BOB LUSE
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 3,585
- 2,893
Kuna Tatizo la Watanzania kufikiri na kufanya Maamuzi magumu yenye manufaa. Makadirio Kwa makampuni wanaruhusiwa kujikadiria kupitia kwenye mfumo bila Tatizo, japo nao mtandao wakati Mwingine ni tatizo.
Shida ipo Kwa Watu binafsi na walipa Kodi ambao hawajasajili makampuni tunazuiwa kufanya makadirio kwenye mfumo (online filing). Jambo hili lingeokoa muda wa mteja kukalia viti vya Serikali masaa matano mpaka SITA. Nchi zingine hata Majirani zetu, huhitaji kufuata huu urasimu.
Mazingira ya kuja kukadiriwa ana Kwa ana pia yanatoa nafasi ya kupokea rushwa Kwa Maafisa wa TRA kwakuwa wanapewa Mamlaka ya kuamua anachokiona kinafaa. Ushauri, Biashara zinafahamika, waweke viwango vya Kodi Kwa Biashara ndogo na pia kuwe na maswali kwenye mfumo ambayo mteja akijaza, mfumo ufanye makadirio ya Haki bila mtu kuja kupanga foleni maofisini.
Nipo Gongo la Mboto ofisi za TRA, kuna watu wamesimama, ofisi Zina feni kwaajili ya Wafanyakazi, Wateja wanajipepea kupata hewa nzuri na kupunguza joto, wateja wamesimama wengine mpaka nje. Mazingira sio rafiki, Maofisa wenyewe wa kukadiria Wana watu wengi, hata ukija, hujui utakaa muda gani. Teknolojia zifanye maisha yetu kuwa rahisi. Kuliko Hali ilivyo.
Sio jambo zuri kuacha kazi kuja kukaa bila kufanya kitu Kwa masaa.
Mungu Ibariki Tanzania, Tupe Akili na Hekima Kwa manufaa ya Taifa.