TRA inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara kufanya makadirio mapema

Nyie kuna siku mliulizwa maswali kuhusu bidhaa fulani za Bakheresa mkakimbia mazima naona leo mmerudi! Mnatakiwa muwe mnajibu maswali!
 
TRA Tanzania kuna dada anafanya kazi mkoa wa Simiyu, kazi yake ni kuweka makadirio makubwa na kuomba omba rushwa, anafikiri biashara ni rahisi hivyo, jaribuni na nyie muone.
Tumepokea lalamiko hili na tutalifanyia uchunguzi na ikibainika muhusika atachukuliwa hatua kali za kisheria.TRA tunatoa wito kwa wafanyabiashara wote nchini mnapotembelea ofisi zetu kamwe msikubali toa pesa ili mpate huduma kwani huduma tunazotoa ni bure hazina garama yoyote ile.
 
Ila TRA Tanzania mngejitahidi kupunguza mlolongo wa kodi, kuna kodi nyingine ni kichekesho. Kila kitu kingekua covered na Kodi moja, sasa Unatoa Huduma moja unakutana na utitiri WA Kodi! Eti kuna kodi inaitwa SDL, WHT, VAT, sijui na nini tena......!
 
Ngugu yangu kodi zimetofautishwa ni sawa huwezi sema anayekula wali maharage alipe sawa na anayekula wali kuku. SDl nijuavyo ni kodi ambayo mtu mwenye wafanyakazi kumi na zaidi ndiye anayelipa sasa kama huna wafanyakazi au unao chini ya hapo huwezi lipa.

WHT yenyewe inatozwa kwenye baadhi ya huduma mfano umepanga jengo au frame utasikia wanaita rental yaani inakatwa abla ya mpokeaji pesa kupewa pesa yake, au wale wanaotuuzia huduma za mawasiliano mawakala huwa nao wakiwa wanalipwa kamisheni wanakatwa wht hata wafanyakazi ile wanaita paye ni WHT.

VAT ni kodi ambayo uki google utaona ni kodi ambayo anayelipa ni mnunuzi wa huduma flani na bidhaa na anayelipa ni mnunuzi siyo mfanyabiashara, ni kodi ya mlaji yaani anayetumia huduma au bidhaa hiyo. Sasa huwezi changanya sababu kila kodi inatozwa kwa eneo lake na viwango havilingani . SDL ni 3.5%, VAT ni 18% rental na mawakala wa simu wht ni 10% paye kuna 8%,20%,25% na 30%
 
Tumepokea lalamiko hili na tutalifanyia uchunguzi na ikibainika muhusika atachukuliwa hatua kali za kisheria.TRA tunatoa wito kwa wafanyabiashara wote nchini mnapotembelea ofisi zetu kamwe msikubali toa pesa ili mpate huduma kwani huduma tunazotoa ni bure hazina garama yoyote ile.
Acha ujinga wewe, usipotoa rushwa wallahi nakuapia, biashara huwezi kudumu miaka mitatu..., hebu acha kazi hapo TRA uje ufanye biashara kwa sheria hizi za sasa uone..
 
TRA Tanzania huwa mnakusanya kodi kwa maendeleo ya wananchi au maendeleo ya wanaccm?
Mm Wiki iliyopita nilifika TRA ofis ya Kimara kwa ajili ya Makadirio ila hilo foleni ni balaa ila nilikomaa balaa sasa imefika zamu yangu saa 8 mchana hivi naambiwa eti TIN yako haijahusishwa kuwa ya Biashara sasa nikajiuliza hii kazi yangu au yenu....kiukweli niliondoka nistaajubu ya Musaa sijarudi tena...wanatangaza watu wakadiriwe halafu unafika ni nyombi huku ni kupotezeana mda tu...

Staff ni wachache na wamezidiwa na umati ule watu wengi waliondoka nadhani wabadilishe mfumo wao tujikadirie tu wenyewe.....
 
Acha ujinga wewe, usipotoa rushwa wallahi nakuapia, biashara huwezi kudumu miaka mitatu..., hebu acha kazi hapo TRA uje ufanye biashara kwa sheria hizi za sasa uone..
Wenyewe wanaona ufahari kuvuka lengo la kukusanya mapato kwa mwaka, ila wakati huo wafanya biashara wanasaga meno kwa maumivu ya kodi, TRA Tanzania vueni tai hizo mje kitaa mjione biashara zilivyo sio mnaota vitambi tu kwa kuumiza watu.
 
Back
Top Bottom