Billal Saadat
Senior Member
- Nov 30, 2022
- 169
- 356
Walianza NEMC sasa ni zamu ya TRA kumgombanisha Rais na wananchi wake anaowapenda.
Ni ukweli usiopingika kuna Taasisi zinamuingiza Mhe. Rais katika mtego na wananchi kadiri siku zinavyokwenda, waliaanza NEMC na sasa ni zamu ya Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA).
Wizara ya fedha na biashara waswahili wanasema mkilikoroga mtalinywa.
Kwa muda mrefu mamlaka ya mapato nchini TRA imekuwa ikilalamikiwa kutokana na kutokuwa na sera rafiki za kibiashara na ukusanyaji wa mapato nchini hali inayopelekea mianya ya rushwa na ukwepaji kodi kwa kiasi kikubwa suala hili Rais Samia amekuwa akichukizwa nalo na kulikemea wakati wote.
Hali si shwari kwa upande wa kitovu chetu cha Biashara kuna tetesi za mgomo wa wafanyabiashara eneo la kariakoo kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 15-05-2023.
Sababu za kuitisha mgomo
1. Urasimu bandarini
2. Usajili wa stoo
3. Kamata kamata hovyo ya wateja kwa ukuaguzi wa risiti
Kariakoo ni soko kubwa sana hapa Afrika mashariki na kati, hili suala likuchukuliwa kwa mzaha wowote ule lina athari kubwa kwa uchumi wa nchi yetu.
Katika robo ya kwanza ya mwaka 2023 (Januari - Machi 2023 kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa ili ongezeka hadi kufikia 5..6% Kiuchumi, hii inamaanisha kuwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika kipindi cha miezi 6 uchumi umekuwa kwa kasi.
Hii ilitoka kauli ya Mhe Rais kuhusu TRA kuacha kukusanya kodi kwa mabavu kuliko changia shughuli za uchumi zinazohusu wananchi masikini kupanda na ilionesha kuwa Wananchi wetu wanazidi kutoka kwenye ufukara kwa kasi tangu awamu ya sita ianze utekelezaji na uboreshaji wa sera zake. Je tunataka kurudisha mafukara wengi zaidi kwa kutengeneza urasimu katika mamlaka yetu ya mapato..?
kwa kipindi cha miaka miwili Pato la Taifa lilifikia Sh. trilioni 200 kwa mwaka 2023 kutoka Sh. trilioni 163 ya mwaka 2021 Hizi zote ni juhudi za Rais Samia katika kusimamia Sekta ya Biashara.
Uchumi wa Tanzania umekuwa mkubwa kuliko baadhi ya nchi za Ulaya na ni wa 6 kwa ukubwa kwa nchi zote za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kazi ya kujenga ni ngumu lakini Kibini tunaweza hichi tunachokifanya kupitia TRA na NEMC tutarudi tulipotoka.
Ukuaji huu wa pato la Taifa umetokana na Rais Samia kutekeleza sera rafiki kwa sekta binafsi, ambayo imeongeza kasi ya uwekezaji, biashara na ukuaji wa uchumi nchini. Kama Rais anatekeleza sera rafiki Kwanini mamlaka yetu ya mapato zinakuwa sehemu ya kuharibu mambo haya mazuri.
kama leo TRA ikianza kuwaharass wafanyabiashara wa ndani tunatafuta kuporomoka kwa sekta ya Biashara itaathiri watu wengi, pamoja na wateja kutoka nchini Jirani wata-opt kuhamia masoko rafiki zaidi tujifunze namna ya kukusanya mapato bila taharuki ya kusumbua uchumi wetu na kumgombanisha Mhe Rais na Wafanyabiara.