Toyota hizi...!

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,754
Si kwamba nazikandia hizi gari za kijapan la hasha. Nimewahi kuzimiliki Chaser mayai na balloon GX90. Kila moja imevuma kwa nyakati zake. Zikisifika kwa wepesi mwendo (kuchanganya haraka) kiyoyozi kama Greece land. Zimepita model nyingi.

Tunamalizia enzi za Harrier TAKO LA NYANI zimechuja haraka baada ya nyingi kupiga chini.

TOYOTA crown bado iko juu lakini nayo inaendelea kuchinja watu. Simlaumu mjapani katengeneza kwa matumizi yake na taratibu zake. Huku hatuzingatii hili kabisa

Mwisho tunaishia kulaumu na kusema TOYOTA hizi....!!!
lakini pamoja na Toyota nyingi kuwa na viwango vidogo vya usalama kulinganisha na gari za ulaya bado tatizo ni letu sisi wenyewe.....!

ELIMU JUU YA VYOMBO VYA MOTO hasa gari nyepesi za kijapani ni finyu mno...! tumepoteza damu changa nyingine Kabuku. Damu ya Rchunga... Rip
IMG-20190523-WA0257.jpeg
IMG-20190523-WA0256.jpeg
IMG-20190523-WA0254.jpeg
 
Pole kwa waliofikwa na hayo. Ukiangalia siku hizi madereva wengi wanajua kukanyaga mafuta na break basi. Sheria na alama za barabarani hawazijui, na wanaozijua baadhi hawazifuati kabisa, achilia mbali kujua uwezo wa gari na namna ya kulihandle barabarani ndio shida kubwa zaidi.
 
Udereva wa mitaani.... Hakuna hata nafasi ya kufundishwa kuhusu uchumi na athari za mwendokasi
 
Back
Top Bottom