CPU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 3,863
- 687
Nimeshindwa hata kushangaa.
Hii kali . . .
Hapa kweli lazima ukose ujasiri wa kushangaa
Hivi ni kweli CAF walikaa wakaamua hivi au waarabu ndo wali-dominate ktk kikao wakapitisha upuuzi huu???
Hivi kweli mashabiki wa Simba wana cha kufurahia hapa kwa muda huu uamuzi ulivyoamuliwa????
Mi naona kuna ujanja hapa . . . .
Waarabu wamesoma alama za nyakati, wameona ngoja tucheze kwanza na TP Mazembe, then wakitolewa watarudi mezani.
Baada ya kuichapa Mazembe 1-0 mechi ya kwanza, wakajipa matumaini. Walivyochapwa 2-0 kule Lubumbashi wakaona KIMEOZA. Wakaamua kukomaa na meza. Then wakajua kwamba hata Simba sasa haijakaa sawa, imesambaratika hivyo wakipanga game ndani ya wiki wana uhakika wa kufuzu. Tena ichezwe game 1 tu kwenye neutral stadium . . . .
Mi sioni mantiki ya kucheza neutral stadium wakati kote Morocco na Tanzania hakuna tatizo, achilia mbali maamuzi haya kichaa ya kuitoa TP Mazembe
Habari ndo hiyo . . . .
Poleni Simba