Wakurugenzi wa wilaya za Dar wamulikwe Kwa hili la kupandisha ushuru wa takataka Kwa wenye maduka mitaani

Wazolee

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
2,701
3,091
Kwa Sasa kilio kikubwa Cha wananchi mitaani hususani wafanya biashara wenye maduka ni kupanda Kwa ushuru wa takataka kutoka tshs 2000 Hadi 5000, 10000 na wengine 20000 Kwa mwezi haijalishi unazalisha taka kiasi gani

Wife ana duka la vitambaa maeneo ya Mbagala mfuko wake wa takataka unaweza ukafika mwezi hauja Jaa kwahiyo hiyo pesa ni kama anatoa sadaka

Jamaa anayekusanya pesa za takataka nilimuuliza Kwa nini mmepandisha sana ushuru wa takataka Kwa wenye maduka akasema ni agizo kutoka Kwa mkurugenzi wa wilaya ya Temeke na ukweli ni kwamba hata sisi tunaokusanya tunapata wakati mgumu sana na tunaona kabisa sio haki ila hatuna la kufanya

Na akasema kibaya zaidi huyo mkurugenzi ameagiza asilimia 18 ya makusanyo iende wilayani akaniambia nielewe vizuri hapa sio 18% ya faida ila ni 18% ya makusanyo Yani haijalishi tumepata faida au hasara wao wanataka 18%

Ukiangalia zile mashine walizopewa na hao wakurugenzi hazitoi control namba ila zinatoa risiti hili linaonyesha kabisa kama hapa Kuna upigaji

Kwanini wanaopewa dhamana ya uongozi katika nchi hi wanakuwa hawana huruma Kwa wananchi na kuwaongezea mizigo Kila siku

Mfanya biashara akienda tu TRA anakutatana na Kodi ya pango 10% hawezi kufanya chochote bila kulipia hiyo Kodi ya pango alafu eti anaanbiwa ukamwambie mwenyewe nyumba wako akurudishie hata hao TRA wanajua kuwa hi Kodi anayelipa ni mfanya biashara na sio mwenye nyumba

Akitoka hapo inakuja Kodi ya makadirio analipa

Akienda manispaa analipia leseni hiyo leseni hapati Hadi alipe Kodi ya service Levy

Akirudi nyumbani anakutatana na ushuru wa takataka 5000 au 10000 Kila mwezi

Mwenyekiti wa mtaa nae anakuja kuchukua 2000 ya ulinzi Kila mwezi

Haya mambo ndio Kuna kipindi wananchi walichoka na wakawapa kura zao wapinzani sio kama wapinzani walikuwa na sera mzuri hapana ila ni Kwa sababu wananchi waliyachoka mambo yanayofanywa na serikali ya CCM
 
Kama hakuna control namba inamaana hiyo 18% inakwenda Kwa wakurugenzi in terms of cash wanakula Kwa urefu wa kamba zao
 
Tatizo ni sisi wananchi wenywewe, tumejaa unafki, wivu na kuchukiana,
Unakuta sehemu mpo wafanyabiashara ishirini lakini hakuna ushirikiano tena dar ndiyo unafki umezidi sana Bora mikoan wanaumoja
 
Tuendelee kukomoana labda ndio shule nzure ya kutoa ubazazi na uzuzu wa kitanzania watz ni mandezi sana kila kitu wanaburuzwa tu.
 
Hili halikubaliki na kitendo hiki Cha CDM kushikamana na ccm inafifisha na kuficha madhaifu ya ccm hakuna wa kuwakosoa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Viongozi wa CDM uwezo wao wa kufikiria ni mdogo sana kipindi kile walibebwa na hasira za wananchi zidi ya CCM ila wao kama wao hamna kitu
 
Kwa Sasa kilio kikubwa Cha wananchi mitaani hususani wafanya biashara wenye maduka ni kupanda Kwa ushuru wa takataka kutoka tshs 2000 Hadi 5000, 10000 na wengine 20000 Kwa mwezi haijalishi unazalisha taka kiasi gani

Wife ana duka la vitambaa maeneo ya Mbagala mfuko wake wa takataka unaweza ukafika mwezi hauja Jaa kwahiyo hiyo pesa ni kama anatoa sadaka

Jamaa anayekusanya pesa za takataka nilimuuliza Kwa nini mmepandisha sana ushuru wa takataka Kwa wenye maduka akasema ni agizo kutoka Kwa mkurugenzi wa wilaya ya Temeke na ukweli ni kwamba hata sisi tunaokusanya tunapata wakati mgumu sana na tunaona kabisa sio haki ila hatuna la kufanya

Na akasema kibaya zaidi huyo mkurugenzi ameagiza asilimia 18 ya makusanyo iende wilayani akaniambia nielewe vizuri hapa sio 18% ya faida ila ni 18% ya makusanyo Yani haijalishi tumepata faida au hasara wao wanataka 18%

Ukiangalia zile mashine walizopewa na hao wakurugenzi hazitoi control namba ila zinatoa risiti hili linaonyesha kabisa kama hapa Kuna upigaji

Kwanini wanaopewa dhamana ya uongozi katika nchi hi wanakuwa hawana huruma Kwa wananchi na kuwaongezea mizigo Kila siku

Mfanya biashara akienda tu TRA anakutatana na Kodi ya pango 10% hawezi kufanya chochote bila kulipia hiyo Kodi ya pango alafu eti anaanbiwa ukamwambie mwenyewe nyumba wako akurudishie hata hao TRA wanajua kuwa hi Kodi anayelipa ni mfanya biashara na sio mwenye nyumba

Akitoka hapo inakuja Kodi ya makadirio analipa

Akienda manispaa analipia leseni hiyo leseni hapati Hadi alipe Kodi ya service Levy

Akirudi nyumbani anakutatana na ushuru wa takataka 5000 au 10000 Kila mwezi

Mwenyekiti wa mtaa nae anakuja kuchukua 2000 ya ulinzi Kila mwezi

Haya mambo ndio Kuna kipindi wananchi walichoka na wakawapa kura zao wapinzani sio kama wapinzani walikuwa na sera mzuri hapana ila ni Kwa sababu wananchi waliyachoka mambo yanayofanywa na serikali ya CCM
Ushuru wa taka inatokana na sheria ndogo za Halmashauri ambazo hutungwa na kupitishwa na Baraza la Madiwani.

Hivyo, mchawi ni madiwani wenu.
 
Back
Top Bottom