwa manufaa za kichama na wakati siasa kwa manufaa ya Taifa.

Bila kufikiria uchaguzi ama umma utafikiriaje, niseme machache tuu.

1. RAISE wetu na kiongozi mkuu wa chama changu, kuna mambo mengi mazuri aliyoyafanya, na machache alliyoyakosea, na hayo machache yametusababishia hasara kubwa sana.

2. Kubebwa na na ushauri wa wachache wasiokuwa na uzoefu wa kuendesha chombo kikubwa kama serekali, kuwapa nyadhifa muhimu na hasassi vijana ambao hawajabaleh kisiasa, na hawajamwaga shahawa za kisiasa, taabu yao watakuwa wanadindisha bila kujua kilekile ni kipi. Ni lazima katika miezi sita ijayo lazima awabadilishe, kuwanyamizisha sio hoja.
3. Raisi amewatelekeza walezi wa chama na nchi, ambao wangemsaidia sana.

Kuna msemo wa kiingereza, unasema NO MAN IS AN ISLAND
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom