TRA: Hatuhusiki kwa namna yoyote ufungaji wa 'The Cask Bar' jijini Mwanza

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuujulisha Umma kuwa, haijahusika kwa namna yoyote na ufungaji wa Bar ya THE CASK iliyopo Jijini Mwanza.

Tunaomba wahusika na Umma wawasiliane na Mamlaka husika juu ya jambo hilo.


TRA.jpg

-
Pia soma
 
Kupitia taarifa yao waliyoweka kwenye mitandao ya kijamii, Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imedai kutohusika kwa namna yoyote katika ufungaji wa Bar ya 'The Cask'

Imewataka wahusika na umma kwenda kwenye mamlaka husika kuhusu jambo hilo.

Pia soma


View attachment 2719768
Yaani mkusanya kodi kakana, lakini aliyefunga kasema waliofungiwa wamekwepa kodi miaka miwili..!!!

HII NI AIBU KUBWA. BANDARI ITATUONYESHA MENGI

CC Moisemusajiografii

Equation x
 
Hayo ni mawazo ya Mkurugenzi na RC Makala full kukurupuka juzi wamesimamisha ujenzi wa jengo kubwa la kibiashara!
Hata mteuzi nae sijui huwa anahongwa au anapigwa kipapai. Makala ameshajichokea, ameonesha hawezi basi system imtupe wachukuliwe vijana bado hii nayo haitasaidia kwasababu the core engine ni katiba mbovu inayowafanya wateuliwa kuwa walamba makalio ili walinde ulaji.
 
Hii Taarifa ya kufungwa kwa The cask bar imetufumbua macho. Tafasiri ya haraka haraka ni kwamba kumbe ukijipendekeza kwa mamlaka unaweza ukafanya biashra milele bila kulipa kodi.

Je haawa matajiti wengine wakubwa wanaoshadadia CCM hali zao za ulipaji kodi zikoje?.

Leo ndo naamini maneno ya mzee mmoja huko mbeya alisema CCM kimekuwa chama cha kuficha maovu. Ukitaka mambo yako ya hOvyo yasikwame jiunge CCM.
 
Back
Top Bottom