TRA fanyeni kazi yenu kwa ufanisi! Watu hawaombi risiti na wenye maduka hawatoi risiti kikamilifu!

sambulugu

JF-Expert Member
Jun 1, 2021
3,941
7,403
Juma mosi nilienda kariakoo kununua bidhaa kwenye duka linalomirikiwa na mtu mwenye asili ya kichina mara baada ya kufika muuzaji akamiambia yafatayo

▪︎Kitu unachotaka kununua ni cha laki na hamsini ila bila risiti laki na thelathini elfu

▪︎Na ukitaka bila risiti kabisa ni laki na ishirini elfu. Wakati niko pale akaja mtu anachukua pisi kama 20 za hiyo bidhaa yule dada akaniambia kaka unamuona huyu pamoja na kwamba anachukua pisi ishirini tunamwandikia risiti ya laki tano ya kutembea nayo iwapo akikutana na TRA isiwe usumbufu kwake!.

▪︎ Nilijiuliza sana kwa jinsi yule dada wa kichina anavyokuwa akiprint risiti za uongo mbele yetu watanzania na je ingekuwa mtanzania yuko huko kwao akifanya hivo ingekuwaje?

OMBI
•Naomba sana serkali iendelee kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi ikiwa ni pamoja na kuomba risiti na hii itasaidia vijana wetu kukua na mtazamo huo wa kutoa kodi!

•serkali ijikite katika kuwafatilia wafanya biashara pasipo kuchoka maana ukwepaji wa kodi upo kwa kiasi kikubwa sana saizi maana anapouza bila kutoa risiti anaiibia serkali

•Serkali itambue bila kuwazoesha watanzania hususani wafanya biashara kutoa kodi kwa uaminifu itapoteza mapato mengi sana!

•Serkali itambue kama mwananchi wa kawaida a anakatwa tozo hivo hivo na mfanya biashara kama ilivo kwa mfanya kazi ni lazima alipe kodi ya serkali!

•Serkali itambue pia kwenye suala la kodi hakuna urafiki hapo kuna uwajibikaji kwa kila upande bila kupepesa macho.

•Serkali iachane na kujipendekeza kwa watu ili kuomekana kuwa ni serkali nzuri ndio maana Mwalimu Nyerere alisema serkali fisadi haikusanyi kodi!

•RAIS SAMIA kwenye hili uwe mkali na mwelevu tofauti na hapo mambo yatakuwa mabaya sana hapo baadae yaani watu hawaombi wala kutoa risiti!

HITIMISHO

Watanzania tuweni wazalendo pamoja na serkali kufanya kazi yake kikamirifu ya kukusanya kodi kupitia TRA. Na hii itatuepusha kukimbizana na watu wa hali ya chini kwa kuweka tozo zisizo na msingi!
 
Juma mosi nilienda kariakoo kununua bidhaa kwenye duka linalomirikiwa na mtu mwenye asili ya kichina mara baada ya kufika muuzaji akamiambia yafatayo
▪︎Kitu unachotaka kununua ni cha laki na hamsini ila bila risiti laki na thelathini elfu
▪︎Na ukitaka bila risiti kabisa ni laki na ishirini elfu
Wak
Mfumo wa TRA ni mbovu. Kipindi Wizara ya Fedha iliwahi shauriwa bidhaa zitambulike/zitozwe kodi toka kiwandani huko china. Lakini viongozi wetu wanapenda vitu vinavyowaongezea umaarufu kisiasa.
 
Ni kweli mimi naamini watanzania walishazoea kukwepa kodi ma ikitokea mtu anafatilia kodi kikamirifu watamuona ni adui yao! Lakini wakumbuke tunakoomba misaada hawana utani kwenye kodi lakini huku tumachekeana!
 
Juma mosi nilienda kariakoo kununua bidhaa kwenye duka linalomirikiwa na mtu mwenye asili ya kichina mara baada ya kufika muuzaji akamiambia yafatayo
▪︎Kitu unachotaka kununua ni cha laki na hamsini ila bila risiti laki na thelathini elfu
▪︎Na ukitaka bila risiti kabisa ni laki na ishirini elfu
W
Tatizo liko kwenye viwango vya kodi. Viwango viko juu ndiyo maana watu wengi wanaona ni bora wakwepe. Na TRA hata siku moja hawatakubali kuishauri serikali kuweka viwango rafiki kwa sababu watakufa njaa. Kodi ikiwa ndogo na kila mtu akilipa bila kukwepa TRA watapata wapi watu wa kuwahonga?
 
Kuna vinchi jirani hapa yaani mpaka raha risiti huombi, ukilipia tu huduma au bidhaa inafyatuliwa chap..
 
Jiangalie wewe....
IMG_20210928_230806.jpg
 
Ni kweli mimi naamini watanzania walishaxoea kukwepa kodi ma ikitokea mtu anafatilia kodi kikamirifu watamuona ni adui yao! Lakini wakumbuke tunakoomba misaada hawana utani kwenye kodi lakini huku tumachekeana!
Kodi enzi na enzi hakuna anayependa kulipa.
 
Kama mtazania mzalendo ungetoa taarifa polisi haraka au TRA task force chap...hapo ungekuwa umesaidia...
Mkuu kweli nilipaswa kufanya hivo ila nilikuwa nimebanwa na shughuli ila niliumia sana!
 
Juma mosi nilienda kariakoo kununua bidhaa kwenye duka linalomirikiwa na mtu mwenye asili ya kichina mara baada ya kufika muuzaji akamiambia yafatayo
▪︎Kitu unachotaka kununua ni cha laki na hamsini ila bila risiti laki na thelathini elfu
▪︎Na ukitaka bila risiti kabisa ni laki na ishirini elfu
Wakati niko pale akaja mtu anachukua pisi kama 20 za hiyo bidhaa yule dada akaniambia kaka unamuona huyu pamoja na kwamba anachukua pisi ishirini tunamwandikia risiti ya laki tano ya kutembea nayo iwapo akikutana na TRA isiwe usumbufu kwake!.
▪︎ Nilijiuliza sana kwa jinsi yule dada wa kichina anavyokuwa akiprint risiti za uongo mbele yetu watanzania na je ingekuwa mtanzania yuko huko kwao akifanya hivo ingekuwaje?
OMBI
•Naomba sana serkali iendelee kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi ikiwa ni pamoja na kuomba risiti na hii itasaidia vijana wetu kukua na mtazamo huo wa kutoa kodi!
•serkali ijikite katika kuwafatilia wafanya biashara pasipo kuchoka maana ukwepaji wa kodi upo kwa kiasi kikubwa sana saizi maana anapouza bila kutoa risiti anaiibia serkali
•Serkali itambue bila kuwazoesha watanzania hususani wafanya biashara kutoa kodi kwa uaminifu itapoteza mapato mengi sana!
•Serkali itambue kama mwananchi wa kawaida a anakatwa tozo hivo hivo na mfanya biashara kama ilivo kwa mfanya kazi ni lazima alipe kodi ya serkali!
•Serkali itambue pia kwenye suala la kodi hakuna urafiki hapo kuna uwajibikaji kwa kila upande bila kupepesa macho.
•Serkali iachane na kujipendekeza kwa watu ili kuomekana kuwa ni serkali nzuri ndio maana Mwalimu Nyerere alisema serkali fisadi haikusanyi kodi!
•RAIS SAMIA kwenye hili uwe mkali na mwelevu tofauti na hapo mambo yatakuwa mabaya sana hapo baadae yaani watu hawaombi wala kutoa risiti!
HITIMISHO
Watanzania tuweni wazalendo pamoja na serkali kufanya kazi yake kikamirifu ya kukusanya kodi kupitia TRA. Na hii itatuepusha kukimbizana na watu wa hali ya chini kwa kuweka tozo zisizo na msingi!
Utaratibu umebadilishwa ndugu ndo mana mapato yanapaa badala ya kushuka. Sasa hivi ni takribani trilion 1.9 kwa mwezi wakati kipindi cha jpm na marisit yake ilikuwa chuni ya hapo. Kupanga ni kuchagua we baki na marisiti yako ambayo haya add value.
 
Back
Top Bottom