Toyota hizi...!

Vihela vinawaua vijana....wengi utakuta gari ya kwanza.....anasafiri nayo 'kuitoa carbon'
 
Halafu inaishia kumtoa yeye roho
Hivi ulimuona yule jamaa aliekufa kwenye Hilux? Alibanwa yuko hai kuanzia usiku hadi saa nane hivi ndio akafa anajiona. Yaani watu hawawezi kumtoa wanabaki wanapiga nae stori. Simjui yule jamaa ila roho iliniuma sana. Hatuna rescue team wala nini, ukipata ajali hadi kupata msaada ni masaa, halafu madogo bado wanafanya mchezo na haya magari. Nakumbuka maneno ya yule jamaa 'haya magari haya...'
 
Mungu wangu huyo sijamuona duu... Rescue team, vifaa na wasamaria walio committed pia...... Alikufa kifo cha maumivu mengi
 
kuliko gx100?
Gx100 Model,iwe ni Chaser au MarkII zilikataliwa mapema sana iliyotamba tamba ni Cresta nayo sasa imeshapotea sokoni.

Gx90 na mdogo wake Gx80/81 kwa ambao wanazo hadi sasa wanaonekana wana magari roho za paka,Kariakoo kuna wahindi wanazo MarkII Grande na Chaser Gx 81 watu wanawagombania wawauzie ila leo hii Gx100 taka hata 1.5Mill hakuna atakayekusimamisha japo kukuuliza bei.
 
Daaaaah, RIP damu changa kabisa aisee.Kuna best yangu huwa anajisifu sana kufuta dsahboard yotee 180, alafu anasema haimtoshi, majuzi kavuta kitu BMW maana dashboard yake 260 KpH. Nimemshauri hashauriki.
 
Hicho chuma ninacho, nitakaa nacho hadi nizeeke
 
Mmh lakini GX MIA hasa Chaser na Cresta bado zinauza japo bei huwa haivuki 4M
 
Daaaaah, RIP damu changa kabisa aisee.Kuna best yangu huwa anajisifu sana kufuta dsahboard yotee 180, alafu anasema haimtoshi, majuzi kavuta kitu BMW maana dashboard yake 260 KpH. Nimemshauri hashauriki.
BMW kwa barabara zetu hizi ukienda sana ni 200 mpaka 210.... Hii speed nilishawahi kujaribu mara moja tu tena sikuenda zaidi ya km 10 nikarudi 180
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…