TRA Arusha wametumwa na CHADEMA?

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,921
31,161
Tangu jana TRA Arusha,wanasambaza massages kwa wafanyabiashara wote wa Jiji hili la Arusha.

Mwisho wa mwezi September 2020 wafanyabiashara wanatakiwa kulipa SDL,VAT & kodi ya mapato awamu ya 3 na kodi za wafanyakazi vinginevyo adhabu kali ikiwemo riba zitatozwa.

Biashara ktk mji huu unaotegemea utalii zimedorora sana hakuna mauzo ya maana na kibaya zaidi TRA haina mpango wa kushusha kiwango cha kodi ya mapato kuendana na hali halisi ya sasa.

Wakati bado hali haijaka sawa TRA wamekuja na vitisho.Tunajiuliza hivi TRA wanetumwa na Lissu au kuna mkakati wa siri wa kuiangamiza CCM.

Sijui hali iko vipi mikoa mingine
 
CCM ndio wanajimalizia kabisa, maisha ya watu yamekuwa magumu kuliko kawaida, halafu hao TRA wanammalizia kabisa mwananchi mnyonge wa hili taifa, biashara zinakufa watu hawana pesa mifukoni halafu wao wanawaza kuwakamua watu kodi tu.
 
Kwani aliemteua kamishina wa TRA humjui?
Lissu hawezi kuongea wapiga kura hata siku moja

Ninachokiona Kamishna wa TRA anarahishisha hoja ya Lissu kuhusu TRA kufilisi wafanyabiashara.

Fikiria mfanyabiashara wa utalii aliyekadiriwa kodi ya mapato kabla ya Corona (January) kwa mujibu wa TRA bado atatakiwa kulipa kiwango kile kile bila kujali athari za Covid 19.
 
Ninachokiona Kamishna wa TRA anarahishisha hoja ya Lissu kuhusu TRA kufilisi wafanyabiashara.

Fikiria mfanyabiashara wa utalii aliyekadiriwa kodi ya mapato kabla ya Corona (January) kwa mujibu wa TRA bado atatakiwa kulipa kiwango kile kile bila kujali athari za Covid 19.
Hapa anawakumbusha wananchi kuwa lisu anasema ukweli
 
Wanafanya hivyo kwa hisani ya CCM na serikali ya awamu ya tano ya Mh. Jospeh Pombe Joseph Magufuli
 
..."Pesa zipo" ... "_hao hata hawajui pesa zinatoka wapi.." ... " nimeyakamua mafisadi na majizi..." kiukweli Wafanyabiashara wa kati na wakubwa 99% wana kilio kikubwa madai audit kodi miaka karibu 10 nyuma na sasa, unaletewa madai kuthibitisha ikiambana na notice zuio akaunti ya biashara bank husika. Ni dharau ni dhihaka kubwa sana kwa kundi hili linalotoa ajira na kuwekeza!!!
 
Kampuni nyingi za utalii zimefunga shughuli zake, wafanyakazi ( Driver guides) wapo nyumbani hawalipwi mishahara.

Hotel zimefungwa hakuna wageni hizo kodi zinatoka wapi ?.
 
Hasira za kodi za awamu ya tatu zipunguze kura kwa mpenda sifa za kukusanya kodi
 
Back
Top Bottom