Tozo za Miamala: Mawakala hatuna majibu tukiulizwa na wateja kuhusu kurudisha makato ya zamani

flulanga

JF-Expert Member
Jul 1, 2016
4,861
6,343
Mawakala tunalia hatuna majibu ya kuwapa wateja wetu pindi waulizapo 'vipi bado hawajarudisha makato ya zamani?' Mawakala tunabaki tunatoa macho na kujibu 'BADO'

Tozo ya mihamala imeathiri kwa kiasi kikubwa wananchi na shughuli nzima ya biashara ya mihamala na biashara nyingine ndogo ndogo.

Kwa jina naitwa heneriko ni wakala wa huduma za kipesa kama vile m-pesa, tigo pesa, airtel money na halo pesa.

Nimeanza biashara hii toka mwaka 2013 miaka miwili baada ya kumaliza shule. Kwa wakati huo biashara hii ilikuwa haina wateja wengi na wala mawakala hatukuwa wengi kama kwa sasa tulivyo wengi. Kadri siku zilivyosonga ndivyo watumiaji wa huduma hii waliongezeka zaidi na hili nililipima mimi mwenyewe kwenye upande wa kipato changu maana kiliongezeka mara dufu na kupata wateja wengi zaidi licha ya watoa huduma kuongezeka kila mahala.

Hapo mwanzo mawakala tulikuwa tunafanya kazi pasipo kukatwa kodi kwenye ingizo la cammision zetu mwisho wa mwezi ila baade tulianza kukatwa kodi ya asilimia kumi (10%) kwa kile tunachokiingiza kila mwisho wa mwezi. Hilo halikubadilisha kitu katika utoaji wangu wa huduma niliendelea kutoa huduma maana niliona nastahili kweli kulipia kodi na kodi kwa upande wangu niliiona ni ya kawaida sanaaaa.

Biashara hii ya uwakala naweza sema ndio biashara ambayo nina uzoefu nayo, hata leo hii ukiniuliza 'biashara gani unauzoefu nayo? Nitakujibu 'uwakala' maana ndio biashara yangu ya kwanza katika maisha yangu.

Naipenda biashara hii kwa sababu malipo yake ni kila tarehe moja nahata kama malipo ni madogo ila nachopenda ni malipo ya pamoja, kwahiyo kama ni kodi ya nyumba utalipa, umeme utalipa, maji utalipa na kodi nyingine utalipa bila shida maana ni pesa inayoingia kwa pamoja. Natoka nimeanza biashara hii naweza sema malipo yake ni ya uhakika endapo tu utafanya kazi. Biashara hii uzuri wake mwingine inahamishika kirahisi unaweza kusema leo nahamia mkoa mwingine na wala mtaji wako usihathirike kwa chochote. Maana wewe silaha yako kubwa ni pesa zako na line (till) zako za kufanyia kazi (mihamala). Vile vile unaweza kuamua kuiacha biashara hii mda wowote na pesa zako zote ukazitoa kama zilivyo.


Changamoto katika biashara hii zipo tena nyingine ni za hatari kabisaaa,

Changamoto hizo ni kama vile:

- Watu kuhisi unapesa nyingi kwahiyo watu wabaya wanaweza kukutengenezea mazingira ya kukuvamia hata kuhatarisha uhai wako.

- Ndugu jamaa na marafiki kuhisi unapesa mda wote kwahiyo wanaishi kwa kukutegemea kuja kukuomba pesa kwa mkopo au hata uwapatie bure pindi wapatapo changamoto inayohitaji uwepo wa pesa. Wanasahau bidhaa yako wakala ni hizo pesa.

- Changamoto nyingine ni kuandamwa na matapeli, watu wabaya mda mwingi wanakujadili wakuingie vipi ili waweze kukutapeli pasipo kutumia nguvu.

- Changamoto nyingine ni upotevu wa pesa pasipo kujua zimepotelea wapi (wengine uhisi labda chuma ulete) hii ni kulingana na maelezo ya mawakala wenzangu ila kwa upande wangu sijathibitisha hili na kama lipo basi Mungu aninusuru. Ila mara nyingi naamini upotevu wa pesa kwa mawakala unatokana na kutokuwa makini na sifuri (0) mfano mteja anaweza kuja kuweka shilingi elfu kumi (10,000) ila ikatokea kwa bahati mbaya ukazidisha sifuri moja badala yake unajikuta umemwekea shilingi laki moja (100,000).

Biashara ya uwakala (mihamala) naweza sema imenisaidia kama kijana kujikomboa kiuchumi. Nimeweza kuishi na mwanamke kama mke na watoto wawili mmoja anasoma shule ya private naweza sema nimeweza kuiondolea serikali mzigo wa kumpatia mtoto wangu elimu bure na badala yake hiyo nafasi inatumiwa na mtoto mwingine, nimeweza kusaidia ndugu zangu kuwatoa hatua moja na kuwapeleka hatua nyingine kimaisha, nimeweza kufahamiana na watu wengi zaidi na wengi kupitia biashara hii wamenitafsiri kuwa mimi ni mtu mwaminifu kwasababu tu naifanya biashara hii kwa weledi na kwa muda mrefu.

Biashara hii naipenda na ninamalengo nayo kwasababu ishajaribu biashara nyingine zinanishinda kwa hiyo mwisho wa siku niliamua kuchukua maamuzi ya kuwekeza zaidi katika hii biashara ya mihamala uwekezaji huo ikiwepo na kukuza mtaji zaidi na kuongeza huduma za kibenk kama vile crdb, nmb hii ni kwa maeneo nilipo ndio soko lake lipo vizuri.

Mwaka huu mwezi huu wa 7 tarehe 15 serikali imeleta kitu wanaita tozo ya mihamala. Tozo hii ni kubwa sana na imeenda moja kwa moja kuathiri biashara hii ya mihamala. Wateja wetu tuliokuwa tunawategemea ndio walipandishiwa tozo hizo kwahiyo wengi wao wamehamia kwenye huduma za kibenk na wale ambao wanawatu wao kwenye mabasi wanatumia madereva na makondakta kusafirishia pesa zao na wale wa maeneo ya karibu wanaona bora hizo pesa wazipeleke moja kwa moja kwa muhusika kuliko kuziweka kwenye simu zao kisha ndio watume.

Tozo hizi zimeathiri mfumo mzima wa hii biashara. Kwa mimi binafsi imeathiri zaidi ya asilimia hamsini (50%) ya kipato changu toka tozo hii ianze. Kwahiyo Ndoto zangu naona zinafifia za kuishi kama mfanyakazi wa kada ya kawaida au hata zaidi.

Tozo hizi zikiendelea zitaathiri maelfu ya vijana maana biashara hii kwa asilimia zaidi ya 75 inafanywa na vijana kwa hiyo serikali inaenda tena kupunguza ajira ambazo vijana walijiajiri kwa mitaji yao au hata kwa kukopa kwenye taasisi mbalimbali.

Ukiachana na mawakala, tozo hii inaenda kuwapunguzia faida wafanya biashara mbali mbali hasa wafanya biashara wadogowadogo. Faida aliyokuwa anaiingiza mfanya biashara itapungua maana uagizaji wa bidhaa utakuwa juu maana hiyo tozo na yenyewe ataiingiza kama ni moja ya gharama ya mzigo aliouagiza. Wafanya biashara wadogowadogo wengi wao hawana uwezo wa kusafiri na kufata bidhaa kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine matokeo yake walitumia huduma za simu kuagiza pesa na kutumiwa bidhaa husika kwa sababu hata mizigo wanayoagiza ni midogo. Ila wafanya biashara wakubwa wanauwezo wakufata bidhaa hiyohiyo kwa ukubwa kwa pamoja. Kwahiyo nachokiona tozo hii inaenda kumuumiza zaidi mfanya biashara mdogomdogo.

Tozo hii pia inaenda kumuumiza mtanzania aishie vijijini. Vijijini hakuna huduma za kibenk kusema labda mwananchi wa kijijini atakuwa na njia mbadala kukwepa tozo hii kama vile mwananchi aishie mjini.

HITIMISHO; serikali iliangalie swala hili kwa haraka. Ni bora ikusanye kodi ndogo ndogo isiyomuumiza mtu yoyote ila ikakusanya kwa watu wengi zaidi. Kuliko kukusanya kodi kubwa kwa watu wachache zaidi ambao hawana njia mbadala yaaani wale wanaosema 'TUTAFANYAJE SASA, HATUNA JINSI' ila hawa pia siku wakipata njia mbadala uwezi kuwapata tena.

Sisemi kuwa hii tozo waifute kabisaaa la hasha!! Bali serikali iangalie uwezekano wa kuipunguzaa kwa asilimia hata 75 katika hiyo tozo walioiongeza, alafu waangalie sehemu nyingine zaidi ya moja pakuifidishia. MWISHO

Wenu mtiifu henerico.
 
Acha waendelee kutiwa kwa sababu CCM walipopora uchaguzi 2020 na kuchukua nchi kwa mabavu wakati kila mtu anajua kuwa CCM haina uwezo tena wa kuongoza, wao walichukua hatua gani?
 
Ijapokuwa wewe umerepost tu lakini muambie Henerico acheze na upepo. Ni kweli watumiaji wa fedha za mitandao ya simu wamepungua sana, ila watumiaji wa huduma za kibenki wameongezeka pia!.

Ni muda sasa aanze kutoa huduma za uwakala wa benki.
 
muwe mnawashauri wakaandamane
Huu ushauri muhimu Sana kwa watanzania wote , nimekumia sana Leo , Sina hata mia nimeomba mtu anitumia tokea wiki moja iliyopita amejizungusha na kusema makoto makubwa , nimetumiwa Leo hii bado analalamika , na hicho kidogo nimekatwa , muhimu Sana
 
Ivi nyie wenye vibanda vya mpesa hamna umoja wenu, uundeni umoja wakati ndo huu, ili iwe rahisi kuandaa maandamano ya kupinga tozo umiza ,
 
Huu ushauri muhimu Sana kwa watanzania wote , nimekumia sana Leo , Sina hata mia nimeomba mtu anitumia tokea wiki moja iliyopita amejizungusha na kusema makoto makubwa , nimetumiwa Leo hii bado analalamika , na hicho kidogo nimekatwa , muhimu Sana
jioni hii nilipita kuweka kwa wakala. Nikakuta jamaa anamlilia dada wakala amsaidie kuhamisha flot kwa wakala mwenzie..dada kakataa. mpaka nikawa natamani kucheka 🤣🤣
 
Walisema watazipitia upya, lakini zilikuwa sound tu zile............bado wanaendelea kukamua na madelu anaendelea kutafuta popularity na misururu ya magari.
 
Back
Top Bottom