Gharama za Lipa kwa simu mbona zimepanda sana?

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,792
15,693
Leo nilikuwa natumia huduma ya Lipa kwa simu kupitia voda, nikalipia bidhaa yenye thamani ya elfu 15 nikakatwa sh. 850, kama sijasahau hii huduma hapo mwanzo ilikuwa na lengo la kumsaidia mteja pale anapolipia bidhaa, ilianza kwa mteja kulipia bidhaa bila kukatwa, then wakaja na makato madogo, sahivi yamezidi kuwa makubwa.

Kwa mwendo huu hii Lipa itakuwa na msaada kweli uliokusudiwa ama ndio wameona dili lipo huku baada ya kubanwa na serikali kwenye M-Pesa kwa makato lukuki? Sijajua kwa mitandao mingine, ila nafikiri kama Voda 'mtandao mama' wamepandisha basi na mitandao mingine itapandisha. Cc vodacom
 
Voda wana wanyonya sana mawakala fikiria wakala kawekeza mtaji na mda plus kodi ya fremu na TRA....zen mtu akitoa 300,000....wakala anapata 1,100/ zen wao vodacom wanachukua elfu sita na usheee
1100 kwa muamala mmoja ni faida nzur mbona ... mawakal wakubwa kwa siku anaweza fanya hata miamala 100 ya design hiyo so kwa siku akapata 110000

Mkuu unatakaje zaid ya hapo
 
Back
Top Bottom